UTANGULIZI
Shukurani zote zinamstahiki Allah peke yake,Rehma na amani
zimwendee Mtume(s.w.a) pamoja na ahli zake na swahaba wake wote.
Amma baad:
Hakika sababu za msingi zilizo nipelekea kuandika ki tabu hiki na
hali iliyo jionyesha ya kushamiri kwa harakati za Raafidhwa za
kuwalingania watu katika dhehebu hili potofu na harakati hizi zimekuwa
kiulimwengu, na kutokana na hatari kubwa ya kundi hili kwa dini ya
uislamu na kutokana na hali ya kughafilika na kuji sahau kwa waislamu
wengi kutokana na hatari ya kundi hili, na kutokana na itikadi yao iliyo
jaa ushirikina, na kuitukana Qur-an na Maswahaba-Radhi za Mwenyezi
Mungu ziwe juu yao-na kupituka mipaka juu ya Maimamu wao, ndio
maana nimeazimia kuandikakitabu hiki na kuyajibu mambo yanayo
watatiza watu kuhusu kundi hili kwa muhtasari, nikufuata nyayo za
Sheikh wetu Sheikh Abdallah bin Abdurahman-aljibrin- Mungu
amuhifadhi-katika kitabu chake "Atlaaliiqaat alaa Matni lumuatiliitiqaad"
na kwa kunukuu katika vitabu vya Raafidhwa ambavyo ni
maaraufu na mashuhuri kwao, na katika vya Ahlusuna miongoni mwa
wema walio tangulia na walio kuja baaada yao amabao waliwajibu
Raafidhwa na kubainisha ubovu wa itikadi zao zilizo simama juu ya
ushirikina, na uongo, na kuchupa mipaka, na matusi.
Na nimejaribu kwa kadri ya uwezo wangu katika kitabu hiki
kuwasimamishia hoja,kupitia vitabu vyao wanavyo vitegemea, kama
alivyo sema Sheikh Ibrahim bin Sulaiman Aljab-han-Mwenyezi Mungu
amrehem-"Nitakusimamishia hojakupitia mdomowako ewe Shi'a.
Mwisho na muomba Allah awanufaishekupitia kitabu hiki wenye
mazingatio kama alivyo sema Allah "Hakika katika hayo mna ukumbusho
kwa wenye kuwa na nyoyo zinazo zingatia, aumwenye kutega sikio na
hali moyo wake uko hadhir" Qaf:37
Natoa shukrani kwa kila alie changia katika kitabu hiki,namuomba
Allah awalipe kila la kheri.
Rehma na amani zimuendee bwana wetu Muhammad na ahli zake
na Maswahaba zake.
Imeandikwa na Abdallah Muhammad Assalafy.
- 4 -
NI LINI LIMEDHIHIRI KUNDI LA RAAFIDHWA?
Lili anza kundi la Raafidhwa wakati alipojitokeza Myahudi
mmoja aitwae (Abdallah bin sabai) akidai kuwa ni Muislam, na kwa
madai ya kuwapenda Ahlul bayt (watu wa nyumbani kwa Mtume) na
akapituka mipaka katika kumtukuza Ally (r.a) na akadai kuwa mtume
alimuusia kuwa khalifa baada yake, kisha akamnyanyua na kumuweka
katika daraja ya uungu na haya yanathibitishwa na vitabu vya kishia.
Kwa mfano Alqmmy katika kitabu chake (Almqaalatu walfiraq)
(1): Anakiri kuwepo kwake (Ibnu sabai) na anamzingatia kwamba ndie
mtu wa mwanzo aliesema kuhusiana na uimamu wa Ally na kurejea
kwake, na akaanzisha kuwatukana Abubakari na Omar na Uthmani na
maswahaba wengine, kama alivyosema Annuubkhty katika kitabu chake
(Firaq Shia) (2). Nakama alivyosema pia Alkushiy katika kitabuchake
maarufu ( Rijaalul-kushiy) (3). Na katika mashia wa sasa hivi wanaosema
kuwepo kwa Abdalla bin Sabai ni Muhammad bin Ally Al muallim
katika kitabu chake ( Abdallah bi Sabai Alhaqiikatul-majuhuula) (4). Na
mtu kukubali jambo ndio dalili kubwa, nahawa wote tulio wataja ni
katika Mashekhe wakubwa wa kiraafidhwa.
Amesema Albaghdaadiy: "Assabaiyya ni wafuasi wa Abdallah
bin Sabai ambae alichupa mipaka katika kumtukuza Ally (r.a) na kudai
kuwa alikuwa ni Nabii, Kisha akachupa mipaka zaidi mpaka akadai kuwa
alikuwa ni Mungu".
Na amesema Albaghdaadiy vilevile: "Na alikuwa Ibnu Saudaiyaani
Ibnu Sabai- Asili yake ni Myahudi katika watu wa Aliirah,
akadhihirisha Uislamu kwa kutaka awena ukubwa kwa watu wa Alkuufa,
akawaambia(watu wa kuufa) kwamba amekuta katika Taurati kwamba
kila Mtume anae waswiy (mrithi) na kwamba Ally (r.a) ndie mrithi wa
Mtume (s.a.w)".
Na amesema Ashihristany kuhusu Ibni Sabai kwamba ndie mtu
wa kwanza aliesema kwamba kuna nasswi (dalili) juu ya uimamu wa
Ally (r.a), na akaeleza kuhusu kundi la Sabaiya kwamba ndilo kundi la
kwanza lililo anzisha itikadi ya kutoweka kwa Imamu wao wa kumi na
mbili(Almahd Almuntadhwar) na kurejea kwake, kisha Shia wakarithi
itikadi hiyo baada yao, pamoja na kutofautiana kwa makundi yao,kuhusu
uimamu wa Ally na ukhalifa wake. Na hayo ni katika athari za Ibni Sabai,
na yaliongezeka makundi ya Shia na itikadi zao na kauli zao yakawa
makundi mengi sana.
Nahivi ndivyo walivyo zua Mashia itikadi ya Alwaswiy, Arrajaa,
Alghaiba, bali itikadi ya kwamba maimamu wao wanasifa za uungu (5)
kwa kumfuata Myahudi Ibnu sabai.
- 5 -
(1) Rejea: Almaqaalaatu wal firaq cha Alqummy uk.10-21
(2) Rejea: Firaqu Shia cha Anuubakhty uk. 19-20
(3) Rejea: aliyoyataja Alkushiy katika riwaya zake mbalimbali kutoka kwa Ibni Sabai na itikadi zake, tazama namba:
170,171,172,173,174 katika uk. 106-108
(4) Na kitabu hiki ni majibu ya kitabu alichokitunga mshia aitwae Murtadhwa Al-askary kwa anuani (Abdallah bin Sabai wa
asaatwiru ukhra) ambae alipinga katika kitabu chake kuwepo kwa Abdallah bin Sabai.
(5) Rejea Usuulu i-itiqaad Ahli Sunna waljamaa cha Allaalakaaiy (1/22-23).
- 6 -
KWANINI SHIA WAMEITWA RAAFIDHWA?
Jina hili kalitaja Sheikh wao Almajlisy katika kitabu chake
(Bihaarul-anwar) akasema katika mlango alio uita, mlango kuhusu (
Ubora wa raafidhwa na uzuri wa kujiita jina hili), kisha akataja kutoka
kwa Sulaiman Al-aamash kuwa amesema: niliingia kwa Abii Abdillah
Jaafar bin Muhammad nikasema kumwambia: Hakika watu wanatuita
Raafidhwa, nini maana ya Raafidhwa? Akasema: wallahi sio wao walio
kuiteni hivyo bali Mwenyezi Mungu alikuiteni hivyo katika Taurati na
Injili kupitia ulimi wa nabii Mussa na nabii Issa. (1)
Na imesemekana kuwa: wameitwa raafidhwa kwa sababu
walikuja kwa Ally bi Hassan wakamwambia: Jitenge na Abubakari na
Omar ili tuwe pamoja nawe, akasema: wao ni vipenzi wa Babu yangu,
siwezi kujitenga nao bali niko pamoja nao, wakasema: hivyo basi
tumekukataa, ndipo wakaitwa Raafidhwa, na akaitwa kila alie muunga
mkono Zaid kuwa ni Zaydiyya. (2)
Na inasemekana:wameitwa Raafidhwa kwa kupinga kwao utawala
wa Abubakari na Omar. (3)
Na imesemekana: Wameitwa hivyo kwa kukataa kwao Dini. (4)
(1) Tazama kitabu (Bihaarul-anwar) cha Almajlisy 65/97. (ambacho ni miongoni mwa marejeo yao muhimu katika vitabu vyao
vya sasa)
(2) Rejea: Attaaliqaat alaa matni lum-atul iitqaad cha Sheikh Abdallah Aljibriin uk.108.
(3) Tazama Maqaalaatul-Islaamiyiin cha muhyi ddiin Abdulhamiid (1/89)
(4) Maqaalatul Islamiyiin 1/89
- 7 -
RAAFIDHWA WAMEGAWANYIKA MAKUNDI MANGAPI?
