Wudhuu´ ni twahara ya wajibu yenye kuondosha hadathi ndogo kama mfano wa mkojo, kinyesi, upepo, usingizi mzito na kula nyama ya ngamia. Kumepokelewa yafuatayo juu ya fadhila zake:
´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna yeyote kati yenu atatawadha vizuri na halafu aseme: “Ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah; hali ya kuwa peke yake hana mshirikina, na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Ee Allaah nijaalie kuwa miongoni mwa wenye kutubu na miongoni mwa wale wenye kujitwaharisha” isipokuwa hufunguliwa milango minane ya Pepo ili aingie kwenye mlango wowote anaotaka.”1
´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kutawadha kwa njia nzuri, basi madhambi yake yanapukuchika kutoka kwenye mwili wake mpaka yaliyoko chini ya makucha.”2
Ameipokea Muslim.
´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kutia wudhuu´ kikamilifu, kutembea kwenda msikitini na kusubiri kati ya swalah mpaka nyingine, kunafuta madhambi.”3
1 Muslim (234), at-Tirmidhiy (55), Ahmad (04/150), Abu Daawuud (170). Nyongeza “Allaah nijaalie kuwa miongoni mwa wenye kutubu na miongoni mwa wale wenye kujitwaharisha” ni ya at-Tirmidhiy.
2 Muslim (03/113).
3 al-Haakim (01/132) na ameonelea kuwa ni Swahiyh kwa masharti ya Muslim.
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
4
Namna ya kutawadha
Namna ya kutawadha
1- Nia. Mtu anatakiwa kunuia wudhuu´ kwa moyo wake bila ya kutamka kwa mdomo, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupatapo kamwe kunuia wudhuu´, swalah wala kitu kingine katika ´ibaadah kwa kutamka. Allaah anajua yaliyomo ndani ya moyo na hivyo hakuna haja ya kuelezea juu yake.4
2- Sema: ”Bismillaah”.5
3- Osha mikono yako mara tatu.6
4 Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
”Kuna maafikiano kwa Waislamu ya kwamba nia mahali pake ni moyoni na sio kinywani. Hili linahusiana na ´ibaadah aina zote; twahara, kutekeleza swalah, zakaah, swawm, hajj, kupeana watumwa, Jihaad na mfano wa hayo. Lau mtu atasema kitu kingine kuliko kile alichonuia, nia inahesabika moyoni, na sio kwa kutamka. Hata hivyo lau mtu atatamka nia na wakati nia haiko moyoni, kuna maafikiano kwa Waislamu juu ya kwamba mtu kama huyo atakosa thawabu.” (Majmuu´-ul-Fataawaa (1/234)).
5 Kwa Jina la Allaah. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: ”Hana wudhuu´ yule asiyetaja Jina la Allaah kabla yake.” (Ahmad (2/418). Abu Daawuud (101), Ibn Maajah (1/140), ad-Daaraqutwniy (1/71), al-Haakim (1/47) na al-Bayhaqiy (1/44). Ni ”nzuri” (Hasan) kwa mujibu wa Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah). Tazama ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (90) na ”Irwaa´-ul-Ghaliyl” (1/122).
Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) ameifasiri Hadiyth hii na kusema: ”Hili linaonyesha kuwa (yaani kusema ”Bismillaah”) ni wajibu na kwamba inafanywa kabla – na hii ndio kauli yenye kujulikana kwa madhehebu (yaani madhehebu ya Hanaabilah).” Tazama (ash-Sharh al-Mumti´ alaa´ Zaad-il-Mustaqni´ (1/127-128)).
6 Imepokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alikuwa akiosha baadhi ya viungo mara moja, mbili na tatu, amesema Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa): ”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitawadha kwa kuosha mara tatu.” (al-Bukhaariy (157).
Dalili ya kwamba aliosha baadhi ya viungo mara mbili, ni Hadiyth ya ´Abdullaah bin Zayd (Radhiya Allaahu ´anh): ”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitawadha na akaosha mara mbili.” (al-Bukhaariy (158)).
