
Adabu za safari na hukumu zake
2
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu
wote, na rehema na amani ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad, na aali
zake na Maswahaba zake wote.
Ama baada ya hayo:
Hii ni makala fupi kuhusu adabu za safari na hukumu zake. Tumepupia
ndani yake kuweka wazi mambo ambayo aghalabu anayahitajia msafiri.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aifanye iwe kwa ajili ya uso wake
mtukufu, na anufaishe kwayo Waislamu wote.
Jumuiya ya Masomo mbalimbali ya Kiislamu katika lugha mbalimbali
Adabu za safari na hukumu zake
Kwanza: Adabu za safari
Mwenye kusafiri kwenda Hija au safari nyingine ya kiibada anafaa
kuzingatia yafuatayo:
Amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu amchagulie muda sahihi wa
safari, kipando, rafiki wa kuendana naye, na muelekeo wa njia ikiwa njia
zitakuwa nyingi. Na awatake ushauri kuhusu safari hiyo watu wenye
uzoefu na wale walio wema. Ama Hija na Umra, ibada hizo ni za heri na
hakuna shaka katika hilo. Na namna ya kumuomba Mwenyezi Mungu
amchagulie jambo ni: Aswali rakaa mbili kisha aombe dua iliyopokelewa
kutoka kwa Mtume - remema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
Ni wajibu kwa mwenye kufanya ibada ya Hija na Umra akusudie katika
Hija yake na Umra yake uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kujiweka
karibu naye, na ajihadhari na kukusudia starehe za kidunia au
kujifaharisha au kupata umaarufu au kujionyesha au kutaka kusikiwa;
kwani kufanya hivyo kunasababisha kuharibika kwa matendo na
kutokubaliwa kwake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:ْ
ُلﻗ)ﺎَﻣﱠﻧِإﺎَﻧَأ ٌَرﺷَﺑ ُْمﻛُﻠْﺛﱢﻣﻰَﺣُوﯾﱠﻲَﻟإِﺎَﻣﱠﻧَأ ُْمﻛُﮭَﻟإِ ٌﮫَﻟإِ ٌِدﺣوَاَنﻣَﻓ َنﺎَﻛُوﺟَْرﯾ َءﺎَﻘِ ﻟ ِﮫﱢﺑَر َْلﻣْﻌَﯾْﻠَﻓ ًﻼَﻣَﻋﺎًﺣِﻟﺎَﺻ
ﻻَ و ْْرِكﺷُﯾ ِدَةﺎَ ﺑِﻌِﺑ ِﮫﱢﺑَر(َدًاﺣَأ
"Sema: 'Mimi ni mwanadamu tu kama nyinyi. Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu
wenu ni Mungu Mmoja tu. Kwa hivyo, mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi,
basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake
3
Mlezi.'" Na katika Hadithi takatifu: "Mimi ndiye niliyejitosheleza zaidi
kuhitaji mshirika. Atakayefanya jambo lolote akamshirikisha pamoja
nami mwingine, nitamuacha yeye na shirki yake (au na mshirika
wake)."
Ni wajibu kwa mwenye kufanya ibada ya Hija na Umra kujifunza
hukumu za Umra na Hija, na kujifunza hukumu za safari kabla ya kuanza
safari; ili asijekuwacha jambo la wajibu au akafanya jambo la haramu.
Amesema Mtume -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemtakia heri, humpa ufahamu wa
dini."
Ni wajibu kwa mwenye kukusudia kufanya Hija au Umra achaguwe
mali halali kwa ajili ya ibada yake ya Hija na Umra; kwa sababu Mwenyezi
Mungu ni mzuri na hakubali isipokuwa kilicho kizuri; na kwa sababu mali
haramu husababisha kutojibiwa maombi.
Kutubia madhambi yote na maasi, na ikiwa aliwadhulumu watu,
atarudisha alichokidhulumu na kuwataka wamwachilie. Ni sawa dhuluma
hiyo iwe ni kuhusiana na heshima, mali au haki nyingine.
