Nakala

Muhutasari wenye 


faida kwa muislamu 


mpya 


  


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye 


kurehemu 


Utangulizi 


Baada ya hayo 


Amewatukuza Mwenyezi Mungu wanadamu na akawafanya 


kuwa bora zaidi kuliko viumbe wake wengi, amesema Mwenyezi 


Mungu Mtukufu: {Na hakika tumewatukuza wanaadamu} (58), 


Ana majina mazuri na sifa za hali ya juu amezithibitisha sifa hizo 


yeye mwenyewe, na akamthibitishia sifa hizo Mtume wake -Rehema 


na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- sifa hizo zimefikia 


upeo wa ukamilifu na uzuri, hakuna chochote mfano wake naye ni 


mwenye kusikia na mwenye kuona. 


Al- rahmaan: Mwenye huruma ya hali ya juu, na yenye kuenea 


viumbe vyake vyote. 


Al- qadiir" Mwenye uwezo uliokamilika hawi mwenye kushindwa 


wala kuchoka. 


Al- malik: yeye ni mwenye kusifika na sifa ya tukufu na ushindi na 


upangiliaji wa mambo, mwenye kumiliki mambo yote na 


kuyaendesha atakavyo. 


Al- samiiu: Ambaye ana diriki kuvisikia vyote vyenye kusikika kwa 


siri na kwa wazi. 


Al- salaam: Aliye salimika na kila upungufu ubaya na aibu. 





Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Al- baswiir: ambaye uoni wake umezunguka kila kitu hata kikiwa 


cha ndani mno na kidogo, mwenye uoni wa vitu, mwenye kuvijua na 


mwenye kuviona undani wake. 


Al- wakiil: Mwenye kusimamia Riziki za waja wake, na 


kuwasimamia masilahi yao, na mwenye kuwapenda vipenzi vyake na 


akawafanyia wepesi na akawatosheleza mambo mbalimbali. 


Al- khaaliq: Mletaji wa vitu na mgunduzi wake kwa namna 


ambayo hakuna mfano wake kabla yake. 


Al- latwiif: Ambaye anawakirimu waja wake na kuwarehemu na 


kuwapa wanachomuomba. 


Al- kaafi: Ambaye huwatosheleza waja wake mambo yote 


wanayoyahitajia kwake. 


Al- ghafuur: Ambaye anawakinga waja wake na shari ya 


madhambi yao, na wala hawaadhibu kwa madhambi hayo. 


Anafikiria muislamu maajabu ya muumba na uwepesi wake, na 


miongoni mwa ajabu ni kutilia umuhimu viumbe kwa udogo wake, 


kwa kupupia kuwalisha na kuwachunga mpaka waweze kujitegemea 


wenyewe, basi kutakasika kwa machafu ni kwake yeye muumba wa 


viumbe na mwenye kuvihurumia, na katika kuvionea huruma 


viumbe, ameviandalia vitu vyenye kuvisaidia na vyenye kutengeneza 


hali zake licha yakuwa viumbe hivyo vina madhaifu makubwa. 


Mtume wangu Muhammad - Rehema na amani za Allah ziwe juu 


yake- 


Muhammad - Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- ni 


Rehema iliyotolewa zawadi. 





Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Naye ni Muhammad mtoto wa Abdillah -Rehema na amani za 


Allah ziwe juu yake- mwisho wa manabii na mitume, alimtuma 


Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa dini ya uislamu kwa watu wote, ili 


awajulishe mambo ya kheri na mambo makubwa katika hiyo kheri ni 


Tauhiid, na anawakataza mambo ya shari na jambo kubwa la shari ni 


ushirikina. 


Ujumbe wake na ujumbe wa manabii wote waliokuwa kabla yake 


ni kulingania katika kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake hana 


mshirika wake. 


Qur'ani tukufu ni maneno ya Mola 


wangu 


Qur'ani tukufu ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo 


ameyateremsha kwa Mtume wake Muhammad- Rehema na amani 


za Allah ziwe juu yake- ili awatoe watu kutoka katika giza 


kuwapeleka katika nuru na kuwaongoza katika njia iliyonyooka. 


