SHIA ITHNA ASHARIA NI WATU GANI?
Maswahaba zake na wote waliyo ongoka kupitia
Muongozo wa Mtume amma baad.
Kitabu hiki ni miongoni mwa mfululizo wa vitabu
Ambavyo ni Muhtasari vyenye malengo ya
kuwabainishia Waislamu na kuwawekea wazi Itikadi za
Mapote [Makundi] yaliyo potea ili wawe na Tahadhari
na Makundi hayo hasa ukizingatia kuwa baadhi ya
Makundi hayo sasa yameanza kuwa na Sauti na
yamekuwa na Harakati za waziwazi katika kueneza
Upotovu wao na Tumeanza mfululizo huu kwa kundi la
[SHIA ITHNA ASHARIA] Hasa miongoni mwa
Makundi mengi ya Kishia kwa sababu Kundi hili ndilo
lenye kudhihiri zaidi.
Pia sababu nyingine iliyo pelekea kuanza na kundi hili ni kwa kuwa kundi hili Mara nyingi hunadi kuwa Madhehebu yao hayatofautiani na Madhehebu ya Ahlus-sunnah na wanadai kuwa wamedhulumiwa tu na kuzuliwa mambo ambayo sii kweli pia kundi hili linafanya Juhudi kubwa sana katika kutetea Itikadi yake na kusambaza Vitabu na Risala mbali mbali ili kueneza Madai yao pia kundi hili limekuwa likifuatilia Vitabu mbalimbali vya Wanachuoni wa Ahlus-sunnah na Kuvirudi wakati Juhudi hizi hatuzioni katika Makundi Mengine, Na kwakuwa Vitabu vya Kishia sasa vime'enea Ueneaji ambao Hatukuuzoea huko Nyuma na wamekuwa wakivieneza kwa njia mbali mbali kila Mahala, kutokana na sababu hizi zimetupelekea kuona Ulazima kuviweka Bayana na kubainisha Itikadi Potovu zilizomo ndani
صفحة 4
yake, Ambazo walijitahidi sana kuzificha Lakini
Tunasema kama Alivyosema Msemaji Mmoja:
(Tutakusimamishieni Hoja kupitia Vinywa Vyenu)!
Tunamuomba Allah Ainyanyue Bendera ya Sunnah na watu wake na Aidhalilishe Batwili na watu wake Allah peke yake ndie anayajua makusudio na ndie Mwenye kuongoza njia iliyo sawa. NB: Kuna baadhi ya Maneno Ambayo nimeongeza yanaumuhimu kwa Msomaji.
Yameandikwa na: ABDULLAHI BIN MUHAMMADI AS-SALAFY
Yame Tafsiriwa na:
YASSINI TWAHA HASSANI
(KONGOLO)
ASILI YA MADHEHEBU YAO
صفحة 5
Miongoni mwa itikadi za Shia ithna asharia: ni
kwamba wanakiri na kukubali kwamba Ushia Asiliyake
ni Uyahudi uliotokana na myahudi anaitwa Ibnu sabai
pia wanakiri kwamba Aly bin abi Twalib -Radhi za Allah
zimwendee- aliwachoma moto pindi walipomfanya
kuwa Mungu na akatangaza wazi wazi kuwa yuko mbali
nao kabisa na yuko mbali na itikadi hiyo.
Rejea kitabu: (Firaqu shia).
cha An-nubukhty. ukurasa. (22).
pia rejea kitabu: (Ikhtiyaaru marifatir-rijaal).
cha Atwuusy. ukurasa wa. (107).
Nao wanasema vilevile na kukiri bali kujifakharisha kwa kuitwa jina la Raafidhwa. Rejea kitabu: (Biharul- anwaar). cha almajlisy. (65/97).
ITIKADI YAO JUU YA ALLAH
Wanasema: Hakika sisi (Mashia) Hatuungani nao (yaani hawaungani na Ahlus-sunnah) katika itikadi ya Mungu wala Mtume wala Imamu kwa sababu wao wanasema kwamba: Mungu wao ni Yule ambaye Muhammadi alikuwa ndio Mtume wake na Khalifa wa Mtume wake alikuwa ni Abubakari. Na sisi (Mashia) Hatumuitakidi Mungu huyo wala Mtume huyo bali sisi Tunaitakidi kwamba Mungu ambaye khalifa wa Mtume wake alikuwa ni Abubakari huyo sio Mungu wetu na wala huyo sio Mtume wetu.
صفحة 6
Rejea kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyya).
cha Niimatullahi Aljazaairy. (2/278).
Na katika itikadi zao wanasema kuwa: Allah
hataonekana siku ya Qiyama na kwamba Allah hasifiwi
kwa mahala wala kwa zama wala haashiriwi na kwamba
yeyote atakaye sema kuwa Allah hushuka katika Mbingu
ya dunia na kwamba ataonekana kwa watu wa peponi
wamuone wazi wazi kama wanavyo uona Mwezi basi
Mtu huyo anakuwa ni sawa na Kafiri.
Rejea kitabu:
(Aqaaidul- Imaamiyyah).
cha Muhammad Ridhwaa Midhfar.
ukurasa (58).
Na wanasema vilevile: hakika Mwenyezi Mungu
atakapo msemesha mja wake siku ya Qiyama atakuwa
Amejishika Kiunoni na mja nae Atasimama mbele ya
Mola wake hali kajishika nae kiunoni huku akitajiwa
Madhambi yake. Pakaulizwa: nini makusudio ya
kujishika kiunoni? Akasema mpokeaji wa habari hii:
Yule msemaji akajishika kiunoni kisha akasema:
yaani hivi kama vile Mtu anavyoongea na ndugu yake
katika jambo la siri kati yao.
Tazama kitabu: (Al-usuulus-sitata ashara). kilicho
hakikiwa na: Dhwiyaud-diin alhamuudy. ukurasa (203).
Na wanasema vilevile: Hakika Allah huteremka siku ya Arafa pindi Jua linapo pinduka Akaja Ardhini akiwa juu ya Ngamia akiwa kawaenea Watu wa Arafa Kuliani na
صفحة 7
Kushotoni.
Angalia kitabu: (Al-usuulus-sitata ashara).
Kilicho Hakikiwa na: Dhwiyaud-diin Alhamuudy.
ukurasa (204).
Na wanasema: Kulielekea Kaburi ni Jambo la Lazima
hata kama litakuwa haliko upande wa Qibla pia
kulielekea kaburi la Mtume kwa Mwenye kulizuru ni
sawa na kuelekea Qibla na huo ndio (Muelekeo wa
Mwenyezi Mungu) yaani alio waamrisha watu kuuelekea
katika hali hiyo.
Angalia kitabu: (Biharul- Anwaar).
cha Almajlisy. (101/369).
Na wanasema kuwa: (Aaah) ni jina miongoni Mwa
Majina ya Allah yaliyo mazuri hivyo Mwenye kusema
neno hilo anakuwa kamwita Allah kwa namna ya
kuomba msaada.
Angalia kitabu: (Mustadrakul-wasaail).
cha Annuury at-twabrasy. (2/148).
Pia wanasema kuwa: Mwenyezi Mungu huwa
anamzuru (kumtembelea) Husein bin Ally na kupeana
naye mkono na Anakaa naye juu ya Kiti.
Rejea kitabu: (Swahiifatul-Abraar).
cha Mirza Muhammad taqy. (2/140).
ITIKADI YAO KUHUSU KUBADILISHWA QUR-ANI
صفحة 8
Wanasema: Qur-an imebadilishwa na kwamba ni
Pungufu na Qur-an ambayo ni sahihi anayo Almahdi wao
anayesubiriwa kuja kwake. Miongoni mwa Wanachuoni
wa Kishia walio weka wazi Itikadi hii ni: Ally bin
Ibrahim Alqummy Pamoja na Niimatullahi Aljazaairy na
Alfaidhul Kaashaany na Ahmad Attwabrasy na
Muhammad Baaqir Almajlisy na Muhammad bin
Nuumaan wanaye muita Almufiid na Abulhasan al-
Aamily na Adnaan Albahraany na Yusuf Albahraany na
Annuury Attwabrasy na Wengineo wengi. Tazama
kitabu: (Ash-shia al-ithnaa asharia wa tahriiful-quran).
cha Muhammad Sayf. Na
kitabu: (Mauqifur-raafidhwa Minal-Quran)
cha Mamadoo kaaraambiiry.
