Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Mwenyezi Mungu, Muharram
Abdullah bin Hamuud Al-Fariih
Tarjama ya
Maulid Makokha
Mwandishi
Msururu wa hukumu Msururu wa hukumu Msururu wa hukumu Msururu wa hukumu Msururu wa hukumu Msururu wa hukumu Msururu wa hukumu Msururu wa hukumu kumi fupi (3)umi fupi (3) umi fupi (3) umi fupi (3)
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
MWEZI WA MWENYEZI MUNGU, MUHARRAM
Mwenyezi Mungu aliuunganisha (huu mwezi) kwa nafsi yake ili kuonyesha utukufu wake, na kuonyesha kuwa Yeye mwenyewe ndiye aliyeuharamisha. Kwa hivyo, hakuna yeyote katika viumbe wake anayefaa kuuhalalisha.
Ibn Rajab alisema, “Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake aliuita (mwezi wa) Muharram kuwa ni 'mwezi wa Mwenyezi Mungu'. Na kuunganisha kwenye jina lake Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mshindi kunaashiria utukufu wake na fadhila zake. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu Mtukufu haunganishi kitu kwenye jina lake isipokuwa viumbe wake maalumu.” [Lataif Al-Ma'arif, uk.90-91]
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
KUUTUKUZA MWEZI WA MWENYEZI MUNGU, MUHARRAM
Mwenyezi Mungu Mtukufu aliitukuza hadhi yake (huu mwezi) katika kitabu chake. Alisema Yeye Mtukufu: Hakika, idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na miwili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, tangu siku alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo, iko minne iliyo mitukufu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msijidhulumu ndani yake nafsi zenu. (Qur-ani 9:36)
Na Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake aliutaja utukufu wake katika sunna yake. Katika vitabu viwili sahihi, kutoka kwa hadithi ya Abu Bakra, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka kwa Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema, “Hakika, zama zimesharejea katika mfumo wake wa kwanza kama ulivyokuwa wakati Mwenyezi Mungu aliziumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na miwili, ambayo miezi minne kati yake ni mitakatifu: Tatu hufuatana kwa mfululizo: Dhul-Qa'da, Dhul-Hijja na Muharram, na (wa nne ni) Rajab wa (kabila la) Mudhar ambao uko kati ya Jumada na Sha’ban.” Na kundi la wanachuoni wanaona kuwa Muharram ndio mwezi bora zaidi kati ya miezi mitukufu [Lataif Al-Ma’arif, uk.70]
Abu Uthman An-Nahdi alisema kutoka kwa watangulizi wema (Salaf), Mwenyezi Mungu awarehemu, "Walikuwa wakitukuza makumi matatu: siku kumi za mwisho za Ramadhani, na siku kumi za mwanzo za Dhu-Hijja, na siku kumi za mwanzo za Muharram [Lataif Al-Ma’arif, uk. 757]
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
UKALI WA KUHARAMISHA DHULUMA KATIKA MIEZI MITUKUFU KULIKO MINGINEYO
Sheikh As-Sa'adii alisema, “Basi msijidhulumu ndani yake nafsi zenu.” 'ndani yake' inawezekana kwamba inamaanisha miezi kumi na miwili. Na inawezekana kwamba inamaanisha hiyo minne mitukufu, na kwamba hili ni kuwakataza kufanya dhuluma ndani yake hususan, pamoja na kuwakataza kufanya dhuluma wakati wote, ili kuongeza uharamu wake, na kwamba dhuluma ndani yake ni jambo kubwa kuliko nyakati zinginezo.” [Tafsir As-Sa'adii, 3/228-229]
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