Yeyote 


atakayeisoma 


atapata 


malipo 


makubwa, na 


atakayeufanyia kazi muongozo wake basi atakuwa amefuata njia 


iliyo sawa. 


Najifunza nguzo za uislamu. 


Amesema Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake: 


"Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: (Uislamu 


umejengwa juu ya mambo matano: Ni kushuhudia kuwa hapana 


Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila ni Mungu mmoja na kwamba 


Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu na kusimamisha swala 





Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


na kutoa zaka na kufunga Ramadhan na kuhiji katika nyumba tukufu 


ya Mwenyezi Mungu". 


1- Ni kushuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa 


haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake na Muhammad ni 


mtume wa Mwenyezi Mungu. 


Amesema Allah Mtukufu:  





 "Basi tambua ya kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki 


ila Mwenyezi Mungu" [Surat muhammad 19] 


Maana ya kushuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa 


kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu: yaani hakuna muabudiwa wa 


haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. 


Kusimamisha swala kunakuwa kwa kutekeleza kwa namna 


ambayo ameelekeza Mwenyezi Mungu Mtukufu na akatufundisha 


Mtume wake-Rehema na amani za Allah ziwe juu yake-. 


Nguzo ya tatu: Kutoa zakah. 


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:  





Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


]


 (Na toeni zaka) [Al-baqara 110]. 


110





 Nayo ni haki ya wajibu katika mali itakapokuwa imefikia kiwango 


maalumu, hupewa aina nane alizozitaja Mwenyezi Mungu katika 


Qur'ani tukufu, miongoni mwao ni mafukara na masikini. 


Na katika kuitekeleza kwake kuna kusifika kwa sifa ya huruma na 


upole, na kusafisha tabia za muislamu na mali yake, na kuziridhisha 


nafsi za mafukara na masikini na kuyapa nguvu mafungamano ya 


kimapenzi na udugu kati ya mtu mmoja mmoja katika jamii ya 


kiislamu, na kwa hivyo muislamu mwema huitoa zaka kwa moyo safi 


na 


kufurahia utekelezaji wake, kwa sababu kutoa zaka 


kunafurahisha watu wengine. 


Na kiwango cha zaka ya mali ni 2.5% katika mali iliyolimbikizwa 


miongoni mwazo ni Dhahabu na fedha, na pesa tasilim na bidhaa za 


biashara zilizo andaliwa kwa ajili ya kuuza na kununua ili kupata 


faida; zinapofikia thamani yake kiwango maalumu na zikazungukiwa 


na mwaka mzima. 


Kama ambavyo ni wajibu kutoa zaka kwa mwenye kumiliki idadi 


maalumu ya wanyama wafugwao (Ngamia, Ngo'mbe, na mbuzi) 


ikiwa wanakula majani ya malishoni mwaka mzima pasina kulishwa 


na mwenye wanyama. 


Na hivyo hivyo ni wajibu kutoa zaka kwa kinachotoka katika ardhi 


miongoni mwa nafaka na matunda, madini na hazina ikiwa zitafikia 


kiwango maalumu. 





 





Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


 


Nguzo ya Nne: kufunga Ramadhani: 


Amesema Allah Mtukufu:  





{Enyi mlioamini Mmefaradhishiwa kufunga, kama 


Walivyofaradhishiwa wale waliokuwa kabla yenu, ili mpate kumcha 


Mwenyezi Mungu}. [Al-baqara 183]. 


Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa tisa katika mwaka 


wa mpangilio wa Hijria (kuanzia kuhama mtume) nao ni mwezi 


mtukufu kwa waislamu, na una nafasi yake maalumu kuliko miezi 


mingine katika mwaka, na kuufunga mwezi huo ni moja ya nguzo 


tano za uislamu. 


Kufunga mwezi wa ramadhani: ni kumuabudu Mwenyezi Mungu 


mtukufu kwa kujizuia na kula na kunywa na kufanya tendo la ndoa, 


na vyote vyenye kufunguza, kwanzia kuchomoza jua mpaka kuzama 


jua katika siku zote za mwezi wa ramadhani wenye baraka. 


Nguzo ya tano Kuhiji nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu. 


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:  





Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


 "


 Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye hijja 


katika nyumba hiyo tukufu kwa mwenye kuweza kufunga safari ya 


kwenda huko " . [Al-Imran: 97].  


