
MASWALI SITINI KATIKA HUKUMU ZA HEDHI NA
NIFASI
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
UTANGULIZI:
Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimuendee Mtume wa Allah,
Muhammad bin Abdillah na wafuasi wake na maswahaba wake na kila atakayepita katika njia yake
mpaka siku ya malipo, baada ya hayo:
Dada yangu Muislam!
Tukitazama maswali mengi ambayo wanaulizwa wanachuoni kuhusiana na hukumu za hedhi katika
ibada, tukaona tuyakusanye maswali yote yanayojirudia mara nyingi, na mara nyingi yanatokea bila
kurefusha, na hilo ni katika kutaka kufupisha.
Dada yangu Muislamu!
Jitihada zetu za kuyakusanya maswali haya, ni ili yawe mikononi mwako daima, hilo linatokana na
umuhimu wa utambuzi wa sheria ya Allah, ili uweze kumuabudu Allah kwa ujuzi na maarifa.
Angalizo: Inaweza kuonekana kuwa baadhi ya maswali yemejirudia kwa yule atakayekipitia kitabu hiki
kwa mara ya kwanza, lakini baada ya mazingatio ataona katika maswali hayo kuna ziada ya elimu katika
jibu moja ziada ambayo haipatiani katika jibu lingine, tukaona tusiyaache maswali hayo.
Kwa utangulizi huu: Tunaomba-Rehema na amani ziwe juu- ya Muhammad na wafuasi wake wote na
Maswahaba wake wote.
*
MIONGONI MWAHUKUMUZAHEDHIKATIKASWALANA
SWAUMU:
Swali la 1:Akitwaharika mwanamke baada ya swala ya Alfajiri, je ajizuie na afunge swaumu siku hiyo?, na
je siku hiyo itahesabika kwake kuwa kafunga au atatakiwa kuilipa siku hiyo?
Jawabu la 1:Akitwaharika mwanamke baada ya kuchomoza Alfajiri, wanachuoni wana kauli mbili juu ya
mwanamke huyu katika kujizuia kula na kunywa na tendo la ndoa mchana wa siku hiyo.
Kauli ya kwanza: Atalazimika kujizuia kula, kunywa, na tendo la ndoa katika masaa yaliyobakia kwa siku
hiyo, lakini haitohesabika kwake siku hiyo, bali atawajibika kuilipa, na hii ndio kauli ya wanachuoni wengi
katika madhehebu ya Imam Ahmad-Allah amrehemu
Kauli ya pili: Hatolazimika kujizuia kula, kunywa, na tendo la ndoa mchana wa siku hiyo, kwa sababu
haikubaliki funga kwa siku hiyo, kwa sababu mwanzo wa siku alikuwa kwenye hedhi, na aliye katika hedhi
hafai kufunga, na kwakuwa swaumu yake si sahihi, basi hakuna faida ya kujizuia kula, kunywa, na tendo
la ndoa, na wakati wa siku hiyo si wakati wa kuheshimiwa kwa upande wake, kwa sababu ameamrishwa
kula mwanzo wa mchana, bali ni haramu kwake kufunga mwanzo wa mchana,Na swaumu ya kisheria: Ni
kujizuia na vyote vyenye kufunguza kwa lengo la kumwabudu Allah toka kuchomoza alfajiri mpaka
kuzama kwa jua.
Na kauli hii-kama unavyoiona- ina nguvu zaidi kuliko kauli ya kwanza ya kujizuia, lakini kwa kauli zote
hizi mbili itamlazimu kulipa siku hii.
Swali la 2:Atakapotwaharika aliyekuwa na hedhi, na akaoga josho kubwa baada ya swala ya Alfajiri, na
akaswali, na akaikamilisha swaumu ya siku yake ile, je anawajibika kulipa siku hiyo?
Jawabu la 2:Atakapo twaharika Mwanamke aliyekuwa katika hedhi kabla ya kuchomoza Alfajiri hata kwa
dakika moja, lakini akapata yakini kuwa ametwaharika, ikiwa ni katika Ramadhani basi atalazimika
kufunga, na inakuwa funga yake siku hiyo ni sahihi, na wala halazimiki kuilipa siku hiyo, kwa sababu
amefunga akiwa ametwaharika, hata kama hakuoga josho kubwa ila baada ya Alfajiri basi hakuna
tatizo.Kama vile Mwanaume akiwa katika janaba lililotokana na tendo la ndoa au kujiotea, na akala daku
na wala hakuoga janaba ila baada ya Alfajiri, funga yake itakuwa sahihi.
kwa uhusiano huu, napenda kutoa angalizo la jambo lingine kwa wanawake, pindi mwanamke atakapo
ijiwa na hedhi, na alikuwa kafunga siku hiyo, baadhi ya wanawake hudhania kwamba hedhi itakapowajia
baada ya kufungua kabla ya kuswali swala ya Ishaa funga yao ya siku hiyo inakuwa imeharibika,Jambo
hilo halina dalili katika sheria, bali hedhi itakapo muijia mwanamke baada ya magharibi walau kwa muda
mchache basi funga yake inakuwa imetimia na ni sahihi.
Swali la 3:Je ni lazima kwa wanawake wenye Nifasi kuswali na kufunga wakitwaharika kabla ya siku
arobaini?
Jawabu la 3:Naam, muda wowote atakapo twaharika mwanamke mwenye nifasi kabla ya siku Arobaini
basi ni lazima juu yake kufunga ikiwa ni ndani ya Ramadhani, ni lazima juu yake kuswali, na inafaa kwa
mume wake kumuingilia; Kwa sababu yuko twahara, hakuna kitu kinachomzuia kufunga na hakuna
kinachomzuia kuswali wala kufanya tendo la ndoa.
Swali la 4:Ikiwa mzunguko wa mwezi wa mwanamke ni siku nane au siku saba, kisha mzunguko wake
ukaendelea mara moja na mara nyingine zaidi ya siku hizo, ni ipi hukumu yake?
Jawabu la 4:Ikiwa mzunguko wa mwanamke huyu ni siku sita au saba, kisha muda wa kuwa na damu
ukarefuka, ukawa siku nane, au saba, au kumi, au kumi na moja, basi hatoswali mwanamke huyu mpaka
atwaharike,Na hilo ni kwa sababu Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- hakuweka ukomo maalumu
wa siku za mzunguko wa hedhi.
]، Na amesema Allah
Mtukufu: "Na wanakuuliza kuhusu hedhi, sema: Huo ni uchafu" [Al-baqara: 222],Muda wowote damu hii
ikiwepo basi mwanamke atabaki katika hali hiyo mpaka atwaharike, na aoge josho kubwa, kisha aswali,
na ukija mwezi wa pili siku zimepungua ukilinganisha na mwezi wa kwanza, basi akitwaharika ataoga
hata kama mwezi huu haukuwa kama ule uliopita.
Na jambo la msingi nikuwa; Muda wowote mwanamke akiwa katika mzunguko wa hedhi basi hatoswali,
uwe mzunguko huo una siku kama mzunguko uliopita, au zimezidi au zimepungua, atakapotwaharika
ataswali.
Swali la 5:Je mwanamke mwenye nifasi anakaa siku arobaini haswali na hafungi, au kinachozingatiwa ni
kukatika ile damu, muda wowote ikikatika anakuwa katwaharika na ataswali, na ni upi muda mchache wa
kutwaharika?
Jawabu la 5:Damu ya uzazi haina wakati maalumu, muda wowote damu ikiwepo atakaa, hatoswali,
hatofunga, na hatoingiliwa na mumewe.
Na pindi akiona katwaharika-hata kabla ya siku arobaini, hata kama hakukaa isipokuwa siku kumi au
tano- basi ataswali, atafunga, na ataingiliwa na mumewe, wala hakuna tatizo katika hilo.
Na jambo la msingi nikuwa; Nifasi ni jambo linahisika, linafungamana na hukumu za kisheria kwa kuwepo
kwake na kutokuwepo kwake, muda wowote ikiwepo basi zinathibiti hukumu zake, na muda wowote
akitwaharika basi hukumu za nifasi hatohusika nazo.
Lakini lau zikizidi zaidi ya siku sitini basi damu hiyo itakuwa ni damu ya ugonjwa, atakaa muda ule ambao
unawafikiana na muda wake wa hedhi pekee, kisha ataoga, na ataswali.