Na wanasema kuwa tamko: (Aali Muhammadi na Aali
Ally) liliondolewa katika Qur-an.
Tazama kitabu: (Minhaajul-baraati sharhu nahjul balaaghah).
cha Habibullah alkhuui. (2/216).
Na wanasema kwamba: hakuna aliye ikusanya Qur-an
yote ispokuwa Maimamu.
(yaani maimamu wa shia ithna asharia)
na kwamba wao ndio wanajuwa Elimu yake yote.
Tazama kitabu: (Usuulul-kaafy). cha Alkulayny.
(1/228).
Na wanasema: Qur-an haiwezi kuwa ni hoja mpaka
atakapo kuja Alqayyim wao. (Mahdy).
Angalia kitabu: (Usuulul-kaafy). cha Alkulainy. (1/169).
صفحة 9
Na wanasema: katika Qur-an kuna sura inaitwa:
Suuratul-wilaaya ambayo inaanza hivi:
(Enyi mlio amini ziaminini nuru mbili…)
kwamba Othman bin Afani aliifuta sura hii kama
wanavyo dai.
Angalia kitabu:
(Faslul-khitwaab fiitahriif kitaab rabbul-arbaab).
cha An-nuur attwabrasy. ukurasa (18).
Na wanasema kwamba: kuna Msahafu unaitwa Mushaf
Faatwimah na kwamba Msahafu huyo ukubwa wake
ni mfano wa Qur-an yetu mara tatu.
Angalia kitabu: (Usuulul-kaafy). cha Alkulainy. (1/239).
Na wanasema: kauli ya Mwenyezi Mungu iliyopo katika
suratil-Maida aya ya (67) Isemayo:
(Ewe Mtume yafikishe yale yaliyo teremshwa kwako
kutoka kwa Mola wako na kama hukufanya hivyo basi
hujafikisha Ujumbe wake).
Mashia wanasema: aya hii ilikuwa hivi:
(Ewe Mtume yafikishe yale yaliyo teremshwa kwako -
Kuhusu Ally- na kama hukufanya hivyo basi hujafikisha
ujumbe wake) wakaongeza katika aya neno:
(kuhusu Ally). Yaani kwamba Mtume -rehma na amani
za Allah ziwe juu yake- Aliliacha huenda kwa
kuwaogopa Wanafiki kama walivyo eleza katika vitabu
vyao vingi tu.
Angalia kitabu:
(Faslul-khitwaab fiitahriif kitaab rabbul-arbaab).
cha An-Nuur attwabrasy. ukurasa (182).
صفحة 10
Na wanasema: Hawamkemei mwenye kusema kuwa
Qur-an imebadilishwa bali mtu kama huyo
wanamzingatia ni miongoni mwa Wanachuoni ambao ni
Mujtahid ama mwenye kukanusha (Wilaya -Utawala
baada ya mtume-) ya ally kwa mashia huyo anazingatiwa
ni Kafiri tena ukafiri usio na shaka ndani yake.
Tazama kitabu: (Al-iitiqaadaat).
cha Ibnu Baabawayhi Alqummy. ukurasa (103).
Na wanasema: kuwa wamewaamrisha wafuasi wao
kuisoma Qur-an hii tuliyo nayo katika Swala zao na
Sehemu nyingine pamoja na kuzifanyia kazi hukumu
zake mpaka atakapo kuja: (Maulaana Swahibuz-zamaan)
yaani Mahdi ndipo Qur-an hii itaondoshwa na
kunyanyuliwa Mbinguni na hapo itakuja Quran aliyo
itunga Amiril-muuminina iwe ndio yenye kusomwa na
kufuatwa hukumu zake.
Tazama kitabu: (Al-an war Annuumaaniyyah).
cha Niimatullahi Aljazaairy (2/363).
Na wanasema kuwa: Msiwafundishe wanawake Surati
Yusuf wala msiwasomeshe sura hiyo maana ndani yake
kuna Fitna lakini wafundisheni Suratin-nuur maana ndani
yake mna Mawaidha.
Rejea kitabu:
(Al-furuu minal kafy) cha Alkulayny (5/516).
AL-IMAAMAH (MRITHI) KWAO NI NGUZO NA ASIYE AMINI NGUZO HII NI KAFIRI
صفحة 11
Wanasema: Hakika asiye amini Al-imaamah basi Imani
yake haikamiliki ispokuwa kwa kuitakidi na kuamini
hivyo.
Angalia kitabu: (Aqaaidul-imaamiyyah).
cha Muhammad Ridhwaa midhfar. ukurasa (78).
Na wanasema: Hakika al-imaamah ni muendelezo wa
Utume na nidalili inayo wajibisha kutumwa Mitume na
kuwatuma Manabii jambo hili pia linawajibisha kuwepo
na Imamu baada ya Mtume.
Angalia kitabu: (Aqaaidul-imaamiyyah).
cha Muhammad Ridhwaa midhfar. ukurasa (88).
Na wanasema: Makusudio yao kuhusu swala la Alimaama
ni kuwa hiki ni cheo cha KiMungu Allah
anamchagua atakaye mpa cheo hiki miongoni mwa waja
wake kutokana na Elimu yake ya tangu kama vile anavyo
Mteua Mtume wake kuufahamisha umati wake juu ya
huyo Imamu na kuwaamuru wamfuate.
Angalia kitabu: (Aslush-shia wa Usuulihaa). cha
Muhammad Hussein kaashiful-ghitwaa. ukurasa (102).
Bali itikadi hii ni katika mambo ya msingi katika dini na
Haitimii Imani ya Mtu ispokuwa kwa itikadi hii. Na kwa
Ibara nyingine wanasema: Hakika Imama ni kuendelea
kwa Utume.
Na wanasema: Hakika Mwenye kupinga Uimamu wa Amiril-muuminina Ally bin Abi Twaalib Radhi za Allah ziwe juu yake na Maimamu wengine baada yake ni kama Mtu aliye pinga Unabii wa Manabii wa Allah na kwamba
صفحة 12
Mwenye kukiri Uimamu wa Ally lakini akampinga hata
Mmoja miongoni mwa Maimamu baada yake ni sawa na
Mtu aliye wakubali Mitume wote lakini akakanusha
Utume wa Muhammadi -rehma na amani za Allah ziwe
juu yake-.
pia wanasema: Mwenye kupinga Uimamu wa yeyote
miongoni mwa Maimamu kumi na mbili ni sawa na
Mwenye kuwapinga Mitume wote.
Angalia kitabu: (Minhaajun-najaat).
cha Alfaidhul-kaashy. ukurasa (48).
*Majina kumi na mbili ya maimamu wa kishia:
1/Ally bin Abi Twalib. (Al-mur-tadhwa)
2/Hassan bin Ally. (Azzakii – al-mujtabaa)
3/Hussein bin Ally. (Shahiid)
4/Ally bin Hussein. (Zainul-aabidiyna)
5/Muhammad bin Ally. (Al-baaqir)
6/Jaafar bin Muhammad. (Aswaadiq)
7/Mussa bin Jaafar.(Al-kaadhwim)
8/Ally bin Mussa. (Arridhwah)
9/Muhammad bin Ally. (Al-jawaadu)
10/Ally bin Muhammad. (Al-haady)
11/ Hassan bin Ally. (Al-askary)
12/Muhammad bin Hassan. (Al-mahdy)
Na wanasema: kwa Mujibu wa makubaliano ya Imaamiyyah wote ni kwamba yeyote Mwenye kupinga Uimamu wa yeyote miongoni mwa Maimamu wao na akakanusha kutekeleza Utiifu ambao Allah kawajibisha juu yao basi mtu huyo ni Kafiri na nimpotevu na
صفحة 13
anastahiki kudumu Motoni Milele.
