Nakala

FADHILA ZA SIKU KUMI


(ZA MWANZO) ZA DHUL-HIJA


 Kiswahili





 Kamati ya Kielimu ya Jumuia ya Kuhudumia Maudhui


 za Kiislamu kwa Lugha Mbalimbali.





FADHILA ZA SIKU KUMI (ZA MWANZO)


ZA DHUL-HIJA


 


FADHILA ZA SIKU KUMI (ZA MWANZO)


ZA DHUL-HIJA


Utangulizi


Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu


Mola Mlezi wa walimwengu, na rehema na amani


zimfikie yule aliyetumwa kuwa rehema kwa


walimwengu, na kwa watu wake, na Maswahaba


zake, na wale waliofuata mwenendo wake, na


wakaongoka kwa muongozo wake, mpaka siku ya


Malipo. Ama baada ya hayo:


Huu ni ujumbe mfupi, uliokusanya mambo


muhimu anayoyahitaji Muislamu katika fadhila za


siku


kumi za mwanzo wa Dhul-Hija.


Tumezikusanya kwa ajili ya mwenye kutembelea


Misikiti Miwili Mitukufu, mwanamume na


mwanamke; ili wawe na elimu na utambuzi na


mambo ya dini yao, tukitaraji kutoka kwa


Mkarimu, Mwingi wa kuneemesha awanufaishe


kwa ujumbe huu, na aufanye kuwa wenye kufaa, na


uwe kwa ajili ya kutaka uso wake tu. Kwani, Yeye


ndiye mbora wa wenye kuombwa na Mkarimu


zaidi anayetarajiwa.


Kamati ya Kielimu ya Jumuia ya Kuhudumia Maudhui


za Kiislamu kwa Lugha Mbalimbali.


1


Fadhila za siku kumi (za mwanzo) za


Dhul-Hija:


Siku kumi  (za mwanzo) za Dhul-Hija, ubora


wake ni mkubwa mno. Ameubainisha Mwenyezi


Mungu Mtukufu katika kitabu chake, na


akaubainisha Mtume wake Muhammadi, rehema


na amani ziwe juu yake, katika mafundisho yake.


Nazo ndizo zile siku ambazo ameapa kwazo


Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya Kitabu


chake katika kauli yake:





 "Ninaapa kwa (wakati wa) Alfajiri. Na kwa


usiku kumi (wa mwanzo wa Dhul-Hija)." [Surat


Al-Fajri: 1-2]  .


Nazo ni siku kumi (za mwanzo) za Dhul-Hija,


kama alivyosema (Abdullahi) bin Abbas,


(Abdullahi) bin Zubairi, Mujahid, (imamu) bin


Kathiri, (imamu) bin Al-Qayyim na zaidi ya


mmoja katika wema waliotangulia na wale


waliofuata baada yao.(1)


Nazo ni siku ambazo kufanya matendo ndani


yake huwa bora zaidi kuliko hata kupigana vita


katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa


hadithi ya (Abdullahi) bin Abbas, radhi za


Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, kwamba


(1) Tazama Tafsiri bin Kathiri 4/106, na Zaadul-Ma'aadi 1/56.


2


alisema: Alisema Mtume, rehema na amani ziwe


juu yake: "Hakuna siku ambazo kufanya matendo


mema ndani yake hupendeza zaidi kwa Mwenyezi


Mungu kuliko hizi siku kumi." Wakasema: "Ewe


Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hata kupigana


Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu?" Akasema


Mtume, rehema na amani ziwe juu yake: "Hata


kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu,


isipokuwa mtu aliyetoka kwa nafsi yake na mali


yake, na akawa hakurudi na chochote katika


hivyo."(1)


Matendo bora zaidi katika siku kumi (za


mwanzo) za Dhul-Hija:


1- Kutekeleza Hija na Umra. Haya ni katika


matendo bora zaidi ndani ya siku kumi hizi; kwa


kauli ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake:


"Atakayehiji na akawa hakusema maneno


machafu wala kutenda matendo machafu, atarudi


kama siku aliyozaliwa na mama yake (akiwa hana


dhambi)."  


Na katika tamko la Muslim: "Atakayeiendea


nyumba hii, na akawa hakusema maneno


machafu wala kutenda matendo machafu, atarudi


(1) Kaipokea Bukhari, na Tirmidhi na tamko hili ni lake.


3


kama siku aliyozaliwa na mama yake (akiwa hana


dhambi)."(1) Kauli yake: "Atakayeiendea nyumba


hii", inajumuisha kwa muktadha wake Hija na


Umra, na kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.  