Dalili ya kwamba aliosha baadhi ya viungo mara tatu, ni Hadiyth ya Humraan: ”´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) aliomba maji kwa ajili ya kutawadha. Kisha akaosha vitanga vyake vya mikono mara tatu, kisha akavuta maji puani na kuyatoa nje, kisha akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mkono wake wa kulia mpaka kwenye konongo mara tatu, kisha akafanya hali kadhalika mkono wake wa kushoto mara tatu, halafu akapangusa kichwa chake, kisha akaosha mguu wake wa kulia mpaka kwenye
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
5
4- Sukutua kinywa na upalize maji puani kisha uyapenge kwa nje. Fanya hivo mara tatu.7
5- Osha uso wako mara tatu. Hili linatakiwa kufanywa kuanzia sikio moja hadi lingine8, na kuanzia maoteo ya nywele mpaka sehemu ya chini ya ndevu9.
6- Osha mikono yako mara tatu; kuanzia kwenye ncha za vidole mpaka kwenye konongo. Anza na mkono wa kulia kisha ndio uende wa kushoto.
7- Pangusa kichwa chako mara moja. Ilowe mikono yako kisha uipanguse kuanzia maoteo ya nywele mpaka zinapoishia kisha urudi tena10.
8- Pangusa masikio yako mara moja. Ingiza vidole vya shahada kwenye masikio na vidole gumba nje ya masikio na uyapanguse.
9- Osha miguu yako mara tatu. Inatakiwa kuanzia kwenye vidole mpaka kwenye fundo za miguu. Aanze kwa mguu wa kulia kisha wa kushoto11.
mafundo ya miguu na baada ya hapo akafanya hali kadhalika mguu wa kushoto. Halafu akasema: ”Nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitawadha namna hii.”” (al-Bukhaariy (164) na Muslim (226)).
7 Tazama Hadiyth ya ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) iliyoko hapo juu.
8 Masikio ni katika kichwa. Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Masikio ni katika kichwa.” (Ibn Maajah (444), Abu Daawuud (143), ad-Daaraqutwniy (103). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika “Irwaa´-ul-Ghaliyl” (84)).
9 ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichambua ndevu kwa vidole vyake.” (Ibn Maajah (430), at-Tirmidhiy (310), Ibn Khuyzamah (1/78-79) na Ibn Hibbaan (3/363). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Imaam al-Albaaniy katika “Irwaa´-ul-Ghaliyl” (92).).
Miongoni mwa walio na maoni haya ni Imaam as-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah), kama alivyotaja Imaam at-Tirmidhiy katika “al-Jaamiy´” yake. Isitoshe hukumu hii inawahusu wanaume peke yao na si kwa wanawake.
10 ´Abdullaah bin Zayd (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea kwamba: ”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipangusa kichwa chake mbele na nyuma; alianzia karibu na maoteo ya nywele yake na akazipangusa mpaka kwenye shingo yake kisha akarudi tena.” al-Bukhaariy (1/251) kwa “Fath-ul-Baariy”, Muslim (235) na at-Tirmidhiy (28)).
11 Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: ”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikawia nyuma katika safari moja. Kisha akatuwahi na ilihali alasiri (Swalat-ul-´Aswr) imeingia. Tukaanza kutawadha huku tukipaka miguu yetu. Hapo akanadi kwa sauti kubwa: “Ole na Moto kwa
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
6
Kuoga (Ghusl)
Kuoga (Ghusl)
Ghusl ni twahara ya wajibu kuondosha hadathi kubwa kama janaba na hedhi.
1- Nia. Nuia kuoga kwa moyo wako bila ya kutamka kwa mdomo.
2- Sema: ”Bismillaah”.
3- Tawadha wudhuu´ mkamilifu12.
4- Jimwagie maji juu ya kichwa mara tatu.
5- Kisha osha mwili uliobaki13.
visigino.” Alisema hivi mara mbili au tatu.” (al-Bukhaariy (1/232) kwa “Fath-ul-Baariy” na Muslim (3/128) kwa Sharh Swahiyh Muslim ya Imaam an-Nawawiy).
Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) ameitilia Hadiyth hii taaliki katika “Sharh Swahiyh Muslim” na kusema: “Sababu ya Muslim kuitaja, ni ili kuonyesha kuwa ni wajibu kuosha miguu na kwamba mtu halipwi kwa kule kuipangusa peke yake.”
