
Mafungamano ya shahada na
Aina za Tawhiidi.
1
Mafungamani ya Shahada na Aina za Tawhiid.
Swali: Je shahada inakusanya vigawanyo vya Tawhid?
Jawabu: ndio shahada inakusanya aina za tawhiid zote, ima kwa kuambatana na
shahada au kulazimiana.
Kwa mfano: mtu anaposema : (Ash’hadu an laa ILLaha ila Allah), mtu
anafahamu kuwa makusudio yake ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika
ibada, na kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika ibada kunaitwa (Tawhid Al
Uluhiya) ambayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika ibada za
wanadamu, tawhidi hii inalazimiana na kuambatana na tawhidiya (Al-
Rububiyyah) ambayo maana yake ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika
vitendo vyake Mwenyezi Mungu kama kuumba na kuhuisha na kufisha na kutoa
rizki nk.
Kwasababu kila mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake hakika
hatamuabudu mpaka awe ni mwenye kukiri Uungu wa Mwenyezi Mungu katika
vitendo vyake, na hii inakusanya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina
yake na sifa zake, kwasababu hii alisema Nabii Ibrahim kumwambia Baba yake:
} Ewe baba yangu! Kwa yakini imenifikia elimu isiyokufikia wewe. Basi nifuate
mimi, name nitakuongoza Njia iliyo Sawa{. (Maryam 43).
Basi tawhid ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika ibada ndio tawhid Al
Uluhiyyah ambayo imekusanya tauhidi ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu
katika vitendo vyake (Tawhid al-rububiyyah) na kumpwekesha Mwenyezi
Mungu katika majina yake na sifa zake (Tawhidi Al As’mai wa swifati).