Swali la 6:Litakapo dondoka tone dogo la damu ya hedhi mchana wa Ramadhani, na ikaendelea damu hii
kumtoka mwanamke ndani ya mwezi wa Ramadhani naye anafunga, je funga yake ni sahihi?
Jawabu la 6:Ndio, swaumu yake ni sahihi, ama haya matone si chochote, yanatokana na mishipa ya
damu, imepokewa kutoka kwa Ally bin Abi twalib-Allah amridhie- amesema: "Hakika matone haya
ambayo yanakuwa mithili ya damu inayotoka puani si hedhi" hivyo ndivyo alivyosema radhi za Allah ziwe
juu yake.
Swali la 7:Mwanamke mwenye hedhi au nifasi akitwaharika kabla ya Al fajiri, je swaumu yake iko sahihi
au la?
Jawabu la 7:Naam, iko sahihi swaumu ya Mwanamke mwenye hedhi atakapo twaharika kabla ya Al fajiri,
na hakuoga josho kubwa la kujitwaharisha isipokuwa baada ya Al fajiri, na hukumu hii ni pamoja na
wanawake walio katika nifasi, kwa sababu kwa wakati huo ni katika watu wanaotakiwa kufunga, na huu ni
mfano wa aliyepatwa na janaba, na ikachomoza Alfajiri akiwa na janaba, swaumu yake ni sahihi;
]، Kutokana na
kauli yake Allah-Mtukufu-: "Na sasa hivi waingilieni na tafuteni yale aliyowaandikieni Allah kwa ajili yenu,
na kuleni na kunyweni mpaka ibainike kwenu nyinyi weupe wa alfajiri ya kweli itokanayo na giza la usiku"
(Al baqara: 187)Na akiruhusu Allah kumuingilia mwanamke mpaka ibainike Alfajiri ya kweli basi
inamlazimu katika hilo kusiwe na kuoga josho kubwa isipokuwa baada ya kuchomoza Alfajiri, kutokana na
hadithi ya Aisha-Radhi za Allah ziwe juu yake- kwamba Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake
alikuwa akiamka asubuhi akiwa na janaba kutokana na kumuingilia mkewe naye akiwa katika
swaumu.Yaani: Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- haogi janaba isipokuwa baada ya kuchomoza
Alfajiri.
Swali la 8:Mwanamke akihisi damu ya hedhi,na Damu hiyo haikutoka kabla ya magharibi, au akahisi
maumivu ya mzunguko wake, je inafaa swaumu yake siku hiyo, au ni wajibu kwake kuilipa?
Jawabu la 8:Pindi akihisi mwanamke aliyotwaharika kuja kwa damu ya hedhi akiwa amefunga, lakini
haikutoka mpaka baada ya kuzama kwa jua, au alihisi maumivu kwa sababu ya hedhi, lakini haikutoka
isipokuwa baada ya kuzama kwa jua, basi swaumu yake hiyo siku ni sahihi, hatoirudia swaumu ile ikiwa
ni swaumu ya lazima, na wala haziharibiki thawabu zake kwa hilo ikiwa ni swaumu ya sunna.
Swali la 9:Pindi mwanamke atakapoona damu, na hakuwa na uhakika kama ni damu ya hedhi, je ni ipi
hukumu ya swaumu yake siku hiyo?
Jawabu la 9:Swaumu yake siku hiyo ni sahihi; Kwa sababu asili ni kutokuwa na hedhi mpaka ibainike
kwake kwamba ile ni hedhi.
Swali la 10:Baadhi ya wakati, mwanamke anaona athari ya damu chache ikiwa katika hali ya matone
yakimtoka katika nyakati tofauti tofauti ndani ya siku moja, baadhi ya wakati anaziona wakati wa
mzunguko wake wa kisheria na mzunguko ukiwa bado haujamtoka, na mara nyingine anaziona wakati
ambao sio wa mzunguko wake, ni ipi hukumu ya swaumu yake katika hizo hali mbili.
Jawabu la 10:Limetangulia jawabu linalofanana na swali hili muda si mrefu lakini kilichobaki ikiwa haya
matone yanatokea katika siku za mzunguko, ikiwa hivyo yatazingatiwa kama ni hedhi ambayo unaijua,
inakuwa ni hedhi.
Swali la 11:Je mwanamke aliye katika mzunguko wa hedhi na nifasi anakula na kunywa mchana wa
Ramadhani?
Jawabu la 11:Ndio, wanakula na kunywa katika mchana wa Ramadhani, lakini bora ikawa kula huko ni
kwa siri akiwa ana watoto ndani ya nyumba kwa sababu jambo hilo huleta tatizo kwa watoto wakiona mtu
anakula mchana wa ramadhani.
Swali la 12:Akitwaharika mwenye hedhi au nifasi muda wa Alasiri, je analazimika kuswali swala ya
Adhuhuri na Alasiri, au je halazimiki kuswali isipokuwa Alasiri peke yake?
Jawabu la 12:Kauli yenye kutegemewa katika swala hili nikuwa: Analazimika kuswali swala ya Alasiri
pekee kwa sababu hakuna dalili juu ya ulazima kwake kuswali Adhuhuri, na asili ni kutokuwa na dhima ya
jambo na Nabii-Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:"Atakaye upata wakati wa swala ya Alasiri
kwa kiwango cha rakaa moja kabla jua halijazama basi ameipata Lasiri",Na hakutaja kwamba amediriki
Adhuhuri, ingekuwa swala ya Adhuhuri ni lazima kwa mtu huyu basi angebainisha Nabii-Rehema na
amani ziwe juu yake- na mwanamke akitokwa na damu ya hedhi, baada ya kuingia wakati wa Adhuhuri
basi haimlazimu akitwaharika kulipa isipokuwa swala ya Adhuhuri pekee na hatolipa Alasiri pamoja na
kwamba swala ya Adhuhuri hujumuishwa na swala ya Alasiri na wala hakuna tofauti kati yake na sura
iliyoulizwa katika swali.
Na kuhusu suala hili, kauli ya kutegemewa nikwamba halazimiki isipokuwa swala ya Alasiri pekee
kutokana na dalili ya kisheria na kiyasi (Kuoanisha mambo), na hivyo hivyo ikiwa ametoharika kabla ya
kutoka wakati swala ya Ishaa, basi halazimiki isipokuwa kuswali swala ya ishaa peke yake, wala
halazimiki kuswali swala ya Magharibi.
Swali la 13:Baadhi ya wanawake ambao zinatoka mimba zao, haiwi hali zao isipokuwa: Ujauzito ukitoka
kabla mtoto hajaumbwa tumboni, au mimba ikatoka baada ya kuumbwa kiumbe na ukadhihiri muundo wa
umbile lake, ni ipi hukumu ya swaumu siku hiyo ambayo katokwa na mimba ile, na swaumu za siku
ambazo ataiona damu inatoka?
Jawabu la 13:Ikiwa mtoto hajaumbwa tumboni basi damu itakayomtoka si damu ya uzazi, na juu ya hili
basi atafunga na kuswali na swaumu yake ni sahihi.
Na ikiwa mtoto ameumbwa basi damu itakayomtoka ni damu ya nifasi, haifai kwake kuswali katika hali
hiyo, wala haruhusiwi kufunga swaumu.
Na kanuni na kigezo katika swala hili ni kuwa; Ikiwa mtoto ameumbwa basi damu itakayomtoka ni damu
ya uzazi (nifasi), na ikiwa hajaumbwa basi damu itakayomtoka siyo damu ya nifasi, na ikiwa damu
itakayomtoka ni damu ya uzazi (nifasi) haitofaa kwake yote yale yasiyofaa kwa wanawake wanaotokwa
na damu ya uzazi (nifasi) na ikiwa si damu ya uzazi (nifasi) basi hatoharamishiwa juu yake
anayoharamishiwa mwanamke mwenye nifasi.
Swali la 14:Mwanamke mjamzito akitokwa na damu mchana wa Ramadhani, je jambo hili lita athiri
swaumu yake?
Jawabu la 14:Itakapotoka damu ya hedhi na mwanamke akiwa amefunga basi funga yake itaharibika,
kutokana na kauli ya Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake-"Hivi haikuwa wakati alipokuwa katika
mzunguko wake wa hedhi haswali wala hafungi?"Na kwa ajili hii tunazingatia hili ni katika mambo
yanayofunguza swaumu, na damu ya uzazi ni mfano wake, na kutoka damu ya hedhi na nifasi vinaharibu
funga ya mtu.
