
MASWALI 60 KWA WAKRISTO
UTATU
Kwa mujibu wa Wakristo wengi, Yesu amekuwa ni Mungu-mtu, mtu kamili
na Mungu kamili. Je, kitu chenye mwisho na kile kisicho na mwisho
vinaweza kuwa ni kimoja? Kuwa “Mungu kamili” maana yake ni kutokuwa
na mwisho na kutohitajia msaada, na kuwa “mtu kamili” maana yake ni
kutokuwa na uungu.
1. Kuwa mtoto ni kuwa chini ya daraja ya uungu na kuwa na uungu ni
kutokuwa mtoto wa yoyote. Vipi Yesu atakuwa na sifa ya utoto na
uungu kwa wakati mmoja?
2. Wakristo wanadai kwamba Yesu alidai kuwa yeye ni Mungu wakati
walipomnukuu katika Yohana 14:9: “…Aliyeniona mimi amemwona
Baba…” Je, Yesu hakusema wazi wazi kwamba: kamwe watu
hawakumuuona Mungu, kama inavyosema Yohana 5:37: “Naye Baba
aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote,
wala sura yake hamkuiona”?
3. Wakristo wanasema kwamba Yesu alikuwa ni Mungu kwa sababu
alikuwa anaitwa mtoto wa Mungu, Mtoto wa mwanadamu, Masiha, na
“mwokozi.” Ezekiel aliandikwa katika Biblia kama ni mtoto wa
Mungu. Yesu alinena kuhusu “waletao amani” kuwa ni Watoto wa
Mungu. Mtu yoyote aliyefuata matakwa na Mipango ya Mungu
alikuwa akiitwa MTOTO WA MUNGU katika utamaduni wa
Kiyahudi na katika lugha yao (Mwanzo 6:2,4; Kutoka 4:22; Zaburi
2:7, Warumi 8:14) neno “Messiah” ambalo kwa Kiebrania
linamaanisha “Mpakwa Mafuta wa Mungu” sio “Kristo”, wala
“Cyrus” na mtu huitwa “Messiah” au “mpakwa mafuta”. Ama kuhusu
neno “mwokozi” liliopo katika Wafalme wa pili 13:5, watu wengine
walipewa jina hilo vile vile bila ya kuwa miuungu. Kwa hivyo, katika
maneno hayo uko wapi uthibitisho unaoonesha kuwa Yesu ni Mungu
wakati neno mtoto halikutumiwa kwake peke yake?
4. Wakristo wanadai kwamba Yesu alikiri kwamba yeye na Mungu
walikuwa ni kitu kimoja kwa maana ya Kimaumbile pale anaposema
katika Yohana 10:30; “Mimi na Baba tu umoja.”, Baadae katika
Yohana 17:21-23, Yesu alinena kwamba wafuasi wake, yeye
mwenyewe na Mungu ni kitu kimoja katika sehemu tano. Sasa kwa
nini walipe neno “Kitu kimoja” la kwanza maana nyingine tofauti na
yale maneno “kitu kimoja” katika sehemu tano nyinginezo?
5. Je, Mungu ni watatu-katika-mmoja na ni mmoja katika watatu kwa
wakati mmoja au ni mmoja kwa wakati huo huo?
6. Ikiwa Mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja, kwa hiyo
hakuna hata mmoja kati ya hao watatu ambae ni Mungu kamili.
Tukikubali kwamba huo ndio ukweli, sasa je, wakati Yesu alipokuwa
duniani, hakuwa Mungu kamili, wala “Baba aliyembinguni” hakuwa
Mungu kamili. Je, hilo halileti mkanganyiko kwa kile alichokuwa
akikisema Yesu kila siku kuhusu Mungu wake na Mungu wetu
aliyembinguni, Bwana wake na Bwana wetu? Je, hilo vile vile
halimaanishi kwamba hakukuwa na Mungu kamili, katika kipindi cha
kati ya dai la kusulubiwa na dai la kufufuka?
7. Ikiwa Mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja, sasa nani
aliyekuwa Mungu huko mbinguni wakati Yesu alipokuwa aridhini?
Je, hili halileti mkanganyiko na yale aliyokuwa akiyasema mara
nyingi juu ya kuwa Mungu aliyembinguni ndiye aliyemtuma?
8. Ikiwa Mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja, je, nani
aliyekuwa Mungu huko mbinguni katika zile siku tatu zilizo kati ya
dai la kusulubiwa na dai la kufufuka?
9. Wakristo husema kwamba: “Baba (B) ni Mungu, Mwana (M) ni
Mungu na Roho Mtakatifu (R) ni Mungu, lakini Baba si mwana, na
Mwana si Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu si Baba”. Kwa hesabu
rahisi na kwa kanuni inakuwa hivi, ikiwa B = G, M = G na R = G;
kwa kufuatanisha inakuwa B = M = R, wakati sehemu ya pili ya
maelezo hayo inaonesha kuwa B№ M№ R (inamaanisha haziko
sawa). “Sasa je, huo si mkanganyiko na imani ya Wakristo juu ya
utatu wenyewe?
