Nakala




 NAMNA YA KUFANYA UMRAH


Mtunzi


Sheikh Abdul-Aziz bin Abdillah bin Baaz


Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu peke yake, na


baada ya hayo:


Huu ni muhtasari mfupi wa matendo ya ibada za


Umrah. Na kwa msomaji, maelezo ya hayo ndiyo


haya:


Mwenye kufanya Umrah atakapofika kwenye Miqat


(sehemu za kunuia Hija au Umrah), inapendekezwa


aoge na kujisafisha. Mwanamke pia atafanya hivyo


hata kama atakuwa katika hedhi au katika damu ya


baada ya kuzaa, isipokuwa hataruhusiwa kuzunguka


Ka'aba mpaka atwaharike na aoge.


Mwanamume anatakiwa kujipaka manukato kwenye


mwili wake kabla ya kuvaa nguo zake za ihram. Ikiwa


haitawezekana kuogea kwenye Miqat, basi hakuna


ubaya ikiwa ataoga anapofika Makka kabla ya


kuzunguka Ka'aba ikiwa hilo litawezekana.


Mwanamume atavua nguo zote za kawaida


zilizoshonwa na kuvaa kikoi na shuka, na


inapendekezwa ziwe nyeupe na safi.


Ama mwanamke, yeye atahirimia katika nguo za


kawaida (isipokuwa hatovaa nikabu, burka na glovu.


Hivyo atavivua na aufunike uso wake na mikono yake


kutokana na wanaume wasio mahram wake kwa nguo


nyinginezo) ambazo hazina mapambo wala si za


umaarufu.


2


Kisha ataweka nia ya kuingia katika ibada (ya Umra)


moyoni mwake na kuitamka kwa ulimi wake


akisema: “Labbayka umrah (Nimekuitikia kwa


kufanya Umra).” au “Allahummma labbayka umrah


(Ewe Mwenyezi Mungu, nimekuitikia kwa kufanya


Umra).”   





Iwapo aliyehirimia Umrah atachelea kuwa


hatoweza kutekeleza ibada zake kwa sababu ni


mgonjwa au anaogopa adui au mfano wa hayo, basi


anaruhusiwa kuweka sharti anapohirimia kwa


kusema: "Ikiwa nitazuiliwa na kizuizi, basi mahali


pangu pa kutoka katika ihram ni pale


kitakaponizuilia." Haya ni kwa mujibu wa Hadithi ya


Dhwiba’ah bint Az-Zubayr, Mwenyezi Mungu


amuwiye radhi.


Kisha atafanya Talbiyah ya Mtume, rehema na


amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake,  ambayo


ni: Labbaika llaahumma labbaika. Labbaika laa


shariika laka labbaika. Innalhamda wanni'imata laka


walmulk laa shariika laka (NimekuitikIa ewe


Mwenyezi Mungu nimekuitikia! Nimekuitikia hauna


mshirika nimekuitikia. Hakika sifa njema na neema


na ufalme ni vyako, nimekuitikia huna mshirika!).





Anapoufikia Msikiti Mtakatifu, atautanguliza mguu


wake wa kulia wakati wa kuingia na aseme: "Kwa


jina la Mwenyezi Mungu, na rehema na amani ziwe


juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ninajilinda kwa


Mwenyezi Mungu Mkuu, na kwa uso wake mtukufu,


na kwa utawala wake wa kale, kutokana na Shetani


aliyelaaniwa. Ewe Mwenyezi Mungu, nifungulie


milango ya rehema zako."


Anapofika kwenye Nyumba ambayo ni Ka’aba,


ataacha kufanya Talbiyah, kisha aende kwenye Jiwe


Jeusi, alielekee, kisha aliguse kwa mkono wake wa


kulia na kulibusu kama hilo litawezekana. Lakini


asiwaudhi watu kwa kuleta msongamano. Aseme


wakati anapoligusa: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu,


na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa." Kama itakuwa


vigumu kulibusu, ataligusa kwa mkono au kwa fimbo


au kwa kitu mfano wake, kisha akibusu kile


alicholigusa kwacho. Na kama itakuwa vigumu


kuligusa, basi ataliashiria na aseme: “Mwenyezi


Mungu ni Mkubwa.” na asibusu kile alichoashiria


kwacho.