12 Bi maana tawadha vile viungo vya wudhuu´ umevyozowea kutawadha.
13 ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amepokea kwamba: ”Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa katika janaba, alikuwa akianza kuoga kwa kuosha mikono yake, kisha anaosha sehemu zake za siri, halafu anatawadha, kisha anachukua maji na kusugua mashina ya nywele mpaka maji yanagusa ngozi, halafu anamwagia maji kichwa mara tatu na mwishoni mwili uliobaki.” (al-Bukhaariy (248) na Muslim (315) na matamshi ni ya kwake).
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
7
Tayammum
Tayammum
Tayammum ni twahara ya wajibu kwa udongo. Inafanywa badala ya wudhuu´ na kuoga kwa yule asiyepata maji au anakhofia kudhurika kwa kuyatumia14.
14 Allaah (Tabaarak wa Ta´ala): "Na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa [mmewaingilia] wanawake kisha hamkupata maji, basi mtayammamu ardhi safi ya mchanga, pakeni nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kusamehe." (04:43)
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
8
Nam
Namna ya Tayammum na ya Tayammum
1- Nia. Nuia kuwa unafanya Tayammum badala ya wudhuu´ au kuoga.
2- Gusa ardhi (kwa mikono) au vile vyenye uhusiano nayo na vina vumbi.
3- Pangusa uso na viganja vyako.
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
9
Kupangusa juu ya Khuff
Kupangusa juu ya Khuff
Khuff ni kitu kinachovaliwa mguuni katika ngozi au mfano wake.
Jawrab (soksi) ni kitu kinachovaliwa mguuni katika pamba na mfano wake.
Hukumu ya kupangusa juu ya soksi za ngozi na za kawaida
Kupangusa juu yake ni Sunnah iliyokuja kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo ni bora zaidi kupangusa juu yake kuliko kuzivua ili mtu aweze kuosha miguu. Dalili ya hilo ni Hadiyth ya al-Mughiyrah bin Shu´bah (Radhiya Allaahu ´anh):
"Siku moja wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anatawadha, nikakimbia ili nimvue soksi zake za ngozi. Ndipo akasema: "Ziache, hakika mimi nilizivaa nikiwa na twahara." Kisha baada ya hapo akapangusa juu yake."15
Uwekwaji wa Shari´ah wa kupangusa ni jambo limethibiti katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kuhusiana na Kitabu cha Allaah, amesema (Ta´ala): يَا أَي هَُّا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلََ الصَّلََةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلََ الْمَرَافِقِ وَامْ سَ وُُا رُِِ وُُ كُِِمْ وَأَ جُْْلَكُمْ إِلََ الْكَ "Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah; osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi, na panguseni vichwa vyenu na [osheni] miguu yenu hadi vifundoni." (05:06)
Kuhusiana na Kauli Yake "miguu yenu", inaweza kusomwa kwa njia mbili sahihi ambazo zote mbili zimesihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Moja inasema "Arjulakum16" na ina ushirikiano na Kauli Yake "Ujuhikum", ikiwa na maana ya kwamba vyote viwili vinatakiwa kuoshwa.
Ama kisomo kingine kinasema "Arjulikum. Hapa ina ushirikiano wa "vichwa vyenu", ikiwa na maana ya kwamba miguu inatakiwa kupanguswa. Kwa hivyo inapata kubainika wazi ya kwamba miguu inaweza kuoshwa na kupanguswa kwa mujibu wa Sunnah. Pale ambapo
15 al-Bukhaariy (206) na Muslim (274).
16 Miguu yenu.
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
10
miguu ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa haina viatu, alikuwa akiiosha, na akiwa amevaa soksi za ngozi, anapangusa juu yake.
Kuhusiana na dalili ya Sunnah kumekuja idadi kubwa juu ya hilo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:
"Moyo wangu hauna mashaka yoyote juu ya upangusaji. Kumekuja Hadiyth arubaini kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake juu ya hilo."17
Mshairi amesema: "Miongoni mwa Hadiyth zilizopokelewa kwa mapokezi mengi ni pamoja na
"Mwenye kusema uongo kwa kusudi"
"Mwenye kumjengea nyumba Allaah na kutarajia malipo"
Kuonekana kwa Allaah, Uombezi na Hodhi
Kupangusa juu ya soksi za ngozi."