Angalia kitabu: (Haqqul-yaqiin Fii Maarifat Usuulid diin)
cha Abdallah bishri (2/189).
Na wanasema: Hakika tamko la Shirki au Kufru kwa
kila asiye itakidi Uimamu wa Amiril-muuminina na
Maimamu wengine miongoni mwa watoto wake na
akawafadhilisha Wengine juu yao Matamko haya
yanamaanisha kuwa watu hao ni wenye Kudumu Motoni
milele.
Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar).
cha Almajlisy. (23/390).
KUMKOSEA KWAO ADABU MTUME MUHAMMADI-REHMA NA AMANI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE- NA MABINTI ZAKE NA WATU WA NYUMBANI KWAKE.
Wanadai kuwa: Pindi Mtume -rehma na amani za Allah
ziwe juu yake- Alipo zaliwa alikaa Masiku kadhaa hana
Maziwa ya kunyonya basi Abuu Twaalib Akamuweka
katika Maziwa yake Allah akateremsha ndani yake
maziwa hivyo Akanyonya kwa siku kadhaa mpaka
Abuu Twalib Alipo mpata Halimatu Saadia na
kumkabidhi ili Amnyonyeshe.
Angalia kitabu: (Usuulul-kaafy).
cha Alkulayny. (1/448).
Na wanasema kwamba: Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- Alikuwa ni Shujaa kuliko Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Bali Mtume hakupewa Ushujaa
صفحة 14
asilani.
Angalia kitabu: (Al-an war annuumaaniyyah).
cha Niimatullahi Aljazaairy. (1/17).
Na wanasema: Mtume -rehma na amani za Allah ziwe
juu yake- Alikuwa hawezi kulala Mpaka Abusu Paji la
Uso wa Faatwima (Binti yake) au kifua chake Kunyonya
Maziwa!!!.
Angalia kitabu: (Bihaarul-Anwaar).
cha Al-majlisy. (42/43).
Na wanasema: Mtume -rehma na amani za Allah ziwe
juu yake- Hakuwa na Mabinti ispokuwa Faatwima ama
Ruqayyah na Ummu kulthum na Zainabu hawa ni watoto
walio lelewa kwake tu.
Angalia:
(Daairatul-maariful-islaamiyyatu ash-shiiyyah) (1/27).
*Mtume wetu Muhammad-rehma na amani za Allah
ziwe juu yake- Alikuwa na watoto saba wakiume wa
tatu na wakike wa nne:
1/Qasim. 2/Abdullahi.
3/Ibrahim. 4/Zainabu.
5/Ruqayyah. 6/Ummu kulthum. 7/Faatwima.
Na wanasema kwamba: Hassan bin Ally-radhi za Allah
ziwe juu yao- yeye ndie Aliwadhalilisha Waumini kwa
sababu Alimbaayii (Alimpa kiapo cha utiifu)
Muawiya-radhi za Allah ziwaendee.
Angalia kitabu: (Rijaalul-kashy).
cha Alkashy. ukurasa (103).
صفحة 15
KUWAKUFURISHA KWAO MAMA WA WAUMINI: BI AISHA NA BI HAFSWA
Mashia wanasema: Hakika Mke wa Mtume anaweza
akawa ni Kafiri kama alivyokuwa Mke wa Nabii Nuhu
na Mke wa Nabii Lutwi. Wanamkusudia katika kusema
hivyo Mke wa Mtume-rehma na amani za Allah ziwe juu
yake- Bibi Aisha Allah amuwie radhi.
Angalia kitabu: (Hadiithul-ifki)
cha Jaafar Murtadhwa. Ukurasa (17).
Na wanasema kwamba: Bibi Aisha Allah amuwie radhi
Aliritadi Baada ya kufa Mtume-rehma na amani za Allah
ziwe juu yake- kama walivyo ritadi wengi miongoni
mwa Maswahaba.
Angalia kitabu:
(Ash-shihaabuthaaqib Fii bayaani maanan-naaswib).
cha Yusuf al-bahraany ukurasa (236).
Na wanasema kwamba: Bibi Aisha-radhi za Allah ziwe
juu yake- Alikusanya Dinari (40) kutokana na khiyana na
Akazigawa kwa watu wenye kumchukia Ally -radhi za
Allah ziwe juu yake-!.
Angalia kitabu: (Mashaariqu anwaaril-yaqiin).
cha Rajab Albisry. ukurasa (86).
Na wanasema kuwa: Bibi Aisha-radhi za Allah ziwe juu yake- Alifanya Faahisha (Zina) na kwamba kauli ya Allah katika suratin-nuur aya (26) Aliposema: {Hao ni wenye kutakaswa na hayo wayasemayo} wakasema: aya
صفحة 16
hii Imekuja kumtakasa Mtume-rehma na amani za Allah
ziwe juu yake- kutokana na Zina na sio Bibi Aisha.
Angalia kitabu: (Aswiraatul-mustaqiim).
cha Zainud-diin An-nabatwi Albayaadhwi. (3/165).
Na wanasema kwamba: Bibi Hafsa-radhi za Allah ziwe juu yake- Alikufuru kwa kauli yake alipo Muuliza Mtume: {Nani kakupa habarihizi}?. Kama ilivyo kuja katika suratu Tahrim aya (3). Na ndipo Allah Akateremsha kuhusu yeye pamoja na Bibi Aisha kauli yake: {Ikiwa Mtatubia kwa Allah bila shaka nyoyo zenu zimekwisha elekea huko}. suratu Tahrim aya (4).
Wanasema: Neno: (Zaaghat) lina maana ya Ukafiri. Na wanadai kuwa Bibi Aisha pamoja na Hafsa walikubaliana kumnywesha Sumu Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- na pindi Allah alipo Mueleza Mtume wake njama zao akataka kuwauwa ndipo wakamuapia kuwa Hawakufanya hivyo na ndipo Allah akateremsha ayah ii: {Enyi mlio Kufuru Msitake Udhuru leo hii… } suratu Tahrim aya (7). Angalia kitabu: (Aswiraatul-mustaqiim). cha Zainud-diin An-nabatwi Albayaadhwi (3/168).
KUCHUPA KWAO MIPAKA KWA ALLY-RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE.
Wanasema: Hakika Allah Alimsemesha Mtume wake -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Usiku wa Miiraji kwa Lugha ya Ally bin Abi Twalib.
صفحة 17
Angalia kitabu:
(kashful-yaqiin Fii Fadhwaaili Amiiril-muuminiin). cha
Hasan bin Yusuf bin Al-mut-har Alhuly. ukurasa (229).
Na wanasema kuwa: Allah Alimsemesha Ally bin abi
Twalib katika Mji wa Twaifu Akiwa pamoja na Jibril.
Angalia kitabu: (Baswaairud-darajaat).
cha Swaffaar. (8/230).
Na wanasema: Hakika Ally bin abi Twalib -radhi za
Allah ziwe juu yake- Ndiye Mwenye kugawa Pepo na
Moto!! Atawaingiza watu wa Peponi Peponi na watu wa
Motoni Motoni!!!.
Angalia kitabu: (Baswaairud-darajaat).
cha Swaffaar). (8/235).
Na wanasema: Hakika Allah Atamuingiza Peponi
Mwenye kumtii Ally hatakama atamuasi Allah! Na Allah
atamuingiza Motoni Mwenye kumuasi Ally hatakama
atamtii Allah!.
Angalia kitabu:
(Kashful-yaqiin Fii Fadhwaaili Amiiril-muuminina).
Cha Hasan bin Yusuf Al-mut-har al-huly. Ukurasa (8).
Na wanasema: Hakika Ally bin Abi Twalib -radhi za
Allah ziwe juu yake- Ndie siri ya Manabii na kwamba
Allah Alimwambia Mtume wake: {Ewe Muhammadi
hakika nilimtuma Ally pamoja na Mitume wengine kwa
siri na nimemtuma pamoja Nawe kwa Dhahiri".
Angalia kitabu: (Al-asraarul-alawiyya).
Cha Muhammad Al-mas-uudy. Ukurasa (181).