Inapendekezwa kwa msafiri aandike wasia wake, na kuandika
anachodai na anachodaiwa. Amesema Mtume - rehema na amani za
Mwenyezi Mungu, ziwe juu yake: "Sio haki ya mtu Muislamu mwenye
jambo analotaka kulitolea wasia alale siku mbili, isipokuwa
ahakikishe kwamba anao wasia wake pamoja naye tayari
umeshaandikwa." Na auwekee wasia huo mashahidi, na alipe madeni
anayodaiwa, na arudishe amana kwa wenyewe au awatake idhini
ziendelee kubakia kwake.
Inapendekezwa kwa msafiri ajitahidi kuchaguwa rafiki mwema na
apupie kwamba yule amchaguaye ni miongoni mwa wanafunzi wenye
kujifunza elimu ya sheria; kwani kufanya hivyo ni sababu ya kufanikiwa na
kuepuka kuingia kwenye makosa katika safari yake na katika ibada yake
ya Hija na Umra. Haya ni kwa ushahidi wa maneno ya Mtume, rehema na
amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Mtu huwa katika mwenendo
wa mwendani wake. Basi na aangalie mmoja wenu ni nani
anayemfanya kuwa mwendani wake." Na kwa maneno yake Mtume,
rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Usifuatane katika
safari zako isipokuwa na Muumini na asile chakula chako isipokuwa
mchamungu."
4
Inapendekezwa kwa msafiri kuwaaga watu wake, jamaa zake wa
karibu, majirani zake na marafiki zake. Amesema Mtume, rehema na
amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Yeyote anayetaka kusafiri,
basi na awaambie wale anaowaacha: Astaudiukumullahu alladhiy laa
tadhwiiu wadaa'iuhu (Ninawaacha katika amana ya Mwenyezi
Mungu ambaye amana zake hazipotei)." Na alikua Mtume - rehema na
amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akiwaaga maswahaba zake
anapotaka mmoja wao kusafiri. Alikuwa akisema: "Astaudiullaaha
diinaka, wa amaanataka, wa khawaatiima a'malika (Ninamkabidhi
Mwenyezi Mungu dini yako, na amana yako na mwisho wa matendo
yako)." Na alikuwa Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe
juu yake - akimwambia msafiri mwenye kumtaka Mtume ampe wasia:
"Zawwadaka llaahut taqwa, waghafara dhambaka, wayassara lakal
khaira haithu ma kunta (Mwenyezi Mungu akupe uchamungu, na
akusamehe dhambi zako na aifanye kheri kuwa nyepesi kwako
mahala popote utakapokuwa)." Na alikuja mtu mmoja kwa Mtume -
rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akitaka kusafiri na
akasema: 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipe wasia.' Akasema:
"Ninakuusia kumcha Mwenyezi Mungu, na kuleta Takbiira kila
unapofika sehemu ya muinuko." Alipoondoka, Mtume, rehema na
amani ziwe juu yake, akamuombea kwa kusema: "Ewe Mwenyezi
Mungu, mkunjie ardhi na umfanyie safari yake kuwa nyepesi."
Asiandamane na kengele wala gitaa wala mbwa katika safari; kwa
ushahidi wa Hadithi ya Abuu Huraira - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu
yake - kwamba Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu
yake, alisema: "Malaika hawaandamani na msafara ambao ndani yao
kuna mbwa au kengele."
Na akitaka kusafiri na mmoja kati ya wake zake, ikiwa ni mwenye mke
zaidi ya mmoja ,atawapigia kura ,na mke yeyote atakeyeangukiwa na kura
ndiye atakaye safiri naye, kwa ushahidi wa hadithi ya Aisha - radhi za
Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwamba alisema: "Alikuwa Mtume -
rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akitaka
kusafiri, anapiga kura kati ya wake zake, na yeyote ambaye utatoka
mshale wenye jina lake, basi huyo ndiye aliyekuwa akisafiri pamoja
naye."