SABABU YA KUUTAJA MWEZI WA MWENYEZI MUNGU,
MUHARRAM KWA HILI JINA
Inasemekana kuwa uliitwa mwezi wa 'Muharram' kwa sababu ni haramu kupigana humo. Ibn Kathir, Mwenyezi Mungu amrehemu alisema, “Wanazuoni walitofautiana kuhusu uharamu wa kuanzisha vita katika mwezi mtukufu, je ulifutwa au haukufutwa kwa kauli mbili: Mmoja yake ambayo ndiyo mashuhuri ni kwamba (huo uharamu) ulifutwa, kwa sababu Yeye Mtukufu alisema hapa, “Basi msijidhulumu ndani yake nafsi zenu.” Na akaamrisha kupigana na washirikina. Nayo kauli nyingine ikasema kuwa kuanzisha vita katika mwezi mtukufu ni haramu, na kwamba uharamu wa (vita katika) miezi mitukufu haukufutwa kwa kauli yake Mtukufu, “Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Kwa hivyo, anayewashambulia, nanyi mshambulieni kwa kadiri alivyowashambulia.” hadi mwisho wa Aya. Na akasema, "Na ikiisha miezi mitukufu, basi wauweni washirikina" [Tafsir Ibn Kathir, 2/468-469]
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
NI SUNNA KUUFUNGA MWEZI WA MWENYEZI MUNGU,
MUHARRAM
Imetajwa katika fadhila za kufunga saumu ndani yake yale aliyosimulia Muslim kutoka kwa hadithi ya Abu Huraira kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema, "Kufunga saumu bora zaidi baada ya Ramadhani ni mwezi wa Mwenyezi Mungu, Muharram". Na wanachuoni wametofautiana, je unafungwa wote au siku nyingi zake tu? kwa kauli mbili. Na maana ya dhahiri ya hii hadithi inaashiria ubora wa kufunga saumu mwezi wa Muharram wote. Lakini baadhi ya wanachuoni walielewa hilo kwamba ni katika mlango wa kuhimiza kufunga sana katika mwezi wa Muharram, na sio kuufunga wote, kwa yale yaliyomo katika Sahihi mbili katika hadithi ya Aisha, Mwenyezi Mungu amuwie radhi kuwa alisema, "Sikuwahi kumuona Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akifunga mwezi mzima kamwe isipokuwa (mwezi wa) Ramadhani. Na sikuwahi kumwona akifunga sana katika mwezi wowote ule zaidi ya mwezi wa Sha’ban." Na hao walijibiwa kuwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwie radhi aliripoti tu kile alichokiona.
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
SABABU ILIYOMFANYA NABII REHEMA NA AMANI ZA MWENYEZI MUNGU ZIWE JUU YAKE KUFUNGA SANA KATIKA MWEZI WA SHA’BAN, NA SIO KATIKA MWEZI WA MWENYEZI MUNGU, MUHARRAM
An-Nawawii alisema, “Pengine hakujua fadhila za Muharram isipokuwa katika mwisho wa uhai wake kabla ya kuweza kuufunga. Au labda alikuwa akipatwa na udhuru ndani yake, zenye kumzuia kufunga sana ndani yake, kama vile safari, maradhi na mengineyo.” [Sharh ya Sahih Muslim, 8/37]
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
SIKU BORA ZAIDI KUFUNGA KATIKA MWEZI WA MWENYEZI MUNGU, MUHARRAM NI SIKU YA 'ASHURA
Nayo ni siku ya kumi ya huo mwezi, na kuifunga kunasamehe mwaka wa kabla yake, kwa yale aliyosimulia Muslim katika hadithi ya Abu Qatada kuwa Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema alipoulizwa kuhusu kufunga siku ya 'Ashura, "Ninatarajia kwa Mwenyezi Mungu asamehe mwaka wa kabla yake." Na Muislamu atapata hii fadhila hata kama atafunga 'Ashura peke yake, na hakuna cha kuchukiza (makruhu) chochote katika kuifunga hiyo peke yake, kulingana na kauli iliyo sahihi. [Al-Ikhtiyaarat Al-Fiqhiyya cha Ibn Taymiyyah, uk.110, Fatwa za Al-Lajna Ad-Daima 1/401].