10. Ikiwa Yesu alikuwa Mungu, kwa nini alimwambia yule mtu
aliemwita Yesu “Bwana Mwema” alimwambia asimwite “mwema”
kwa sababu hakuna mwema ila Mungu wake aliyembinguni peke
yake?
11. Kwanini Wakristo wanasema kwamba Mungu ni watatu katika mmoja
na mmoja katika watatu, wakati Yesu alisema katika Marko 12:29.
“Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja” kama ilivyo katika sehemu
nyingi ndani ya Biblia.
12. Ikiwa kuamini utatu lilikuwa ni jambo la lazima ili uwe Mkristo, kwa
nini Yesu hakulifundisha na wala hakulisisitiza jambo hilo kwa
Wakristo katika zama zake? Je, vipi hao wafuasi wa Yesu
wachukuliwe kuwa ni Wakristo bila ya kulisikia neno utatu? Kama
ingekuwa utatu ndio uti wa mgongo wa Ukristo, Yesu angeliufundisha
na angeliusisitizia na angeliufafanua kwa watu wake kikamilifu.
13. Wakristo wanadai kwamba Yesu alikuwa Mungu kama
walivyomnukuu katika Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno,
naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu”. Hayo
ni maneno ya Yohana na si maneno ya Yesu, vile vile, neno la kwanza
la Kigiriki kwa ajili ya Mungu ni “HOTHEOS” ambalo linamaanisha
“Mungu” likiwa na M kubwa, wakati neno la pili la Kigiriki kwa ajili
ya Mungu ni “TONTHEOS” ambalo linamaanisha “mungu” likiwa na
“m” ndogo. Je, huko si kukosa uaminifu kwa wale waliotafsiri Biblia
ya Kigiriki? Je, nukuu hiyo ya Yohana 1:1 iliyotambuliwa na kila
mwanazuoni wa Kikristo aliyeisoma Biblia kwamba imeandikwa na
Myahudi aitwae Philo Alexandria kabla ya Yesu na Yohana?
14. Je, neno “god” au “TONTHEOS” pia halikutumika kuashiria wengine
kama ilivyo katika Wakorinto 2 4:4 (Na Shetani ndie) mungu wa
ulimwengu huu na katika Kutoka 7:1 “Angalia, nimekufanya wewe
kuwa kama Mungu kwa Farao; ?
WOKOVU:
Wakristo wanasema kwamba “MUNGU AEMTOA” mwanawe wa pekee
ili kutuokoa sisi”. Je, Mungu alimtoa Yesu kumpa nani wakati yeye Mungu
ndiye mmiliki wa ulimwengu wote?
15. Ikiwa ilikubalika kwa utukufu wa Mungu kuwa awe na watoto, basi
angeumba mamilioni ya watoto kama Yesu. Sasa kuna jambo gani
kubwa kumhusu huyu mtoto wa pekee?
16. Kwa nini Biblia inasema kwamba Yesu alitaka kufa msalabani, huku
yule mtu aliyesulubiwa pale msalabani alikuwa anapiga kelele
“Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” kwa mujibu wa
Matayo 27:45 na Marko 15:33?
17. Ikiwa Mungu alitaka kutuokoa, Je, angeshindwa kutuokoa bila
kumtoa muhanga Yesu?
18. Mungu yeye mwenyewe ni haki, na haki inataka kusiwepo na mtu
anayepaswa kuadhibiwa kwa madhambi ya wengine, vile vile
haipaswi kuadhibiwa watu wengine kwa kuwaokoa wengine: Je! Dai
la kwamba Mungu amemtoa muhanga Yesu ili kutuokoa haliteti
mkanganyiko kama kweli Mungu ni mpenda haki? Je, Dai hilo
halitofautiani na maana halisi ya haki?
19. Watu wanatoa muhanga vitu vyao ili kupata vitu vingine
wasivyokuwa navyo ikiwa haiwezekani kuwa navyo vyote viwili kwa
wakati mmoja. Wakristo wanasema kwamba “Mungu alimtoa
muhanga mtoto wake wa pekee ili kutuokoa; Tunajua kwamba Mungu
ni Mwenye nguvu; Mungu alimtoa Muhanga Yesu kwa nani?
20. Kutoa muhanga kitu maana yake ni kwamba huwezi kukipata tena
kile ulichokitoa; sasa kuna siri gani katika kutolewa Muhanga Yesu
wakati Mungu aliweza kumrudisha Yesu baada ya kusulubiwa (kwa
mujibu wa maneno ya Wakristo)?
21. Ikiwa
Wakristo wote wameokoka kwa kupitia Yesu na
wanakwenda Peponi (kwenye uzima wa milele) bila kujali matendo
yao, kwa hiyo mafundisho ya Yesu hayana umuhimu wowote na
maana ya maneno “uovu” au “wema” hayana umuhimu wowote.
Ikiwa hali sivyo hivyo, kwa hiyo wale Wakristo ambao wanamwamini
Yesu lakini hawafuati mafundisho yake wala hawajatubu watakwenda
motoni?
22. Vipi Wakristo wanayachukulia matendo kama kitu kisicho na
umuhimu baada ya kuwa kitu kimoja wakati Yesu aliposema katika
Matayo 12:36; “Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana,
watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya
hukumu.”?