Na mwanamke mjamzito akitokwa na damu mchana wa ramadhani basi ikiwa ni hedhi basi hiyo ni hedhi
kama ilivyo hedhi ya mwanamke asiye mjamzito, na inaathiri swaumu yake, na ikiwa siyo hedhi basi
haiathiri funga yake.
Na damu ya hedhi ambayo inaweza mtokea mwanamke mwenye mimba ni damu ya hedhi ambayo
haikatiki kwake tangu kubeba ujauzito huo, bali inamjia katika zile nyakati zake alizozizoea kuwa damu ya
hedhi humuijia, basi hedhi hii kwa kauli yenye kutegemewa inathibiti kwake na inachukua hukumu za
hedhi ya kawaida.
ama ikikatika damu hiyo ya hedhi naye bado mjamzito, kisha ikawa baada ya hapo anaona damu katika
wakati ambao siyo wa mzunguko wake wa kisheria, hili haliathiri funga yake, kwa sababu hii si hedhi.
Swali la 15:ikiwa mwanamke anaona damu siku moja akiwa katika mzunguko wake, na siku inayofuata
haoni damu mchana kutwa, ni kipi juu yake anatakiwa kufanya?
Jawabu la 15:Linalo onekana ni kwamba, hii twhara au ukavu (katika sehemu za siri) uliopatikana wakati
wa siku zake za hedhi, utafuata (hukumu za) hedhi, hautohesabika kama ni twhara, pamoja na hilo
ataendelea kujizuia kwa yale anayojizuia kwayo mwanamke aliye katika hedhi.
Na wamesema baadhi ya wanachuoni: Mwanamke mwenye kuona damu siku moja, na siku nyingine
akaona yuko twahara, basi ile damu (aliyoiona) ni hedhi, na ule usafi (aliouona) ni twahara mpaka zifike
siku kumi na tano.Na ikifika siku ya kumi na tano, inakuwa damu itokayo baada ya hapo ni damu ya
ugonjwa (Istihadhwa). Na hili ndilo limetajwa kuwa ni sahihi na wanachuoni wengi katika madhehebu ya
Imam Ahmad ibn Hanbali (Allah amrehemu).
Swali la 16:Katika siku za mwisho za hedhi au kabla ya kutwaharika, mwanamke ikiwa haoni athari ya
damu ya hedhi, je anaruhusiwa kufunga siku hiyo? ikiwa haoni maji maji meupe yakitoka katika tupu
yake, au afanye nini?
Jawabu la 16:Ikiwa ni kawaida ya mwanamke, haoni maji maji meupe kama ilivyo kwa baadhi ya
wanawake basi mwanamke huyu atafunga swaumu yake, na ikiwa kawaida yake anaona maji maji
meupe, basi hatofunga mpaka aone maji maji hayo yamekatika.
Swali la 17:Ni ipi hukumu ya mwanamke mwenye hedhi na anaetokwa damu ya uzazi (Nifasi) kusoma
Qur'ani akiwa anatizama au kile alichohifadhi katika hali ya dharura, mfano yeye ni mwanafunzi au ni
mwalimu?.
Jawabu la 17:Hakuna tatizo kwa mwanamke aliye katika hedhi au damu ya uzazi (Nifasi) kusoma Qur'ani
ikiwa ni kwa hitajio, kama vile mwalimu wa kike, au mwanafunzi wa kike ambaye anasoma uradi wake
(kiwango anachohitaji kusoma katika Qur'ani) usiku au mchana.
Ama kisomo-Namaanisha: Kusoma Qur'ani kwa ajili ya kutafuta ujira na thawabu za kisomo-jambo bora
asisome; kwa sababu wanawachuoni wengi au wengi wao wanaona kwamba mwanamke aliye katika
hedhi haifai kwake kusoma Qur'ani.
Swali la 18:Je analazimika mwanamke aliye katika hedhi kubadili nguo zake baada ya kutwaharika,
pamoja na kuwa nguo hizo hazikudondokewa na damu yoyote wala uchafu wowote?.
Jawabu la 18:Haimlazimu yeye kufanya hivyo, kwa sababu hedhi haichafui (hainajisi) mwili, bali damu ya
hedhi inachafua inacho kutana nacho pekee na kwa hili Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake
aliamrisha wanawake pindi zinapogusa damu za hedhi nguo zao wasafishe pale palipopatwa na damu
kisha waswalie nguo zao.
Swali la 19:Mwanamke amefungua katika Ramadhani siku saba, alikuwa akitokwa damu ya uzazi, na
hakulipa siku hizi mpaka akajiwa na Ramadhani ya pili, na akazungukiwa katika Ramadhani ya pili na
siku saba ambazo alikuwa ananyonyesha (hakufunga) kwa hoja alikuwa na maradhi, na imekaribia
kuingia Ramdhani ya tatu, tupeni faida, Allah awalipeni thawabu.
Jawabu la 19:Ama akiwa mwanamke huyu kama alivyojieleza-kuwa yeye ni mgonjwa na wala hawezi
kulipa-, basi wakati wowote akiweza kulipa basi na afunge; kwa sababu yeye ana udhuru hata kama ikija
Ramadhani ya pili.
Ama ikiwa mwanamke huyu hana udhuru wowote ule, alikuwa akijifanya mgonjwa na anafanya uzembe,
huyu hairuhusiwi kwake kuchelewesha kulipa Ramadhani mpaka Ramadhani ya pili.Amesema Aisha
(Radhi za mwenyezi mungu ziwe juu yake na amani): "alikuwa nikidaiwa swaumu ambayo natakiwa
kulipa, basi siwezi kuzilipa isipokuwa katika mwezi wa Shaaban".
Na kwa namna hiyo, ni juu ya mwanamke huyu aitizame nafsi yake, ikiwa hana udhuru basi anapata
dhambi, na juu yake kutubia kwa Allah, na apupie kulipa swaumu zilizo juu yake, ikiwa ana udhuru
hakuna shida juu yake, hata kama ikichelewa mwaka au miaka miwili.
Swali la 20:Baadhi ya wanawake wanaingiwa na Ramadhani ya pili na wao hawajafunga baadhi ya siku
katika Ramadhani iliyopita, ni lipi jambo la lazima juu yao kufanya?.
Jawabu la 20:Jambo la lazima juu yao: Kutubia kwa Allah juu ya jambo hili; kwa sababu haifai kwa
mwenye deni la swaumu za Ramadhani akachelewesha mpaka Ramadhani ya pili bila udhuru; kutokana
na kauli ya Aisha-Radhi za Allah ziwe juu yake- "Ilikuwa ninaokuwa na deni la swaumu natakiwa kulipa,
basi siwezi kuzilipa isipokuwa katika mwezi wa Shaaban".
Na hii inaonyesha ya kwamba haiwezekani kuchelewesha kulipa mpaka ramadhani ya pili, ni juu yake
atubie kwa Allah-mshindi aliyetukuka- kwa yale aliyoyafanya, na alipe siku alizoziacha baada ya
ramadhani ya pili.
Swali la 21:Mwanamke atakapo tokwa na damu ya hedhi adhuhuri, akiwa hajaswali swala ya adhuhuri, je
analazimika kuilipa swala ile baada ya kutwaharika?
Jawabu la 21:Katika hili kuna tofauti baina ya wanachuoni, wapo wanaosema haimlazimu mwanamke
huyu kuilipa swala hii, kwa sababu hakufanya uzembe na wala hatopata dhambi; na kwakuwa
anaruhusiwa kuichelewesha swala mpaka ukikaribia mwisho wa wakati wa swala.
Wengine wanasema: Analazimika kuilipa, namaanisha kuilipa swala ile iliyompita kabla ya hedhi kutoka,
kutokana na ujumla wa maneno ya Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake-"Atakaye idiriki rakaa katika
swala basi amediriki swala"
Na kwa kujiepusha kuingia katika madhambi: Bora ailipe, maana ni swala moja, hakuna ugumu katika
kuilipa.
Swala la 22:Atakapo ona mjamzito damu kabla ya kujifungua kwa siku moja au siku mbili, je ataacha
kufunga na kuswali kwa ajili ya damu hiyo au lipi afanye?