Hijja inakuwa kwa mwenye uwezo wa kufunga safari kwenda 


huko mara moja katika umri wake, nako ni kukusudia nyumba 


tukufu na viwanja vitukufu vya Makkah kwa ajili ya kutekeleza ibada 


maalumu katika wakati maalumu, na hakika alifanya hijja Mtume 


Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- na pia mitume wengine 


walifanya hijja kabla yake, na akamuamrisha Mwenyezi Mungu 


ibrahim -Amani iwe juu yake- awaite watu kuja kutekeleza ibada ya 


hijja kama alivyolieleza hilo Mwenyezi Mungu Mtukufu katika 


Qur'an tukufu akasema:  





 Na tukamwambia utangaze kwa watu habari za hijja watakujia 


wengine kwa miguu na wengine juu ya kila mnyama aliyekonda kwa 


uchovu wa safari watakujia kutoka kila njia ya mbali " [Al Haji: 27]. 


Najifunza nguzo za imani: 


Na kutenda kwa viungo vya nje: kama vile swala na kuhijji, na 


kufunga n.k. na viungo vya ndani vyenye kuhusiana na moyo kama 


kumpenda Mwenyezi Mungu na kunyenyekea, na kutegemea kwake 


na kumtakasia ibada yeye. 


Na wanaielezea wabobezi kwa ufupi kuwa Imani ni kuitakidi 


moyoni, na kutamka kwa ulimi na kutenda kwa viungo, nayo inazidi 


kwa kutii na hupungua kwa maasi. 


10 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Kumuamini Mwenyezi Mungu kunapelekea kupwekesha katika 


uumbaji wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na 


kunajumuisha mambo yafuatayo: 


Kuamini uwepo wake kutakasika na machafu ni kwake na 


mtukufu. 


Kuamini uumba wake kutakasika na machafu ni kwake na 


mtukufu, na kuwa yeye ni mmiliki wa kila kitu, na muumba wake na 


mwenye kuruzuku na mwendeshaji wa mambo yake. 


Kuamini Uungu wake -kutakasika ni kwake- na kuwa yeye ndiye 


anayestahiki kuabudiwa peke yake hana mshirika wake kwa 


chochote, ibada hizo ni: kama vile swala, na dua, na kuweka nadhiri, 


na kutaka msaada, na ibada zingine zote. 


Kuamini majina yake mazuri na sifa zake za hali ya juu ambazo 


amezithibitisha yeye mwenyewe au mtume wake Muhammad- 


Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akapinga 


sifa alizozipinga katika nafsi yake au kazipinga Mtume- Rehema za 


Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- miongoni mwa majina na 


sifa, na kuwa majina yake na sifa zake zimefika ukomo wa ukamilifu 


na uzuri, na kuwa yeye hakuna chenye kufanana naye naye ni 


mwenye kusikia na kuona. 


Nguzo ya pili: Kuwaamini Malaika: 


Na hao Malaika ni viumbe wakubwa hakuna awezaye kudhibiti 


nguvu zao na idadi yao isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na 


kila mmoja katika wao ana sifa na majina na kazi zao ambazo 


amezifanya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa maalumu kwao tu, na 


miongoni mwao ni Jibrili- Amani iwe juu yake- aliyewakilishwa kwa 


11 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


ajili ya wahyi anateremka nao kutoka kwa Mwenyezi Mungu 


kwenda kwa mitume wake. 


Nguzo ya tatu: Kuamini vitabu: 


Na vitabu vya mbinguni ambavyo amevitaja Mwenyezi Mungu 


katika kitabu chake ni: 


Qur'ani tukufu: Aliiteremsha Mwenyezi Mungu kwa mtume wake 


Muhammad - Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- 


Zabuur: Aliiteremsha Mwenyezi Mungu kwa mtume wake Daudi- 


Rehema na amani ziwe juu yake 


Nguzo ya Nne : Kuwaamini mitume. 


Ni kusadikisha kusikokuwa na shaka kwamba Mwenyezi Mungu 


ametuma katika kila umma mtume, anawalingania watu 


kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika wake, na 


kupinga kila kinachoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu 


Mtukufu. 