23. Wakristo wanasema kwamba watu wanakwenda Peponi kwa kupitia
Yesu tu! Wakati Paulo anasema katika 1 Wakorintho 7:8-16 kwamba
Mume asieamini anakubalika kwa Mungu kwa sababu anaunganishwa
na mke wake na kinyume chake, na watoto wao wasio na dini vile vile
wanakubalika kwa Mungu. Kwa hivyo kumbe watu wanaweza
kwenda Peponi bila ya kumwamini Yesu; kutokana na maneno hayo.
24. Vipi Biblia inasema kwamba Waisraeli wote wameokoka ingawa
hawamwamini Yesu? Je, Hili halipingani na dai la Biblia ya kuwa njia
ya pekee ya kwenda Peponi ni kwa kupitia Yesu tu?
25. Kwa mujibu wa Wakristo, wale wote ambao hawakubatizwa
watakwenda motoni. Kwa hivyo hata watoto wachanga nao
watakwenda motoni kwa vile walikufa kabla ya kubatizwa; kwa vile
walizaliwa na dhambi la asili la kurithi? Je, hili halipingani na maana
ya neno haki; kwanini Mungu awaadhibu watu kwa madhambi
wasiyoyatenda?
ROHO MTAKATIFU
Sehemu pekee katika Biblia alipotajwa Roho Mtakatifu ni katika Yohana
14:26; “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba
atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote niliyowaambia. “Ni kipi kile
ambacho Roho Mtakatifu ameleta au kufundisha kwa miaka 2000 iliyopita?
26. Wakristo wanasema kwamba Msaidizi maana yake ni Roho Mtakatifu
(Yohana 14:26) Yesu alisema katika Yohana 16:7-8. “Lakini mimi
nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana
mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu;” Hii haiwezi
kumaanisha Roho Mtakatifu; kwa vile Roho Mtakatifu inasemekana
kwamba alikuwepo hata kabla ya Yesu hajazaliwa kama ilivyo katika
Luka 1:41 “Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu”. Hapa, Roho
Mtakatifu vile vile alikuwepo wakati wa Yesu: sasa vipi hii imaanishe
kwamba ni sharti aondoke Yesu ndipo Roho Mtakatifu aweze kuja?
27. Katika Yohana 16:7-8, inasema; “Bali mimi nikienda zangu,
nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha
ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.” Je, hii
“Yeye” hapa inamaanisha nini? Je, viwakilishi hivyo havimaanishi
mtu mwanamume?
28. Je, Roho Mtakatifu anazungumza na Wakristo wema na waovu vile
vile? Je, Roho Mtakatifu yu pamoja nao wakati wote au wakati fulani
tu? Je, ni wakati gani anaanza kumtembelea mtu atakaye kuwa
Mkristo?
29. Utasemaje kuwa wewe ni Mkristo ikiwa Roho Mtakatifu yu ndani ya
Mkristo mwingine? Inakuwaje Wakristo wengi wanawapumbaza watu
kwa kudai kwamba Roho Mtakatifu yu ndani yao tu! Na baadaye
wanabadilisha dini?
30. Je, Roho Mtakatifu anaamuru kile ambacho Wakristo wanapaswa
kukifanya bila ya uhuru wa kuchagua hata kidogo au anawaongoza tu
na wao wana uhuru wa kufuata au kuto fuata?
31. Ikiwa Roho Mtakatifu anaamuru kile Wakristo wanachopaswa
kukifanya, kwa nini Wakristo wanafanya maovu na madhambi? Vipi
unaweza kuuelezea ubadilishaji wa dini na kuingia dini na imani
mbali mbali kunakofanywa na Wakristo wengi? Je, Wanaambiwa
kufanya hayo na Roho Mtakatifu?
32. Ikiwa Roho Mtakatifu anawaongoza Wakristo tu, na wako huru
kufanya wanavyotaka, sasa ni vipi tutajua kwamba waandishi wa
Biblia hawakufanya makosa wakati walipoziandika?
33. Ikiwa Wakristo wanaamini kwamba Roho Mtakatifu huwajia na
kuzungumza nao kila siku, kwanini hawamuulizi Roho Mtakatifu
kuhusu chapisho lipi la Biblia wanalopaswa kulifuata kwa vile kuna
machapisho mengi?
KAZI YA UJUMBE WA YESU
Hivi bila ya kuazima kutoka katika dini na mifumo mingine, Ukristo
unaweza kuwapa wanadamu mfumo kamili wa maisha? Huku Ukristo ukiwa
umefungika kwa maisha ya kiroho tu na hautoi sheria, sasa vipi jamii
itaweza kuamua sheria zipi ni sahihi na zipi ni makosa?
34. Kwa nini Wakristo wanasema kwamba Yesu alikuja kwa ajili ya
ulimwengu mzima wakati yeye alisema kuwa alitumwa kwa
Mayahudi tu? Alimwambia yule mwanamke Mkananayo
aliyemuomba amtibie bintiye aliyekuwa anasumbuliwa na mapepo:
“Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.” na pia
alisema; Si vyema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”
(Matayo 15:21-28).