Jawabu la 22:Mjamzito atakapoiona damu siku moja au siku mbili kabla ya kujifungua, huku akiwa na
uchungu wa kujifungua, basi damu hiyo ni damu ya uzazi (Nifasi), kwa ajili ya damu hiyo hatoswali na
wala hatofunga, isipoambatana damu hiyo na uchungu wa kujifungua, basi damu hiyo iliyoharibika
haizingatiwi, na wala haimzuii mwanamke kufunga wala kuswali.
Swali la 23:Ni yapi maoni yako kuhusu kumeza vidonge vya kuzuia mzunguko wa mwezi wa damu ya
hedhi kwa ajili ya Kufunga pamoja na watu?
Jawabu la 23:Mimi ninatahadharisha kuhusu hilo, na hilo ni kwa sababu vidonge hivi vina madhara
makubwa, limethibiti hilo kwangu kupitia matabibu, na anaambiwa mwanamke: Hilo jambo ameliandika
Allah kwa mabinti wa Adam, basi tosheka kwa lile alilokuandikia Allah Mtukufu, na ufunge siku ambazo
hakuna kizuizi, kitakapo patikana kizuizi basi fungua kwa kuridhia yale ambayo Allah Mtukufu amekadiria.
Swali la 24:Mwanamke baada ya miezi miwili tangu kukatika kwa damu ya uzazi (Nifasi), akaanza kuona
vitone vidogo vya damu, je atafungua, na wala hatoswali? au ni kipi atafanya?.
Jawabu la 24:Matatizo ya wanawake katika damu ya hedhi na damu ya uzazi (Nifasi) ni bahari isiyo na
ufukwe, na katika sababu za matatizo hayo: Matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba au kuzuia damu ya
hedhi, na watu hawakuwa wakijua matatizo haya mengi,Sahihi, haya matatizo yalikuwepo tangu
alipopewa Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- Utume, bali yalikuwepo tangu alipopatikana
mwanamke, lakini kwa wingi wake katika sura hii ambayo anafikia mwanadamu haelewi namna ya
kutatua matatizo haya, hili ni jambo la kuhuzunisha sana.
Lakini kanuni ya ujumla: Mwanamke akitwaharika, akaona kutwaharika baada ya damu ya hedhi na damu
ya uzazi: Yakatoka maji maji meupe wanayajua wanawake- basi baada ya mwanamke kutwaharika
ukitoka uchafu, unjano, au tone, au unyevu, hivi vyote si hedhi, na havimzuii vitu hivyo kuswali, kufunga
na wala havizuii tendo la ndoa baina ya mwanaume na mwanamke kwa sababu vitu hivyo si damu ya
hedhi.Alisema Ummu Atwiyah: "Tulikuwa hatuoni unjano na uchafu kuwa ni kitu"amesimulia Al Bukhari na
akazidisha Abu Daud: (wakiona vitu hivyo) Baada ya kutwaharika.Mtiririko wa wapokezi wake ni sahihi.
Na kuhusu hili tunasema: Kila kitakachotokea katika vitu hivyo baada ya kutwaharika kwa uhakika, vitu
hivyo havimdhuru mwanamke na wala havimzuii kuswali swala zake, na kufunga swaumu zake, na
havimzuii kuingiliwa na mume wake lakini ni lazima kwa mwanamke huyu asifanye haraka asubiri mpaka
aone kuwa katwaharika.Kwa sababu baadhi ya wanawake damu ikikauka, hufanya haraka na
hujitoharisha kwa kuoga kabla hajaona kule kutwaharika kunakotakiwa.Na kwa hivyo, walikuwa
wanawake walioishi kipindi cha Mtume wakiagiza Kursuf yaani; pamba yenye damu, iende kwa mama wa
waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, alikuwa akiwaambia; Msifanye haraka mpaka muone maji
maji meupe ambayo hutoka baada ya hedhi kumalizika.
Swali la 25:Baadhi ya wanawake damu inaendelea, na wakati mwingine inakatika siku moja au siku mbili
kisha inarejea, je ni ipi hukumu katika hali hii kuhusu swaumu yake na swala yake na ibada zingine.
Jawabu la 25:Linalofahamika kwa wanachuoni walio wengi ni kwamba: Mwanamke anapokuwa katika
siku zake, zikiisha siku zake, basi anajitwaharisha kwa kuoga, na ataswali na kufunga na atakacho kiona
baada ya hapo siku moja au siku mbili si hedhi kwa sababu siku chache za kutoharika baina ya hedhi
mbili kwa wanachuoni hawa ni siku kumi na tatu.
Na wamesema wanachuoni wengine kwamba: Bali kwa mwanamke huyu atakapo ona damu basi hiyo ni
hedhi, na wakati wowote akitwaharika basi ametwaharika, hata kukiwa hakuna baina ya hedhi ya kwanza
na ya pili siku kumi na tatu.
Swali la 26:Lipi bora kwa mwanamke: Akaswali usiku ndani ya mwezi wa Ramadhani nyumbani kwake,
au msikitini, hasa hasa msikitini kukiwa na mawaidha na ukumbusho? Ni upi muongozo wako kwa
wanawake ambao wanaswali msiktini?.
Jawabu la 26:Bora akaswali katika nyumba yake, kutokana na ujumla wa kauli ya Mtume-Sala na salama
ziwe juu yake-"Na Nyumba zao ni bora kwao wao"Na ni kwa sababu mwanamke kutoka nyumbani kwake
hakujasalimika na fitna katika nyakati nyingi, na kuwa mwanamke kubakia nyumbani kwake ni bora
kwake, kuliko kutoka kwenda msikitini, ama mawaidha na mazungumzo ya kheri inawezekana akayapata
kupitia kanda.
Na muongozo wangu kwa wanawake ambao wanaswalia msikitini: Watoke katika nyumba zao wakiwa
hawaja jipamba kwa mapambo, wala kujipulizia manukato.
Swali la 27:Ni ipi hukumu ya mwanamke kuonja chakula mchana wa Ramadhani akiwa amefunga.
Jawabu la 27.Hukumu yake: Hakuna shida juu ya jambo hilo, akiwa na haja ya jambo hilo, lakini akiteme
kile alichokionja (asimeze).
Swali la 28:Mwanamke kapata ajali, na alikuwa mwanzo wa mimba yake, mimba ikatoka baada ya
kutokwa na damu nyingi, je inajuzu kwake kufungua, au anaendelea kufunga? Akifungua je atapata
dhambi?
Jawabu la 28:Tunasema: Hakika mjamzito hatokwi na damu ya hedhi, kama anavyosema Imam Ahmad:
Wanawake wengi hujua ujauzito kwa kukatika hedhi,na hedhi kama walivyosema Wanawachuoni,
ameiumba Allah-Mtukufu- kwa hekima ya kuwa ni chakula cha mtoto aliye tumboni, mimba itakapo anza
hedhi hukatika.
Lakini baadhi ya wanawake inaweza ikaendelea kwake damu ya hedhi kama kawaida kama ilivyokuwa
kabla ya mimba, huyu atahukumiwa kuwa hedhi yake ni hedhi ya kawaida, kwa sababu hedhi kwake
iliendelea na wala haikuathirika na mimba, hedhi hii itamzuia na yale yote ambayo yanayozuiwa na hedhi
ya siku zote ya mwanamke asiyemjamzito, hivyo, itawajibisha yale ambayo yanawajibika kwa mwenye
hedhi, na itadondosha yale yote ambayo yanadondoshwa na hedhi ya kawaida (ikiwemo swala n.k)
Na kwa ufupi ni kwamba: Damu inayomtoka mjamzito iko katika aina mbili:
Aina moja wapo inahukumiwa kuwa ni hedhi, nayo ni ile ambayo inaendelea kutoka kwake kama
ilivyokuwa ikitoka kabla ya mimba, basi maana ya jambo hili ni; Mimba haijamuathiri, hii itakua ni hedhi ya
kawaida.
Na aina ya pili, ni damu inayotoka wakati wa mimba, ima kwa sababu ya ajali, au alibeba kitu, au
kudondoka toka juu ya kitu fulani na mfano wake, damu hii si hedhi, bali ni damu ya ugonjwa.kwa hiyo,
haimzuii damu hii kuswali, wala kufunga, bali anakuwa katika hukumu ya wanawake waliotoharika.