Na amesema Mtume, rehema na amani ziwe juu


yake. "Kufanya Umra mpaka Umra nyingine


kunafanya


mtu kusamehewa madhambi


yanayofanyika baina ya Umra hizo mbili. Na Hija


iliyokubalika haina malipo isipokuwa Pepo."(2)


2- Kufunga siku tisa (za mwanzo za Dhul


Hija) au zitakazowezekana katika hizo. Hili ni


kwa kauli ya Mtume, rehema na amani ziwe juu


yake: "Hakuna siku ambazo kufanya matendo


mema ndani yake hupendeza zaidi kwa Mwenyezi


Mungu kuliko hizi siku kumi." Na swaumu ni


miongoni mwa matendo mema matukufu zaidi


ambayo alihimiza juu yake Mtume, rehema na


amani ziwe juu yake, na akahamasisha juu yake.


Miongoni mwake ni kauli yake, rehema na amani


ziwe juu yake: "Hakuna mja yeyote atakayefunga


siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu,


isipokuwa Mwenyezi Mungu atauweka mbali kwa


(1) Kaipokea Bukhari na Muslim.


(2) Kaipokea Bukhari na Muslim.


4


siku hiyo moja uso wake na moto misimu


sabini."(1)


3- Ni sheria kuchinja udhuhiya siku ya


kuchinja na siku za Tashriiq (kubanika


nyama). Imethibiti kuwa Mtume, rehema na


amani ziwe juu yake: "Alichinja siku ya Idi kondoo


wawili weupe wenye pembe. Aliwachinja kwa


mkono wake, akataja jina la Mwenyezi Mungu juu


yake, akatoa takbira na akaweka mguu wake juu


ya shingo zao."(2)


Na imesimuliwa kutoka kwa Aisha, radhi za


Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwamba


alisema: Alisema Mtume wa Mwenyezi Mungu,


rehema na amani ziwe juu yake: "Hajawahi


kufanya mwanadamu tendo lolote siku ya


kuchinja (siku ya Idi) linalopendeza zaidi kwa


Mwenyezi Mungu kuliko kumwaga damu. Na


hakika kitaletwa kichinjwa hicho siku ya Kiyama


kikiwa na pembe zake, nywele zake na kwato


zake. Na hakika damu hiyo hufika kwa Mwenyezi


Mungu katika mahali (pa kukubalika) pake kabla


(1) Ameipokea Bukhari na Muslim.


(2) Ameipokea Bukhari na Muslim.


5


haijadondoka katika Ardhi. Basi zisafisheni


kwavyo (vichinjwa) nafsi zenu."(1)


Na zinapoingia siku kumi (za mwanzo) za Dhul


Hija; atajizuia aliyekusudia kuchinja kunyoa


nywele zake na ngozi yake; kwa mujibu wa


hadithi ya Ummu Salama, radhi za Mwenyezi


Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume,


rehema na amani ziwe juu yake, ya kwamba


alisema: "Mtakapouona mwezi mwandamo wa


Dhul-Hija, na akataka mmoja wenu kuchinja;


basi ajizuie kunyoa nywele zake na kupunguza


kucha zake." Na katika tamko jingine: "...basi


kamwe asichukue chochote katika nywele zake


wala katika kucha zake mpaka atakapochinja


dhabihu wa Idi."(2)


4- Takbira (kusema: Allaahu Akbaru), na


tahlil (Laa ilaaha illa llaahu), na kumtaja


Mwenyezi Mungu ndani ya siku hizi kumi na siku


za Tashriiq (kubanika nyama); kwa hadithi ya


Abdallah bin Omari, radhi za Mwenyezi Mungu


ziwe juu yao, kutoka kwa Mtume, rehema na


amani ziwe juu yake, kwamba alisema: "Hakuna


siku tukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu


wala zinazopendeza zaidi kufanya matendo


(1) Kaipokea Tirmidhi.


(2) Kaipokea Muslim.


6


ndani yake, kuliko siku hizi kumi (za mwanzo za


Dhul-Hija). Basi zidisheni sana ndani yake:


Tahlili - yaani kusema: Laa ilaaha illa llaah


(hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu),


na Takbiri - yaani kusema: Allaahu Akbaru


(Mwenyezi Mungu ni Mkubwa), na Tahmidi -


yaani kusema: Alhamdulillaah (sifa njema ni za


Mwenyezi Mungu)."(1)


Na takbira zina aina mbili, kama ifuatavyo:


Aina ya kwanza: Takbira zisizo na mipaka. Nazo


ni zile ambazo hazihusiani na baada ya swala;


bali zinaruhusika nyakati zote.