Imekuja katika kitabu (Daairatul-maarif) kuwa "Makundi ya Shia
ambayo ni mashuhuru yako zaidi ya sabini na tatu"(1)
Bali imepokewa kutoka kwa Raafidhwa Mir baaqir Addaamand
(2) kwamba makundi yote yaliyotajjwa katika Hadithi, Hadithi ya
kugawanyika kwa Umma wa Muhammad katika makundi sabini na tatu
yamekusudiwa makundi ya Mashia, na kwamba lililotajwa kuwa ni kundi
lililosalimika ni kundi la imaamiyya.
Na ametaja Almaqriizy kuwa makundi yao yanafikia mia tatu .
Na amesema Ashihristany: "Hakika Raafidhwa wamegawanyika katika
makundi matano:Alqiisaaniyya, Azaydiyya, Al imaamiyya, Alghaaliyya,
Al ismaailiyya," (4)
Na amesema Albaghdaady: " Hakika Raafidhwa baada ya zama za
Ally (r.a) wako makundi manne: Zaidiyya, Imaamiyya, Kiisaaniyya, na
Alghulaatu" (5)
Lakini yakupasa kutambua kuwa Zaydiyya si katika kundi la
Raafidhwa ispokuwa kundi la Aljaaruudiyya.
(1) Rejea: Daairatul Maarif (4/67)
(2) Ni Baaqir bin Muhammad Al-istiraabaady, Maarufu kama Al-miir Addamaad, amekufa mwaka 1041.Tazama maelezo yake
katika kitabu (Alkunaa-wal-alqaab) cha Abbaas Alqummy 2/226
(3) Ni Almaqriizy (2/351)
(4) Rejea: Almilal wannihal cha Ashihristaany uk.147
(5) Rejea: Alfarqu bainal-firaq, cha Albaghdaady uk.41
- 8 -
NI IPI ITIKADI YA ALBADAA WANAYO IAMINI RAAFIDHWA?
Al badaa maana yake ni kudhihiri baada ya kutoweka, au kwa
maana ya kuanzishwa kwa rai mpya. Na neno hili (Albadaa kwa maana
zote mbili linamaanisha kuwepo hali ya kutojua jambo kisha kujua
kunakuja baadae, na mambo yote haya mawili kwa Allah ni muhali, aliki
Raafidhwa wanainasibisha sifahii ya ( Albadaa) kwa Mwenyezi Mungu.
Imepokewa kutoka kwa Rayyaani bin Asswalt kwamba
amesema:" nilimsikia Arridhwaa akisema: hajapata Mwenyezi Mungu
kumtuma nabii yoyote ispokuwa kwa kuharamisha pombe na kukiri
(Albadaa) kuwa ni katika sifa za Allah" (1)
Na kutoka kwa Abdalla amesema: 'Hajapata kuabudiwa
Mwenyezi Mungu kwa jambo lolote kama Albadaa" (2) katukuka
Mwenyezi Mungu na hayo kutukuka kukubwa kabisa.
Tazama ndugu yangu Muislam jinsi wanavyo mnasibishia Allah
sifa ya ujinga. Ilihali Mwenyezi Mungu anasema: " Hakuna alioko katika
Mbingu na Ardhi ajuae Ghaibu (yasio onekana au hayaja tokea) ila
Mwenyezi Mungu" Annaml 65
Badala yake wanaitakidi kuwa Maimamu wao wanajua elimu
zote, wala halifichikani kwao jambo lolote. Je hii inaweza kuwa itikadi ya
Uislamu aliyo kujanayo Muhammad (s.a.w)?
(1) Rejea; Usuullkaafi uk.40
(2) Rejea: Usuululkaafi cha Alkulayny katika kitabu tauhiid (1/331)
- 9 -
NI IPI ITIKADI YA RAFIDHWA KUHUSU SIFA ZA ALLAH?
Raafidhwa ndio watu (kundi) wa mwanzo waliopinga sifa za Allah na
kudai kuwa kumthibitishia baadhi ya sifa ni kumfanya kuwa ana
kiwiliwili. Sheikhul-islamu ibnu taymiya kamtaja mtu wa kwanza kuleta
itikadi hii katika Raafidhwa kuwa ni Hisham bin Al-hakam(1) na Hishamu
bin Saalim aljawaliiqiy na Yunusi bin Abdirahamani Alqummiy na abuu
jaafari al-ahwal(2).
Wote waliotajwa hapo juu ni katika mashekhe wakubwa wa
Ithnashariya,kisha wakawa jahmiyya wanaopinga sifa za Allah,kama vile
wengi wao katika riwaya zao nyingi walivyomsifu mwenyezi mungu kwa
sifa mbaya ambazo waliziambatanisha na sifa ambazo zinathibiti kwa
Allah(s.w)
Amepokea Ibnu Baabawaihi zaidi ya riwaya sabini (70) zinazosema
kuwa Allah, "hasifiki kwa zama,wala sehemu,wala namna,wala
kutikisika, wala kuhama toka sehemu hadi sehemu nyingine,wala hana
sifa miongoni mwa sifa za kimaumbile,wala huwezi kumuhisi,wala yeye
si kiwiliwili,wala hana sura".(3)
Na kwahiyo mashekhe wao wakafuata njia hii potofu,pamoja na
kuzikataa sifa za Allah zilizo thibit katika Qur-an na Sunna za mtume
(s.a.w)
Vilevile wanapinga na kukataa kuteremka kwa Allah (s.w)katika
mbingu ya dunia katika theluthi ya usiku kama ilivyo thibiti katika
hadithi sahihi,na wanasema kwamba Qur-an imeumbwa (sio maneno ya
Allah) na wanapinga kumuona Allah siku ya kiyam(hataonekana).
Imekuja katika kitabu (Bihaarul-an-waar) kwamba Abuu Abdillah
Jaafar Asaadiq,aliulizwa kuhusu Allah(s.w) je ataonekana siku ya
Qiyama?
Akasema ametakasika mwenyezi mungu na hilo kutakasika kuliko
kukubwa,hakika macho hayaoni isipokuwa kitu chenye rangi na
umbile,na mwenyezimungu ndie muumbaji wa rangi na maumbile(4).
Bali wamesema, lau kama mtu atamnasibisha Allah na baadhi ya
sifa, kama vile kuonekana, basi anahukumiwa kama ameritadi (katoka
katika uislamu). Haya yamepokewa kutoka kwa shekhe wao Jaafar
Annajafy(5).
(1)Rejea;Minhaaju sunna(1/20) cha sheikh Ibnu Taymiya.
(2)Rejea Itiqaadaatu firaqulmuslimiin walmushrikina uk.97
(3)Rejea; attauhiid cha Baabawayhi uk 57
(4)Rejea: Bihaarul-answer cha al majlis (4/31)
(5)Rejea: kashful ghitwai ukurasa wa 471
- 10 -
Lakini ni muhimu utambue (ndugu msomaji wa kitabi hiki)
kwamba Allah kathibitisha mwenyewe katika Qur-ani kuwa waumini
watamuona siku ya qiyama kama ilivyo kuja katika suratl qiyama "Nyuso
sikuhiyo zitakuwa ni zenye kung'ara.ni zenye kumtazama mola
wake."alqiyama:22-23.
Naimethibiti katika sunna sahihi za mtume,kama ilivyo katika
sahihi al bukhari na muslim,katika hadithi ya Juraiji bin Abdillah
Albajaly, kasema: "Tulikuwa tumeketi na mtume (s.a.w)akautazama
mwezi usiku wa tarehe 14 akasema:" "Hakika mtamuona mola wenu
kama mnavyouona mwezi huu, hampati shida katika kuuangalia."(1)
Na aya na hadithi zinazothibitisha jambo hili ni nyingi hatuwezi
kuziorodhesha zote.
1-Rejea katika bukhari no(544) na muslim no:(633) kwa faida
- 11 -
NI IPI ITIKADI YA RAAFIDHWA KUHUSU QUR-ANI HII TULIYONAYO
AMBAYO ALLAH KACHUKUA AHADI YA KUIHIFADHI?
Hakika Raafidhwa,ambao katika zama zetu ndio wanaitwa (SHIA)
wanasema: Hakika Qur-ani tuliyonayo siyo Qur-ani ile aliyoiteremsha
Allah(s.w) kwa mtume (s.a.w) bali imebadilishwa, ikazidishwa na
kupunguzwa.