Lakini ajali ikisababisha mtoto kushuka au mimba ambayo iliyokuwa tumboni, atakuwa kama
walivyosema Wanawachuoni: Mimba ikitoka na imebainika kwake umbile la mwanadamu, basi damu
itakayotoka baada ya kutoka mtoto itahesabika kuwa ni damu ya uzazi, ataacha kuswali, na kufunga, na
mumewe atajitenga naye mpaka atwaharike.
Na akitoka mtoto ambaye hajakamilika basi haizingatiwi kuwa ni damu ya uzazi, bali ni damu iliyoharibika,
haimzuii mwanamke kuswali, wala kufunga, wala kingine chochote.
wamesema Wanachuoni: Muda mchache ambao kinabainika kiumbe: Ni siku themanini na moja; kwa
sababu mtoto yupo tumboni kwa mama yake.Kama alivyosema Abdullah bin Masoud-Radhi za Allah
ziwe juu yake- Ametuhadithia mkweli mwenye kusadikishwa, akisema: "Hakika mmoja wenu hukusanywa
umbile lake katika tumbo la mama yake siku arobaini, kisha linakuwa pande la damu mfano wa siku hizo,
kisha linakuwa pande la nyama mfano wa siku hizo, kisha hutumwa Malaika na anaamrishwa kuandika
mambo manne; kuandika riziki yake, kifo chake, muovu au mwema".Na wala haiwezekani kuumbwa
kabla ya hizo siku, mara nyingi kiumbe hakibainiki kabla ya siku tisini, kama walivyosema baadhi ya
Wanachuoni.
Swali la 29:Mimi ni mwanamke ilitoka mimba ikiwa katika mwezi wa tatu, mwaka umepita sasa, na
sikuswali mpaka nilivyotwaharika, waliniambia, ulikuwa unatakiwa kuswali, basi kipi natakiwa kufanya, na
mimi sifahamu idadi ya siku maalumu?.
Jawabu la 29.Jambo linalofahamika kwa wanawachuoni ni kwamba: Mwanamke pindi itakapotoka mimba
yake ikiwa imetimiza miezi mitatu basi yeye hatoswali, kwa sababu aliyetoka ni mtoto aliyebainika umbile
lake na damu inayotoka inakuwa ni damu ya uzazi hivyo hatoswali ikiwa inatoka damu hiyo.
wanasema wanachuoni: Inawezekana kubainika umbile la mtoto tumboni zikitimia siku 81 na hizi ni chini
ya miezi mitatu, akiwa na yakini kwamba mimba imetoka ikiwa na miezi mitatu, damu itakayomtoka
inakuwa damu iliyoharibika, haachi swala kwa sababu hiyo.
Na jambo hili ni juu ya mwanamke kukumbuka, ikiwa mtoto aliyetoka ilikuwa kabla ya siku 80 basi
atazilipa swala zile, ikiwa hajui ni swala ngapi kaziacha?Basi akadirie, na ajitahidi kujua idadi, kisha
dhana yake kubwa ikiwa katika idadi fulani ya swala zilizompita, basi azilipe kwa idadi hiyo.
Swali la 30:Muulizaji wa kike anauliza:Yeye tangu awajibikiwe na swaumu anafunga Ramadhani, lakini
halipi siku zake alizofungua kwa sababu ya mzunguko wa damu ya hedhi, na kwa sababu ya kutokujua
idadi ya siku alizofungua, kwa hiyo, yeye hivi sasa, anaomba muongozo lile la lazima juu yake kulifanya.
Jawabu la 30:Inasikitisha kutokea hili baina ya wanawake wa waumini, hakika huko kuacha- namaanisha:
Kuacha kulipa siku ambazo ni lazima kwao kufunga-ima ni kwa sababu ya kutokujua, na ima ni kwa
sababu ya uzembe, yote mawili ni msiba, kwa sababu ujinga dawa yake ni kusoma na kuuliza,Ama
kuzembea, dawa yake ni kumcha Allah mshindi aliyetukuka, na kujichunga kujua Allah anakuona, na
kuogopa mwisho wa mambo, na kupupia yale ambayo Allah anayaridhia.
Juu ya mwanamke huyu, atubie kwa Allah kwa yale aliyoyafanya, na aombe msamaha, ajitahidi kuzijua
siku alizoacha kadiri ya uwezo wake kisha atazilipa, na kwa kufanya hili hatolaumiwa, natarajia Allah
atakubali toba yake.
Swali la 31:Ni ipi hukumu ya mwanamke kafikiwa na mzunguko wa hedhi baada ya kuingia wakati wa
swala? Je inawajibika kwake yeye kulipa akitwaharika? Na hivyo hivyo pindi akitwaharika kabla ya kutoka
muda wa swala?
Jawabu la 31:Kwanza: Mwanamke akiingia katika mzunguko wa damu ya hedhi baada ya kuingia wakati
wa swala basi inawajibika kwake akitoharika alipe swala ambazo alipatwa na mzunguko katika wakati
wake, ikiwa hajaswali kabla ya kuingiwa na hedhi.Na hali hiyo ni kwa mujibu wa neno lake Mtume rehema
na amani za Allah zimfikie:"Mwenye kuipata rakaa moja ya swala basi kwa hakika atakuwa ameipata
swala".Ikiwa mwanamke ataupata muda wa swala kiasi cha rakaa moja, kisha akaingia katika hedhi kabla
hajaswali, itamlazimu kukidhi (kulipa) swala hiyo pindi atakapo twaharika.
103
:ءﺎﺳﻧﻟا]
Pili: Ikiwa mwanamke atatwaharika kutokana na hedhi kabla muda wa swala haujatoka, basi
itamuwajibikia kulipa swala hiyo. Na lau atatwaharika kabla ya jua kuchomoza kwa kiasi cha rakaa moja
itamuwajibikia kulipa swala ya alfajiri,Na lau atatwaharika kabla ya jua kuzama kwa kiasi cha rakaa moja
itamuwajibikia kuswali swala ya Alasiri,Na lau atatwaharika kabla ya usiku kufikia katikati itamuwajibikia
kulipa swala ya Ishaa,Na ikiwa atatwaharika baada ya nusu ya usiku, haitamuwajibikia swala ya Ishaa,لﺎﻗ
]، Allah Mtukufu anasema:
"...Na mtakapopata amani mkawa katika salama, hapana vita, basi simamisheni swala, kwa hakika swala
kwa waumini ni faradhi iliyopangiwa wakati maalumu" [Annisai: 103],Yaani: Ni faradhi iliyopangiwa wakati
maalumu, haifai kwa mtu kuitowa swala nje ya wakati wake (akaswali baada ya kutoka muda wake), wala
kuiswali kabla ya kuingia wakati wake.
swali la 32:Iwapo imeingia kwangu desturi ya mwezi (hedhi) na hali nikiwa katikati ya swala, nitatakiwa
kufanya nini ? na je, nitawajibika kulipa swala hiyo baada ya muda wa hedhi?
103
jawabu la 32:Ikiwa mwanamke itamtokea hedhi baada ya kuingia wakati wa swala; kwa mfano
mwanamke akafikwa na hedhi baada ya kupinduka jua kwa nusu saa, basi bila shaka baada ya
kutwaharika kutokana na hedhi yake atailipa swala hii ambayo uliingia muda wake na hali akiwa na
twahara.
]. Na hiyo ni kwa mujibu wa kauli ya Allah
Mtukufu: "..Kwa hakika swala imekuwa juu ya waumini ni faradhi iliyopangiwa wakati maalumu" [An-Nisai:
103]
Na wala mwanamke hatolipa swala zilizomkuta akiwa ndani ya hedhi; kwa mujibu wa kauli ya Mtume
rehema na amani za Allah zimfikie- katika hadithi ndefu:"je, si pale mwanamke anapoingia katika hedhi
haswali na wala hafungi?"Na wanachuoni wamekubaliana kuwa mwanamke halipi swala ambayo ilimpita
akiwa katika hedhi.