Inapendekezwa kwa msafiri asafiri siku ya Alhamisi mwanzo wa
mchana ikiwa ni wepesi kwake; kwa sababu Mtume -rehema na amani za
Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -alikuwa akifanya hivyo. Amesema Kaab
ibnu Maalik - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Ni mara chache
5
sana alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu
yake, akitoka kwenda safarini isipokuwa angetoka siku ya Alhamisi."
Inapendekezwa kwa msafiri aombe dua ya kutoka nyumbani wakati
wa kusafiri na wakati mwingine usiokuwa wa safari. Atasema wakati wa
kutoka: "Bismillahi. Tawakkaltu ala llahi walaa haula walaa quwwata illa
billah. Allahumma inniy auudhubika an- adhwilla au udhwalla, au azilla au
uzalla, au adh-lima au udh-lama, au aj-hala au yuj-hala alaiyya (Kwa jina la
Mwenyezi Mungu. (Ninatoka) nimetegemea kwa Mwenyezi Mungu na
hapana uwezo wala nguvu ila vyote vinatokana na Mwenyezi Mungu. Ewe
Mola wangu wa haki, ninajilinda kwako kutokana na kupotea au
kupotezwa, au kuteleza au kutelezeshwa, au kudhulumu au kudhulumiwa,
au kuwa mjinga au kufanywa mjinga)."
Inapendekezwa kwa msafiri aombe dua ya safari anapopanda
mnyama wake, au gari lake, au ndege, au kipando kingine chochote. Hivyo
atasema: "Allahu Akbar, Allahu Akbar, sub-hanalladhii sakhara lana
haadha, wamaakunna lahuu muqriniina, wainna ilaa rabbina
lamunqalibuuna. Allahumma inna nas-aluka fii safarina haadha al-birra
wat-taqwaa, waminal amali maa tar-dhwaa. Allahumma hawwin 'alaina
safarana haadha, wat-wi 'anna bu'udahu. Allahumma antas-swaahibu
fis-safar, wal-khaliifatu fil-ahli. Allahumma inniy a'udhubika min
wa'athaais-safar, waka-aabatil man-dhwar, wasuu-il munqalabi fil maali
wal-ahli (Mwenyezi Mungu ni mkubwa, Mwenyezi Mungu ni mkubwa,
Mweyezi Mungu ni mkubwa. Utakasifu ni wa Mwenyezi Mungu ambaye
ametutiishia haya na tusengeliweza kuyadhibiti, na kwa hakika kwa Mola
wetu Mlezi bila shaka tutarejea. Ewe Mola wetu wa haki, tunakuomba
katika safari yetu hii wema na uchamungu, na tufanye matendo
unayoyaridhia. Ewe Mola wetu wa haki, tufanyie wepesi safari yetu hii, na
ufupishe umbali wake. Ewe Mola wetu wa haki, hakika Wewe ndiye
mwenza katika safari hii, na mchungaji wa familia yangu. Ewe Mola wetu
wa haki, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na ugumu wa safari, na
ubaya wa mtizamo na kurudi kubaya kwenye mali na familia)."123
Inapendekezwa kwa msafiri asisafiri peke yake pasina kuwa na mtu
wa kufuatana naye; kwa maneno ya Mtume - rehema na amani za
3 Maana ya neno "Wa'athaais-safar" ni ugumu wa safari. Maana hii inapatikana kwenye
kitabu kiitwacho Al-ifswaahu 'an Ma'aani As-swihaah (4/284).
2 Neno hili linamaanisha muonekano mbaya na mtu kuwa katika hali ya kuvunjika
kunakotokana na huzuni. Al-ifswaahu 'an Ma'aani As-swihaah (4/284).
1 Neno "Al-munqalab" ni kurudi. Maana hii inapatikana katika kitabu kiitwacho
Al-ifswaahu 'an Ma'aani As-swihaah (4/284).
6
Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Lau wangetambuwa watu yaliyopo
kwenye upweke ninavyotambuwa mimi, asingesafiri msafiri wakati
wa usiku akiwa peke yake."