Na jamuhuri wa wanachuoni wa hadithi wa kishia wanaitakidi
kwamba Qur-ani imebadilishw, hii ni kwa mujibu wa maneno ya Annuri
attwabrisiy katika kitabu chake (Faslul-khitwaab fii tahriif kitabu rablarbaab)(
1)
Na amesema Mohammad ibn Yaaqub Alkulayny, katika kitabu
chake (Usuulul kafi) katika mlango aliouita (Hawakuikusanya Qur-ani
yote isipokuwa maimamu)(anakusudia maimamu wao) kisha akaleta
riwaya ifuatayo: "Kutoka kwa Jaabir, amesema:nilimsikia Abu Jaafar
akisema: Hajapata kudai mtu yoyote kuwa kaikusanya Qur-ani yote kama
alivyo iteremsha Allah ispokuwa atakuwa ni muongo. Hakuna
alieikusanya na kuihifadhi kama alivyoiteremsha Allah ispokuwa Ally
bin Abii Twaalib na maimamu baada yake"(2).
Na imepokewa toka kwa Jaabir toka kwa Jaafar (mwenyezimungu
amrehemu) kwamba amesema: "Hawezi kudai mtu yoyote kwamba
anayo Qur-ani kamili ispokuwa walioachiwa wasia"(3)
1-Rejea: Faslulkhitwab cha Hussein bin Mahdi Taqiyyun-nuury Ahwabrasy uk.32
2-Rejea: Usululkaafi cha Alkulayn (1/228)
3-Rejea: Usululkafi cha Alkulayn (1/285)
- 12 -
Na imepokewa kutoka kwa Hisham bin Saalim, toka kwa Abii
Abdillah (Jaafari) amesema: "Hakika Qur-ani aliyokujanayo Jibrilu kwa
mtume (s.a.w) ni aya 17,000."(1)
Maana ya maneno hayo ni kwamba Qur-ani wanayoidai
Raafidhwa ni zaidi ua Qur-ani hii tuliyonayo, ambayo Allah kachukua
ahadi ya kuihifadhi zaidi ya mara tatu. Tunamuomba Allah atukinge na
upotevu wao.
Na ametaja Ahmadi Attwabrisi katika kitabu chake (Al-ihtiyaaJ)
kwamba Omar alimwambia Zaid bin Thaabit: Hakika Ally alikuja na
Qur-ani, ndani mnafedheha za muhajiriina na answari, na tumeonelea
tutaje Qur-ani_ nyingine_na tuyaondoe mambo yote ya fedheha za
muhajirin na answari, Zaid akakubaliana nae katika hilo.
Kisha akasema: Endapo mtamaliza kuiandika Qur-ani kama jinsi
mtakavyo nyinyi, halafu Ally akadhihirisha Qur-ani aliyonayo, je
hatakuwa kabatilisha kazi mliyoifanya?. Omar akasema: hivyo ni lipi la
kufanya? Zaid akasema: wewe ndio utajua ufumbuzi, Omar akasema:
Hakuna ujanja zaidi ya kumuuwa Ally ili tupate kupumua, akafanya
mipango ya kumuuwa Ally kupitia Khaalid bin Waliid, lakini hakuweza.
Pindi Omar alipotawala ukhalifa, alimuomba Ally awape Qur-ani
ili waibadilishe,akasema Umar: Ewe abal hassan(Ally) Waonaje
ungetuletea Qur-ani uliyokuwa umeileta kwa Abuu Bakari ili
tuwaunganishe watu katika msahafu mmoja? Akasena (Ally) Hakuna
uezekano wa jambo ulitakalo, kwani nilikuwa nimeuleta kwa Abuu
Bakari ili kunsimamishia hoja na ili msijekusema siku ya Qiyama
"Hakika sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo" Surat al aaraaf: 172 au
msijekusema "Haikutujia" Al araaf: 129, hakika hii Qur-ani hawaigusi
isipokuwa walio twaharika, na wale waliousiwa katika wanangu(kizazi
changu). Omar akasema: je kunamuda maalumu wa kuidhihirisha? Ally
akasema: Ni pale atakapo simama mtoto katika watoto wangu
akiidhihirisha na kuwaamrisha watu kuifuata.(2)
1-Rejea: usululkaaf cha alkulayny (2/634) kathibitisha shekhe wo riwaya hii katika kitabu chake (Qiraatu al-uquul) (12 525)
Akasema: hadithi hii ni thiqa(yakutegemewa)
2-Rejea: Al-ihtijaaj cha Attwabrisy, uk. 225 na kitabu Faslulkhitwab uk. 7
- 13 -
Na kwa vyovyote vile watakavyo jidai Mashia kukikana kitabu
(Annur) cha Attwabrisy, Kwa itikadi yao ya (Taqiya), Hakika kitabu
hicho kimejaa(kimesheheni) mamia ya dalili toka kwa wanazuoni wao
katika vitabu vyao tegemezi, zinazothibitisha kwamba wao wanaitikadi
na kuamini kuwa Qur-ani imebadilishwa isipokuwa hawapendi kuamsha
makelele ( na malumbano) kuhusu itikadi yao hii juu ya Qur-ani.
Na inabain kuwa kuna Qur-ani mbili, moja inayojulikana kwa
waislamu wote, na nyingine ni makhsusi(maalumu) imefichwa, na hiyo
ndio kunapatikana ndani yake surat Al wilaya, ambayo mashia wanadai
kwamba iliondolewa katika Qur-ani.
Pia katika aya ambazo wanadai kufutwa katika Qur-ani, ni ile
aliyoitaja Amry Attwabrasy katika kitabu chake (Faslulkhitwab fii tahriif
titab rabil arbaab) ambayo ni (Na tukainua utajo wako kwa ally ambaye
ni mkwe wako) Wanadai imeondolewa katika suratl-inshiraah(alam
nashrah) wala hawaoni haya katika madai yao haya hali yakuwa wanajua
wazi kuwa sura hii ni makkiyyah(imeteremshwa makkah) na Ally
hakuwa mkwe wa mtume makkah.
- 14 -
NI IPI ITIKADI YA RAAFIDWA KUHUSU MASWAHABA WA MTUME
(S.A.W)
Imejengeka itikadi ya Raafidwa juu ya kuwatukana na
kuwakufurisha masahaba wa mtume (s.a.w) rehema na amani zishuke juu
yao, Ametaja alkulayn katika kitabu(Furuul-kaafy) kutoka kwa Jaafary
(a.s) "waliritadi watu woote baada ya mtume (s.a.w) isipokuwa watu
watatu,Nikasema: ni kina nani hao watatu? Akasema ni Miqdaad ibnu
As-wad, na Abudhari al-ghifariy, na Salmaan al-faarisy".(1)
Na ametaja Almajlisy katika kitabu (Bihaarul-an-waay) kwamba
mtumishi wa Ally ibnul-Husain kasema: Nilikuwa naye (a.s_ katika
baadhi ya sehemu alizokuwa akijitenga, nikasema kumwambia: Hakika
mimi ninashakia baadhi ya haki kwako,naomba nieleze kuhusu watu
hawa wawili, Abubakari na Omar, Akasema: Nimakafiri na kila mwenye
kuwapenda ni kafiri". Pia imepokewa toka kwa Abi Hamza Athumaly
kwamba alimuuliza Ally bin Alhusain kuhusu Abubakari, Akasema;
"Nikafiri na kila atakaemuunga mkono pia ni kafiri.(2)1
1-Rejea: FURUUL-KAAFY cha Alkulayny uk.115 1
2- Rejea:BIHARUL-AN-WAR cha Almajlisy 69/137-138.
- 15 -
Na katika tafsiri ya Alqummy katika kauli yake mwenyezi mungu
"Na mwenyezi mungu anakataza kutenda kila makosa, na hasa madhambi
yaliyo pita mipaka kwa ubaya, na kila kisicho pendeza, hali kadhalika
anakataza kumfanyia ubaya mtu."nnahl ;90" Wametafsiri (Faahisha)Kuw
ni Abubakari na (Munkari) Kuwa ni Omar) na (Albagh-yi) Kuwa ni
Uthmani.(1)
Na ametaja Almajlisy katika (Biharul-an-war) Kuwa:Habari
zinazo onesha(elezea) ukafiri wa Abubakari na Omari na mfano wao, na
juu ya malipo ya kuwalaani na kujitenga nao, na habari zinazoelezea
uzushi wao ni nyingi kiasi kwamba haitoshi kuelezea katika kitabu hiki
au katika vitabu mbalimbali, lakini haya machache tuliyoyataja yanatosha
kwa mtu ambae Mwenyezi Mungu kataka kumuongoza katika njia iliyo
nyooka.(2)
Bali kataja Almajlis katika (Biharul-an -war) Riwaya mbalimbali
kwamba Abubakari na Omar na Uthmani na Muawiya (wenyezi mungu
awarehemu) kwamba watakuwa katika masanduku ya moto.(3)
- 16 -
Na wanasema(Raafidhwa) katika kitabu chao (Ihqaaql-haq) cha
Al-mar-ashy:"Ewe mwenyezi mungu mrehemu muhammad pamoja na
ahli zake, na walaani masanamu wawili wa kiquraish, na matwaaghuti
wao, na mabinti wao..." (4) wakiwa wanawakusudia Abubakari na Omar
na bibi Aisha na Hafswa bint Omar, mwenyezi mungu awarehemu.