صفحة 18
Na wanasema kwamba: Ally -radhi za Allah ziwe juu
yake- ni Alama na Dalili ya Muhammadi na
Muhammadi-rehma na amini za Allah ziwe juu yake-
Alilingania juu ya Utawala wa Ally.
Angalia kitabu: (Baswaairud-darajaat).
cha Swaffaar. Ukurasa (91).
Na wanasema kwamba: Allah hakuwahi kumtuma
Mtume yeyote Ispokuwa Alimtaka kuutambua Utawala
wa Ally kwa kupenda au kwa kukarahishwa.
Angalia kitabu: (Al-asraarul-alawiyya).
Cha Muhammad Al-mas-uud. Ukurasa (190).
Na wanasema kuwa: Hakika Dini ya Mtu haikamiliki
ispokuwa kwa kuutambua Utawala wa Amirilmuuminina
Ally bin Abi Twalib.
Angalia kitabu: (Al-ihtijaaj). Cha Attwabrasy. (1/57).
Na wanasema: Hakika Mtume -rehma na amani za
Allah ziwe juu yake- Alisema: "Sikilizeni Jibril Alinijia
akanambia: {Ewe Muhammadi Mola wako anakuamrisha
Umpende Ally bin Abi Twalib na Anakuamrisha
Kuutambua Utawala wake}.
Angalia kitabu: (Baswaairud-darajaat).
cha Swaffaar. Ukurasa (92).
Na wanasema: Ally bin Abi Twalib Ataingia Peponi
kabla ya Muhammadi -rehma na amani za Allah ziwe juu
yake-Angalia kitabu: (Ilalush-sharaai).
Cha Ibnu Baabawayhi Alqummy. Ukurasa (205).
صفحة 19
Na wanasema kuwa: Radi ni katika Amri ya kipenzi
chenu alipo ulizwa Msemaji nani kipenzi chetu?
Akasema: Amiril muuminina Ally bin abi Twalib.
Angalia kitabu: (Al-ikhtiswaas).
Cha Almufiid. Ukurasa (327).
Wanasema kuwa: Ally bin abi Twalib -radhi za Allah
ziwe juu yake- Anauwezo wa Kufufua na Kuondoa
Matatizo kwa wenye Matatizo.
Angalia kitabu: (Uyuunul-muujizaati).
Cha Husein Abdul-wahaab. Ukurasa (150).
Na Risala (Halaalul-mashaakil).
Na wanasema: Hatoingia Peponi yeyote ispokuwa kwa
Idhni ya Ally bin abi Twalib.
Angalia kitabu: (Manaaqibu Amiril-muuminina).
Cha ally bin Maghaazily. Ukurasa (93).
Na wanasema kuwa: kila Mwenye kum-khaalifu Ally
basi huyo ni Kafiri na kila Mwenye kumfadhilisha
Yeyote juu yake basi huyo anakuwa Karitadi.
Angalia kitabu:
(Bishaaratul- mustwafaa lishiiatil- murtadhwaa). (2/79).
Na wanasema kuwa: Mwenyezi Mungu Alijifakharisha
Mbele ya Malaika wake kwa ajili ya Ally bin abi Twalib.
Angalia kitabu:
(Bishaaratul- mustwafaa lishiiatil- murtadhwaa). (1/66).
Wanasema: Manabii wote na Mitume walitumwa hali yakuwa wameamrishwa kukiri Utawala wa Ally bin abi Twalib.
صفحة 20
Angalia kitabu: (Al-maalimuz-zulfaa).
Cha Shekh wao Haashimul-bahraany. Ukurasa (303).
Na wanasema: Ally bin abi Twaalib -radhi za Allah
ziwe juu yake- Aliashiria kwa mkono wake Angani mara
likatanda Wingu na Mawingu yakapandana kisha
yakamtolea Salamu kisha Ally Akamwambia Ammar:
Panda Pamoja nami na Useme:
"Bismillahi Majreeha wamursaahaa".
Kama ilivyo kuja katika suurat Huud aya (41).
Ammar Akapanda kisha wakatoweka machoni kwetu.
Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar). Cha Almajlisy.
Na wanasema kuwa: Mbwa Aliwang`ata Maswahaba
wawili kwa ajili ya kumlipizia kisasi Ally bin abi
Twaalib na kwamba Punda Alishuhudia kuwa Ally ni
Walii wa Allah na ndie aliepewa wasia wa utawala baada
ya Mtume - rehma na amani za Allah ziwe juu yake-.
Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar).
Cha Almajlisy. (41/247). Na (17/306).
KUCHUPA KWAO MIPAKA KWA FAATWIMA RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE
Wanasema kama: Fatwima na Hassan na Husein na wengine miongoni mwa kizazi cha Husein, ni maasuumin (Hawakosei).
صفحة 21
Angalia kitabu:
(Aqaaidul-imaamiyya).
Cha Muhammad ridhwaa. Ukurasa (89) na (98).
Na wanasema: Lau kama sio Ally basi Muhammadrehma
na amani za Allah ziwe juu yake- asingeumbwa,
na lau kama sio Fatwima basi nisingelikuumbeni.
Angalia kitabu:
(Al-asraarul-faatwimiyya).
Cha Muhammad almas-uudy. Ukurasa (98).
Na wanasema: Hakika Faatwima ni sehemu ya Uungu!
Utukufu wangu nimeudhihirisha katika umbile la
Mwanamke.
Angalia kitabu:
(Al-asraarul-faatwimiyya).
Cha Muhammad Almas-uudy. Ukurasa (355).
Na wanasema kuwa: Faatwima alikuwa akiongea na
Mama yake huku akiwa tumboni mwake.
Angalia kitabu:
(faatwimatu zahraa minal-mahdi ilal-lahdi).
Cha Muhammad alqaz-wiiny. Ukurasa (38).
KUWAFADHILISHA KWAO MAIMAMU WAO JUU YA MANABII PAMOJA NA KUCHUPA KWAO MIPAKA
Mashia wanasemakuwa: Hakika Maimamu wa Shia ithna asharia ni bora kuliko Manabii na Mitume -rehma
صفحة 22
na amani za Allah ziwe juu yao-.
Angalia kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyya).
Cha Niimatullahi aljazaairy. (3/308).
Na wanasema: Hakika Maimamu wa Shia wana Elimu
ya yaliyo kuwepo na yatakayo kuwepo na kwamba
hakifichikani kwao kitu chochote (yaani wanajua ghaibu)
na kwamba wao hawafi ispokuwa kwa kutaka kwao.
Angalia kitabu: (Usuulul-kaafy).
Cha Alkulayny. (1/258-260).
Na wanasema: Hakika Imamu katika Maimamu wao
anayo Daraja yenye kusifiwa mbele ya Allah na anao
utawala ambao unanyenyekewa na kila kitu hapa
Ulimwenguni.
Angalia kitabu: (Tahrirul-wasiila).
Cha Al-khumainiy. Ukurasa (52).
Na wanasema: Hakika Maimamu wao Kumi na mbili
wanao Utawala usio kuwa kwa viumbe wote na kwamba
utawala huo ni sawa na utawala wa Allah kwa viumbe
wake.
Angalia kitabu: (Misbaahul-fuqaaha). -
Cha Abul-qaasim al-khuui. (5/33).
Na wanasema: Hakika sisi kwa Allah tunazo hali (yaani
Maimamu wao kumi na mbili) hali ambazo hazipati
yeyote si Malaika alie karibu wala Mtume alie tumwa.
Angalia kitabu: (Tahrirul-wasiila).
Cha Al-khumainiy. Ukurasa (94).
صفحة 23
Na wanasema: Hakika Maimamu kumi na mbili Hakuna
Pingamizi kabisa kuwa Mambo ya Ulimwengu yanaenda
kwa Idhini yao na kuwa wanaipitisha lailatul-qadri na
mengineyo na Hakuna Pingamizi kabisa kuwa jambo hili
limethibiti.
Angalia kitabu: (Al-burhaanul-qaatwii).
Ambacho ni mkusanyiko wa majibu na mambo ya
kiitikadi na sheria.
cha shekh wao: Muhammad taqiyyul-bahjat.