Ili tawafu iwe sahihi, ni sharti kwamba mwenye


kutufu awe safi kutokana na hadathi ndogo na kubwa.


Kwa sababu, tawafu ni kama swala, isipokuwa


iliruhusiwa kuzungumza ndani yake.


Ataiweka Al-Ka’aba upande wake wa kushoto na


aizunguke mara saba. Kila anapofika kwenye kona ya


Yemeni, ataigusa kwa mkono wake wa kulia


4


ikiwezekana na kusema: “Kwa jina la Mwenyezi


Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.” lakini


asiibusu. Ikiwa itakuwa vigumu kwake kuigusa,


ataiacha na kuendelea na tawafu yake, na asiiashirie


wala asiseme: "Mwenyezi Mungu ni mkubwa.” Kwa


sababu hilo halikusimuliwa kutoka kwa Mtume,


rehema na amani ziwe juu yake.


Ama Jiwe Jeusi, kila anapokuwa sawa nalo,


ataligusa na kulibusu kama tulivyotaja hapo awali.


Vinginevyo, ataliashiria tu na kusema: "Mwenyezi


Mungu ni Mkubwa." Inapendekezwa kutembea kwa


hatua za haraka fupi fupi katika mizunguko mitatu ya


kwanza ya Tawafu ya Kufika Makka, kwa wanaume


tu.


Pia inapendekezwa kwa mwanamume kufanya


Idhtwibaa katika Tawaf al-Qudum (Tawafu ya


kuingia Makka) katika mizunguko yote. Idhtwibaa


inamaanisha kuweka sehemu ya katikati ya upande


wa juu wa shuka yake chini ya kwapa lake la kulia na


ncha zake mbili kwenye bega lake la kushoto.


Na ni sunna pia kufanya dhikri na kuomba dua kwa


wingi, kiasi iwezekanavyo katika mizunguko yote.


Hakuna dua wala dhikri makhsusi katika tawafu.


Bali mtu ataomba na kumjata Mwenyezi Mungu kwa


dua na utajo wowote anaoweza. Na atasema baina ya


pembe mbili za Al-Ka'aba:





 "Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera


mema, na utulinde kutokana na adhabu ya Moto!"  


Haya atayasema katika kila mzunguko. Kwa sababu,


hili lilithibiti kutoka kwa Mtume, rehema na amani za


Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.


Ataumaliza mzunguko wa saba kwa kuligusa Jiwe


Jeusi na kulibusu ikiwezekana, au kuliashiria huku


akisema “Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni


Mkubwa).” kulingana na maelezo yaliyotajwa kabla


ya muda mfupi. Baada ya kukamilisha mzunguko


huu, atavaa shuka lake kwa kuliweka juu ya mabega


yake na kona zake mbili za upande wa juu ataziweka


kwenye kifua chake.


Kisha ataswali rakaa mbili nyuma ya Maqam


Ibrahim ikiwa itakuwa rahisi kufanya hivyo. Lakini


kama hataweza kufanya hivyo, basi ataswalia mahali


popote pale Msikitini. Baada ya Al-Fatihah, atasoma:


“Sema, ‘Enyi makafiri.’ katika rakaa ya kwanza, na:


“Sema, ‘Yeye Mwenyezi Mungu ni wa Pekee.’”


katika rakaa ya pili. Hilo ndilo bora zaidi, lakini


akisoma kitu kingine, basi hakuna tatizo. Kisha,


baada ya kumaliza rakaa mbili hizi, ataelekea kwenye


Jiwe Jeusi, ikiwa hilo litawezekana.