1
1-Rejea: Tafsiri ya Alqummy uk 1/390
2-Rejea: Biharul-an-war cha Almajlisy30/230
3-Rejea: Biharul-an-war cha Almajlisy 30/236
4-Rejea: Ihqaaqul-haq 1/337.angalia dua ya masanamu wawili mwisho wa kitabu.
- 17 -
Na ametaja Almajlisy katika risala yake aliyo iita"Al-aqaaid" akasema: Na katika mambo
yanayozingatiwa kuwa ni muhimu sana katika dini ya Imaa miyyah ni kuhalalisha Mut-a, na Hajj
tamatui, na kujitenga mbali na watu watatu(Abubakari na Omar na Uthumani na Muawiya na Yazid
bin Muawiya, na kila aliye mpiga vita Amiril-muuminina Ally) (1)
Na katika siku ya Ashuraa (Rafidhwa)huleta mbwa na wakamita Omar, kisha wanaanza kumpiga
kwa fimbo na mawe mpaka anakufa, kisha wanaleta mtoto wa Mbuzi kisha wanamuita Aishan na kisha
wanaanza kumnyonyoa manyoya yake na kumpiga hadi anakufa.(2)
Pia huwa wanasherehekea siku aliyo uwawa Omar bin Alkhatwaabi, na wanamuita Abuu luu lu atilmajuusy
ambae alimuuwa Omar kuwa ni shuja wa dini(3)
Tunamuomba mwenyezi mungu awarehemu maswahaba wote pamoja wake zake mtume (s.a.w) ambao
ni mama w waumini.
Hebu tizama ndigu msomaji ubaya na chuki zilizo bebwa na kundi hili potofu lililo toka katika
uislamu, na mambo wanayosema juu ya watu wema kama hawa, ambao ndio watu bora baada ya
mitume, watu ambao mwenyezimungu kawasifu, na mtume wake pia, na umma wa kiislamu
umekubaliana juu ya uadilifu wao na ubora wao, bali hata historia inashuhudia ubora wao na juhudi
zao kubwa katika dini hii ya uislamu.
1-Rejea: Risaalatul-aqaaidi cha Almajlisy uk 85
2-Rejea: Tabdiil dhwalaam wa tanbii haan-myaam cha shekh Ibrahim aljabhaan uk 27
3-Rejea: Abbaasul-qummy (Alkunaa wal-alqaab 2/55
- 18 -
RAAFIDHWA WANAFANANA NA MAYAHUDI
Amesema sheikhul islamu bin taymiyyah mungu amrehemu,(ushahidi
juu ya hilo ni kwamba,Matatizo ya Rafidhwa ndio matatizo ya
Mayahudi,Kwa sababu Mayahudi wanasema:Ufalme haupaswi kuwa
isipokuwa katika kizazi cha Daudi,Na Raafidwa wanadai kuwa
utawala(al imama) haupaswi kuwa isipokuwa kwa mtoto wa Ally (R.A).
Pia mayahudi wanasema:Hakuna jihadi katika njia ya Allah mpaka
atakapo kuja Masihi Dajjali ashuke na upanga.Na Raafidwa wanasema:
Hakuna jihadi katika njia ya Allah mapaka atakapokuja Mahdi na utoke
wito wa jihadi kutoka mbinguni.
Pia Mayahudi huchelewesha sala zao mpaka nyota zinapo kusanyika,
Vilevile Raafidwa nao huchelewesha magharibi mpaka nyota
zikusanyike,Ilhali hadithi ya Mtume(S.A.W) Inatufundisha
kwamba(Hautaacha kuwa ummati wangu katika kheri muda wa kuwa
hauicheleweshi sala ya magharibi mpaka kukusanyika kwa nyota)1
Mayahudi waliigeuza Taurati,Vilevile Raafidwa nao wameigeuza Qurani.
Mayahudi wanapinga jambo la kupangusa katika khofu: Vilevile
Raafidhwa wanalipinga jambo hilo.
Mayahudi wanamchukia Malaika Jibrilu, Wanasema: Huyo ni adui yetu
miongoni mwa malaika.Vilevile Raafidwa wanasema: Jibrilu alikosea
kuleta utume kwa Muhammad(S.A.W).1
Vilevile Mayahudi na Wakristo wamewashinda Raafidwa kwa mambo
mawili,Kwanza: waliulizwa Mayahudi: Ni nani aliye bora katika watu wa
mila yenu? Wakasema: wabora kwetu ni wafuasi wa Musa.Nawa
wakristo wakaulizwa:ninani aliebora katika mila yenu? Wakasema: Ni
wanafunzi wa nabii Issa(Yesu).
Raafidwa wakaulizwa ninani M-baya zaidi na muovu katika mila yenu?
Wakaema wafuasi wa Muhammad(S.A.W)1
Na ametaja Sheikh Abdallah al-jamiily katika kitabu chake (Badhlul
majhuud fii mushabahati arrafidwa lil yahuud) Kwamba katika mambo
mbayo Raafidwa wamefanana na Mayahudi ni,Mayahudi na
Maraafidhwa wanawakufurisha watu wote wasiokuwa miongoni mwao
na kuzihalalisha damu zao na mali zao,Kisha sheikh akasema: Mayahudi
wanawagawa watu katika mafungu mawili tu(Mayahudi na
ummamiyuun) Ummamiyuun ni kila asiekuwa Yahudi,na wanaitakidi
kwamba wao ndio waumini pekeyao,Ama Ummamiyuun wao ni makafiri
- 19 -
NI IPI ITIKDI YA RAAFIDWA JUU YA MAIMAMU?
Raafidwa wanadai maimamu wao ni (Maasuumiin) yaani
wamehifadhiwa na madhambi, na kwamba wanajua ghaibu. Kayanukuu
haya alkulayniy katika kitabu (usuulul-kaafy) : "Kasema Imamu Jaafar
Asswadiq : Sisi ni hazina ya elimu ya Mwenyezimungu, Sisi ni wafasiri
wa amri za Mwenyezi Mungu,Sisi ni watu tuliokingwa na dhambi,
Imeamrishwa tutiiwe, na imekatazwa tusiasiwe, Sisi ndio hoja ya
Mwenyezi Mungu ya wazi kwa viumbe vilivyo chini ya ardhi na mbingu
na vilivyo juu ya Ardhi". (1)
Pia kasema Alkulayny katika (Alkaafy) Katika mlango aliouita
mlango kuhusu (kwamba maimamu pindi wanapotaka kujua jambo basi
hujua tu), Imepokewa toka kwa Jaafar kwamba amesema "Hakika imamu
anapotaka kujua basi hujua tu, na kwamba wao wanajua muda wa kufa
kuwa ni lini, na kwamba wao hawafi ila kwa hiyari yao wenyewe" (2)
Na amesema Alkhumainiy katika kitabu chake (Tahriirul-wasla)
kwamba "Hakika Imamu anayo nafasi tukufu, na daraja ya juu, na
utawala wa kufanya kila kitu viko chini ya utawala wake vyote vilivyo
katika ulimwengu" na akasema pia "Hakika sisi (anakusudia maimamu
wa ithnasharia) tunazo hali Fulani kwa Mwenyei Mungu ambazo hazipati
malaika wala nabii yoyote".(3)
(1)Rejea: Usuululkaafy cha Alkulayniy 1/165
(2)Rejea: Usuululkaafy cha Alkulayniy 1/258
(3)Rejea: Tahriirul-walah cha Alkhumainy uk.52,94
tu wala hawamjui Allah (s.w).Imekuja katika kitabu chao (Attilmuud)
Kwamba: Mataifa yoote wasiokuwa Mayahudi ni washirikina.
Wamemkufurisha hata Nabii Issa (A.S),Kama ilivyokuja katika
Attilmuud, wamemsifu na kumtaja kuwa ni kafiri,wala hamjui Mungu.
Raafidwa nao wanaitakidi kwamba wao ndio waumini pekeyao,na kila ambae si Raafidwa basi ni kafiri wala
hana fungu lolote katika uislamu.
Ama kuhusu sababu za Raafidwa kuwakufurisha wailamu ni kwakuwa hawaitakidi(Al wilaya) Ambayo ndio
itikadi ya Raafidwa, na kwamba jambo hili ni nguzo katika nguzo za Uislamu na kila asie itakidi hivi basi huyo ni
kafiri kwa mujibu wa imani yao ni kama ambae hajatamka shahada mbili,au ni sawa na alie acha sala tano, bali
Alwilaya kwao ni jambo ambalo limetangulizwa juu ya nguzo zote za Uislamu.
Amepokea Albarqiyu kutoka kwa Abdallah(a.s) kwamba amesema(hakuna yoyote anaefuata mila ya Ibrahimu
isipokuwa sisi tu na wafuasi wetu, Ama watu wengine wote wamejitenga na mila yake.)