Ukurasa (41).
Na wanasema: Hakika mawaswii (Yaani Maimamu
kumi na mbili wa kishia) Wanabebwa tumboni na
wanatoka kwenye mapaja lakini hawaguswi na Uchafu
(wakati wa kuzaliwa).
Angalia kitabu: (Madiinatul-maajiz).
cha Haashimul-bahrany. (8/22).
Na wanasema: Hakika Allah na Malaika wake na
Mitume wake pamoja na Waumini huwa wana zuru
kaburi la Ally bin Abi Twalib.
Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy).
Cha Alkulayny. (4/580).
Na wanasema: Imamu ni kama Nabii ni lazima awe kaepushwa na mambo yote machafu ya dhahiri na ya siri tangu utotoni mwake mpaka kufa kwake ya kufanya kwa kukusudia au hata kwa kusahau kwa kuwa Maimamu ndio wenye kuihifadhi sheria na wenye kuisimamia halizao katika hili ni kama hali ya Mitume. Angalia kitabu:
صفحة 24
(Aqaaidul-imaamiyya).
Cha shekh wao: Ibrahim zanjaany. (3/179).
Na wanasema: Malaika wameumbwa ili kuwa
watumishi wa Ahlul-baiti.
Angalia kitabu:
(Bihaarul-anwaar).
Cha Almajlisy. (26/335).
KUWAKUFURISHA KWAO MASWAHABA WOTE ISPOKUWA WATATU TU MIONGONI MWAO
Mashia wanasema: Maswahaba wote watukufu
Wamekufuru na Kuritadi kiongozi wa kuritadi alikuwa ni
Abubakari na Omari na Othman na Khalid bin waliid na
Muawiya bin Abi Sufyaan na Mughiirat bin Shuubah -
radhi za Allah ziwe juu yao-
Ispokuwa watatu tu katika Maswahaba.
Angalia kitabu:
(Ar-raudhwatu minal-kaafy).
Cha Alkulayny. (8/245).
CHUKI ZAO JUU YA ABUBAKARI NA OMARI NA OTHMANI –RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAO
Mashia wanasema: Na imani yetu katika kuwatenga nikwamba tunajitenga mbali na Masanamu wanne: Abubakri na Omari na Othmani na Muawiya pamoja na
صفحة 25
wanawake wanne: Aisha na Hafswa na Hindu na
Ummul-hakam (Dada yake na Muawiya) na tunajitenga
mbali kabisa na wafuasi wao wote na tunaitakidi kuwa
wao ni viumbe waovu kabisa miongoni mwa viumbe wa
Allah juu yamgongo wa Ardhi na tunaamini kwamba
haiwezi kutimia imani ya mtu kumuamini Allah na
Mtume wake na Maimamu ispokuwa kwa kujiweka
mbali kabisa na maadui zao.
Angalia kitabu:
(Haqqul-yaqiin).
Cha Almajlisy. Ukurasa (519).
Na wanasema: Hakika Abubakari na Omari ni Makafiri,
na kila Mwenye kuwapenda naye ni Kafiri.
Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar).
Cha Almajlisy. (69/137-138).
Na wanasema: Abubakari na Omari wamelaaniwa na
wamekufa wakiwa ni makafiri, nani wenye
kumshirikisha Mwenyezi Mungu mtukufu.
Angalia kitabu: (Baswaairud-darajaat).
Cha As-swaffaar. (8/245).
Na wanasema: Sababu iliyompelekea Mtume -rehma na
amani za Allah ziwe juu yake- kwenda na Abubakari
Pangoni ilikuwa ni kuchelea asije kuwafahamisha
Makafiri wa Kikuraishi Mahala alipo.
Angalia kitabu: (Tafsiirul-burhaani).
Cha Haashimul-bahraany. (2/127).
صفحة 26
Na wanasema kwamba: Abubakari alikuwa akiswali
nyuma ya Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu
yake- hali yakuwa Kaning'iniza Sanamu Shingoni
mwake kisha analisujudia.
Angalia kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyyah).
Cha Niimatullahil-jazaairy. (1/53).
Na wanasema: Omari alikuwa na Maradhi ambayo tiba
yake ni Maji ya Wanamume (Yaani Mpaka Aingiliwe
nyuma)! Na kwamba Bibi yake ni Motto wa zinaa.
Angalia kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyyah).
Cha Niimatullahil-jazaairy). (1/63).
Na kitabu: (Aswiraatul-mustaqiim).
Cha Zainud-din annabatwy albayadhwy. (3/28).
Na wanasema: Tunaitukuza siku ya Tairuuz nisiku
ambayo Majusi huitukuza (Baniani) na kuisheherekea
siku aliyo uwawa Omari bin Khatwaab -radhi za Allah
ziwe juu yake- na wana Mwita alie Muuwa Omari kuwa
ni (Baba shujaa wa dini) na wanahimiza kulizuru kaburi
lake kutokana na kazi kubwa aliyo ifanya ya kumuuwa
Omari -radhi za Allah ziwe juu yake.
Angalia kitabu: (Aqdu durar Fii Baqri Batnu Omar).
Cha Yaasin As-swawaaf. Ukurasa (120).
Na wanasema: Kusoma dua ya kuwalaani Masanamu wawili wa Kiquraishi (Abubakari na Omari) ni katika Ibada tukufu za kujikurubisha nazo kwa Allah, na wamemwita abubakari na omari kuwa ni Aljibti na Twaaghuuti (Jibti ni Uchawi Twaaghuti ni Shetani).
صفحة 27
Angalia kitabu: (Ihqaaqul-haqq).
Cha Al-mar-ashy. (1/337).
Na wanasema kwamba: Mahdi wao wauongo
atamfufua Abubakari na Omari, Awasulubu na kisha
kuwachoma Moto kisha Amfufue Bibi Aisha -radhi za
Allah ziwe juu yake- na Amsimamishie Hadd.
(Adhabu kwa Sababu ya zinaa).
Angalia kitabu: (Ar-raj-a).
cha Ahmad al-ahsaani. Ukurasa (1116) na (161).
Na wanasema: Hakika Othmani -radhi za Allah ziwe juu
yake- Alikuwa ni Mzinifu na Khanithi na alikuwa ni
Mpiga Dufu.
Angalia kitabu: (As-siraatul-mustaqiim).
Cha Zainud-diin annabtwy albyaadhwy. (3/30).
KUHUSU MAHDI WAO WA KUZUA NA KAULI ZAO JUU YA KUREJEA KWAKE
Na Wanasema kuwa: Jibril na Miikaail na Kursy na
Lauhil-mahfuudh na Kalamu vyote hivi ni vyenye
kudhalilika na kumnyenyekea Mahdi wa kishia, sababu
sifayake ni Saffah (M-mwagaji damu).
Angalia kitabu: (Aqaaidul-imaamiyya).
Cha Muhammad ridhwaa midhfar. Ukurasa (102).
Na wanasema Kuwa: kiwiliwili cha Mahdi wa kishia ni kiwiliwili cha Israaili. (Chaguo la Mungu). Angalia kitabu:
صفحة 28
(Al-imaamul-mahdy minal wilaadati iladh-dhuhuur).
Cha Muhammad qazwiiny. Ukurasa (53).
Na wanasema kuwa: Mahdi wa Mashia atakuja na Amri
Mpya na Kitabu Kipya na Hukumu Mpya na Atakuwa ni
Mkali sana kwa Waarabu hatokuwa na uamuzi juu yao
zaidi ya Upanga tu Hatampa Nafasi yeyote ya kutubia
wala hato'ogopa lawama ya mwenye kulaumu kwaajili ya
Allah.
Angalia kitabu:
(Al-ghaibah).
Cha Muhammad an-nuuman. Ukurasa (154).
Na wanasema: Pindi atakapo kuja Mahdi hakutakuwa
kitu kati yake na Waarabu na Maquraishi, ispokuwa
Upanga tu.
Angalia kitabu:
(Al-ghaibah).
Cha Muhammad an-nuuman. Ukurasa (154).