Wasafiri wanafaa kumchagua moja wao kuwa kiongozi; ili iwe rahisi
zaidi kukusanya jambo lao pamoja, na kuwafanya kukubaliana zaidi, na
lenye nguvu zaidi katika kupata malengo yao. Amesema Mtume - rehema
na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Watakapotoka watu
watatu katika safari yoyote, basi wamfanye mmoja wao kuwa
kiongozi."
Awe na pupa ya kufanya yale ambayo Mwenyezi Mungu
amemuwajibishia miongoni mwa ibada, na kujiepusha na
yaliyoharamishwa, na ajipambe kwa tabia njema, na amsaidie mwenye
kuhitajia msaada, na atoe elimu kwa mwenye kuitafuta na kuihitajia, na
awe mkarimu kwa mali yake, kwa kuitoa katika masilahi yake mwenyewe
na katika masilahi ya ndugu zake na kuwatekelezea mahitaji yao.
Inafaa aongeze matumizi na vinavyohitajika safarini, kwa kuwa shida
inaweza kumtokea na mambo yakaenda tofauti.
Inafaa awe katika safari ni mwenye uso wa bashasha, roho safi,
akijitahidi kuingiza furaha kwa anayesafiri pamoja naye, ili awazoee
wengine na azoeleke.
Anafaa kuwa na subira kwa kila kinachomkuta miongoni mwa
muamala mgumu wa wenye kusafiri pamoja naye, na wanapokwenda
tofauti na maoni yake, na aamiliane nao kwa namna iliyo nzuri, ili awe ni
mwenye kuheshimiwa baina yao na mwenye kupewa taadhima nyoyoni
mwao.
Inapendekezwa kwa wasafiri wanapofika mahala pa kushukia, wakae
pamoja. Kwa maana, baadhi ya Maswahaba wa Mtume - rehema na amani
za Mweyezi Mungu ziwe juu yake - walikuwa wanapofika sehemu ya
kushukia, wanatawanyika kwenye njia za milimani na mabonde. Akasema
Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika
kutawanyika kwenu na kwenda kwenye njia hizi za milimani na
mabonde kunatokana na Shetani." Kwa hivyo, baada ya hapo wakawa
wanakusanyika pamoja kiasi kwamba ingekunjuliwa nguo juu yao
ingewatosheleza wote.
Inapendekezwa kwa msafiri atakapofika mahala pa kushukia akiwa
katika safari yake au akafika sehemu ya kushukia akiwa hayuko safarini,
aombe dua iliyothibiti kutoka kwake Mtume -rehema na amani za
7
Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Ninajikinga kwa maneno ya
Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari ya alichokiumba."
Kwani hakika akiyasema maneno hayo, hatodhuriwa na kitu chochote
mpaka atakapoondoka mahala pale.
Inapendekezwa amtukuze Mwenyezi Mungu (kwa kusema: Allahu
Akbar) katika sehemu zenye miinuko, na kumtakasa (kwa kusema:
subhanallah) anaposhuka kwenye sehemu na mteremko na mabonde.
Amesema Jaabir - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Tulikuwa
tunapopanda miinuko, tunamtukuza Mwenyezi Mungu (kwa kusema:
Allahu Akbar), na tunapoteremka, tunamtakasa (kwa kusema:
subhanallah)." Na wala wasipaze sauti zao kwa kuleta Takbira. Amesema
Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Enyi watu
zioneeni huruma nafsi zenu. Kwani nyinyi hamumuombi kiziwi wala
aliye mbali. Hakika Yeye yu pamoja nanyi. Hakika Yeye ni Msikivu,
aliye karibu."
Inapendekezwa kwenda safari wakati wa usiku na haswa mwanzo wa
usiku, kwa maneno ya Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu
ziwe juu yake: "Shikamaneni na kusafiri wakati wa usiku, kwani
hakika ardhi hukunjwa wakati wa usiku."
Inapendekezwa kwake azidishe Dua awapo safarini; kwa maneno ya
Mtume - rehema na amani ziwe juu yake: "Dua za aina tatu ni zenye
kukubaliwa bila shaka. Katika dua hizo ni dua ya aliyedhulimiwa,
dua ya msafiri na dua ya mzazi kwa mtoto wake."