KUFUFUKA KWA YESU
Ikiwa utasoma Matayo (28: 1-10), Marko (16:1-20), Luka (24:1-12), na
Yohana (20:1-18) utakuta habari zenye kutatanisha: Maandika yote hayo
yanakubali kwamba kaburi lilikuwa linalindwa kwa muda wa siku tatu. Hata
hivyo, maandiko hayo yanaonesha kugunduliwa kwa kaburi kuwa ni tupu
katika hali tofauti.
1 Matayo (28) na Yohana (20) zinaeleza kwamba Maria Magdalena na
Maria wengine walikuwa ndio watu wa kwanza kuliona lile kaburi.
2 Marko (16) inaeleza kwamba Maria Magdalena, Maria mama, James
na Salome walikuwa wa kwanza kuliona kaburi likiwa tupu.
3 Marko (28) inaeleza kwamba kulikuwa na tetemeko la ardhi ambalo
lililoondosha jiwe lililokuwa juu ya kaburi. Anasema kwamba
Malaika ndie aliesababisha hivyo: Maandiko mengine hayataji
kuwepo kwa tetemeko la ardhi.
4 Matayo na Marko wanasema kwamba mwanamume mmoja tu
aliyevaa mavazi meupe ndiye alikuwa malaika.
5 Luka inasema wanamume wawili waliovalia mavazi meupe, ambao
walikuwa malaika, ndio waliokuwa wamekaa juu ya kaburi. Yohana
inasema kwamba wale wanawake wawili hawakumkuta mtu yoyote
kwa mara ya kwanza walivyokwenda kwenye kaburi, lakini
waliporudi tena, waliwaona watu wawili, mmoja alikuwa Malaika na
mwingine alikuwa Yesu.
6 Matayo inasema kwamba, wakati walinzi walipotoa taarifa hizi kwa
Kuhani mkuu, yule Kuhani mkuu aliwalipa kiasi kikubwa cha pesa, na
kuwaambia “Mnapaswa kusema kwamba wafuasi wake walikuja
nyakati za usiku na kuiba mwili wake”. Alidai kwamba askari
walichukua pesa na kusambaza habari hiyo na toka hapo, hadithi
ilikuwa ni yenye kuzunguka kati ya Wayahudi; mpaka leo (kwa
mujibu wa Matayo). Maandiko mengine hayasemi chochote kuhusu
jambo hilo.
35. Ni maelezo yapi ambayo ni ya kweli?
36. Kwa nini Yesu alipojitokeza baada ya tendo la kusulubiwa
inachukuliwa kama ndio kigezo (uthibitisho) wa kufufuka kwake
wakati kuna maelezo yasemayo kwamba si yeye aliyesulubiwa wala
aliyekufa kwani aliyesulubiwa ni mtu mwingine wakati Mungu
akimwokoa Yesu?
37. Vipi Matayo alijua dai au hoja ya makubaliano kati ya wale askari na
yule kiongozi? Hivi mtu hawezi kusema kwamba kuna mtu
aliyewalipa wale wanawake kiasi kikubwa cha pesa na akawaambia
waeneze maneno yale ya kwamba Yesu alifufuka, pamoja na uthabiti
huo huo kama ule wa habari ya Matayo.
38. Kwanini walimwamini yule mtu aliekuwa na mavazi meupe? Kwa
nini walimuamini kwamba alikuwa ni malaika? Maelezo ya Yohana
ni ya kustaajabisha sana, kwa vile yeye alisema kuwa Maria
hakumtambua Yesu (ni yupi kati ya wale watu wawili) wakati
alipokuwa akizungumza nae, hali alimtambua tu wakati yule mtu
alipomwita Maria kwa jina lake?
39. Vipi lile kaburi lililokuwa tupu lina thibitisha kwamba Yesu
alisulubiwa? Je, Mungu hawezi kumtoa mtu mwingine kutoka
kaburini na kumfufua?
40. Injili inaaminiwa kuwa ni maneno asilia ya Mungu, yanasadikiwa
kwamba yalisemwa na Roho Mtakatifu kwa wafuasi wake ambao
waliyaandika. Ikiwa chanzo chake ni kimoja, kwanini yasilingane
katika kulizungumzia tukio lile muhimu? (la kufufu Yesu).
41. Vipi Matayo, Marko, Luka na Yohana waliweza kuchukuliwa kama
mashahidi walioona Yesu akifufuka wakati Biblia inatuambia
kwamba hakuna mtu aliyemuona Yesu akitoka ndani ya kaburi?
BIBLIA
Ikiwa Wakristo wanachukulia Agano la Kale kwamba ni maneno ya Mungu,
kwa nini walibatilisha baadhi ya maandiko katika Agano la Kale ambayo
yalikuwa yakizungumzia adhabu (kwa mfano adhabu ya uzinzi)?
42. Kwanini Marko 16:9-20 haipo kwenye machapisho mengi ya Biblia
wakati katika baadhi ya machapisho imejitokeza kama tanbihi ya
chini ya ukurasa tu au imewekwa katika mabano? Je, tanbihi ya chini
ya ukurasa katika Biblia nayo inachukuliwa kuwa ni maneno ya
Mungu, hasa hasa wakati inapozungumzia jambo muhimu kama la
kupaa kwa Yesu?