Ama ikiwa atatwaharika, na hali ilikuwa imebaki katika muda wa swala kiasi cha rakaa moja na zaidi, basi
ataswali swala hiyo ambayo ni ya wakati aliotwaharika ndani yake. Na hii ni kwa mujibu wa kauli yake
Mtume rehema na amani za Allah zimfikie:"Mwenye kupata rakaa moja katika swala ya Alasiri kabla jua
halijazama, basi kwa hakika atakuwa ameipata swala ya Alasiri".Na ikiwa mwanamke atatwaharika ndani
ya wakati wa Alasiri, au kabla ya kuchomoza jua, na ikawa imebaki kabla ya kuzama jua au kuchomoza
jua kwa kiasi cha rakaa moja, basi ataswali Alasiri kwa mnasaba wa swala la kwanza, na ataswali Alfajiri
kwa mnasaba wa swala la pili.
swali la 33:Mimi nina mama mzazi ambaye anafikia umri wa miaka sitini na tano, na yeye katika kipindi
cha miaka kumi na tisa hajapata mtoto. Na hivi sasa ana kipindi cha miaka mitatu akiwa na ugonjwa wa
kutokwa na damu,-na inavyoonekana nikuwa-maradhi hayo yaliimpata katika wakati huo vile vile
atakabiliwa na ibada ya swaumu. Je ni nini nasaha zenu kwake? Na je, nini atakachotakiwa kufanya ?
Jawabu la 33:Hukumu ya mfano wa mwanamke kama huyu aliyefikwa na ugonjwa wa kutokwa na damu:
anatakiwa aache kuswali na kufunga katika kipindi cha desturi yake iliyotangulia kabla ya kufikwa na
ugonjwa huu. Hivyo basi iwapo ilikuwa kawaida yake anapata hedhi katika mwanzo wa kila mwezi kwa
muda wa siku sita kwa mfano, basi atakaa katika mwanzo wa kila mwezi kwa muda wa siku sita na hali
ya kuwa haswali wala hafungi, na zitakapoisha siku hizo basi ataoga na ataswali na atafunga.
Na namna ya swala ya mwanamke kama huyu na mfano wake: ataosha tupu yake kwa ukamilifu, halafu
ataifunga na atatawadha, na atakuwa akifanya hivyo baada ya kuingia wakati wa kila swala ya faradhi, na
atafanya hivyo hivyo atakapokuwa anataka kuswali swala za suna zisizokuwa faradhi.
Na katika hali kama hii, na kutokana na tabu anazopitia, itakuwa inajuzu kwake kukusanya swala ya
Adhuhuri na Laasiri, na swala ya Magharibi na Ishaa: kwa kufanya kwake hivi ataswali swala mbili kwa
mara moja; Yaani swala ya Adhuhuri na Alasiri.Na twahara moja pia kwa ajili ya swala mbili: Yaani swala
ya Magharibi na Ishaa, na Alfajiri itakuwa pekee. Hivyo basi badala ya kuswali mara tano ataswali mara
tatu tu.
Na hapa nitarudia maelezo mara ya pili, ninasema: Pindi atakapotaka kujitwaharisha ataosha tupu yake,
na ataifunga kwa kitambaa au mfano wa kitambaa, ili ipungue ile hali ya kutoka damu. Kisha atatawadha,
na ataswali Adhuhuri rakaa nne na Alasiri rakaa nne. Na Magharibi rakaa tatu na Ishaa rakaa nne, na
Alfajiri rakaa mbili. Kwa maana kwamba asipunguze rakaa hizo. Kama wanavyodhania baadhi ya watu
wasiokuwa na elimu na maarifa.Lakini inajuzu kwake kukusanya kati ya swala ya Adhuhuri na Alasiri, na
kati ya swala ya Magharibi na Ishaa, ima kwa kutanguliza au kwa kuchelewesha, na ikiwa atataka kuswali
swala ya sunna kwa udhu huo huo aliyoswalia swala hizo za faradhi, hapana ubaya wa kufanya hivyo.
swali la 34:Nini hukumu ya mwanamke kukaa katika msikiti mtukufu wa Makka au msikiti wa Madina, na
hali akiwa na hedhi; kwa nia ya kusikiliza mafunzo ya hadithi za Mtume rehema na amani za Allah
zimfikie, na kusikiliza hotuba?
Jawabu la swali la 34:Haijuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kukaa ndani ya msikiti wa Makka au msikiti
mwingine wowote. Lakini inajuzu kwake kupita na kukatisha ndani ya msikiti kwa nia ya kutimiza haja
yake humo, na mfano wa hilo;Kama alivyosema Mtume rehema na amani za Allah zimfikie,
alipomuamrisha mama Aisha alete Msala, mama Aisha akasema: Msala uko msikitini na mimi nina hedhi.
Mtume wa Allah rehema na amani zimfikie akasema "Hedhi yako haiko mkononi mwako",Na ikiwa
mwanamke mwenye hedhi atakatisha msikitini, na hali ya kuwa damu yake haichuruziki ndani ya msikiti,
basi hapana ubaya wowote juu yake.1
Ama ikiwa mwanamke huyo anataka tu kukaa msikitini hilo halitajuzu kisheria.
Na dalili ya hilo: Ni kuwa Mtume rehema na amani za Allah zimfikie aliwaamrisha wanawake kutoka
katika swala ya iddi ili kuhudhuria mahala pa tukio la swala ya iddi (wanawake walioachwa huru kutokana
na utumwa na mabinti wanaotawa na wanawake wenye hedhi) isipokuwa tu ameamrisha wenye hedhi
wajitenge na mahala pa kuswalia.Hivyo hilo linajulisha kuwa mwanamke mwenye hedhi haijuzu kwake
kukaa msikitini kwa nia ya kusikiliza hotuba au kusikiliza darasa na hadithi.
*
MIONGONI MWAHUKUMUZATWAHARAKATIKASWALA:
Swali la 35:Je kinachotoka kwa kuchuruzika toka kwa mwanamke (katika sehemu zake za siri)- kikiwa ni
rangi nyeupe au ya njano- ni najisi au tohara? je unawajibika udhuu kwa hicho kinachotoka? pamoja na
kujuwa na kutambua kwamba kinaendelea kutoka bila kukatika, na ipi hukumu ikiwa kitaacha kutoka?
hususani ni kwamba wengi katika wanawake wasomi wanazingatia kile kinachotoka ni unyevunyevu wa
kawaida na wa asili, hailazimiki kuchukua Udhu?
Jawabu la swali la 35:Kinachodhihiri kwangu baada ya utafiti ni kuwa: Kinachochuruzika kutoka kwa
mwanamke ikiwa hakitoki kwenye kibofu basi kinatoka katika mfuko wa uzazi na kitakuwa ni twahara.
Lakini kinatengua udhu pamoja na kuwa ni twahara: Kwa sababu kitu kinachotengua udhu si sharti kiwe
najisi, kwani huoni upepo unaotoka sehemu ya nyuma hauna umbo, lakini pamoja na hivyo unatengua
udhu.
Na kwa ajili hiyo tu, ikiwa damu hiyo itamtoka mwanamke na hali akiwa na udhu basi damu hiyo itatengua
udhu wake, na itamuwajibikia kutawadha udhu mpya.
Na ikiwa damu hiyo inaendelea kutoka haitatengua udhu wake, lakini atatawadha kwa ajili ya swala pindi
utakapoingia muda wake. Na kwa udhu huo huo ataswali swala ya sunna na atasoma Qur'ani, na
atafanya lolote katika mambo ya halali kwake.Na hivi ni kama walivyosema wasomi kuhusu mtu mwenye
1 Neno "Khumra" lililotumika katika hadithi: Ni Mswala unaotumika kuswalia. Na Mswala huo umeitwa
hivyo kwa sababu unafunika uso.
ugonjwa wa kutokwa na mkojo mfululizo, hii ndiyo hukumu ya mwenye kutokwa na damu katika kadhia ya
twahara, anakuwa twahara, na katika swala la kutenguka udhu wake, mkojo huo unatengua udhu ila tu
ikiwa unatoka mfululizo wakati huo hautatengua udhu. Lakini mwanamke hatatawadha kwa ajili ya swala
ila baada ya kuingia muda, na awe muangalifu.
Ama ikiwa damu hiyo inakatika, na ikawa desturi yake ni kukatika katika nyakati za swala, basi
ataahirisha swala mpaka wakati ambao damu inakatika, madhali tu hahofii kupitwa na kipindi cha swala.
Ikiwa atahofia kupitwa na kipindi cha swala basi itambidi atawadhe na atajifunga na kujihifadhi na kuswali.
Na hapana tofauti kati ya damu ndogo na damu nyingi; Kwa sababu zote hizo zinatokea katika njia moja;
hivyo basi ikiwa ni nyingi au kidogo zote hizo zinatengua udhu. Hii ni tofauti na damu inayotoka katika
maeneo mengine ya mwili kama damu au matapishi, vitu hivyo havitengui udhu vikiwa kidogo au vikiwa
vingi.