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
HEKIMA KATIKA KUFUNGA SIKU ZA 'ASHURA
Ufafanuzi wa hekima ya kufunga siku ya 'Ashura ilikuja katika hadithi ya Ibn Abbas katika Sahihi mbili: Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alipofika Madina, aliwapata (Mayahudi) wakifunga siku fulani, yani 'Ashura. Walisema, "Hii ni siku kuu. Nayo ndiyo siku ambayo Mwenyezi Mungu alimwokoa (Nabii) Musa, na akawazamisha watu wa Fir'awn. Kwa hivyo, Musa akaifunga ili kumshukuru Mwenyezi Mungu." Kwa hivyo, (Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) akasema, "Mimi ninamstahili zaidi Musa kuliko wao." Kwa hivyo, akaifunga (siku hiyo) na akaamrisha ifungwe.
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
SUNNA NI KUFUNGA SIKU YA TISA PAMOJA
NA SIKU YA ‘ASHURA
Na hilo ni kwa sababu ya kuwahalifu Watu wa Kitabu; kwa yale aliyosimulia Muslim katika hadithi ya Ibn ‘Abbas, Mwenyezi Mungu awawiye radhi, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alipofunga siku ya ‘Ashura, na akaamrisha kwamba ifungwe, wakasema, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika, hii ni siku ambayo Mayahudi na Wanaswara wanaitukuza.” Mtume wa Mwenyezi Mungu Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akasema, “Utakapokuwa mwaka ujao, Mwenyezi Mungu akipenda, tutafunga siku ya tisas.” Na katika riwaya, “Kama nitabaki hadi mwaka ujao, bila shaka nitafunga siku ya tisa”. Akasema: Lakini mwaka ujao haukuja isipokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alikuwa ameshakufa. Na ama hadithi zilizokuja kuhusu kufunga siku moja kabla yake na baada yake, na vile vile kuhusu kufunga siku moja kabla yake au baada yake, sio sahihi
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
kwamba zilitoka kwa Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, lakini kuna simulizi sahihi zilizokomea kwa Ibn Abbas – Mwenyezi Mungu amuwiye radhi - Na kwa sababu ya hiyo, mwenye kufunga ‘Ashura na siku moja kabla yake na siku moja baada yake, au akatosheka na kuifunga na kufunga siku moja baada yake ili kuwahalifu Mayahudi, basi hatalaumiwa.
Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa
Mwenyezi Mungu, Muharram
HUKUMU YA KUFUNGA ‘ASHURA KWA KUWEKA NIA MCHANA
Inaruhusika kufunga siku za mwezi wa Mwenyezi Mungu, Muharram, ikiwemo siku ya ‘Ashura na Tasu’a (siku ya tisa) kwa kuweka nia mchana, kulingana na kauli iliyo sahihi, lakini lililo kamilifu zaidi ni kuweka nia usiku. [Sharh ya Sahih Muslim cha An-Nawawii 8/276, Ash-Sharh Al-Mumti’ cha Sheikh Ibn ‘Uthaimin 6/359] Na inaruhusika kufunga ‘Ashura kwa mwenye deni la saumu; kwa sababu kulipa deni la saumu kuna wakati mpana. Na hata akifunga ‘Ashura pamoja na nia kulipa deni la saumu, basi atapata malipo, kulingana na kauli iliyo sahihi. [Angalia: Majmu’ Fatwa na risala za Sheikh Ibn Uthaymiyn, 20/48]
Taasisi ya Iqtida ya sayansi na waqfu
Tunashughulika na kueneza Sunna za Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na nyiradi zake za kila siku
Ili kuwasiliana nasi, bonyeza kwenye ikoni
Pakua programu zetu
Programu ya ANDROID kwenye
Pakua kwenye
Programu ya ANDROID kwenye
Pakua kwenye