Na kuwa mitume wote hao ni wanadamu wanaume na ni waja 


wa Mwenyezi Mungu, nakuwa wao ni wakweli na wenye 


kukubaliwa, ni wacha Mungu na ni waaminifu, ni waongofu 


walioongoka, na akawatia nguvu Mwenyezi Mungu kwa miujiza 


yenye kujulisha ukweli wao, na hakika wao walifikisha yote 


aliyowatuma Mwenyezi Mungu, na kuwa wao wote walikuwa 


kwenye haki na muongozo uliokuwa wazi. 


Na kwa hakika ulinganiaji wao ulikuwa mmoja kwanzia wa 


mwanzo wao mpaka wa mwisho wao katika msingi wa dini, nao ni 


12 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


kumpwekesha Mwenyezi Mungu- aliyetakasika na Kutukuka- katika 


kumuabudu na kutokumshirikisha. 


Nguzo ya Tano: Kuamini siku ya 


mwisho. 


Amesema Allah Mtukufu:  





 "Mwenyezi Mungu, Ambaye hapana Mola apasaye kuabudiwa 


kwa haki ila yeye, Ndiye Atakaye wakusanya nyinyi Siku ya Kiyama 


isiyokuwa na shaka, kwa kuhesabiwa na kulipwa. Na hakuna yeyote 


mkweli zaidi wa maneno anayoyatolea habari kuliko Mwenyezi 


Mungu". [Al-nisaa 87]. 


Ni kusadikisha kusikokuwa na shaka kila kinachohusiana na siku 


ya mwisho miongoni mwa yale aliyoyaeleza Mola wetu mtukufu 


katika kitabu chake kitukufu au aliyotusimulia Mtume Muhammad 


Rehema na Amani ziwe juu yake- kama kufa mwanadamu, na 


kufufuliwa kukusanywa, na uombezi, na mizani, na hesabu, pepo, na 


moto, na mengine yasiyokuwa hayo yenye kuhusiana na siku ya 


mwisho. 


Nguzo ya sita: Kuamini Qadar kheri zake na shari zake. 


Amesema Allah Mtukufu:  


13 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 





 "Hakika sisi kila kitu tumekiumba kwa kipimo chake mahsusi". 


[Al- qamar 49]. 


Kuamini kuwa kila jambo linalotokea kwa viumbe miongoni mwa 


matukio ya duniani, basi hutokea kwa kujua Mwenyezi Mungu, na 


amelikadiria- kutakasika na machafu ni kwake- na upangiliaji wake 


yeye peke yake hana mshirika wake, nakuwa haya makadirio 


yameandikwa kabla ya kuumbwa mwanadamu, na hakika 


mwanadamu anamatashi, na yeye ndiye mfanyaji wa vitendo vyake 


kiuhakika, lakini vyote hivyo havitoki nje ya ujuzi wa Mwenyezi 


Mungu matashi yake na kupenda kwake. 


Na Kuamini Qadari kunakuwa katika ngazi Nne nazo ni: 


Ngazi ya pili: Kuamini aliyoyaandika Mwenyezi Mungu kwa kila 


lililopo mpaka kusimama kiyama. 


Ngazi ya tatu: Kuamini matashi ya Mwenyezi Mungu yenye 


kutekelezwa na uwezo wake uliotimia, basi lolote alitakalo huwa na 


asilolitaka haliwi. 


Ngazi ya Nne: Kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ni muumba wa 


kila kitu, hana mshirika wake katika kuumba kwake. 


Ninajifunza Kutawadha (Udhu) 


Na Amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu 


yake na amani- (Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, hutoka 


madhambi yake mwilini mwake). 


14 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Basi huenda mja kwa Mola wake hali yakuwa ni mwenye 


kujisafisha usafi wa kihisia (unaoonekana) kwa kutawadha, na usafi 


wa kimaana (usioonekana, kama usafi wa moyo) kwa kutekeleza 


ibada hizi, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kufuata 


muongozo wa Mtume -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe 


juu yake-. 


Yanayopaswa kufanywa ukiwa na Udhu: 


1- Swala ya aina yoyote sawa iwe ya Faradhi au iwe ya Sunnah. 