***
Pili: Twahara (usafi) katika safari
Ni wajibu kwa msafiri atilie umuhimu usafi wake. Kwa hivyo,
atachukuwa udhu kutokana na hadathi ndogo na ataoga kutokana na
Janaba.
Na ikiwa hakupata maji, au ikiwa ana maji machache anayoyahitajia
kwa ajili ya kupikia na kunywa, basi atafanya Tayammam.
Na namna ya kutayammamu ni: Aipige ardhi kwa mikono (kwa ndani
ya mikono) yake miwili, na aupake uso wake na viganja vyake kwayo.
Twahara ya kutayammam ni twahara ya muda tu. Kwa hivyo, wakati
wowote akipata maji, tayammamu yake inaharibika, na itamlazimu
kuyatumia maji. Na ikiwa alifanya tayammamu kwa sababu ya kupata
Janaba kisha akapata maji, basi itamlazimu kuoga. Na kama akitayammam
8
kwa sababu ya kukidhi haja kubwa kisha akapata maji, basi itamlazimu
atawadhe. Imekuja katika hadithi kwamba: "Udongo safi ni udhu wa
Muislamu hata kama atakosa maji miaka kumi. Akiyapata maji, basi
amche Mwenyezi Mungu na ayagusishe kwenye mwili wake."
Kupangusa juu ya khofu mbili ni jambo la kisheria katika Qur'ani na
Sunnah na ni makubaliano ya Ahlussunnah.
Kuna masharti kadhaa kwa ajili ya kupangusa juu ya khofu mbili na
chenye kufanana na nazo:
1. Khofu mbili hizo au soksi mbili hizi zinapaswa kuwa zinaruhusika
na ni safi.
2. Azifae akiwa na twahara.
3. Ziwe ni zenye kufunika sehemu za faradhi.
4. Iwe kupangusa ni katika kupatwa na hadathi ndogo. Hairuhusiki
kupangusa kwa kupatwa na Janaba wala kwa jambo ambalo linalazimisha
kuoga.
5. Iwe kupangusa ni ndani ya wakati uliowekwa kisheria, nao ni
mchana na usiku kwa mkazi, na michana mitatu na masaa yake ya usiku
kwa msafiri. Muda huu kulingana na kauli sahihi huanzia pale mtu
alipangusa kwa mara ya kwanza ya baada ya kuharibika kwa udhu, na
huisha kwa kutimia masaa 24 kwa mkazi, na kwa masaa 72 kwa msafiri.
Na kupangusaji juu ya khofu hubatilika kwa moja kati ya mambo haya
matatu:
1. Likitokea jambo lenye kuwajibisha kuoga kama vile janaba, basi
kunaharibika kupangusa juu ya khofu na inamlazimu mtu huyo kuoga.
2. Ikiwa atazivua khofu baada ya kuwa amekwishapangusa juu yake.
3. Ikiwa muda unaozingatiwa kisheria utaisha, basi upangusaji
utakuwa batili.
***
Tatu: Hukumu za kupunguza swala safarini
Kupunguza swala katika safari ni bora kuliko kuswali swala kamili;
lakini kama msafiri atakamilisha swala rakaa nne, basi swala yake itakuwa
ni sahihi lakini atakuwa amekwenda kinyume na kilicho bora.
9
Anapunguza swala msafiri atakapokuwa ametoka na kuziwacha kabisa
nyumba zote za kijiji chake au mji wake, na huu ndio msimamo wa
madhebu ya wengi wa maulamaa.
Ikiwa atasafiri baada ya kuingia wakati wa swala, ana haki ya
kupunguza swala kwa sababu amesafiri kabla ya muda wake kwisha.
Ama kukusanya swala kati ya Adhuhuri na Alaasiri na kati ya
Magharibi na Isha, hilo ni Sunna kwa msafiri anapohitajia kufanya hivyo.
Itakapokuwa safari imeshika kasi na imeshaendelea, basi afanye
litakalokuwa rahisi kwake kama vile kutanguliza au kuchelewesha.