Hizi ndio dalili kutoka katika Kitabu na Sunnah zenye kuruhusu kupangusa kwavyo. Hata hivyo ni lazima kutimie masharti yafuatayo ili kupangusa juu ya soksi za ngozi kusihi. Masharti hayo ni mane:
Sharti ya kwanza: Mtu alikuwa na twahara wakati alipozivaa. Dalili ya hilo ni pale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomwambia al-Mughiyrah bin Shu´bah:
"Ziache, hakika mimi nilizivaa nikiwa na twahara."18
Sharti ya pili: Soksi za ngozi au za kawaida ziwe safi. Haijuzu kupangusa juu yake ikiwa zina najisi. Dalili ya hilo ni kuwa siku moja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaswalisha Maswahabah zake na huku amevaa sandala. Ghafla akazivua katikati ya swalah na baadaye akaeleza kuwa Jibriyl amemueleza kuwa zina vitu vyenye kuudhi au uchafu19. Hii ni dalili yenye kuonesha kuwa haijuzu kuswali kwenye kitu kilicho na najisi. Mwenye kupangusa juu ya kilicho najisi kwa maji kinachafuka. Kwa hivyo si sahihi ya kwamba kinazingatiwa kuwa ni twahara.
17 Tazama "al-Musnad" (04/363).
18 al-Bukhaariy (206) na Muslim (274).
19 Abu Daawuud (650) na Ahmad (03/92).
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
11
Sharti ya tatu: Kupangusa iwe katika hadathi ndogo. Haitakiwi iwe baada ya janaba au yale yenye kuwajibisha kuoga. Dalili ya hilo ni Hadiyth ya Swafwaan bin ´Assaal (Radhiya Allaahu ´anh):
"Tunapokuwa safarini Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametuamrisha kutovua soksi zetu za ngozi kwa michana mitatu na nyusiku zake. Hili halihusiani na [wakati wa] janaba, isipokuwa baada ya kukidhi haja kubwa, ndogo na usingizi."20
Kujengea juu ya Hadiyth hii iliyotajwa, kupangusa kunashurutishwa iwe katika hadathi ndogo na si hadathi kubwa.
Sharti ya nne: Kupangusa iwe ndani ya muda uliopangwa katika Shari´ah; mchana mmoja na usiku wake kwa ambaye ni mkazi na michana mitatu na nyusiku zake kwa ambaye ni msafiri. Hili linatokamana na Hadiyth ya ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh):
"Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefanya mchana mmoja na usiku wake kwa mkazi na michana mitatu na nyusiku zake kwa msafiri."21
Bi maana kupangusa juu ya soksi za ngozi. Ameipokea Muslim.
Muda huu unaanza pale mara ya kwanza anapoanza kupangusa baada ya hadathi na unaisha masaa 24 kwa ambaye ni mkazi, na masaa 72 kwa ambaye ni msafiri. Tukadirie mtu ametawadha kwa ajili ya swalah ya Fajr Jumanne na akabaki na wudhuu´ wake mpaka aliposwali ´Ishaa usiku wa kuamkia Jumatano kisha akalala, halafu baada ya hapo akaamka ili aswali Fajr Jumatano na akapangusa saa kumi na moja, hapo ndipo unaanza muda wa kuhesabu kuanzia saa kumi na moja asubuhi ya Jumatano22. Lau tutakadiria kuwa alipangusa kabla ya saa kumi na moja, basi anapata kuswali Fajr ya alkhamisi hii kwa upanguso huu na vilevile kuswali atakayo maadamu yuko na twahara, kwa sababu wudhuu´ hautenguki kwa kuisha kwa muda - haya ndio maoni yenye nguvu kabisa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuweka kikomo cha muda wa twahara. Alichofanya ni kuweka kikomo cha muda wa kupangusa. Kwa hivyo muda ukitimia haifai kupangusa, lakini hata hivyo ikiwa mtu yuko na twahara basi twahara yake inaendelea, kwa sababu twahara hii imethibiti kwa mujibu wa dalili ya Kishari´ah na kila kilichothibiti kwa dalili ya Kishari´ah hakitenguki
20 Ahmad (04/239), an-Nasaa´iy (127), Ibn Maajah (478), at-Tirmidhiy (96), Ibn Khuzaymah (01/98-99) na Ibn Hibbaan (04/155). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika "Irwaa´-ul-Ghaliyl" (104).)