2- Kutufu Al-qaaba (nyumba tukufu) 


Nina tawadha na Ninaoga kwa kutumia maji safi. 


Maji safi ni kila maji yaliyoteremka toka mbinguni, au 


yakachimbuka kutoka ardhini na yakabakia katika asili ya umbile 


lake, na hayakubadilika moja kati ya sifa zake tatu, nazo ni, Rangi, 


Ladha, na Harufu, hayakubadilika kwa kitu chenye kuondosha usafi 


wa maji. 


Hatua ya kwanza: (1) Kutia nia na mahala pake ni moyoni, na 


maana ya nia: ni kuazimia moyoni kufanya ibada kwa kujikurubisha 


kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. 


Hatua ya pili: (2) kuosha viganja viwili: 


Hatua ya tatu (3) kusukutua. 


Kusukutua ni Kuingiza maji mdomoni na kuyazungusha humo, 


kisha kuyatoa. 


Hatua ya Nne: Kupandisha maji puani: 


15 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Kupandisha maji puani: ni kuyavuta maji kwa pumzi mpaka 


kwenye kilele cha pua. 


Kisha kuyatoa: nako ni kutoa kila kilichoko ndani ya pua miongoni 


mwa kamasi na vinginevyo kwa kuvuta pumzi. 


16 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Mipaka ya uso: 


Na weupe ni ule uliopo kati ya nywele na nyama ya sikio. 


Na nywele ambazo ziko juu ya mfupa uliotokeza, unaoelekeana 


na tundu la sikio lenye kupita mpaka ndani ya kichwa na kutumbukia 


mpaka kigingi cha sikio. 


Na vile vile kunakusanya kuosha uso kila kilichoko wazi kuanzia 


nywele nyingi za ndevu na zilizo shuka katika ndevu. 


Hatua ya sita: Kuosha mikono miwili kwa kuanzia ncha za vidole 


vya mikono miwili mpaka kwenye fundo mbili. 


Na huingia kwenye fundo mbili kuosha mikono miwili 


iliyofaradhishwa. 


Hatua ya saba: Kukipaka maji kichwa kizima pamoja na masikio 


mawili mara moja . 


Ataanza mwanzo wa kichwa chake akienda na mikono yote 


mpaka kichogoni kisha atairudisha mpaka sehemu aliyoanzia. 


Na ataingiza vidole vyake viwili ndani ya masikio yake. 


Na akifuatishia kwa vidole gumba juu ya mgongo wa masikio 


yake, na atapaka hivyo nje ya masikio yake na ndani. 


Hatua ya Nane: Kuosha miguu miwili kuanzia vidole vya miguu 


miwili mpaka kwenye kongo mbili, na huingia kwenye kongo mbili 


kuosha miguu miwili iliyofaradhishwa. 


Kongo mbili ni: mifupa miwili iliyoota chini ya miundi. 


17 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Na udhu huharibika kwa mambo haya yafuatayo: 


1- kutoka kitu katika moja ya njia mbili kama mkojo, na haja 


kubwa, na upepo, na manii, na madhii. 


2- Kuondokwa na akili kwa kulala usingizi au kuzimia, au kulewa, 


au kupatwa na wenda wazimu. 


3- kila chenye kulazimisha kuoga kama janaba, na Hedhi, na 


Nifasi. 


Na akikidhi mwanadamu haja yake anapaswa kuondosha najisi, 


ima kwa maji safi, na hii ndiyo njia bora zaidi, au pasina kutumia 


maji safi kwa vitu vinavyoondosha najisi kama mawe na karatasi na 


vitambaa na mfano wake. na kwa sharti iwe kuondoa huko ni kwa 


kufuta mara tatu au zaidi kwa kitu chenye kutakasa na kilicho safi na 


halali kukitumia. 


Kufuta juu ya Khofu mbili au soksi mbili 


Katika hali ya kuvaa khofu mbili au soksi mbili, basi yawezekana 


kufuta juu yake pasina kuwa na haja ya kuosha miguu miwili, kwa 


masharti ambayo ni: 


1- 


Ziwe 


zimevaliwa baada ya twahara iliyokamilika 


iliyosababishwa ima na hadathi ndogo au kubwa ambapo ilioshwa 


katika twahara hiyo miguu miwili. 