Na imekuja katika tafsiri ya Alqummy, kuwa imepokewa kutoka kwa Abdallah(a.s) kwa amesema(Hakuna
yoyote alie katika mila ya Uislamu isipokuwa sisi,mpkaka siku ya Qiyama)1
- 20 -
Bali imefikia hali kwa Maraafidhwa waliochupa mipaka katika
kuwatukuza na kuwafadhilisha (kuwafanya bora) maimamu
wao,wamewafanya bora juu ya manabii wote isipokuwa Muhammad
(s.a.w) (1)
Hawakuishia hapo tu, bali wanasema kuwa maimamu wao
wanautawala wa mwisho kabisa. Ameyataja haya Alkhui katika kitabu
chake (Misbaahul-faqaaha) akasema: Ni wazi kwamba hakuna shaka
kabisa juu ya utawala wao juu ya viumbe wote, kama ilivyo bainisha
katika maneno yao, kwa kuwa wao ndio sababu ya ulimwengu, na wao
ndio sababu ya kupatikana viumbe, maana kama si wao basi watu wote
wasingeliumbwa, bali wameumbwa kwa ajili yao, na kuwepo kwao ni
kwaajili yao….. na utawala walionao maimamu ni kama utawala wa
Mwenyezi Mungu juu ya viumbe wake".(2)
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde na upotevu wao huu!!
Vipi maimamu wawe ndio sababu ya kupatikana viumbe? Vipi wawe
sababu ya kuwepo ulimwengu? Vipi watuwote waumbwe kwaajili ya
maimamu wao, ilhali Mwenyezi Mungu anasema katika sura
Adhaariyaati 56 "Sikuwaumba majini na watu ila tu wapate kuniabudu".
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atukinge na itikadi potofu kama
hii inayopingana na qur-ani na suna za Mtume (s.a.w).
Kasema Sheikhul-islamu bin Tayimiya (Wanadai Raafidwa kuwa
dini inafuata matakwa ya wanachuoni wao,halali ni ile wanao ihalalisha
wao, na haramu ni ile wanao iharamisha wao,na dini ni yale
wanayoyataka wao".
(1) Rejea: mir-aatul-uquul fii shar-hi akhbari rasuul cha Almajlisiy 2/290
(2) Rejea: mis-baulfuqaaha cha Abil-qaasim Alkhui 5/33
(3) Rejea: minhaajusunna cha IbnuTayymiya 1/482.
- 21 -
NI IPI ITIKADI YA KUREJEA WANAYO IAMINI RAAFIDWA?
Raafidwa wamezua bid-a (uzushi) wanayoiita (AR-RAJ-A),
Kasema Almufiid kuwa: "Wamekubaliana Imamiya juu ya kurudi
(kufufuka) wengi katika watu waliokufa".(1)
Na itikadi hii inakusudia kufufuka kwa imamu wao wa mwisho
wanaemuita (Al-qaaim) atatoka katika zama za mwisho akitokea katika
pango, ambaye atakuja kuwauwa wapinzani wake wote na kuwarejeshea
mashie haki zao walizo porwa na makundi mbalimbali katika historia ya
kuwepo kwao.(2)
Amesema Assayid almurtadhwa katika kitabu chake (Almasaailu
annaaswira) kwamba Abubakari na Omar, watasulubiwa katika zama
hizo(za kutoka kwake) huyo imamu wao wa kumi na mbili wanaimuita
(Qaaim ahali Muhammad) na kwamba mti utakuwa mbichi kabla ya
kusulubiwa kwao lakini baada ya kusulubiwa kwao utakauka.(3)
Na amesema Almajlisy katika kitabu (Haqul-yaqiin) kutoka kwa
Muhammad Albaaqir: " pindi atakapodhihiri Almahdi, basi atamfufua
bibi Aisha kisha amsimamishie hadd (adhabu)". (4)
Kisha wakayapanua makusudio na maana ya Arraj-a na kudai kuwa
Mashia wote watafufuka na maimamu wao, na wagomvi wao nao
watafufuka na maimamu wao.
Itikadi hii potofu inatubainishia chuki kubwa zilizo fichika katika
nafsi zao ambazo zinawapelekea kueleza upotofu kama huu, na itikadi hii
ndio iliwapelekea As-abaiyya wakakanusha kuwepo siku ya mwisho.
(1) Rejea:Awaailul-maqaalaat cha Almufiid uk.5
(2) Rejea:Alkhtuutul-ariidhwa, cha muhibuddin alkhaatwib uk.80
(3) Rejea: Awaailul-maqaalsst cha Almufiid uk.95
(4) Rejea: Haqul-yaqiin cha Muhammadul-baaqir Almajlisy uk.347
- 22 -
Na madhumuni ya kurejea ni kulipiza kisasi kwa wagomvi wao,
lakini ni akina nani wagomvi wao? Riwaya ifuatayo itakubainishia ndugu
msomaji chuki waliyonayo Raafidhwa dhidi ya Ahlusunna, na jinsi
walivyo karibu zaidi na Mayahudi na Manaswara: Ameeleza Almajlisy
katika kitabu chake (Biharul-anwar),kutoka kwa Abii baswiir kapokea
toka kwa Abu Abdillah(a.w) amesema: alisema: Ewe abu muhmmad:
kanakwamba ninatazama kushuka kwa (alqaim) katika masjidis-sahla
akiwa na watu wake na familia yake….mpaka akasema…
nikamwambia,Atakuwa na msimamo gani kuhusu Ahlu dhimma?
Akasema:Atawapa amani kama alivyowapa amani mtume (s.a.w), na
watatoa kodi hali ya kuwa ni madhalili,nikasema, je waliokufanyieni
uadui? Akasema :Hapa ewe Abu muahammad,yeyote alietukhalifu katika
dola yetu hatakuwa na nafasi yoyote, hakika Mwenyezi mungu
katuhalalishia damu zao, wakati atakapokuja Alqaim, lakini pindi
atakaposimama huyo msimamaji wetu, atalipiza kisasi kwa ajil ya
Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwaajili yetu pia.91)
Hebu tazama ndugu muislamu jinsi gani huyo Mahdi wa Mashia
atawapa amani Mayahudi na Manaswara, halafu awapige vita Ahlu
sunna!
(1) Rejea: Biharul-anwar cha Almajlisy 25/376.
- 23 -
NI IPI ITIKAD YA "TAQIYYAH" KWA RAAFIHDHWA?
Amesema taqiya mmoja wa wanazuoni wao wa zama hizi kuwa
"Taqiya ni kitendo cha mtu kusema au kufanya kinyume na vile anavyo
itakidi, kwa lengo la kujikinga na madhara yeye au mali yake au kulinda
utu na heshima yake" (1)
Na wanadai kwamba mtume (s.a.w) alifanya (Taqiya) wakati
alipokufa kiongozi wa wanafiki Abdallh bin Ubayi bin Saluul, pindi
alipokuja kumswalia, kisha Omar (r.a) akamwambia Mtume (s.a.w) Hivi
Mwenyezimungu si kakukataza kumsalia mtu huyu mnafiki?, Mtume
(s.a.w) akamwambia wewe unajua ni nini nimesema? Nimesema : Ewe
mola wangu mjaze ndani yake moto, na ulijaze kaburi lake moto, na
umuingize motoni" (2)
Hebu tazama nduguyangu muislamu vipi wanamzulia na
kumnasibisha Mtume (s.a.w) na uwongo?! Hivi inaingia akilini kwamba
maswahaba wa mtume (s.a.w) wanamtakia reham na Mtume (s.a.w)
akimlaani?!.
Na amenukuu Alkulayny katika (Usuulul kafii):"kasema Abu
Abdillah : Ewe Omar hakika asilimia tisa ya dini ipo katika taqiya, na
hana dini asiyekuwa na Taqiya, na Taqiya inaingia katika kila kitu
isipokuwa katika pombe na kupangusa juu ya khofu".
Na amenukuu vilevile Alkulayny toka kwa Abi Abdillah kwamba
amesema "icheleeni dini yenu, na ikingeni kwa Taqiya, kwa hakika hana
imani asiyekuwa na Taqiya"(3)
(1) Rejea: Ashiatul miizaan, cha Muhammad JawadMughniyat uk.47
(2) Rejea: Furuu-ulkafii, kitabul janaiz uk 188
(3) Rejea: Usuulul kafii uk 482-483.
- 24 -
Bali imefikia hali kwa Raafidwa wanajuzisha kuapa kwa asiye kuwa
Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa Taqiya!!
Ameyaeleza hayo Alhurul aamily katika kitabu chake (Wasaailu shia)
kuwa imepokewa kutoka kwa ibu Bukhari, toka kwa Zuraara toka kwa
Abi Jaafar (r.a) amesema: nilisema kumwambia Abu jaafar : Hakika sisi
tunapita kwa watu wanatutaka tuape juu ya mali zetu na ilhali
tumeshakwisha zitolea zaka, akasema (Abujaafar): Ewe Zurara pindi
utakapo chelae hilo basi wewe apa kwa vyovyote vile
watakavyotaka,Nikamuuliza : Hata kuapa kwa talaka? Akasema kwa
chochote watakacho taka.