Na wanasema: Haikubakia baina yetu na Waarabu
ispokuwa Kuchinjana kisha msemaji akaashiria Shingoni
mwake.
Angalia kitabu: (Al-ghaibah).
Cha Muhammad an-nuuman. Ukurasa (155).
Na wanasema kwamba: Mahdi wao atakapo kuja Atauvunja Muskiti wa Makkah na Muskiti wa Madina na Atahukumu kwa Sheria ya watu wa Daawud na Atamsemesha Allah kwa jina lake la Kiebrania sihivyo tu bali Atauwa Theluthi mbili ya watu wa Ardhini.
صفحة 29
Angalia kitabu:
(Biharul-anwaar). Cha Al-majlisy.(52/338).
Na kitabu: (Uswuulul-kaafy). Cha Al-kulainy. (1/397).
Na kitabu: (Alghaibah).
Cha Annuumaany. Ukurasa (326).
Na kitabu: (Arraj'a).
cha Ahmad al-ahsaai. Ukurasa (51).
Na wanasema: Jihadi haifai wala hairuhusiwi mpaka atakapo kuja Mahdi wao wakudai kutoka katika Pango lake. Angalia kitabu: (Wasaailush-shia). Cha Al-hurr al-aamily. (11/37).
KUCHUPA KWAO MIPAKA KULIKO KUBAYA KATIKA IBADA ZA MAKABURI
Mashia wanasema kuwa: Kulizuru kaburi la husein bin
Ally ni bora kuliko kwenda Kuhiji Makkah si hivyo tu
bali wanasema kuwa wanao kwenda kumzuru Husein ni
watakasifu ama wanao kuwa katika Mauqifu (Arafa)
katika Hijja ni Watoto wa Zinaa.
Angalia kitabu:
(Biharul-anwaar). Cha Al-majlisy. (98/85).
Na wanasema: Hakika kulizuru kaburi la Husein bin Ally-radhi za Allah ziwe juu yake- Nisawa na kufanya Hijja Milioni mbili (2,000,000) na Umra Milioni mbili (2,000,000) na kupigana Jihadi Milioni mbili (2,000,000) na Thawabu za kila Hijja na Umra na Jihadi ni sawa na Thawabu za Aliye Hijji na akafanya Umra na akapigana
صفحة 30
Jihadi Pamoja na Mtume -rehma na amani za Allah ziwe
juu yake- Pamoja na Maimamu waongofu.
Angalia kitabu:
(Nuurul-ayni fil-mashyi ilaa ziyaarati qabril-husaini).
Cha Muhammad al-istwihbaanaaty.
Ukurasa (265).
Na wanasema kwamba: Karbalaa (Alipo zikwa
Husaini) ni Ardhi takatifu katika Uislamu na ina Utukufu
kushinda Makkah na Madina na kuliko hata Baitulmaqdis.
(Muskiti wa palestina).
Angalia kitabu:
(Misbaahul-jinaani).
Cha shekh wao Abbaas al-kaashaany.
Ukurasa (360).
Na wanasema kuwa: Kula Udongo ulipo katika Kaburi
la Husein -radhi za Allah ziwe juu yake- ni Shifaa
(Dawa) ya kila Ugonjwa.
Angalia kitabu:
(Almizaar)
cha Shekh wao Almufiid.
Ukurasa (125).
Pia wanasema kwa uongo na uzushi kuwa: Abu abdillahi (Jaafar As-swaadiq) -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Amesema: Wallahi laiti kama ninge kusimulieni juu ya Fadhila za kulizuru kaburi la Husein na juu ya ubora wa kaburi lake basi mgeliacha kufanya Hijja moja kwa moja na hakuna yeyote miongoni Mwenu ambaye ange fanya Hijja, olewako! Hivi hujuwi kama
صفحة 31
Allah kaifanya Ardhi ya Karbalaa (Aliko zikwa Husein)
kuwa ni Haram (Sehemu takatifu) yenye amani na yenye
kubarikiwa kabla ya kuifanya Makkah kuwa ni
Haramu?!.
Angalia kitabu: (Kaamiluz-ziyaaraat).
Cha shekh wao Ibnu quuluwayhil-qummy.
Ukurasa (449).
Na wanasema: Hakika kuswali katika Mashaahid zao
(Makaburi) ni bora kuliko kuswali Miskitini bali
wanasema: swala katika Msikiti wa Ally bin Abi Twalib
malipo yake ni makubwa kuliko kuswali katika Msikiti
Mtakatifu wa Makkah.!!
Angalia kitabu: (Manhajus-swaalihiina).
Cha Shekh wao Ally as-sistaany. (1/187).
Na wanasema kuwa: Hakika Sikukuu kubwa katika Uislamu sio Eidul-fitri wala Eidul-adhwhaa bali ni Eidi ya (Ghadiir) Eidi ya kizushi wala haina asili katika Uislamu. Angalia kitabu: (Eidul-ghadiir). Cha Shekh wao Muhammad ash-shiiraazy. Ukurasa (11). *Ghadiir: Ni sehemu Baina ya Makkah na Madina sehemu ambayo Mtume alimsifu Ally…
KUWAPENDA KWAO MAKAFIRI NA KHIYANA ZAO NA UDANGANYIFU WAO
Mashia wanasema: Na miongoli mwa makosa waliyo yafanya watu wa Kuufa, nikwamba wao walimchoma choma Visu Hassan bin Ally na wakamuuwa Husein -
صفحة 32
radhi za Allah ziwe juu yao- Baada ya kuwa walimwita.
Angalia kitabu: (Taariikhul-kuufa). Ukurasa (113).
Na wanasema: Hakika Husein Alisema: Ewe Mwenyezi
Mungu nakuomba Uhukumu Baina yetu na baina ya
watu walio Tuita ili watunusuru waka Tuuwa.
Angalia kitabu: (Muntahal-aamaal). (1/535).
Na wanasema: Husein alisema: Hakika watu hawa
wamenihofisha (Yaani mashia wa kuufa -iraqi) Nahizi
hapa Barua za watu wa kuufa nao ni wenye Kuniuwa.
Angalia kitabu: (Maqtalul-husaini).
Cha Abdurrazzaaq almuqrim. Ukurasa (175).
Na wanasema kwamba: Ally bin Husein -rehma na
amani za Allah ziwe juu yake- Aliwaona watu wa Kuufa
Wakiomboleza na Kulia, Akawaambia: Mnaomboleza na
Kulia kwa Ajili Yetu! Ni nani Aliye Tuuwa??(Bila kua
nyinyi).Angalia kitabu: (Nafsul-mahmuum).
Cha Abasi al-qummy. Ukurasa (357).
Na wanasema: kisha wakampa Husein Baia (Utawala)
katika watu wa Iraq, watu elfu ishirini (20,000) kisha
wakamtelekeza na wakamtokea pamoja na viapo vyao,
vya utiifu wakamuuwa. Angalia kitabu:
(Aa'yanush-shia). Cha Muhsinul-amiin. (1/32).
Na wanasema: Niwaajibu kuwanusuru Maaduwi wanao Shambulia Dola (Nchi) ya Kiislamu nakuto waziwiya Makafiri wanao Washambulia Waislamu. Angalia: Fat'wa Aliyoitowa kiongozi wao Mkubwa: As-sistaany.
صفحة 33
Tarehe: (4/3/2003). Baada ya Marekani kuishambulia
Iraq. Na kutilia Mkazo jambo hilo Anasema shekh wao
Swaadiq Ash-shiirazy, Anaye ishi Irani:
Nilazima kusaidiana Na Marekani katika kuangusha
Utawala wa Iraq.
Angalia: (Jariidatul-watwaniyya al-kuwaitiyya-al jumua)
(27/9/2002).
Na wanasema: Hakika Muislamu yeyote Mwenye
kupigana Jihadi dhidi ya Makafiri basi Anahesabiwa ni
Muuwaji Hapa Duniani na Akhera.
Hakuna anaekufa Shahidi Ispokuwa Shia Imaamiyya,
Hata akifia kitandani kwake.
Angalia kitabu: (Tahdhiibul-ahkaam).