2- Ziwe khofu au soksi mbili ni twahara na si zenye najisi. 


Na iwe upakaji ni katika muda uliowekwa kwa ajili hiyo. 


4- Na khofu hizo au soksi ziwe ni halali, zisiwe kwa mfano ni za 


wizi au za kupora. 


18 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Khofu mbili: ni zile zenye kuvaliwa katika mguu, na hutokana na 


ngozi nyembamba na mfano wake, na mfano wa khofu ni viatu 


vinavyositiri miguu miwili. 


Soksi mbili ni: ni zile ambazo huzivaa mtu mguuni mwake 


zinazotokana na kitambaa na mfano wake na ndiyo zinazojulikana 


kwa jina la (Shurraab). 


Hekima ya kuweka sheria ya kufuta juu ya khofu mbili: 


Hekima ya kuweka sheria ya kufuta juu ya khofu mbili: nikufanya 


wepesi kwa waislamu, ambao inakuwa kwao ni taabu kuvua khofu 


na soksi na kuosha hasa miguu miwili katika wakati wa masika na 


baridi kali na safarini. 


Muda wa kupaka: 


Mkaazi: (asiye kuwa msafiri) atapaka usiku na mchana (masaa 24) 


Na Msafiri: atafuta siku tatu na usiku wake (masaa 72) 


Ataanza kuhesabu muda wa kufuta kuanzia mwanzo wa kufuta 


khofu mbili au soksi mbili baada ya kupatwa na hadathi. 


Sifa za ufutaji juu ya khofu mbili au soksi mbili: 


1- Hulowanishwa mikono miwili: 


2- Hupitishwa mkono juu ya unyayo kuanzia kwenye vidole 


mpaka mwanzo wa muundi 


3- Hupakwa unyayo wa kulia kwa kutumia mkono wa kulia na 


unyayo wa kushoto kwa mkono wa kushoto. 


Venye kuharibu ufutaji: 


19 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


1- Vyote vyenye kuwajibisha kuoga: 


2- Kuisha muda wa kupaka: 


20 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Kuoga : 


Ikitokea kwa mwanaume au mwanamke kitendo cha kujamiiana, 


au wote wawili yakawatoka manii kwa kutamani wakiwa katika hali 


ya kulala au kuamka, ni wajibu juu yao kujitwaharisha, na vile vile 


mwanamke akitwaharika kutoka kwenye Hedhi na nifasi ni wajibu 


kwake kuoga kabla ya kuanza kutekeleza swala au kufanya mambo 


ambayo yanalazimu twahara. 


Na sifa ya kuoga ni kama ifutavyo: 


Na aueneze muislamu mwili wake wote kwa maji kwa njia yoyote 


ile, na katika hayo ni kusukutua, na kupandisha maji puani, na ikiwa 


ataeneza mwili wake kwa maji, itaondoka kwake hadathi kubwa, na 


itakuwa imetimia twahara yake. 


Hutahadharishwa mwenye janaba kufanya mambo yafutayo 


mpaka aoge: 


01- Kuswali: 


02- Kutufu Al-qaaba (nyumba tukufu) 


03- Kukaa msikitini na yafaa kwake kupita tu pasina kukaa. 


04- Kushika msahafu 


05- Kusoma Qur'ani 


Kutayammam 


Ikiwa hajapata muislamu maji ambayo atajitwaharishia au 


hakuweza kuyatumia maji kutokana na maradhi na mfano wake na 


21 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


akahofia usimpite wakati wa swala basi atatayamamu kwa kutumia 


udongo. 


Na sifa zake ni apige pigo moja kwa mikono yake miwili kisha 


apake kwa mikono hiyo uso wake na viganja vyake tu, na ni sharti 


udongo uwe twahara. 


Na Tayamamu huharibika kwa mambo yafuatayo: 


1- Huharibika Tayamamu kwa kila chenye kuharibu Udhu. 


2- Yakipatikana maji kabla ya kuanza ibada ambayo 


ametayamamu kwa ajili yake 


Amemfaradhishia Mwenyezi Mungu Muislamu kusali swala tano 


usiku na mchana nazo ni: Al-fajiri, na Adhuhuri, na Alaasiri, na 


Magharibi, na Ishaa. 