Na imepokewa toka kwa Sumaa toka kwa Abii Abdillah (a.s) amesema:
"Pindi mtu atakapo apa kwa Taqiya hakuna tatizo maadam kalazimishwa,
na kalazimika kufanya hivyo".(1)
Raafidhwa wanaitakidi kuwa Taqiya ni faradhi ambayo madhehebu yao
hayasimami bila ya Taqiya, na wanaitumia hasahasa katika mazingira
magumu, hivyo inatakiwa ndugu muislamu utahadhari sana na hawa
Raafidhwa.
(1) Rejea: wasaailu shia cha Al-hurril-omily 16/136-137.
- 25 -
NI IPI ITIKADI YA UDONGO WANAYOIAMINI RAAFIDHWA?
Makusudio ya udongo katika itikadi ya Raafidhwa, ni udongo wa
kaburi ya Hussein (r.a) Ameeleza mmoja wa wapotevu miongoni mwao
aitwae Muhammad Amnuumanul-haarithy,ambae wanamuita (Asheikhul
mufiid) katika kitabu chake (Al mazaar) imepokewa kutoka kwa Abi
Abdillah kwamba amesema:" katika udongo wa kaburi ya
Hussein,kunapatikana ponyo la kila maradhi,nao ndio dawa iliyo kubwa
kabisa'.
Na amesema Abdallah : wafanyieni tahniki ( yaani watilieni
mdomoni mara tu baada ya kuzaliwa kwao) watotowenu kwa udongo wa
kaburi ya Hussein.
Na akasema vilevile: Alitumiwa Abdul Hussein Arridhwa mzigo
(furushi la nguo) kutoka khurasaan ndani yake mkiwa na
udongo,akaulizwa alie tumwamzigo huo, Ni kitu gain hiki?
Akasema:Huu ni udongo kutoka katika kaburi ya Hussein.Hapakuwa
panatumwa mzigo wowote isipokuwa ndaniyake panawekwa udongo,
anasema:Udongo huu ni amani kwa idhini ya Mwenyezi mungu. Na
inasemakana kwambamtu mmoja alimuuliza swaadiq kuhusu kutumia
udongo wa kaburi la Hussein, akajibu kumwambia: Pindi utakapoula basi
sema hivi: Ewe Mola wangu hakika mimi nakuomba kwa haki ya ufalme
ulioushika,na kwa haki ya Mtume aliye hifahiwa,nakuomba umpe rehma
Muhammda (s.a.w) pamoja na watu wa nyumba yake, na ujaalie udongo
huu kuwa ni ponyo la kila ugonjwa,na uwe ni kitulizo cha amani
kutokana na kila khofu, na niulinzi kutokana na kila baya.
Pia Raafidhwa wanadai kwamba, Mashia wameumbwa kwa
udongo maalum,na Sunni wameumbwa kwa udongo mwingine kisha
ukachanganywa udongo huo wote,basi maasi na maovu yanayofanya
Mshia yeyote ni kutokana na athari ya udongo walioumbiwa Masunni. Na
kheri na uongofu anaekuwanayo Sunii yeyote ni kutokana na athari za
Udongo walioumbwa shia.Pidni itakapofika siku ya qiyama, basi maovu
ya Mashia watabebeshwa Masunni, na mema ya Masunni watapewa
Shia.(1)
(1) Rejea: Ilaalu asharaa uk. 490-491. Biharul anwar 5/247-248
- 26 -
NI IPI ITIKADI YA RAAFIDWA KUHUSU AHLU SUNNAH?
Miongoni mwa itikadi mbaya za Raafidwa ni kwamba
wanahalalisha damu na mali za Ahlu sunnah Amepokea aswadiq katika
(Al-ilal) kutoka kwa Daa-uudi bin Farqad amesema: "Nilimuuliza abu
abdillah, unasemaje kuhusu Naasiby? (Naswibi wanakusudia
Ahlusunnah), akasema:Damu yake ni halali, hatakama utaweza
kumuangushia ukuta au kumzamisha baharini basi fanya
hivyo.Nikamuuliza vipi kuhusu mali yake? Akasema pindi utakapoweza
kuichukua basi ichukue".(1)
Pia Raafidhwa wanaitakidi kwamba kizazichao ndio kizazi safi,
Ameeleza Hashimu Albaharany katika tafsiri yake(Alburhan) imepokewa
toka kwa maytham bin Yahya,kutoka kwa Jaabir bin Muhammad,
amesema"Hakuna mtoto yoyote azaliwaye isipokuwa Ibilisi anakuwa
haadhir katika kuzaliwa kwake,anapojua mtotohuyo ni katika Shia basi
shetani mkubwa anamkinga huyo mtoto kutokanan na ibilisi, na kama sio
katika shia basi shetani huingiza kidolechake katika sehemu zake za
nyuma(katika makalio ya mtoto), nah ii ndio sababu ya kuwa mtoto wa
kiume huzaliwa kaelekea chini, na kama ni mtoto wa kike basi shetani
huingiza kidole chake katika utupu wake, hivyo anazaliwa akiwa ni
muovu, na ndio maana mtoto huzaliwa analia sana"(2)
Bali mashie wanaitakidi kwamba watu wote ni watoto wa zinaa
isipokuwa Shia peke yao!! Ameeleza Alkulayny katika kitabu chake
(Arraudhwatu minalkafi) kutoka kwa Abi Hamza,kutoka kwa Abu Jaafar
(a.s) kwamba amesema: "Nilisema kumwambia, hakika baadhi ya jamaa
zetu wanazua uwongo na kuwatuhumu wasio waungu mkono, akamjibu
kuwa, kuachana nao ni bora zaidi, kasha akasenma: Wallah ewe Abu
Hamza hakika watu wote ni watoto wa zinaa isipokuwa Shia".(3)
(1) Rejea: almahaasin Annafsaaniya uk166
(2)Rejea: Tafsirul burhani cha Hashim Albahrany 2/300
(3) Rejea: Arraudhwatul minalkafi cha Alkulayny 8/285.
- 27 -
Na katika itikadi za raafidwa wanaona kwamba Ahlusunna ukafiri
wao ni mkubwa zaidi kuliko ukafiri wa Mayahudi na manaswara, kwa
sababu wao asili yao ni Makafiri, ama Ahlisunna kwamba wao
wameritadi,na ukafiri wa kuritadi ni mkubwa zaidi, hii ni kwa mujibu wa
ijmai, na ndio mana wanakuwa bega kwa bega dhidi ya waislamu, kama
historia inavyojieleza.(3)
Imekuja katika kitabu (wasaailu shia) kutoka kwa Alfudhwail bin
yasaar amesema: "Nilimuuliza Abu Jaafar je naruhusiwa kumuozesha
Naswibii mwanamke wa kirafidwa? Akasema: Hapana, kwa sababu
Naswibii ni kafiri" (4)
Na manaswibii kwa ahlusunna ni wale ambao wanamchukia Ally
bin Abitwaalib(r.a), lakini Raafidwa wao wanawaita ahlusunna Naswibii,
kwa sababu wanamtanguliza Abubakari na Omar na Uthmani juu yaAlly,
pamoja na kwamba kumtanguliza Abubakari na Omar n Uthmani juu ya
Ally ndivyo ilivyo kuwa zama za Mtume (s.a.w), na ushahidi wa haya ni
kauli ya ibni Omar: ". Na amezidisha Attwabrani katika Alkabiir:
"Tulikuwa tukifadhilishwa baina ya watu katika zama za (s.a.w)
tunamfadhilisha Abubakari kisha Omar Kisha Uthmani " Amepokea
bukhari. Na amezidisha Attwabrani katika alkabiir: "Na Mtume (s.a.w)
alikuwa akilijua hilo wala hatukemei katika hilo". Pia ibnu Asskir
amesema :"tulikuwa tukimfadhilisha Abubakari na Omar na Uthmani na
Ally".
Amepokea imamu Ahmad na wengineo kutoka kwa Ally bin Abi
twalib kwamba amesema: Mbora wa umma huu baada ya Mtume (s.a.w)
ni Abubakari kisha Omar, na laiti ningependa ningemtaja wa tatu".
Amesema Imamu Ahnad kwamba athari hii ni mutawaatir.(5)
(4) Rejea: wasaail shia cha Alhurul aamily (7/431) Attahdhiib (7303)
(5)Attaaliqaat alaa matni lumuatul-iitqaad cha sheikh Jibrin uk.910
- 28 -
NI IPI ITIKADI YA RAAFIDHWA KUHUSU NDOA YA MUT'A NA INA
UBORA GANI KWAO?