43. Kwa nini Biblia ya Kikatoliki ina vitabu 73 ndani yake wakati Biblia
ya Kiprotestanti ina vitabu 66 tu ndani yake? Wakati zote mbili ya
Kikatoliki na Kiprotestanti zinadai kuwa na maneno kamili ya Mungu,
ipi inatakiwa iaminiwe na kwa nini; kwa kigezo gani?
44. Ni wapi zinakotoka hizo tafsiri mpya za Biblia wakati ile Biblia ya
asili haipo au haipatikani popote? Maandiko ya kizamani ya Kigiriki
ambayo yenyewe ni tafsiri hayafanani na yanatofautiana yenyewe kwa
yenyewe.
45. Unawezaje kuyachukua maandiko ya waandishi ambao kamwe
hawakumuona Yesu kwamba ni sahihi, kama vile Marko na Luka?
46. Kwa nini nusu ya Agano Jipya imeandikwa na mtu ambae kamwe
hakuonana na Yesu katika maisha yake? Paulo anadai alionana na
Yesu alipokuwa njiani toka Jerusalemu kuelekea Damaskasi bila
kutoa ushahidi wowote wa kuonana naye? Paulo alikuwa ndie adui
mkubwa wa Ukristo; Je, hilo halitoshi kutilia shaka juu ya usahihi wa
kile alichokiandika? Kwa nini Wakristo wanayaita maandiko ya
vitabu hivyo vya Agano la Kale kwamba ni “MANENO YA
MUNGU” wakati wale waliyoyapitia Biblia ya RSV wanasema
kwamba mwandishi wa SAMWELI hajulikani na yule alieandika (na
kuyakusanya)
maandishi
ya
kale
(KUMBU KUMBU)
“HAJULIKANI HUENDA YALIKUSANYWA NA KUHARIRIWA
NA EZRA”.!!!
UTATA
47. Kulingana na mambo yanayotatanisha katika Biblia, ni vipi Wakristo
wanaweza kuamua kwa wingi wa theluthi mbili yapi ni maneno ya
Mungu na yapi si maneno ya Mungu kama tangulizi ya baadhi ya
Biblia zinavyosema kama ilivyosema ile ya RSV?
48. Kwanini Luka katika maandiko yake anazungumzia kupaa kwa Yesu
kuwa ilikuwa ni siku ya Pasaka, na katika Matendo ya Mitume,
maandiko ambayo yanajulikana kama yeye ndiye mwandishi,
anasema alipaa siku arobaini baadae?
49. Ukoo wa Yesu umetajwa katika Matayo na Luka tu. Matayo
iliorodhesha vizazi 26 kutoka Joseph hadi Daudi wakati Luka yeye
iliorodhesha vizazi 41. ni Joseph tu anayeungana na Daudi katika
orodha zote mbili. Hakuna jina jingine hata moja lingana! Ikiwa hayo
yalitolewa na Mungu neno kwa neno, vipi yatofautiane? Baadhi
wanadai kwamba moja ni kwa ajili ya Maria na moja ni kwa ya
Joseph, lakini ni wapi alipotajwa Maria katika maandiko yote mawili?
50. Ikiwa Musa aliandika vitabu vya kwanza kabisa vya Agano la Kale,
Musa aliwezaje kuandika taarifa ya kifo chake mwenyewe? Musa
alikufa katika kitabu cha tano akiwa na miaka 120 kama ilivyotajwa
katika Kumbukumbu la Torati; 34:5-10
51. Katika chapisho la King James, kwa nini linaeleza miaka 7 (saba) ya
ukame katika Samweli 2 24:13 huku likieleza miaka 3 (mitatu) tu ya
ukame katika Mambo ya Nyakati 1- 21:12? Kwa nini yote yalibadilika
katika chapisho jipya la kimataifa na machapisho mengine?
52. Vile vile Katika chapisho la King James, kwa nini inasema kwamba
JEHOIACHINI alikuwa na miaka minane wakati alipoanza kuongoza
katika Mambo ya Nyakati 2 (21:12) huku ikisema alikuwa na miaka
kumi na nane katika Wafalme 2 24:8? Kwa nini baadae zote
zilibadilika na kuwa 18 katika chapisho jipya?
53. Katika machapisho yote, kwa nini yanasema kwamba Daudi aliwauwa
waendesha magari ya Farasi MIA SABA wa Kisyria na wapanda
farasi arobaini elfu kama ilivyooneshwa katika Samweli 2 10:18 huku
ikisema watu elfu saba ambao walipigana kupitia magari ya farasi na
wapiganaji wa miguu 40 elfu katika Mambo ya Nyakati 1 19:18?
54. Katika machapisho yote, kwa nini yanasema kuwa majosho elfu mbili
katika Wafalme 1 7:26 huku katika Mambo ya Nyakati 2 4:5 linasema
ni majosho elfu tatu?