Najiandaa kwa ajili ya swala 


Ukiingia muda wa swala hujitwaharisha muislamu kutokana na 


hadathi (Uchafu) ndogo na kubwa, ikiwa amepatwa na hadathi 


kubwa. 


Na hadathi kubwa ni: kila kinachomlazimisha muislamu kuoga. 


Na hadathi kubwa ni: kila kinachomlazimisha muislamu 


kutawadha. 


Husali muislamu akiwa katika twahara na katika sehemu safi 


kutokana na Najisi, akiwa ameusitiri uchi wake. 


Anajipamba muislamu kwa mavazi yanayofaa wakati wa swala na 


husitiri kwa mavazi hayo mwili wake, na haifai kwa mwanaume 


22 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


wakati wa kuswali aache wazi sehemu yoyote kuanzia sehemu ya 


kitovuni mpaka magotini. 


Ni wajibu kwa mwanamke kuusitiri mwili wake wote ndani ya 


swala isipokuwa uso na viganja viwili. 


Hazungumzi muislamu akiwa katika swala maneno yasiyokuwa 


maalumu kwa ajili ya swala, na kumsikiliza imamu, na wala asigeuke 


geuke katika swala yake, na ikiwa atashindwa kuyahifadhi maneno 


maalumu kwa ajili ya swala, basi atamtaja mola wake na kumsabbihi 


mpaka amalize swala. 


Ninajifunza Swala: 


Hatua ya kwanza 1: Kutia nia kwa ajili ya faradhi ninayotaka 


kuitekeleza, na mahala pake ni moyoni. 


Baada ya kutawadha naelekea Qibla, na ninaswali nikiwa 


nimesimama ikiwa naweza kufanya hivyo. 


Hatua ya pili 2: Nina inua mikono yangu miwili usawa wa mabega 


mawili na ninasema (Allahu Ak-baru) huku nikinuia kuingia katika 


swala 


Ninasoma baada ya suratil faatiha kilicho chepesi kwenye Qur'ani 


katika rakaa ya kwanza na ya pili tu katika kila swala, na kusoma 


huku siyo lazima lakini kufanya hilo kuna malipo makubwa. 


Hatua ya 6; Ninasema (Allahu akbaru) Mwenyezi Mungu ni 


mkubwa-kisha nina rukuu mpaka unakuwa mgongo wangu 


umelingana sawa na mikono yangu miwili inakuwa juu ya magoti 


mawili hali ya kutawanya vidole, kisha ninasema katika kurukuu 


(Ametakasika Mola wangu Mtukufu). 


23 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Hatua ya 7: Ninainuka kutoka kwenye kurukuu kwa kusema 


(Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumuhimidi) 


Hatua ya Nane 8: Ninasema (Mwenyezi Mungu ni mkubwa) 


Hatua ya tisa 9: Ninasema: Allahu akbaru (Mwenyezi Mungu ni 


mkubwa na ninainuka kutoka kwenye kurukuu mpaka ninalingana 


sawa) hali ya kunyoosha mgongo huku nikikalia mguu wa kushoto 


na nikiusimamisha mguu wa kulia, na ninasema (Rabbihg-firly)- ewe 


Mola wangu nisamehe. 


Hatua ya kumi 10: Ninasema (Allahu akbaru) Mwenyezi Mungu ni 


mkubwa -na ninasujudu mara nyingine tena mfano wa sijda ya 


kwanza. 


Hatua ya kumi na moja 11: Nina inuka kutoka katika sujudu na 


ninasema: (Allahu Ak-baru) mpaka niwe sawa nikiwa nimesimama, 


na ninafanya hivyo katika rakaa zilizobakia kama nilivyofanya katika 


rakaa ya kwanza. 


Hatua ya kumi na mbili 12. Kisha baada yake nitageuka upande 


wa kulia na kusema "Assalaam alaikum warahmatullahi" kisha 


nageuka upande wangu wa kushoto nakusema Assalamu alaikum 


warahmatullahi" na kwa kufanya hivyo ninakuwa nimekamilisha 


sala. 


Stara ya mwanamke wa kiislamu: 


Na huchunga mwanamke wa kiislamu katika mavazi yake mipaka: 


Kwanza: Vazi kuenea mwili mzima. 