Zinaanza takbira zisizo na mipaka katika Idil


Adhha kuanzia siku ya kwanza ya siku kumi (za


mwanzo) za Dhul-Hija mpaka siku ya mwisho


katika siku za Tashriiq (kubanika nyama), katika


nyakati zote: usiku, mchana, barabarani, sokoni,


msikitini, nyumbani na maeneo yote yanayofaa


ndani yake kutajwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.


Aina ya pili: Takbira zenye mipaka: Nazo ni zile


zinazofungamanishwa na swala katika idil


(1) Kaipokea Ahmad.


7


Adhha hasa. Na wakati wake na namna yake ni


kama ifuatavyo:


Kwanza: Zitaanza takbira zenye mipaka baada


ya swala ya Alfajiri siku ya Arafa, na zitamalizika


baada ya swala ya Laasiri siku ya tatu katika siku


za Tashriiq (kubanika nyama). Hili ni kwa


asiyekuwa hujaji. Na ama hujaji, yeye zitaanza


takbira zenye mipaka kuanzia Adhuhuri ya siku


ya kuchinja.


Pili: Namna ya kufanya takbira: Allaahu


Akbaru, Allaahu Akbaru. Laa ilaaha illa


llaahu, wallaahu Akbaru, Allaahu Akbaru


walillaahil Hamd. Yaani: Mwenyezi Mungu ni


Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa. Hakuna


mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa


Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni


Mkubwa. Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, na kila


sifa njema ni zake Yeye Mwenyezi Mungu.(1)


5- Pupa ya kutekeleza swala ya Idi kwa


asiyekuwa hujaji, kutoa takbira wakati wa


kuiendea na kusikiliza hotuba. Kwani, hilo ni


miongoni mwa alama kubwa za Uislamu.


Na kwa sababu ya ukubwa wa jambo lake,


wameamrishwa kuiendea wanawake mpaka


mabikira na wenye hedhi. Imesimuliwa kutoka


(1) Tazama: Al-Mughni, cha bin Qudama 3/290, na Ashsharhul


Kabiir pamoja na Al-Muqni wal-Inswaaf 5/380.


8


kwa Ummu Atwiya, radhi za Mwenyezi Mungu


ziwe juu yake, kwamba alisema: "Tulikuwa


tukiamrishwa kutoka siku ya Idi mpaka tukawa


tunawatoa


mabikira


majumbani


mwao


wanamojihifadhi, vile vile mpaka tukawa


tunawatoa wenye hedhi, kisha wanakaa (uwanjani)


nyuma ya wanawake. Wakawa wanatoa takbira


kwa takbira zao, na wanaomba kwa dua zao, na


wanataraji baraka za siku hiyo na utakasifu wake."


Na katika tamko jingine: "Na aliwaamrisha


wenye hedhi wajitenge mbali na mahali


wanaposwalia Waislamu."(1)


6- Kukithirisha matendo mema, miongoni


mwa ibada za sunna: Kama vile swala, sadaka,


kusoma Qur'ani Tukufu, kuamrisha mema na


kukataza mabaya, kumtendea wema jirani,


kuunga udugu na mengineyo miongoni mwa


matendo mema, kwa ujumla wa kauli yake


rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna siku


ambazo kufanya matendo mema ndani yake


hupendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko hizi


siku kumi." Wakasema: "Ewe Mjumbe wa


Mwenyezi Mungu! Hata kupigana Jihadi katika njia


ya Mwenyezi Mungu?" Akasema Mtume wa


Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake:


"Hata kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi


(1) Ameipokea Bukhari na Muslim.


9


Mungu, isipokuwa mtu aliyetoka kwa nafsi yake na


mali yake, na akawa hakurudi na chochote katika


hivyo."(1)


Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye mwenye


kuombwa atunufaishe kwa yale tuliyojifunza, na


atufunze yale yenye kutunufaisha. Hakika Yeye


ndiye Mpaji, Mkarimu. Na rehema na amani


nyingi zimuendee Nabii wetu Muhammadi na


watu wake.


 (1) Kaipokea Bukhari na Tirmidhi, na tamko hili ni lake.


10





Yaliyomo


 


Utangulizi ................................................................................... 1


Fadhila za siku kumi (za mwanzo) za Dhul-Hija: .... 2


Matendo bora zaidi katika siku kumi (za mwanzo)


za Dhul-Hija: ............................................................................. 3



 



Machapisho ya hivi karibuni

FADHILA ZA SIKU KUMI ...

FADHILA ZA SIKU KUMI (ZA MWANZO) ZA DHUL-HIJA

Mafungamani ya Shahad ...

Mafungamani ya Shahada na Aina za Tawhiid.

Namna ya swala ya mtu ...

Namna ya swala ya mtume (s.a.w). na Namna ya kutawadha