Kisha atatoka aende kwenye Safaa na apande juu


yake au asimame hapo karibu. Kupanda juu yake


ndiyo bora zaidi ikiwezekana. Kisha atasoma maneno


ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:





 "Hakika vilima vya Safaa na Marwa ni katika alama


za Mwenyezi Mungu." [Al-Baqarah: 158]


Na inapendekezwa kwamba aelekee Kiblah, amsifu


na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Atasema: “Hakuna


mungu ila Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu


ni Mkubwa. Hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi


Mungu asiye na mshirika. Ufalme ni wake, na sifa


njema ni zake, naye ni Muweza wa kila kitu. Hakuna


mungu ila Mwenyezi Mungu peke yake, alitekeleza


ahadi yake, na akamnusuru mja wake, na akayashinda


makundi (ya maadui) peke yake.” Kisha ataomba


awezacho huku ameinua juu mikono, na atairudia


dhikri hii na dua hii mara tatu.


Kisha atateremka na atembee akienda Marwah


mpaka afikie alama (taa ya rangi ya kijani kibichi), na


hapo mwanamume ataharakisha mwendo wa


kutembea mpaka afikie alama ya pili.


Ama mwanamke, yeye haruhusiwi kuharakisha


mwendo katika kutembea. Kwa sababu yeye ni uchi.


Kisha atatembea na kupanda juu ya Marwah au


kusimama hapo karibu. Kupanda juu yake ndiyo bora


zaidi ikiwezekana. Kisha atasema na kufanya juu ya


7


Marwah namna aliyoyasema na kuyafanya juu ya


Safaa. Kisha atateremka chini na kutembea katika


sehemu aliyotembea na kuongeza kasi katika sehemu


ambayo aliongeza kasi mpaka afike Safaa. Atafanya


hivyo mara saba. Kwenda kwake ni raundi, na kurudi


kwake ni raundi pia. Ikiwa atafanya sa'yi huku


amepanda, basi hakuna ubaya, hasa inapobidi.


Inapendekezwa kwamba afanye dhikri na kuomba


dua kwa wingi katika sa'yi yake awezavyo. Pia


inapendekezwa kwamba awe safi kutokana na


hadathi kubwa na ndogo. Hata hivyo, ikiwa ataifanya


bila twahara, basi hilo litamtosheleza.


Anapomaliza Sa’yi, mwanamume atanyoa nywele


za kichwa chake au atazifupisha. Kuzinyoa ndiyo


bora. Lakini ikiwa kuwasili kwake Makka ni karibu


na wakati wa Hija, basi kuzifupisha ndiyo bora kwake


ili aweze kunyoa sehemu ya kichwa chake iliyosalia


wakati wa Hija. Ama mwanamke, yeye atakusanya


nywele zake na kuzipunguza kiasi cha ncha ya kidole


au chini ya hivyo. Mtu aliyehirimia Umrah


atakapofanya kile kilichotajwa, basi Umrah yake


itakuwa imekamilika, na sifa njema ni za Mwenyezi


Mungu. Hapo, kila alichoharamishiwa kwa sababu ya


ihram, sasa kitakuwa halali kwake.


Mwenyezi Mungu atuwezeshe sisi na ndugu zetu


Waislamu wote katika kuifahamu dini yake na kuwa


imara ndani yake, na aikubali kutoka kwa kila mtu.


Kwani, Yeye aliyetakasika ni Mpaji, Mkarimu.


8


Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu


ya mja wake na Mtume wake, Nabii wetu


Muhammad, na aali zake, Maswahaba wake, na


wafuasi wake waliomfuata kwa wema mpaka Siku ya


Malipo.


Mukhtasari Mfupi wa matendo ya ibada za Umrah.


Ulitolewa na Ofisi ya Mheshimiwa, mtunzi wake,


tarehe 13/2/1416 Hijria (Mkusanyiko wa Fatwa na


Makala ya Sheikh, Ibn Baaz 17/425 .


9



Machapisho ya hivi karibuni

Mafungamani ya Shahad ...

Mafungamani ya Shahada na Aina za Tawhiid.

Namna ya swala ya mtu ...

Namna ya swala ya mtume (s.a.w). na Namna ya kutawadha

FADHILA YA SUNNA ZA M ...

FADHILA YA SUNNA ZA MTUME (S.A.W)