Ama ikiwa msafiri hana hitajio la kukusanya, basi asikusanye, mfano
awe ameshuka na kukaa mahala ambapo hataki kuondoka hapo mpaka
ifike saa ya swala inayofuata, basi lililo bora kwake ni kutokusanya. Kwa
sababu hahitaji kufanya hivyo. Na ndiyo maana Mtume - rehema na amani
za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - hakukusanya alipokuwa ameshuka na
kukaa Mina katika Hija ya Kuaga kwa sababu hakuhitaji kufanya hivyo.
Ama swala za sunnah, ataziswali msafiri kwa namna anavyoziswali
mkazi. Kwa hivyo ataswali swala ya Dhuha, Tahajjud, Witiri na zinginezo
miongoni mwa swala za sunna isipokuwa sunna za kabla na baada ya
swala ya Adhuhuri, Maghari na Isha. Sunnah katika hizo ni kuwacha
kuziswali.
Ni sahihi kuswalia swala za sunnah juu ya kipando kama vike ndege,
gari, meli na vyombo vinginevyo vya usafiri. Ama swala za Faradhi, hizo ni
lazima kuteremka kwa ajili ya kuziswalia chini isipouwa
itakaposhindikana.
Swala ya msafiri anayeswali nyuma ya mkazi ni sahihi, na atakamilisha
msafiri kama swala ya imamu wake. Ni sawa ameikuta swala yote au
amekuta rakaa moja au chini ya hivyo. Hata kama ataingia pamoja naye
katika Tashahhud ya mwisho kabla ya kutoa salamu, basi atakamilisha
swala hiyo bila kufupisha. Hivi ndiyo sahihi kutoka katika kauli za
wanazuoni.
***
Nne: Adabu za kurudi kutoka katika ibada ya Hija, Umra au safari
Anapaswa afanye haraka kurudi na wala asikae muda mrefu katika
safari pasina kuwa na haja ya kukaa muda mrefu; kwa maneno ya Mtume
-rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Safari ni kipande
cha adhabu. Inamzuia mmoja wenu kula na kunywa na kulala kwake.
10
Kwa hivyo, akimaliza mmoja wenu hitajio lake, basi na afanye haraka
arudi kwa watu wake."
Na akitaka kurudi kwenye mji wake, atasoma dua ya safari wakati wa
kupanda kwake kipando chake na atazidisha kwa kusema: "Aaibuuna
taaibuuna aabiduuna lirabbina haamiduuna (Tunarejea, tunatubia,
tunafanya ibada na tunamsifu Mola wetu Mlezi)."
Inapendekezwa kwa msafiri wakati wa kurudi kutoka safari yake
aseme kilichothibiti kutoka kwa Mtume - rehema na amani ziwe juu yake -
alipokuwa akirudi kutoka vitani au Hija au Umra. Alikuwa akipiga takbira
katika kila muinuko wa ardhi mara tatu kisha anasema: "Laailaha illa llahu
wahdahuu laashariikalah, lahul mulku walahul hamdu wahuwa 'alaa kulli
shay-in qadiir. Aayibuuna, taaibuuna, saajiduuna, lirabbina haamiduuna.
Swadaqallahu waa'dahu, wanaswara 'ab-dahu, wahazamal ahzaaba
wah-dahu (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi
Mungu mmoja peke yake, asiye na mshirika. Ni wake ufalme na sifa njema
ni zake, naye ni Muweza wa kila kitu. Tunarejea, tunabatubia makosa yetu,
tu naabudu, tunasujudia na tunamsifu Mola wetu Mlezi. Alitimiza
Mwenyezi Mungu ahadi yake, na alimnusuru mja wake, na aliyashinda
makundi ya maadui peke yake)."
Inapendekezwa kwa msafiri atakapouona mji wake, aseme hivi:
"Aayibuuna, taaibuuna, 'aabiduuna, lirabbinaa haamiduuna (Tunarudi,
tunatubia, tunaabudu, na tunamuabudu Mola wetu Mlezi)" na
ayarudirudie maneno hayo mpaka auingie mji wake. Hii ni kwa sababu
Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alifanya
hivyo.