Cha Atwuusy. (6/98).
KUICHUKIA KWAO MAKKAH NA MADINA
Mashia wanasema: Hakika watu wa Makkah wanamkufuru Mwenyezi Mungu wazi wazi, na watu wa Madina niwaovu kuliko watu wa Makkah, niwaovu zaidi yao mara sabini (70). Angalia kitabu: (Usuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (2/410).
CHUKI ZAO KWA MISRI NA SHAM
Wanasema kuwa: Watu wa Misri wamelaaniwa kwa Ulimi wa Daaud, na miongoni mwao wamegeuzwa kuwa
صفحة 34
Manyani na Nguruwe.
Na wanasema kuwa: Allah hakupata kuwakasirikia
wana wa Izraail ispokuwa aliwaingiza (Misri) na pindi
alipokuwa Radhi nao basi aliwatoa humo.
Na wanasema kwamba: Abu Jaafar Imamu wao
ambaye wanasema ni Maasuumu (Hafanyi dhambi)
Alisema: Hakika Mimi nachukia kula kitu chochote
kilicho pikwa katika vyungu vya Misri, wala sipendi
kuosha kichwa changu kutokana na Udongo wake, usije
kuniambukiza Udhalili na kuniondolea Ghera (wivu)
wangu, Jitengeni na Misri wala msitamani kuishi humo.
Pia nadhani alisema: kuishi katika nchi hiyo
kunamrithisha mtu tabia ya Udayuthi (kuridhia maasi).
Angalia kitabu: (Tafsiirul-qummy). Cha Alqummy.
(2/241). Na kitabu: (Tafsiirul-bur-haan).
Cha Hashimul-bahraany. (1/456).
Na kitabu: (Furuu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (6/501)
Na kitabu: (Bihaarul-anwaar). Cha Almajlisy. (60/211).
Na wanasema: Bora ya Ardhi ni ardhi ya Sham, na watu wa baya ni watu wa Sham. na watu wa Roma walikufuru lakini hawakutufanyia Uaduwi, lakini watu wa Sham walikufuru na wakatufanyia Uaduwi, na wala msiseme: sisi niwatu wa Sham lakini semeni sisi niwatu wa sehemu mbaya. Angalia kitabu: (Tafsiirul-bur-haan). Cha Hashimul-bahraany. (1/456). Na kitabu: (Usuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (2/410). Na kitabu: (Tafsiirul-qummy). Cha Alqummy. (2/241).
صفحة 35
ULAJI WAO WA KHUMUS (MOJA YA TANO) KWA VIGOGO WAO WAVAAJI WA VIREMBA VIKUBWA
Mashia wanasema kuwa: Mali ya Khumus,
(mali ikigawiwa mafungo matano fungo moja ndio
linaitwa khumus) Ambayo ni maalumu kwa watu wa
Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yaowanapaswa
kuichukuwa watu wa Viremba (vigogo wao)
kwa hoja kwamba wao wanasimamia nafasi ya Imamu
wao aliye jificha kwenye Pango.
Angalia kitabu: (Wasaailush-shia).
Cha Alhurrul-aamily. (6/383).
WANADAI KUJIPIGA MAKOFI NA KUJICHOMA VISU NI MIONGONI MWA MAMBO YA KUJIKURUBISHA
Mashia wanadai kuwa: Kujipiga piga Makofi na Kujichoma visu na kuvaa mavazi Meusi siku ya Ashura na kuomboleza ni miongoni mwa mambo Makubwa ya kujikurubisha kwa ajili ya Husain -radhi za Allah ziwe juu yake- na kwamba matendo hayo ni katika matendo mazuri. Angalia fataawa za Muhammad kaashif Alghitwaa, na Ar-rauhany, na At-tabrizy. na rejea nyingi miongoni mwa rejea za al-imaamiyyah.
KUHIMIZA KWAO MUT'A NA KUSTAREHE NA WANAWAKE MAKAHABA
صفحة 36
Mashia wanasema: Mtu anaweza kuowa (kwa ndoa ya
Mut'a) mpaka mara Elfu moja, (1000) kwa sababu
Mwanamke wa Mut'a hapewi Talaka wala hana Mirathi,
bali anahesabiwa ni Mwenye kukodiwa tu.
Angalia kitabu: (Al-istibswaar).
Cha Abii Jaafari atwuusy. (3/155).
Na wanasema: Hakika Mtoto aliye zaliwa katika Mut'a
ni bora kuliko aliye zaliwa katika Ndoa ya kudumu.
Angalia kitabu: (Manhajus-swaadiqiin).
Cha Almulla fat-hullah al-kaashaany. Ukurasa (356).
Na wanasema kuwa: Inajuzu kufanya Mut'a na
Wanawake wazinifu na ambao ni maarufu kwa
(Uchangudoa-Ukahaba) bali wanadai kuwa
kumepokelewa Mahimizo juu ya jambo hilo.!
Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar).
Cha Almajlisy. (100/319-320).
Na wanasema kwamba: Mwanamke wa kufanya nae
Mut'a Haesabiwi katika Ile idadi ya Wanawake Wanne,
kwa sababu yeye Haachwi kwa kupewa Talaka wala
hana haki ya Mirathi, bali yeye ni Mwenye kukodiwa tu.
Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy).
Cha Alkulainy. (5/415).
Na wanasema: Inajuzu kufanya Mut'a na Wanawake Warembo hata kama watakuwa Wameolewa, au hatakama ni Wazinifu. Angalia kitabu:
صفحة 37
(Alfuruu minal-kaafy).
Cha Alkulainy. (5/462).
Na wanasema kuwa: Uchache wa muda wa Mut'a ni
kustarehe na Mwanamke mara moja tu.
Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy).
Cha Alkulainy. (5/460).
Na wanasema kwamba: Inajuzu kufanya Mut'a na
Mwanamke Mzinifu hata kwa Kumlazimisha hasa akiwa
ni miongoni mwa Wanawake Maarufu kwa Ukahaba.
Angalia kitabu: (Tahriirul-wasiilah).
Cha Khumainy. (2/256).
TAQIYYA NA KUSEMA UONGO NI KATIKA ASILI YA MADHEHEBU YAO
Mashia wanasema: Inajuzu kutumia Taqiyya na maana
yake ni: (Mtu kudhihirisha mambo ambayo ni kinyume
na vile anavyo itakidi moyoni) au kama alivyo eleza
mmoja wa wanachuoni wao kwamba taqiyya nikusema
au kufanya kinyume na unavyo itakidi kwa lengo la
kujiondolea madhara au kulinda heshima yako.
Angalia kitabu: (Ash-shiatu fil-miizaan).
Cha Muhammad Jawaadu Maghniyah. Ukurasa (48).
Na wanasemakuwa: Sehemu kubwa ya Dini ni Taqiyya,
wala hana Dini asie kuwa na Taqiyya.
Angalia kitabu:
(Uswuulul-kaafy).
Cha Alkulainy. (2/217).
صفحة 38
Na wanasema: Hakika Nyinyi mko katika Dini ambayo
Mwenye kuificha basi atampa utukufu na Mwenye
kuiweka wazi basi Mwenyezi Mungu Atamdhalilisha.
Angalia kitabu:
(Uswuulul-kaafy).
Cha Alkulainy. (2/222).
Na wanasema: Hakika Husein Alikuwa akinyonya kidole cha Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- kiasi cha kumtosha siku mbili mpaka tatu. Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (1/465).
KUWAKUFURISHA KWAO WAISLAMU PAMOJA NA CHUKI ZAO KUBWA JUU YA WAISLAMU
Mashia wanasema kuwa: Hakuna yeyote aliyopo katika
Mila ya Kiislamu zaidi yetu (Yaani Maimamu wa Ithna
Ashariyya Pamoja na Wafuasi wao miongoni mwa Shia
Imaamiyya).
Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy).
Cha Alkulainy. (1/223-224).
Na wanasema kwamba: Mahdi wao Atarejea ili aje
kuwalipizia kisasi Mashia kutoka kwa Maaduwi zao
ambao ni Waislamu, ama Mayahudi na Wakristo wao
Atafanya nao Suluhu na kuwasalimisha.
Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar).
Cha Almajlisy. (52/376).
صفحة 39
Na wanasema kuwa: Mwenye kuturudi Sisi ni sawa na
Mwenye kumrudi Allah, na anakuwa ni sawa na aliye
mshirikisha Allah.
Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy).
Cha Alkulainy. (1/67).
Na wanasema kuwa: Watu wote ni Watoto wa Zinaa
Ispokuwa Mashia tu.
Angalia kitabu: (Arraudhwatu minal-kaafy).
Cha Alkulainy. (8/285).
Na wanasema: Hakika Mtoto yeyote anapo zaliwa Ibilisi
miongoni mwa Maibilisi huwa anahudhuria kuzaliwa
kwake, Pindi anapojuwa kuwa Mwenye kuzaliwa ni
Miongoni Mwetu, Basi huwa anamkinga kutokana na
Shetani, na kama atakuwa mwenye kuzaliwa sio katika
sisi basi Shetani humuingiza kidole Matakoni mwake
akiwa ni kijana. na kwa ajili hiyo anakuwa ni Mwenye
kuziniwa!!!, Na akiwa ni wakike basi hutia kidole chake
katika Utupu wake (Sehemu ya siri ya mbele)!!! Na kwa
ajili hiyo anakuwa ni Muovu.
Angalia kitabu: (Tafsiirul-ayaashy).
Cha Muhammad al-ayaashy. (2/218).
Na wanasema kwamba: Hakika yeyote ambaye sio
katika Shia ithna asharia, au asiye muamini hata mmoja
miongoni mwa Maimamu kumi na mbili, au
akamkanusha hata mmoja wao, basi huyo ni Kafiri, na
Akhera mafikio yake ni Motoni.
Angalia kitabu: (Jaamiu ahaadiithi shia).
Cha Alburuujirdy. (1/429).
صفحة 40
Na wanasema: Hakika habari zinafidisha juu ya hukumu ya Ukafiri na Ushirikina huko Akhera kwa kila ambaye sio katika Shia ithna asharia. Angalia kitabu: (Tanqiihul-maqaal). Cha Abdallah Almaamaqany. (1/208).
CHUKI ZAO KWA AHLUS-SUNNA ZIMEPITA KIWANGO
Mashia wanasema: Hakika Naaswib (yaani Muislamu)
damu yake ni halali, lakini mimi nakuepushia shari,
ikiwa utaweza kumuangushia Ukuta, au Kumzamisha
kwenye Maji, ili asije kukutolea ushahidi basi fanya
hivyo, akauliza muulizaji: na vipi Mali yake? Akasema:
Ichukuwe, ikiwa kama kuna uwezekano.!
Angalia kitabu: (Wasaailu sh-shia).
Cha Alhurrul-Aamaly. (18/463).
Na wanasema: Hakika Diya ya Sunni (yaani pindi
Akiuliwa) ni sawa na Diya ya Beberu, na Beberu nibora
kuliko Yeye. na Diya yao hailingani na Diya ya ndugu
yao Mdogo ambaye ni Mbwa wa kuwinda, wala
hailingani na ya ndugu yao Mkubwa ambaye ni
Myahudi.
Angalia kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyyah).
Cha Niimatullahi Aljazaairy. (3/308).
Na wanasema: Chukuwa mali ya Naaswib (Muislamu) Popote utakapo ipata na utupatie sisi Khumusi tu. (Moja ya tano).
صفحة 41
Angalia kitabu: (Wasaailu sh-shia).
Cha Alhurrul-Aamaly. (6/340).
Na wanasema: Hakika siku ya Qiyama, mema waliyo
yafanya Ahlus-sunnah watapewa Shia, na makosa waliyo
yafanya Shia watapewa Ahlus-sunnah, kisha watupwe
Motoni.
Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar).
Cha Almajlisy. (5/247-248).
Na wanasema: Ahlus-sunnah ni najsi (Wachafu) na
Damu zao ni halali na Mali zao piya, na kwamba wao ni
watu wa Motoni, na wala hawatatoka ndani ya Moto.
Angalia kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyyah).
Cha Niimatullahi aljazaairy. (2/306).
Na kitabu: (Haqqul-yaqiin Fii Maarifati Uswuulud-diin).
Cha Abdallah Bishri. (2/188).
Na wanasema: Shia akimwita Mshia mwenzake (Ewe
sunni) basi ana adhibiwa, na imethibiti juu yake kisheria
kupewa adhabu itakayo mpa fundisho.
Angalia kitabu:
(hayaatul-muhaqiq alkarkry wa aatharuhu). (6/237).
UZUSHI WA MASHIA
Mashia wanadai kuwa: Eti kundi miongoni mwa Malaika walizozana kuhusu jambo Fulani, kisha wakamtaka mwanaadamu awe muamuzi baina yao, Allah akawateremshia wahyi, kuwa chaguweni kati ya
صفحة 42
Wanaadamu, wakamchaguwa Ally bin Abiitwalib.
Angalia kitabu: (Musnad faatwima).
Cha Husein Attuwaisir kaany. Ukurasa (296).
Na wanasema kwamba: Punda aitwae (Ghufair)
alimsemesha Mtume -rehma na amani za Allah ziwe zuu
yake- Akamwambia: Namtowa Fidia Baba yangu na
Mama yangu, hakika Baba yangu Alinisimulia kutoka
kwa Baba yake, kutoka kwa Babu yake, kutoka kwa
Baba wa Babu yake, kwamba: Alikuwa na Nabii Nuhu
katika Safina (Jahazi) Nabii Nuhu akasimama kisha
Akampakusa katika Matako yake, kisha Akasema:
Atatoka katika Mgongo wa Punda huyu, Punda ambaye
atapandwa na Bwana wa Mitume wote na wa Mwisho
wao, hivyo namshukuru Allah aliye nijaalia kuwa Mimi
ndiye Yule Punda.!!!
Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy)
Cha Alkulainy. (2/237).
Na wanasema kuwa: Imamu wao Albaaqir
Alitengeneza Tembo wa Udongo kisha Akampanda Yule
Tembo, akaruka naye mpaka Makkah.!!! Angalia kitabu:
(Madiinatul-maajiz). Cha Haashimul-bahraany. (5/10).
Na wanasema: Mikojo na Mavi ya Maimamu wao hamna Uchafu wowote wala Harufu mbaya, bali ni kama Miski (Mafuta uzuri namba moja) na Mwenye Kunywa Mikojo ya Maimamu wao na Mavi yao na Damu zao Allah Atamziwiya kuingia Motoni, na ata Muingiza Peponi. Angalia kitabu: (Anwaarul-wilaaya).
صفحة 43
Cha A'ayatullah Al-aakhundi Mulaa zainul-Aabidiina
alkalbaaikaany. Ukurasa (440).
Na wanasema: Hakika Ushuzi na Mavi ya Maimamu
zao vina harufu kama ya Miski.!!!
Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy).
Cha Alkulainy. (1/319).
Na wanasema: Kuvaa Viatu vyeusi kunasababisha
mambo matatu, Nikasema: Nimambo gani hayo?
Akasema: kunasababisha: Kudhoofika kwa nuru ya
Macho, na kurefusha dhakari (Sehemu ya siri inakuwa
ndefu) na kunamjengea Mtu kuwa na Huzuni.
Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy).
Cha Alkulainy. (6/465).
Na wanasema: Kuvaa Viatu vya njano kunasababisha
mambo matatu: kunaleta nuru ya Macho, na kuikomaza
Dhakari, na kuondowa Huzuni.
Angalia kitabu:
(Alfuruu minal-kaafy).
Cha Alkulainy. (6/465).
Na wanasema: Kula Karoti kunachemsha Bandama, na
kusimamisha Dhakari (sehemu ya siri) na kunaongeza
Nguvu za tendo la ndoa.
Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy).
Cha Alkulainy. (6/372).
Na wanasema: Hakika Sheitwani huwa anakuja na kumkalia Mwanamke kama vile Mwanamume anavyo mkalia, na yanatokea kama yale yanayo tokea kwa