55. Katika chapisho la King James, kwa nini linasema kwamba Solomoni
alikuwa na vikalio vya farasi elfu nne katika Mambo ya Nyakati 2
9:25, huku likisema kwamba
Solomoni alikuwa na vikalio vya
farasi arobaini elfu katika Wafalme 1 4:26? Kwa nini yalibadilika yote
mawili na kuwa arobaini elfu Katika chapisho jipya?
56. Mwanzo 1, uumbaji wa Mungu umeanzia majani kisha miti, ndege,
nyangumi, ng`ombe na vitambaavyo na mwisho mwanamume na
mwanamke. Mwanzo 2, hata hivyo, inauweka uumbwaji wa
mwanamume kabla ya ng`ombe na ndege na mwanamke. Baadaye na
wanyama. Vipi itawezekana kufafanua haya?
QURAN NA WAKRISTO
Ketengo hiki hakihitaji wala hakihoji, lakini sana sana kunampatia msomaji
baadhi ya aya za Quran ambazo zinauelekeza Ukristo kwa upekee, na watu
wa kitabu kwa ujumla. Sehemu kubwa ya Quran inahusika na au
inafungamana na Wakristo na Wayahudi na nimeamua kuchagua aya
zinazofungamana na maudhui ya makala hii.
1 “Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam;
Alimuumba kwa udongo kisha Akamwambia: “Kuwa”; basi akawa.”
(Quran 3:59)
2 “Sema: “Enyi watu mliopewa Kitabu (cha Mwenyezi Mungu.
Mayahudi na Manasara)! Njooni katika neno lilio sawa baina yetu na
baina yenu: ya kwamba tusimwabudu yoyote ila Mwenyezi Mungu,
wala tusimshirikishe (Mwenyezi Mungu) na chochote; wala baadhi
yetu tusiwafanye wengine kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu
(au pamoja na Mwenyezi Mungu). Wakikengeuka, semeni:
“Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu, (tumenyenyekea amri za
Mwenyezi Mungu).”
3 “Enyi watu mliopewa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahimu, na
hali Taurati na Injili havikuteremshwa ila baada yake? Basi je,
hamfahamu?”
4 “Ibrahimu hakuwa Myahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu,
mtii; wala hakuwa katika washirikina.”
5 “Watu wanaomkurubia zaidi Ibrahimu ni wale waliomfuata yeye
(katika zama zake) na Mtume huyu (Muhammad) na waliomwamini
(Mtume huyu). Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa wenye
kuamini.”
6 “Baadhi ya watu waliopewa Kitabu wanapenda wakupotezeni; lakini
hawapotezi ila nafsi zao; na (hali wenyewe) hawatambui.”
7 Enyi mliopewa Kitabu! Mbona mnazikataa Aya za Mwenyezi Mungu,
hali mnajua (kuwa ndiyo ndizo)?
8 Enyi mliopewa Kitabu! Mbona mnachanganya haki na batili, na
mnaficha haki, hali mnajua?” (Quran 3:64-71)
9 “Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake.
Naye Akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa).” (Quran
3:85)
10 “Na kwa (ajili ya) kusema kwao: “Sisi tumemuua Masihi Isa, mwana
wa Maryamu, Mtume wa Mungu,” hali hawakumwua wala
hawakumsulubu, bali walibabaishiwa (mtu mwengine wakamdhani
Nabii Isa). Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika) hiyo
(ya kumwua nabii Isa)wamo katika shaka nalo (jambo hilo la kusema
kauawa). Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo) hili (la kuwa
kweli wamemwua Nabii isa), ispokuwa wanafuata dhana tu. Na kwa
yakini hawakumwua. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua Kwake, na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima.” (Quran
4:157-158).
11 “Enyi watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala
msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo kweli. Masihi Isa bin
Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na (ni kiumbe aliyeumbwa
kwa) tamko Lake (tu Mwenyezi Mungu) alipompelekea Maryamu. Na
ni roho iliyotoka Kwake (Mwenyezi Mungu kama roho nyengine).
Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na Mitume Yake; wala msiseme
“watatu …” Jizuieni (na itikadi hiyo); itakuwa bora kwenu. Bila shaka
Mwenyezi Mungu ni Mungu Mmoja tu. Ni mbali na Utakatifu Wake
kuwa ana mwana. Ni vyake (vyote) vilivyomo mbinguni na vilivyomo
ardhini; na Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa kutosha. Masihi (Nabii
Isa) hataona unyonge kuwa mja wa Mwenyezi Mungu, wala Malaika
waliokurubishwa (na Mwenyezi Mungu hawataona unyonge kuwa
waja wa Mwenyezi Mungu). Na watakaoona unyonge uja wa Mungu
na kutakabari, basi Atawakusanya wote Kwake (Awatie Motoni). Na
ama wale walioamini na kufanya vitendo vizuri, basi Atawapa ujira
wao (sawa sawa), na kuwazidishia fadhila zake. Lakini wale walioona
unyonge na kufanya kiburi, basi Atawaadhibu kwa adhabu iumizayo,
wala hawatapata rafiki wala msaidizi (yoyote) mbele ya Mwenyezi
Mungu. (Quran 4:171-173)
12 “Na kwa wale waliosema: “Sisi ni Wakristo,” Tulichukua ahadi kwao,
lakini wakaacha sehemu (kubwa) ya yale waliyokumbushwa, kwa
hivyo Tukaweka baina yao (wenyewe kwa wenyewe) uadui na
bughudha mpaka Siku ya Kiama. Na Mwenyezi Mungu atawaambia
walivyokuwa wakiyafanya. Enyi watu wa Kitabu! Amekwisha
kufikieni Mtume wetu, anayekudhihirishieni mengi mliyokuwa
mkiyaficha katika Kitabu, na husamehe mengi. Bila shaka imekwisha
kufikieni nuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Kitabu
kinachobainisha (kila jambo). Kwa (Kitabu) hicho Mwenyezi Mungu
huwaongoza wenye kufuata radhi Yake katika njia za salama, na
huwatoa katika kiza kuwapeleka katika nuru kwa amri Yake, na
Huwaongoza katika njia iliyonyooka. Kwa yakini wamekwisha kufuru
wale waliosema: “Mwenyezi Mungu ni Masihi bin Maryamu.” Sema:
“Ni nani atakayemiliki (kuzuilia) chochote mbele ya Mwenyezi
Mungu kama Yeye angetaka kumwangamiza Masihi mtoto wa
Maryamu, na mama yake na vyote vilivyomo katika ardhi?” Na
ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake ni wa Mwenyezi
Mungu (tu peke yake). Huumba Apendavyo. Na Mwenyezi Mungu ni
Muweza juu ya kila kitu.” (Quran 5:14-17)
13 “Bila shaka wamekufuru wale waliosema, “Mwenyezi Mungu ni
Masihi (isa) bin Maryamu.” Na (hali ya kuwa) Masihi alisema: “Enyi
wana wa Israili! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola
wenu. Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi
Mungu atamharamishia Pepo, na mahali pake (patakuwa) ni Motoni.
Na madhalimu hawatakuwa na wasaidizi (wa kuwasaidia Siku ya
Kiama).”
14 Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: “Mwenyezi Mungu ni
mmoja katika (wale waungu) watatu; (Yeye ndiye wa tatu wao).” Hali
hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja (tu peke yake). Na kama
hawataacha hayo wayasemayo, kwa yakini itawakamata – wale
wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao – adhabu iumizayo.
15 Je! Hawatubu kwa Mwenyezi Mungu na kumwomba msamaha? Na
Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa
kurehemu.
16 Masihi bin Maryamu si chochote ila ni Mtume (tu). (Na) bila shaka
Mitume wengi wamepita kabla yake. (Hawajaona)? Na mamake ni
mwanamke mkweli. (Na) wote wawili walikuwa wakila chakula (na
wakenda choo. Basi waungu gani wanaokula na kwenda choo)?
Tazama jinsi wanavyogeuzwa (kuacha haki).
17 Sema: “Je! Mnawaabudu – badala ya Mwenyezi Mungu (peke yake) –
wale ambao hawawezi kukudhuruni wala kukunufaisheni? Na
Mwenyezi Mungu ndiye Asikiaye (na) ndiye Ajuaye.”
18 Sema: “Enyi watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu
bila haki, wala msifuate matamanio ya watu waliokwisha potea toka
zamani; (nao ndio hao wanavyuoni wenu) na wakawapoteza wengi, na
(sasa) wanapotea njia iliyo sawa, (hawataki kumfuata Nabii
Muhammad).” (Quran 5:72-77)
19 Na (kumbukeni) Mwenyezi Mungu atakaposema: “Ewe Isa bin
Maryamu! Je, wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama
yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu?” aseme (Nabii
Isa): “Wewe umetakasika na kuwa na mshirika. Hainijuzii mimi
kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uwongo).
Kama ningalisema bila shaka Ungalijua; Unayajua yaliyomo nafsini
mwangu, lakini mimi siyajui yaliyo nafsini Mwako; hakika Wewe
ndiye Ujuaye mambo ya ghaibu.
20 “Sikuwaambia lolote ila yale Uliyoniamrisha: ya kwamba,
‘Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wenu.’ Na nilikuwa shahidi juu
yao nilipokuwa nao; na Uliponikamilishia muda wangu, Wewe ukawa
Mchungaji juu yao, na Wewe ni Shahidi juu ya kila kitu.
21 Ikiwa Utawaadhibu, basi bila shaka hao ni waja wako; na
Ukiwasamehe basi kwa hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu (na)
Mwenye hikima; (Hutaambiwa kuwa wamekushinda kuwatia adabu).”
22 Mwenyezi Mungu atasema: “Hii ndiyo Siku ambayo wakweli
utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mbele yake
mito. Humo watakaa milele. Mwenyezi Mungu amewawia (amewapa)
radhi; nao wawe radhi Naye. Huku ndiko kufaulu kukubwa.” (Quran
5:116-119)
23 Na Mayahudi wanasema: “Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu;” na
Wakristo wanasema: “Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu”; haya
ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga
maneno ya wale walio kufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu
awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!
24 Wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu
badala ya Mwenyezi Mungu na (wamemfanya) Masihi mwana wa
Maryamu (pia mungu), hali hawakuamrishwa ispokuwa kumuabudu
Mungu Mmoja, hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Yeye.
Ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo.
25 Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao,
lakini Mwenyezi Mungu amekataa ispokuwa kuitimiza nuru Yake,
ijapokuwa makafiri wanachukia.
26 Yeye ndiye Aliyemleta Mtume Wake kwa uongofu na Dini ya haki ili
Aijaalie kushinda (Dini hii) dini zote; ijapokuwa watachukia hao
washirikina.
27 Enyi mlioamini! Wengi katika makasisi (wanavyuoni wa Mayahudi
na Manasara) na watawa (wao) wanakula mali za watu kwa batili na
kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu. Na wale wakusanyao dhahabu
na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape
habari za adhabu inayoumiza (inayowangoja)
28 Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika Moto wa Jahanamu, na kwa
hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo
yao, (na huku wanaambiwa): “Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia
(mliyojikusanyia) nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa
mkikusanya.” (Quran 9:30-35)
MUHAMMAD AU YESU?
Wakristo wanadai kwamba utabiri wa Kumbukumbu la Torati 18:18
unamuhusu Yesu na sio Muhammad. Hiyo aya inasema: "Mimi
nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami
nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote
nitakayomwamuru.” Kumbukumbu la Torati 18-18 Hoja ya pekee
wanayoikimbilia katika tafsiri hiyo ni kuwa wote wawili Musa na Yesu
walikuwa Mitume. Ingawa hoja hiyo inapingana na madai yao ya kuwa
Yesu alikuwa ni Mungu na si Mtume. Mitume wengi wa Kiyahudi
walifanana na Musa. Hata hivyo, kama tutamlinganisha Muhammad na
Musa, tupata kuwa:
Muhammad alikuwa ni Mwarabu, na Waarabu wanatokana na Ismaili, mtoto
wa Ibrahimu, huku Musa alikuwa ni Myahudi, na Wayahudi wanatokana na
Isaka, mtoto wa Ibrahimu, kwa kuwa neno NDUGU ZAO linaashiria watoto
wa mtoto wa kwanza kuwa ndugu wa mwingine. Hili halikubaliki kwa Yesu,
kwa kuwa alikuwa ni Myahudi.
Kwa mujibu wa Wakristo, Yesu alienda Motoni kwa siku tatu huku Musa
akiwa hajaenda. Kwa hiyo, Yesu si kama Musa. (Katika Uislamu, hakuna
yoyote katika hao Manabii watatu aliyeingia Motoni)
Musa na Muhammad walizaliwa na baba na mama huku Yesu alizaliwa na
mama tu.
Musa na Muhammad walioa na kuwa na watoto, huku Yesu akiwa hajaoa
kabisa.
Musa na Muhammad walipata matatizo na mambo magumu kutoka kwa
watu wao mara ya kwanza, lakini mwishoni walikubaliwa na watu wao.
Huku Yesu alikuwa amekataliwa na watu wake mwanzoni na anaendelea
kukataliwa na Wayahudi hadi leo hii. “Alikuja kwake, wala walio wake
hawakumpokea.” Yohana 1:11
Musa na Muhammad walikuwa na nguvu, kando na kuwa Mitume. Wote
wawili walitekeleza adhabu kubwa, hilo likiwa ni mfano, huku Yesu hakuwa
na madaraka kwa watu wake. “Yesu akajibu, ufalme wangu sio wa
ulimwengu huu”, Yesu amesema katika 18:36.
Musa na Muhammad walileta sheria mpya huku Yesu hakuleta.
Musa alilazimishwa kuhama alipokuwa mkubwa aende Median huku
Muhammad pia, alilazimishwa ahame alipokuwa katika hatua moja ya
maisha yake, kuelekea Madina. Huku Yesu hajalazimishwa kuhama katika
utuuzima wake.
Musa na Muhammad wote wawili walikufa vifo vya kawaida na kisha wote
walizikwa, huku jambo hilo haliwezi kuongelewa kwa Yesu. Yesu
hakuuliwa wala hakusulubiwa kabisa kabisa, kwa mujibu wa Quran na
hakufa kwa kifo cha kawaida kama ilivyothibitishwa na Wakristo ambao
wanaamini kasulubiwa.
MASWALI YA MWISHO
57. Kwa nini, ewe kiongozi wa Kikristo, huji kusikiliza na kujifunza dini
ya kweli ya Yesu?
58. Ukiwa kama Mkristo, uliyeusoma Uislamu na ikiwa ni hivyo, je,
uliusoma kutoka kwa Waislamu wa kweli?
59. Kama Mkristo, je, unakubali kwa uadilifu na wema kuwa ni lazima
uchunguze kile kinachosemwa na Uislamu juu ya Mungu, Yesu,
pamoja na maisha haya na ya baadae?
60. Kwa kuwa ni Mkristo, je, pia, waamini kile tunacholazimika
kuhesabiwa kwa Muumba wetu na kwamba Muumba ni mkamilifu na
Muadilifu? Kama muumini mwaminifu kwa Mungu. Je, hulazimiki
kutafuta ukweli usiobadilishwa bilia kujali matokeo yake?