Asije kwa mke wake usiku ikiwa alika mbali kwa muda mrefu pasina
kuwa na haja ya kuja usiku isipokuwa ikiwa aliwafikishia kuwa anakuja, na
akawapa habari kwamba atafika usiku. Hii ni kwa sababu Mtume - rehema
na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikataza hilo. Amesema
Jaabir ibnu Abdillah - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao: "Mtume -
rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikataza
kwamba mwanamume asiwapigie hodi familia yake usiku." Na
miongoni mwa hekima ya kutofanya hivyo, ni vile riwaya nyingine
ilivyotafsiri: "Ili mwanamke mwenye nywele zilizotimka achane nywele
zake, na mwanamke ambaye mumewe hayuko anyoe nywele za sehemu za
siri." (4) Na katika riwaya nyingine:4 "Alikataza Mtume -rehema na
4 Neno "Ash-shaa'tha" linamaanisha mwanamke mwenye nywele matimtimu ambazo
hazijapakwa mafuta kwa muda mrefu. Na "Al-istihdaad" ni kutumia alaa iliyotengenezwa
11
amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - mwanamume kuwagongea
watu wa familia yake usiku ili kuchunguza kama wanamfanyia
khiyana au kutafuta makosa yao."
Inapendekezwa kwa mwenye kutoka safarini aanzie msikiti ambao
upo jirani naye na aswali humo rakaa mbili; kwa sababu Mtume -rehema
na amani ya Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa akifanya hivyo
Inapendekezwa kwa msafiri atakapofika kutoka safarini, awaonyeshe
huruma watoto wa nyumbani kwake na majirani zake na awafanyie wema
watakapompokea. Imepokelewa kutoka kwa Ibnu Abbas - radhi za
Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwamba alisema: Alipofika Mtume,
rehema na amani ziwe juu yake, katika mji wa Makkah, walimpokea
watoto wadogo wa Banii Abdul Mutwalib. Basi akambeba mtoto mmoja
mbele yake na mwingine mgongoni kwake." Naye Abdullahi ibnu Jaafar -
radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alisema: "Alikuwa Mtume
-rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - anaporudi
kutoka safarini, analakiwa pamoja nasi. Basi siku moja alilakiwa
pamoja nami na Hassan au Hussein na akambeba mmoja wetu mbela
yake na mwingine nyuma yake mpaka tunaingia Madinah."
Inapendekezwa kutoa zawadi, kwa kuwa kutoa zawadi kuna furahisha
nyoyo na kuondoa chuki. Na inapendekezwa kuikubali zawadi na kulipa
juu yake. Na inachukiza kuikataa pasina kuwepo kizuizi cha kisheria.
Ndiyo maana amesema Mtume -rehema na amani za Mwenyezi Mungu
ziwe juu yake: "Peaneni zawadi, mtapendana." Na zawadi ni sababu
miongoni mwa sababu za kuleta upendo baina ya Waislamu.
Akifika msafiri katika mji wake, imependekezwa kukumbatiana, kwa
sababu ya yale yaliyothibiti kutoka kwa Maswahaba wa Mtume - rehema
na amani za Mwenyezi mungu ziwe juu yake - kama alivyosema Anas -
radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Walikuwa wanapokutana,
wanasalimiana mikononi, na wanaporudi kutoka safarini,
wanakumbatiana."
***
kwa chuma kama vile wembe katika kunyoa sehemu za siri. Nalo neno "Al- maghiiba" ni
mwanamke ambaye mume wake amekaa mbali na yeye kwa muda mrefu. Tazama
At-Tahriir fii sharh Swahih Muslim, cha Al-Asbahaaniy (292)
12
Yaliyomo
Adabu za safari na hukumu zake 3
Kwanza: Adabu za safari 3
Pili: Twahara (usafi) katika safari 8
Tatu: Hukumu za kupunguza swala safarini 9
Nne: Adabu za kurudi kutoka katika ibada ya Hija, Umra au safari 10
13