21 Muslim (276).
22 Kwa msemo mwingine ni kwamba hapa ndipo unaanza upangusaji wa mara ya kwanza, katika hali ni kuanzia alfajiri ya Jumatano kwenda mbele masaa 24, katika hali hii ni mpaka alfajiri ya alkhamisi.
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
12
isipokuwa kwa kupatikana dalili ya Kishari´ah. Hakuna dalili yoyote yenye kuonesha kuwa wudhuu´ unatenguka kwa kuisha muda wa kupangusa. Jengine ni kwamba msingi unasema mtu anabaki katika hali aliyokuwemo mpaka kubainishwe chenye kuitengua.
Haya ndio masharti yanayotakiwa kutimizwa ili mtu aweze kupangusa juu ya soksi za ngozi. Pamoja na hivyo ni kwamba kuna masharti mengine kwa mtazamo wa baadhi ya wanachuoni ambayo yanaweza kujadiliwa.
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
13
Ni vipi mgonjwa hujitwaharisha?
Ni vipi mgonjwa hujitwaharisha?
Ni wajibu kwa mgonjwa kujitwahirisha na maji, hivyo atawadhe kwa hadathi ndogo na kuoga kwa hadathi kubwa.
Ikiwa hawezi kujitwahirisha na maji, ima kwa kutoweza au kwa kuchelea maradhi yasije kuzidi au kuchelewa kupona, afanye Tayammum.
Tayammum inafanywa kwa kupiga vitanga vya mikono mara moja kwenye ardhi ilio safi. Baada ya hapo apanguse uso wake wote na mwishoni apanguse mikono yake.
Ikiwa hatoweza kujitwahirisha mwenyewe, basi mtu mwingine amtawadhishe au amsaidie kufanya Tayammum.
Ikiwa kuna kiungo cha mwili kilicho na donda, akioshe na maji. Hata hivyo ikiwa kunamuathiri, apanguse juu yake kwa kulowa mkono wake kisha apanguse juu yake. Ikiwa hata huko kupangusa kunamuathiri, basi afanye Tayammum.
Ikiwa kuna kiungo cha mwili ambacho kimevunjika na kimefungwa bendeji au plasta, basi apanguse juu yake kwa maji badala ya kupaosha. Hahitajii kufanya Tayammum kwa sababu upangusaji unachukua nafasi ya uoshaji.
Inajuzu kufanya Tayammum kwenye kuta au vitu vyengine ambavyo vina vumbi. Ikiwa kwenye kuta ambao mtu anafanya Tayammum kuna rangi, mtu asifanye Tayammum hapo isipokuwa kama kuna vumbi.
Ikiwa haiwezekani kufanya Tayammum kwenye ardhi, kuta au kitu kingine kilicho na vumbi, ni sawa kumimina udongo kwenye chombo au kijitambara halafu mtu afanye Tayammum kutoka humo.
Mtu akifanya Tayammum kwa ajili ya swalah kisha akabaki na twahara yake mpaka kukaingia wakati wa swalah nyingine, aswali na Tayammum yake ile ya kwanza na wala asifanye Tayammum mara nyingine, kwa sababu bado yuko na twahara na haikutenguliwa na kitu23. Hali kadhalika inahusiana akiwa na janaba; atarudi kufanya Tayammum tu pale ambapo
23 Abu Hurayrah amepokea ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
"Udongo msafi ni twahara ya Muislamu, hata kama hatopata maji kwa miaka kumi. Atapopata maji, basi amche Allaah na aoshe ngozi yake, kwani hilo ni bora kwake." (Abu Daawuud (332), an-Nasaa´iy (332) na ad-Daaraqutwniy (01/187). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy (Irwaa´-ul-Ghaliyl" (153).)
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
14
atapata janaba nyingine. Lakini pamoja na hivyo Tayammum anayofanya katika muda huu ni kwa ajili ya hadathi ndogo.