Ama itikadi ya baadhi ya wanawake kuhusu damu hiyo kwamba haitengui udhu hili mimi sijui linatokana
na asili ipi, isipokuwa kauli ya Ibn Hazmi Allah amrehemu yeye anasema: Damu hii haitengui udhu, lakini
hakuleta dalili yoyote juu ya kauli yake hii na lau angetaja dalili yoyote kutoka katika kitabu na sunna na
kauli za Maswahaba hiyo ingelikuwa ni hoja.
Na ni juu ya mwanamke kumcha Allah na apupie kujitwaharisha; kwa sababu swala haikubaliwi bila ya
twahara, japo ataswali mara mia. Kwani baadhi ya wanachuoni wanasema: Mtu anayeswali bila ya
twahara anafanya kufuru; kwa sababu kufanya hivyo ni kuzifanyia kejeli aya za Allah-Aliyetakasika na
Kutukuka.
Swali la 36:Atakapo tawadha mwanamke ambaye anatokwa na kinachomtoka katika sehemu zake za siri
bila kukatika kwa ajili ya swala ya lazima, je ni sahihi kwake yeye akaswali swala za sunna anazotaka na
kusoma Qur'ani kwa ule udhu aliouchukua kwa ajili ya ile swala ya lazima mpaka swala ya lazima
nyingine inayofuata?
Jawabu la 36:Atakapo chukua udhu mwanamke kwa ajili ya swala ya lazima katika mwanzo wa wakati
wake basi ni juu yake akaswali swala za sunna anazotaka na kusoma Qur'ani mpaka utakapo ingia
wakati wa swala nyingine.
Swali la 37:Je ni sahihi kwa huyo mwanamke kuswali swala ya dhuha kwa udhu wa swala ya Al fajiri?
Jawabu la 37:Hilo si sahihi, kwa sababu swala ya dhuha ni swala ya wakati maalumu, ni lazima kuchukua
udhu kwa ajili ya swala ya dhuha ukiingia wakati wake, kwa sababu huyu mwanamke ni mfano wa yule
mwanamke anayetokwa na damu ya ugonjwa, na alimuamrisha Nabii-rehema na amani ziwe juu yake
mwanamke anayetokwa na damu ya ugonjwa achukue Udhu kwa kila swala (anayotaka kuswali).
Na wakati wa swala ya Adhuhuri: Ni toka kupinduka kwa jua (kuelekea Magharibi) mpaka wakati wa
swala ya Alasiri.
Na wakati wa swala ya Alasiri: Ni toka wakati wa kutoka swala ya Adhuhuri mpaka jua likiwa la njano, (na
wakati wa) dharura(kwa ajili ya swala ya Lasiri) ni mpaka kuzama kwa jua.
Na wakati wa Magharibi: Ni toka kuzama kwa jua mpaka kupotea kwa wekundu unaotokea angani wakati
wa kuzama kwa jua.
Na wakati wa swala ya Ishaa: Ni kutoka wakati umepotea ule wekundu unaotokea angani wakati wa
kuzama kwa jua mpaka nusu ya usiku.
Swali la 38:Je ni sahihi kwa huyu mwanamke kuswali kisimamo cha usiku itakapopita nusu ya usiku kwa
udhu ule wa Ishaa?
Jawabu la 38:Hapana, itakapopita nusu ya usiku inawajibika kwa mwanamke huyu kuchukua Udhu tena,
na pamesemwa kuwa: Sio lazima kuchukua udhu mpya na hii ndio kauli yenye nguvu yenye kufanyiwa
kazi.
Swali la 39:Ni upi muda wa mwisho wa swala ya Ishaa, na vipi utautambua?.
Jawabu la 39:Wakati wa mwisho wa swala ya Ishaa ni nusu ya usiku, na hilo hutambuliwa kwa kugawa
baina ya kuzama kwa jua na kuchomoza alfajiri mara mbili, nusu ya kwanza inaisha muda wa mwisho wa
swala ya Ishaa, na inabakia nusu ya mwisho haina wakati bali ni kizuizi baina ya Ishaa na Alfajiri.
Swali la 40:Atakapo chukua udhu mwanamke anayetokwa na chenye kutoka kwa kukatikakatika (hakitoki
mfululizo sehemu za siri) na baada ya kumaliza kuchukua udhu na kabla ya swala yake, kikatoka mara
nyingine, nini afanye mwanamke huyu?
Jawabu la 40:Ikiwa kile kinachotoka kiliacha kutoka basi asubiri mpaka ule muda ambao kinaacha kutoka,
ama ikiwa hana hali inayofahamika, muda wa kutoka na muda wa kuacha kutoka, basi atachukua udhu
baada ya kuingia wakati wa swala, ataswali, na halazimiki juu yake chochote.
Swali la 41:Kipi kinalazimu pindi hicho kinachotoka (sehemu za siri) kikigusa mwili au nguo?
Jawabu la 41:Ikiwa kile kinachotoka ni tohara (kisafi) basi hakuna kinachomlazimu, na kikiwa ni
najisi-nacho ni kile kinachotoka katika kibofu- basi inawajibika juu yake akoshe (mwili au nguo hizo)
Swali la 42:kuhusu udhu kutokana na kile chenye kutoka, je inatosha akaosha vile viungo vya udhu peke
yake?
Jawabu la 42:Ndio, inatosha hilo, ikiwa kinachotoka ni tohara, nacho ni kile kinachotoka katika mfuko wa
uzazi na sio kinachotoka katika kibofu.
Swali la 43:Ni ipi sababu ya kutonukuliwa kutoka kwa Mtume- Rehema na amani ziwe juu yake- hadithi
yoyote yenye kuonyesha juu ya kutenguka kwa udhu kwa kile kinachotoka, pamoja na kwamba
Maswahaba wa kike walikuwa wakipupia juu ya kutaka kujua mambo katika dini yao?
Jawabu la 43:Kwa sababu kinachotoka hakimjii kila mwanamke.
Swali la 44:Yule mwanamke ambaye alikuwa hachukui udhu kwa kutokujua hukumu yake, anawajibika
nini juu yake mwanamke huyo?
Jawabu la 44:Juu yake mwanamke huyo ni kutubu kwa Allah (Mshindi aliyetukuka) na awaulize
wanazuoni juu ya hilo.
Swali la 45:kuna wanao nasibisha kwako kauli ya kutochukua udhu kwa kutoka kile chenye kutoka
(sehemu za siri)?
Swali la 45:Mwenye kuninasibishia kauli hii sio mkweli, jambo linalodhihiri ni kwamba yeye kafahamu
kutoka katika kauli yangu: Kwamba hakitengui Udhu.
Swali la 46:Ni ipi hukumu ya uchafu unaomtoka mwanamke kabla ya hedhi kwa siku moja au zaidi au
chini ya hapo, na kinaweza kuwa chenye kutoka kikawa mfano wa uzi laini mweusi au kahawia au mfano
wa hiyo? Ni ipi hukumu lau ikiwa baada ya hedhi?
Jawabu la 46:Hiyo ikiwa ni mwanzo wa hedhi basi hiyo ni hedhi, na hutambuliwa hilo kwa maumivu
ambayo yanamkuta aliye na hedhi kwa kawaida.
Ama uchafu baada ya hedhi, atasubiri mpaka uondoke; kwa sababu uchafu unaoungana na hedhi nao ni
hedhi; kutokana na kauli ya Aisha- Radhi za Allah ziwe juu yake: Msifanye haraka mpaka muone tohara
baada ya hedhi. Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.
*
MIONGONI MWAHUKUMUZAHEDHIKATIKAHIJANA
UMRA:
Swali la 47:Vipi anaswali mwanamke anayetokwa na damu ya hedhi rakaa mbili za baada ya kuhirimia?
Na je inafaa kwa mwanamke mwenye hedhi kusoma na kurudia rudia Adhkari katika nafsi yake? au
haifai?
Jawabu la 47Jambo la kwanza: Tunapaswa kujua kwamba Ihram (Nia ya kuanza Hija au Umra) haina
swala yoyote; kwa sababu haikuja kutoka kwa Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- kwamba
ameweka sheria kwa umma wake kuwe na swala maalum kwa ajili ya Ihram, si kwa kauli yake, au
kitendo chake, au kufanyika kitu mbele yake akakipitisha.