Ndoa ya mut'a inafadhila kubwa kwa Raafidhwa, kama wanavyo
dai, imekuja katika kitabu (Manhaju sswadiqiin) cha fat'hullah
Alkaashan, kapoke a toka kwa Asswaadiq: Hakika Mut'a ni katika dini
yangu na dini ya baba yangu, basi mwenye kuifanya hiyo anatekeleza
dini yetu, na mwenye kuipinga,huyo atakuwa anaipinga dini yetu, bali
huyo anaifuata dini nyingine isiyokuwa dini yetu, Na mtoto anaezaliwa
katika ndo ya mut'a ni bora kuliko anaezaliwa katika ndoa ya kawaida,
Na mwenye kuipinga mut'a huyo ni kafiri ameritadi, (1)
Amenukuu Alqummy katika kitabu (Man laa yahdhuruhul- faqiih)
kutoka kwa abdallah bin sinani, kutoka kwa Abdillah amesema: "Hakika
mwenyezi mungu mtukufu katuharamishia kinyaji chochote chenye
kulevya, na akatupa badalayake mut'a" (2)
Naimekuja katika (Tafsiri ya manhaju sswaadiqiin) ya Mullah
Fat'hullah Alkaashaany: "Amesema mtume (s.a.w) Mwenye kufanya
mut'a mara moja, basi huachwa huru na moto theluthi yake, na mwenye
kufanya mara mbili huachwa huru na moto theluthi mbili, na mwenye
kufanya mara tatu,basi huachwa huru na moto yeye mzima"
Na katika kitabu hichohicho, imekuja kuwa "kasema Mtume
(s.a.w) mwenye kufanya mut'a mara moja, basi huyo kasalimika na
ghadhabu za Mwenyezi mungu, na atakae fanya mara mbili atafufuliwa
pamoja na watu wema, na atakaefanya mara tatu huyo atakuwa nami
peponi".
Pia katika kitabu hichohicho kwamba amesema Mtume(s.a.w)
mwenye kufanya mut'a mara moja, anakuwa katika daraja ya Hussein, na
mwenye kufanya mut'a mara mbili yuko katika daraja ya Hassan, na
mwenye kufanya mut'a mara tatu, anakuwa katika daraja ya ally bin
Abitwaalib, na mwenye kufanya mara nne daraja yake ni kama daraja
yangu"(3)
(1) Rejea: manhaju sswaadiqiin cha Mullah Fut'hullah Alkaashany 2/495
(2) Rejea;man laa yah dhuruhulfaqiih cha ibnu baabawaihi Alqummy uk. 330
(3) Rejea: Tafsir Manhaju sswaadiqiin cha mullah Fut'hullah Alkaashany 2/ 492-493
- 29 -
Na marafidhwa hawakuainisha idadi maalumu katika swala la
mut'a, imekuja katika (Furuu ul kaafy) na (Attahdhib) na (al-istibuswari)
kutoka kwa Zuraara kapokeya toka kwa Abiabdillah, kasema :"Aliulizwa
kuhusu mut'a kwamba je nikatika wanawake wa nne walio ruhusiwa?
Akasema:waweza kuowa mpaka elfu moja, kwa sababu wao ni mwenye
kukodiwa. Na pia imepokewa kutoka kwa Muhammad bin muslim,
kutoka kwa Abi Jaafar kwamba, alisema kuhusu ndoa ya mut'a: kwamba
hao sikatika wale wa nne, kwa sababu mwanamke anaye olewa ndoa ya
mut'a hapewi talaka, wala hana fungu lolote katika mirathi,bali yeye ni
mwenye kukodiwa tu ".(1)
Vipi hali hii na ilihali Mwenyezi Mungu anasema "Na wale ambao
tupu zao wanazilinda.Isipokua kwa wake zao au kwa (wanamwake) wale
iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao ndio wasio
laumiwa.(Lakini)Anaye taka kinyume cha haya basi hao ndio warukao
mipaka (Ya Mwenyezi Mungu).(Almu-uminun 5-7).
Kwa hiyo aya hizi zinatubainishia kwamba ndoa zinazo ruhusiwa
ni mke na wale iliyo wamiliki mikono ya kuume,na kinyume na hawa
basi ni haramu, hivyo mut'a ni zinaa, tunamuomba Mwenyezi Mungu
atukinge na shari.
Amesema sheihk Abdallah bin Jibrin kwamba (Raafidhwa katika
kuhalalisha mut'a wanaitumia aya iliyokuja katika suratun nisaai aya ya
24 " Na pia (mmeharamishiwa)wanawake wenye(waume zao) isipokua
wale iliyo wamiliki mikono yenu ya kuume(ndio)sheriya ya Mwenyezi
Mungu juu yenu.Na mmehalalishiwa(kuowa wanawake)wasio hawa
muwatafute kwa mali zenu, kwa kuwaowa bila ya kufanya zinaa. Basi
wale mnao waowa miongoni mwao wapeni mahari yao yalyio lazimishwa
.Wala si vibaya kwenu katika (kutoa) yale mliyo ridhiana badala ya yale
yaliyo tajwa.Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na mwenye
hekima."Annisaai:24
(1) Rejea: Alfuruu minal kaafi cha Alkulayny 5/451 na Attahdhib 2/188.
- 30 -
Na jawabu la hoja hii ni kwamba: Hakika aya zote hizi kuanzia
aya ya 19 hadi aya ya 23 zinazungumzia ndoa, kisha baada ya kutaja wale
walio haramishwa kwa nasabu na kwa sababu zingine akasema
Mwenyezi Mungu "Mmehalalishiwa wanawake wengine wasio kuwa
hawa walio tajwa, basi pindi mtakapo waoa ili kustarehe nao kihalali,
basi wapeni mahari zao mlizo kubaliana, na kama wakisamehe chochote
katika hizo mahari zao kwa ridhaa zao basi hakuna ubaya katika hilo."
hivyo ndivyo walivyo ifasiri aya hii kongamano la maswahaba na walio
kuja baada yao".(1)
Hata Shekh wa kundi la Attusy katika kitabu chake (Tahadhiibulahkaam)
ameitaja kwa ubaya ndoa ya Mut`a, anasema:"Kama akiwa
mwanamke anatoka katika nyumba ya watu watukufu basi haifai kumuoa
katika ndoa ya mut`a, kwa kuchelea aibu itakayo ipata familia yake na
udhahalili utakao mpata yeye". (2)
Bali hali imefikia kwa hawa Rafidhwa wanahalalisha kumuendea
mwanamke kinyume cha maumbile.Yamekuja haya katika (Alistibswaar)
kutoka kwa Ally bin Alhakam amesema;"Nilimsikia swaf
wani anasema:Nilimuuliza Ar-ridhwaa nikasema:Hakika mmoja katika
wafuasi wako kanituma nikuulize jambo ambalo yeye kaogopa na kaona
aibu kukuuliza,akasema;nilipi ?akasema:Je inafaa mtu kumuingili mke
wake kinyume cha maumbile? Akasema:Ndio inafaa." (3)
(1) Ni katika maneno ya Shekhe Ibnu Jibrin.na dalili nyingine ya kuharamisha mut`a katika suna za Mtume(s.a.w) ni Hadithi ya
Rabiu bin Sabura Aljuhany kwamba babayake alimuhadithia kwamba alikuwa pamoja na Mtume (s.a.w) akasema:"Enyi watu
hakika mimi nilkuwa nimekuruhusuni kufanya Mut`a ,hakika Mwenyezi mungu ameiharamisha mpaka siku ya Qiyama,yoyote
ataye kuwa na mwanamke ambaye kamuoa ndoa ya Mut`a basi na amuache,na wala asichukue chochote alichokuwa kampa".
Kaipoke Muslim Nnambari (1406).
(2)Rejea: Tahdhiibul-ahkaam cha attusy 7/227 .
(3) Rejea: Al-istibswaar cha Attuusy (3/243).
- 31 -
NI IPI ITIKADI YA RAFIDHWA KUHUSU NAJAF NA KARBALAA,
NA JE KUNA FADHILA GANI KATIKA KUZURU SEHEMU
HIZI?
Mashia wanaitakidi sehemu yalipo makaburi ya watu walio dai
kuwa ni maimamu wao, au ambao ni maimamu kweli, kwa sehemu hizo
ni sehemu takatifu,hivyo Alkuufa ni haram(sehemu takatifu),pia Karbalaa
ni haram,na Qumm nayo ni haram. Na wanayo riwaya wanayo dai
kuwa imepokelewa kwa Asswaadiq kwamba, Mwenyezi mungu anayo
haram yake ambayo ni makka,na Mtume wake anayo haram yake ambayo
ni Madina,na amiiril-mu`uminiina anayo haram yake ambayo ni
Alkuufa,na sisi tunayo haram yetu ambayo ni qumm.