Ni wajibu kwa mgonjwa kuuosha mwili wake kutokana na najisi. Ikiwa hatoweza kufanya hivo, basi aswali katika hali aliyomo. Swalah yake ni sahihi na wala hahitajii kuirudi.
Ni wajibu kwa mgonjwa kuswali na nguo zilizo safi. Nguo zake zikiwa na najisi, basi ni wajibu kwake ima azioshe au ajibadilishe kwa nguo zingine. Ikiwa pia hatoweza kufanya hivyo, aswali katika hali aliyomo24. Swalah yake ni sahihi na wala hahitajii kuirudi.
Ni wajibu kwa mgonjwa kuswali mahala ambapo ni pasafi. Hata hivyo ikiwa mahala hapo pana najisi, ni wajibu paoshwe, kupabadilisha kwa nafasi ilio safi au kupafunika kwa kitu kilicho kisafi. Ikiwa pia hatoweza kufanya hivo, aswali pale alipo. Swalah yake ni sahihi na wala hahitajii kuirudi.
Haijuzu kwa mgonjwa kuchelewesha swalah kuitoa nje ya wakati wake kwa hoja ya kwamba hawezi kujitwahirisha. Bali anatakiwa kujitwahirisha kadri na anavyoweza kisha aswali swalah anayotaka kuswali kwa wakati wake, hata kama najisi iliyompata kwenye mwili wake, nguzo zake au sehemu haiwezi kuondoshwa. Amesema (Ta´ala): فَاتَّ قُوا اللَّ هَ مَا ا تَِْطَ تُْْمْ
"Basi mcheni Allaah muwezavyo." (64:16)
Ikiwa mtu25 ana ugonjwa wa kutokwa na mkojo hovyo, anachotakiwa ni kutawadha kwa kila swalah ya faradhi baada ya kuingia wakati wake. Aoshe tupu yake na kuifunga kitu kisafi chenye kuzuia nguo au mwili wake usinajisike. Halafu baada ya hapo atawadhe na kuswali. Mtindo huu anatakiwa kufanya kila wakati anapotaka kuswali swalah ya faradhi. Akihisi uzito,
24 Imaam Ibn Qudaamah al-Maqdisiy (Rahimahu Allaah) amesema: "Ikiwa hajui ni wapi kwenye nguo, au kitu kingine, najisi imeshika basi aioshe mpaka pale atapokinaika." (´Umdat-ul-Fiqh, uk. 15, Maktabah ar-Rushd, ar-Riyaadh, 1422/2001).
Imaam Bahaa´-ud-Diyn al-Maqdisiy (Rahimahu Allaah) amefasiri maneno hayo yaliyopo hapo juu na kusema: "Bi maana aioshe mpaka pale atapokinaika kuwa ameondosha najisi. Hali kadhalika inahusiana na yule mwenye kunajisi moja katika mikono yake pasi na kujua ni mkono upi aliounajisi; aioshe yote miwili. Hali kadhalika akijua kuwa nguo yake imeingiwa na najisi lakini bila ya kujua ni wapi paliponajisika; aioshe yote. Haya, kwa sababu kwa usalama wote aweze kufikia hali ya twahara." (al-´Uddah fiy Sharh-il-´Umdah, (01/11), Mu´assasah ar-Risaalah, Beirut, 1421/2001).
25 Sawa awe mwanaume au mwanamke.
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
15
basi inajuzu kwake kujumuisha Dhuhr na ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa. Kuhusiana na swalah ya Sunnah, anatakiwa kufanya yale tuliyoyataja ikiwa anataka kuswali. Ikiwa hilo litapitika karibu na mida ya swalah ya faradhi, wudhuu´ wa swalah ya faradhi unatosheleza.
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
16
Ni vipi mgonjwa huswali?
Ni vipi mgonjwa huswali?
Ni wajibu kwa mgonjwa kuswali hali ya kuwa amesimama, hata kama ataswali kwa kuinama au kwa kushegamia ukuta au bakora.
Ikiwa hawezi kuswali kwa kusimama, basi aswali kwa kukaa. Njia bora ya kufanya hivo ni kukaa kwa kuingiza mguu ndani ya mwingine nafasi ya kusimama na kuinama26.