Jambo la pili: Mwanamke huyu mwenye hedhi ambaye ameingia katika hedhi kabla hajahirimia, anaweza
kuhirimia akiwa katika hedhi.Kwa sababu Mtume- Rehema na amani ziwe juu yake-alimuamrisha Asmaa
bint Umeysi, mke wa Abubakari-Radhi za Allah ziwe juu yao- pindi alipopata damu ya nifasi katika eneo
la Dhul Hulayfah, akamuamrisha akoge na aweke nguo sehemu inayotoka damu, na ahirimie, na hivi pia
anafanya mwanamke mwenye hedhi, anabakia katika ibada yake aliyohirimia mpaka atoharike, kisha
azunguke nyumba ya Allah na azunguke Swafah na Marwah.
Na ama kauli yake katika swali: Je anaweza kusoma Qur'ani? Basi jawabu ni ndio, na mwanamke
mwenye hedhi anaruhusiwa kusoma Qur'ani akiwa na haja au akiona kuna masilahi juu ya hilo, ama
kama hakuna haja wala masilahi, bali anasoma tu kama ibada na kujikurubisha kwa Allah, lililo bora
asisome.
Swali la 48:Amesafiri mwanamke kwenda katika Hijja, na akajiwa na mzunguko wa mwezi (Hedhi), toka
siku tano kabla ya safari yake, lakini baada ya kufika katika sehemu ya kuhirimia, akaoga na akaingia
katika ibada ya Hijja kwa kuhirimia, lakini yeye hajatoharika na mzunguko wake wa hedhi, alipofika katika
mji wa Makka akabakia nje ya eneo tukufu, hakufanya chochote katika metendo matukufu ya Hijja na
Umra, na akakaa siku mbili katika mji wa Minah, kisha akatoharika, akajitoharisha kwa kukoga, na
akatekeleza matendo yote ya Umrah akiwa ametoharika, kisha ikamrudia damu akiwa katika Twawaf ya
Hijja (kuzunguka Al-Kaaba kwa ajili ya Hijja) isipokuwa aliona haya na akakamilisha matendo ya Hija,
hakumwambia msimamizi wake mpaka baada ya kufika katika mji wake, ni ipi hukumu ya hilo?
Jawabu la 48:Hukumu ya hilo: Damu iliyompata wakati anazunguka Al-Kaaba wakati wa Hijja, ikiwa ni
damu ya hedhi ambayo anaijua kwa ile kawaida yake na ugonjwa wake basi hakika kule kuzunguka
kwake Kaaba kwa ajili ya Hija (Twawaful ifadha) hakuko sahihi, inamlazimu arudi katika mji wa Makka; ili
aweze kutufu twawaful Ifadha (kuzinguka Kaaba kwa ajili ya Hijja), ahirimie kufanya ibada ya Umra katika
maeneo ya kuhirimia kisha atekeleze ibada ya Umrah kwa kutufu (Kuzunguka Kaaba) na kuzunguka
swafah na Marwah na apunguze nywele kisha ndio atufu twawaful Ifadha (kuzunguka Kaaba kwa ajili ya
Hijja)
Ama ikiwa hii damu sio damu ya hedhi, ni damu ya kawaida inayojulikana, bali imetokana na
msongamano mkubwa au hofu na yanayofanana na hayo, basi kuzunguka kwake kuko sahihi kwa wale
wanaoshurutisha twahara (katika wanazuoni) mtu akiwa anazunguka Kaaba.
Ikiwa ameshindwa kurudi, katika swala la mwanzo, kiasi kwamba yuko katika miji ya mbali, basi Hijja
yake ni sahihi, kwa sababu hana uwezo wa kufanya zaidi ya vile alivyofanya.
Swali la 49:Amefika mwanamke amehirimia kwa ajili ya Umra, na alipofika katika mji wa Makka akapata
hedhi, na msimaizi wake analazimika kusafiri kwa haraka, na hana msimamizi mwingine katika mji wa
Makka, ni ipi hukumu yake?
Jawabu la 49:Atasafiri pamoja naye, na atabakia katika ibada yake akiwa amehirimia, kisha atarejea
akitoharika, na hili ikiwa atakuwa Saudia; kwa sababu kurejea akiwa hapo ni jambo jepesi, na wala halina
tabu ndani yake jambo hilo, hahitaji hati za kusafiria na mengineyo.
Ama akiwa anatoka nje ya Saudia, na ni tabu kwake kurudi, basi atajihifadhi, atazunguka Al-Kaaba,
atazunguka Swafah na Marwah na amalize ibada yake ya Umrah katika safari hiyo hiyo, kwa sababu
kuzunguka kwake Kaaba wakati huo ni dharura, na dharura huruhusu mambo yaliyokatazwa.
Swali la 50:Ni ipi hukumu ya mwanamke wa kiislamu ambaye amepatwa na damu ya hedhi katika siku za
Hijja, je ile Hijja itamtosheleza (Itakubalika)?
Jawabu la 59:Hili haliwezekani kulijibu mpaka ijulikane ni muda gani huyu mwanamke kapatwa na damu
ya hedhi, na hilo ni kwa sababu baadhi ya matendo ya Hijja hayazuiliwi na hedhi kufanyika, na mengine
yanazuiliwa, mfano: Kuzunguka Kaaba, hawezi kuzunguka mpaka awe na udhu (Tohara), na mengine
katika matendo ya Hijja anaweza kuyafanya akiwa na hedhi.
Swali la 51:Nilikuja kufanya Hija yangu ya lazima mwaka jana, nilifanya matukio yote ya Hija isipokuwa
Twawaful Ifadha (kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Hijja) na Twawaful wadaa (Kuzunguka kaaba kwa ajili ya
kuaga), nilizuiwa na udhuru wa kisheria, nikarudi nyumbani kwangu katika mji wa Madina nikiazimia
kurudi siku katika masiku ili nizunguke Kaaba mizunguko niliyoiacha, kutokana na mimi kutojuwa mambo
ya dini, nimehalalika na kila kitu, nimefanya mambo yote ambayo nakatazwa katika ihraam, nikaulizia
kurudi ili nizunguke Kaaba nikaambiwa: Hauwezi tena kurudi, kwani tayari umeharibu ibada yako,
inakulazimu kurudia Hija mara nyingine mwaka unaokuja, pamoja na kuchinja Ngamia au Ng'ombe, je
fatwa hii ni sahihi? Je kuna njia nyingine, ni ipi hiyo, na je Hija yangu imeharibika? Na je natakiwa
kurudia? Nipe faida kwa yale ninayotakiwa kuyafanya, Allah awabariki.
Jawabu la 51:Na hili pia ni katika balaa, kutolewe Fatwa bila ya elimu, na wewe katika hali hiyo
unawajibika kurudi katika mji wa Makka, na ukatufu Twawaful ifadha pekee (Kuzunguka Kaaba kwa ajili
ya Hijja).
Ama kuzunguka Al-Kaaba kwa lengo la kuaga (Twawaful Wadaa) hulazimiki kufanya hivyo madamu
ulikuwa na hedhi wakati unatoka katika mji wa Makka, kwa sababu mwenye hedhi halazimiki kufanya
mzunguko huo;kutokana na hadithi ya bin Abbas-Radhi za Allah ziwe juu yao- Aliwaamrisha watu jambo
lao la mwisho katika ibada ya Hija liwe ni kuzunguka Kaaba, isipokuwa aliwafanyia wepesi waliopatwa na
hedhi.Na katika Riwaya ya Abu Daudi: Jambo lao la mwisho katika ibada ya Hija liwe ni kuzunguka
Kaaba.Na ni kwa sababu Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- alipo ambiwa kwamba Swafiya
ametufu (amezunguka Kaaba kwa mzunguko wa Hijja) basi akasema: (Na arudi basi).Imeonesha hadithi
hiyo kwamba mzunguko wa Kaaba kwa kuiaga Kaaba unadondoka kwa mwanamke mwenye hedhi.
286
:ةرﻘﺑﻟا]
Ama mzunguko wa Kaaba kwa ajili Hijja huo ni lazima, na kwa kuwa amehalalika na kila kitu kwa kutojua,
hilo halimdhuru kitu, kwa sababu asiyejua anapofanya katazo katika makatazo ya Ihiramu, hana
dhambi.