Na Kar-balaa kwa Mashia ni bora kulikko Alqaaba. Imekuja katika
kitabu(Bihaarul-anwar)kutoka kwa Abii Abdillah kwamba kasema;
"Hakika Mwenyezi mungu aliiteremshia Alqaaba wahyi(ufunuo)lau kama
si udongo wa Kar-balaa nisingelikufanya bora ,na lau kama si mwili wa
yule aliyeko katika udongo wa Kar-balaa nisingekuumba,wala nisinge
umba nyuba ambayo kwayo umejifakharisha,basi tulia na uwe ni Mkia
dhalili na si mwenye kibri kwa ardhi ya kar-balaa,la sivyo nitakutupa
katika Jahannam" (1)
Bali rafidhwa wanaona kuzuru kaburi la Husein huko karbalaa ni
bora kuliko nguzo ya tano ya uislamu(Hijja)!!. Amesema Almajlisy
katika kitabu chake (Bihaarul-anwar)Kutoka kwa bashiir addahaan
amesema;"Nilimuuliza Abuu Abdillah(a.s) Endapo itanipita hijja alafu
nikaenda katika kaburi ya Husein? Akasema:Vizuri sana ewe
Bashir,muumini yeyote atakae liendea kaburi la Husein hali ya kutambua
haki yake,katika siku ambayo sio siku ya idd,basi huandikiwa thawabu za
Hijja 20 na Umra20 zenye kukubaliwa,na thawabu za kushiriki katika
vita 20 vya Jihadi pamoja na Mtume au Imamu muadilifu, na atakaye
liendea siku ya Arafa hali ya kujua haki zake basi huandikiwa thawabu za
Hijja 1000 na Umra 1000 zenye kukubaliwa,na thawabu za kupigana
Jihadi 1000 pamoja na Mtume au Imamu muadilifu.
(1)Rejea kitabu Albihaar(10/107)
- 32 -
Pia katika kitabu hicho hicho wametaja kwamba wanao zuru kaburi
la hussein huko karbalaa ni watu safi,na wanaokuwa wamesimama Arafa
ni watoto wa Zinaa!!"imepokewa toka kwa Ally bin Asbaatwi kwamba
kapokea toka kwa Abi Abdillah(a.s) kuwa kasema:Hakika Mwenyezi
mungu Mtukufu anaanza kuwatazama wanao zuru kaburi la hussein usiku
wa kuamkia Arafa.Akasema:Nikamuuliza,Kabla hajawatazama walioko
katika kisimamo cha Arafa?akasema;Ndio,nikamuuliza,kwanini iwe
hivyo? akasema: Kwa sababu katika watu walioko Arafa mna watoto wa
zinaa tofauti na wale walioko Karbalaa hakuna mtoto wa zinaa kati yao".
(1)
Bali kiongozi wao mkuu Ally Assistaany katika kitabu
chake(Minhaajus-swaalihina)Amefadhilisha kuswali katika makaburi
kuliko kuswali katika Miskiti!! Kasema katika mas-ala nambari
562:Inapendeza kuswali katika makaburi ya maimamu (a.s)bali
imesemekana kuwa ni bora kuliko kuswali miskitini, na imepokewa
kwamba kuswali katika kaburi la imamau ally bin Abi twaalib(a.s)ina
ubora wa swala laki mbili. (2)
Bali Shekh wao Abbas Alkaashaany katika
kitabuchake(Maswaabiihul-jinaani)kapituka mipaka katika kuitukuza
Karbalaa mpaka akasema:" Hapana shaka kwamba Karbalaa ndio sehemu
takatifu zaidi katika uislamu,na imepewa utukufu ambao haikupewa
sehemu yoyote ardhini,na hii ni kwa mujibu wa dalili nyingi zilizo
pokewa kuhusu jambo hili,hivyo ikafanywa ndio ardhi ya Allah(s.w)iliyo
tukuzwa na kubarikiwa,na ni ardhi iliyo nyenyekea, na ni ardhi iliyo
teuliwa na ndio haram ya Alla yenye baraka na amani,na ndio haram ya
Mtume,na ndio kitovu cha uislamu,na ni katika sehemu ambazo Allah
anapenda kuomba na kuabudiwa katika sehemu hizo,na ndio ardhi
ambayo udongo wake ni tiba, hakika sifa hizi na nyinginezo zilizopo
katika ardhi ya karbalaa,hazipatikani katika sehemu yoyote ardhini,hata
katika alkaaba". (3)
(1) Rejea;Bihaarul-anwar cha Almajsliy 85/98
(2) Rejea:Minhaajus-swalihiin cha Assisaany 1/187
(3)Rejea; Maswaabiihul-jinaan cha Abbaasi Alkaashaany uk 360.
- 33 -
Pia imekuja katika kitabu(Almazaar) cha Muhammad
Annuumaan,wenyewe wanamuita (Ashaikhulmufiid) akielezea ubora wa
Masjid alkuufa:Imepokewa toka kwa Abii Jaafar Albaaqir amesema:"Lau
watu wangejua fadhila zinazo patikana katika masjidulkuufa basi
wangeliuandalia matumizi na vipandwa kutoka sehemu mbalimbli ili
kuuendea,hakika swala ya faradhi katika msikiti huo ni sawa na Hijja ,na
swala ya sunna ni sawa na umra."(1)
Pia imekuja katika kitabu hicho hicho katika mlango aliyo uita
(Yasemwayo wakati wa kusimama katika kaburi) kwamba mwenye
kumzuru Hussein anatakiwa kuashiria kwa mkono wake wa kuume, na
aseme katika dua ndefu kabisa,miongoni mwake maneno
yafuatayo:"Nimekujia kukuzuru,nikitaraji uthibitishwe unyayo wangu,na
nina yaqini kwamba Mwenyezi mungu Mtukufu anawaondolea waja
wake matatizo yao kupitia kwenu, na kwa sababu yenu anateremsha
rehma,na kupitia nyinyi anaizuia ardhi isiwadidimize watu wake,na
kupitia nyinyi kayathibitisha mjabali yake.Ninamuelekea Mola wangu
kupitia kwenu ili mnikidhie haja zangu,na mnisamehe madhambi yangu."
(2)
Hebu tazama ndugu msomaji jinsi watu hawa walivyo tumbukia
katika ushirikina ,kwa kumuomba asiye kuwa Allah awakidhie haja
zao,na kuomba kusamehewa madhambi yao kwa asiye kuwa Allah, vipi
wamefikia katika hali hii,na ilihali Mwenyezi Mungu anasema"Hakuna
anaye samehe madhambi ila Allah".Al-imraan: 135. Tunamuomba Allah
atukinge na ushirikina.
(1)Rejea:Kitaabul-mazaar cha sheikh Almufiid uk. 20.
(2)Rejea:kitaabul-mazaar cha sheikh Almufiid uk. 99.
- 34 -
NI MAMBO GANI AMBAYO RAAFIDHWA WAMETOFAUTIANA NA
AHLU SUNNAH?
Amesema Nidhwaamud-diin muhammad al-a`adhwamy katika
utangulizi wa kitabu chake (Ash-shiiatu wal-mut`a) :"Hakika tofauti
zilizopo kati yetu na Ahlusunnah sio tofauti za kifiqhi peke yake, kama
vile mas`ala ya Mut`a n.k hapana,bali asili ya tofauti zetu ni katika
mambo ambayo ndiyo misingi ya dini(Mambo ya kiitikadi) kama haya
yafuatayo:
(1)Rafidhwa wanadai kwamba Qur-ani imebadilishwa,hivyo ina
mapungufu. Nasisi tunasema:hakika Qur-ani ni maneno ya Allah
yaliyo timia wala hayana mapungufu
yoyote,hayakubadilishwa,wala hayatabadilishwa aidha kwa
kupunguzwa au kuongezwa mpaka siku ya Qiyama. Kama alivyo
sema Allah "Hakika sisi tumeuteremsha ukumbusho(Qur-ani),na
hakika sisi tutauhifadhi". Alhijri 9
(2)Rafidhwa wanadai kuwa maswahaba wa Mtume(s.a.w) waliritadi
baada ya kufa Mtume(s.a.w)ispokuwa wachache tu,na wakafanya
khiyana katika dini hasa hasa Makhalifa watatu;Abubakari,Omar
na Othman. Na kwa hiyo Makhalifa hawa watatu ni Makafiri na ni
wapotevu kwa mujibu wa imani ya kishia. Nasisi tunasema;Hakika
maswahaba wa Mtume(s.a.w) ndio viumbe bora baada ya
Mitume,na kwamba wote ni waadilifu,hawawezi kumsingizia
Mtume(s.a.w),na ni wakweli katika yale waliyo yanukuu kutoka
kwa Mtume(s.a.w).
(3)Rafidhwa wanadai kuwa:Hakika maimamu wao kumi na mbili ni
maasuumiin(wamehifadhiwa na madhambi),na kwamba wanajua
ghaibu na wanayo elimu yote waliyo pewa Malaika ,Manabii na
Mitume,na kwamba wanajua mambo yote yaliyo pita na
yajayo,halifichikani kwao jambo lolote,na kwamba wao wanazijua
lugha zote za ulimwenguni na kwamba dunia yote ni ya kwao. Na
sisi tunasema kwamba: Wao ni viumbe kama viumbe
wengine,wamo miongoni mwao wanachuoni,na Makhalifa.Wala
haifai kuwanasibisha na jambo ambalo wao hawakujinasibisha nalo
bali wao walikataza mambo hayo na kujitenga mbali nayo kabisa.