Ikiwa hawezi kuswali kwa kukaa, aswali kwa kulala, huku ameelekea Qiblah - na kulalia ubavu wa kulia ndio bora zaidi27. Ikiwa hawezi kuelekea Qiblah, aswali kwa kuelekea popote pale. Swalah yake ni sahihi na wala hahitajii kuirudi.
Ikiwa hawezi kuswali kwa kulalia ubavu, aswali kwa kulala na huku miguu yake imeelekea Qiblah. Ikiwa hawezi kuelekeza miguu yake Qiblah, aswali vile anavyoweza na wala hahitajii kuirudi.
Ni wajibu kwa mgonjwa kurukuu na kusujudu pindi anaposwali. Ikiwa hawezi, ainamishe kichwa chake kwa vyote viwili28 na afanye kule kuinama kwa ajili ya Sujuud ndio kuwe kurefu kidogo kuliko kuinama kwa ajili ya kurukuu. Akiweza kufanya Rukuu´ peke yake na asiweze kufanya Sujuud, arukuu wakati wa Rukuu´ na kuinama kwa ajili ya Sujuud. Hata hivyo ikiwa ataweza kufanya Sujuud peke yake na asiweze kufanya Rukuu´, asujudu wakati wa Sujuud na kuinama kwa ajili ya Rukuu´.
Ikiwa hatoweza kuinamisha kichwa kwa ajili ya Rukuu´ na Sujuud, aashirie kwa macho. Afumbe kidogo kwa ajili ya Rukuu´ na afumbe zaidi kidogo kwa ajili ya Sujuud. Kuashiria kwa kidole kama wanavyofanya baadhi ya wagonjwa sio sahihi na sijui kuwa jambo hilo lina msingi wowote katika Kitabu, Sunnah au maoni ya wanachuoni.
26 Tazama hapa http://www.herahospital.org/articles.php?action=show&id=187
27 ´Imraan bin al-Huswayn (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: "Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu mtu mwenye kuswali swalah kwa kukaa. Akasema: "Ni bora akiswali swalah kwa kusimama. Yule mwenye kuswali swalah kwa kukaa anapata nusu ya thawabu za mwenye kusimama na mwenye kuswali swalah kwa kulala anapata nusu ya thawabu za mwenye kukaa."" (al-Bukhaariy (1115))
Imaam Ibn Hajar (Rahimahu Allaah) amefasiri maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yaliyotajwa hapo juu "kwa kulala" na kusema: "al-Ismaa´iyliy amesema: "Neno "kwa kulala" ina maana ya "kulalia ubavu."" (Fath-ul-Baariy bi Sharh Swahiyh al-Bukhaariy (1115)
28 Bi maana kwa ajili ya kurukuu na kusujudu.
Ahkaam-ut-Twahaarah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
17
Ikiwa hawezi kuswali kwa kuinamisha kichwa au kwa kuashiria kwa macho, aswali kwa moyo wake. Hivyo alete Takbiyr29, asome na anuie Rukuu´, Sujuud, Qiyaam na Qu´uud30 kwa moyo wake - na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia.
Ni wajibu kwa mgonjwa kuswali swalah zote kwa wakati wake na kufanya yale yote ya wajibu ambayo anaweza. Akipata uzito wa kuswali kila swalah kwa wakati wake, basi ajumuishe baina ya Dhuhr na ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa. Afanye hivyo ima mjumuisho wa kutangulia kwa njia ya kwamba aswali ´Aswr wakati wa Dhuhr na ´Ishaa wakati wa Maghrib, au mjumuisho wa kuchelewesha kwa njia ya kwamba aswali Dhuhr wakati wa ´Aswr na Maghrib wakati wa ´ishaa. Afanye lile litakalokuwa na wepesi kwake. Kuhusiana na Fajr haijumuishwi na ilio kabla yake wala ilio baada yake.
Ikiwa mgonjwa atakuwa safarini na anatibiwa nje ya mji wake, afupishe swalah zenye Rakaa nne. Hivyo aswali Dhuhr, ´Aswr na ´Ishaa kila moja Rakaa mbili. Afanye hivi mpaka pale ataporudi katika mji wake, sawa ikiwa muda utarefuka au utakuwa mfupi.
29 Kusema "Allaahu Akbar".
30 Staili ya kukaa, ima kati ya Sajdah mbili au Tashahhud.