Pili: Lisiwe vazi analolivaa mwanamke ni kwa ajili ya kujipamba. 


24 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Tatu: Na lisiwe jepesi linaloonyesha mwili wake 


Nne: Liwe pana na siyo finyu likasifu sehemu ya mwili wake 


Katika sifa za waumini: 


Ni mkweli katika mazungumzo yake wala hasemi uongo. 


Anatekeleza ahadi na miadi. 


Hatendi uovu katika ugomvi. 


Anatekeleza amana. 


Anampendelea ndugu yake muislamu anayoyapenda katika nafsi 


yake. 


Ni mkarimu. 


Anaridhika na alichokipanga Mwenyezi Mungu na anamshukuru 


katika hali ya raha na husubiri katika hali ya matatizo. 


25 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


Anasifika nakuwa na haya. 


Moyo wake umesalimika na vinyongo na mwili wake umesalimika 


na kuwashambulia watu wengine. 


Anawasamehe watu. 


Hali Riba wala hafanyi miamala ya riba. 


Hafanyi zinaa. 


Hanywi pombe. 


Anawatendea wema majirani zake. 


Hadhulumu wala kufanya hiyana. 


Haibi walala hafanyi hila za kuiba. 


Ni mwenye kuwatendea wema wazazi wawili, hata kama siyo 


waislamu, na huwatii kwenye mambo mema. 


Na huwalea watoto wake kwa tabia njema, na anawaamrisha 


kutekeleza wajibu wa sheria, na anawakataza kufanya mambo 


machafu na ya haramu. 


Hajifananishi kwa matendo yasiyokuwa ya waislamu katika 


mambo yao maalumu ya kidini au Ada zao ambazo zimekuwa alama 


na nembo yao. 


Na kwa hakika ametuweka Mwenyezi Mungu katika ulimwengu 


huu kwa hekima kubwa na wala hakutuumba kimchezo mchezo; na 


lengo ni kumuabudu yeye peke yake hana mshirika wake, na 


akatuwekea dini ya kimalezi iliyotimia na kuenea, hupangilia mambo 


26 


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya 


yetu yote maalumu na yasiyokuwa maalumu, na imehifadhi sheria 


hii yenye uadilifu mambo ya dharura katika maisha, na mambo hayo 


ni: kuhifadhi Dini yetu, na nafsi, na heshima, na akili, na mali, na 


mwenye kuishi kwa kufuata maamrisho ya sheria na akawa ni 


mwenye kujiepusha na mambo ya haramu kwa hakika mtu huyo 


atakuwa kahifadhi dharura hizi, na ataishi kwa furaha na mwenye 


matumaini katika maisha yake bila shaka. 


Na mahusiano haya makubwa ni hali ya hisia zinazobebwa na 


kuneemeka kwa kumuabudu mwingi wa rehema, na kuwa na 


shauku ya kukutana naye na kuuchochea moyo wake kupaa katika 


anga ya furaha kwa kuhisi kwake utamu wa imani. 


Ndiyo ikiwa atahisi mwanadamu kila wakati yuko mbele ya 


muumba wake, na akamjua kwa majina yake na sifa zake zilizo nzuri, 


na akamuabudu kama vile anamuona, na akatakasa ibada yake kwa 


ajili ya Mwenyezi Mungu, na wala hakukusudia katika Ibada hiyo 


isipokuwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu -kutakasika ni kwake


, ataishi maisha mazuri yenye furaha katika dunia na mwisho mzuri 


huko akhera. 


Hata matatizo ambayo yanamtokea muumini katika dunia, kwa 


hakika joto lake huondoka kwa baridi ya yakini, na kuridhia Qadari 


ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumshukuru yeye kwa Qadari 


zake kheri zake na shari zake na kuridhika kwa hayo yote kwa 


ukamilifu. 


Na rehema na amani za Allah ziwe juu ya Mtume wetu 


Muhammad na ali zake na Maswahaba zake. 


 



Machapisho ya hivi karibuni

MASWALI SITINI KATIKA ...

MASWALI SITINI KATIKA HUKUMU ZA HEDHI NA NIFASI

Muhutasari wenye fai ...

Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya