
NDOTO NJEMA
Sifa za ukamilifu zote ni za Allah, tunamhimidi, tunamuomba
msaada, tunamuomba msamaha, na tunajilinda na Allah kutokana
na shari za nafsi zetu, na kutokana na amali zetu mbovu, yule
ataongozwa na Allah, basi hakuna wa kumpoteza, na
atakayempoteza hakuna wa kumuongoza, nashuhudia ya kwamba
hapana apasaye kuabudiwa ila Allah peke yake, hana mshirika, na
nashuhudia kuwa Nabii wetu Muhammad ni mja wake na mtume
wake, swala na salamu za Allah nyingi zimshukie yeye, watu wake,
na masahaba wake.
(Ammaa ba'd) Ama baada ya himdi hii:
Mcheni Allah - enyi waja wa Allah - kama ipasavyo kumcha,
na mchungeni [chungeni amri zake na makatazo yake] katika siri
na minong'ono.
[Ayyuhal muslimuun] Enyi Waislamu:
Allah amewatimizia waja wake neema za dhahiri na za batini,
kaika hali ya kuwa macho kwao na kulala kwao, Naye aliyetakasika
anapelekesha mambo usiku na mchana; na Allah kwa hekima yake
ameficha elimu ya ghaibu kwa viumbe, na hakuna njia ya kujua
ghaibu isipokuwa kile ambacho Allah anawajulisha Mitume wake
(yaani isipokuwa kile ambacho Allah aliwaambia Mitume wake),
[Allah] aliyetakasika amesema:
{Yeye ndiye mjuzi wa ghaibu, wala hamdhihirishii yeyote
)1( [Hotuba hii] imetolewa siku ya ijumaa, tarehe kumi na sita ya mwezi wa Safar, mwaka wa elfu moja mia
nne na arobaini na tano hijria, katika Masjid An-Nabawi.
NDOTO NJEMA 2
alqasim.com-a
ghaibu yake * isipokuwa Mtume aliyemridhia, basi hakika
humwekea huyo walinzi mbele yake na nyuma yake} [Al-Jinn: 27]
Na miongoni mwa neema za ndani za Allah na maajabu ya
uumbaji wake mzuri; ni kwamba amewaachia sehemu ya Unabii ili
kupata kujua baadhi ya ghaibu, [Allah] huwajulisha anaowataka
katika waja wake ndani ya usingizi wao, amesema Nabii swala na
salamu za Allah zimshukie: (Hakuna kilichobakia katika Unabii
isipokuwa yenye kubashiria. Waliuliza: Na yenye kubashiria ni
nini? Akasema: Ndoto nzuri.) [Imepokelewa na Bukhari], kwa
hivyo, katika ndoto nzuri kuna maarifa ya ajabu ya Allah na fadhila
zake ambazo humfanya muumini azidi katika imani yake, kwani
inamjulisha yaliopita, ya wakati ulio na mustakabali, jambo lenye
kumkomboa kutokana na uoga wa waganga na mfano wao, na mnao
ndani yake [ndoto njema] msisitizo (yaani motisha) wa kufanya
mema, kuonya dhidi ya uovu, na habari njema na onyo.
Inayo ndoto cheo adhimu katika sheria ya Kiislamu, kwani
ipamoja na Manabii katika mitihani na matukio magumu mno, nayo
ni ufunuo [wahyi] kwao peke yao, Ibrahim alimwambia Ismail,
Amani iwe juu yao:
{Ewe mwanangu, hakika mimi naona usingizini kuwa
nakuchinja} [As-Saffat:102].
Allah aliinua hadhi ya Ibrahim kwa kuisadikisha ndoto na kutii
amri ya Mola wake, akamwachia sifa ya kweli kizazi baada ya
kizazi, Allah Mtukufu amesema:
{Na tukamwachia (sifa njema) kwa waliokuja baadaye * salamu
kwa Ibrahim (kutoka kwa mola wake) * hivyo ndivyo
tunavyowalipa wafanyao mema} [As-Saffat:108-110].
Maisha ya Yusuf salamu zimshukie yalianza na ndoto:
NDOTO NJEMA 3
a-alqasim.com
{Ewe babangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja, jua na
mwezi, nimeota zinanisujudia} [Yusuf:4], Ikatimia ndoto yake kwa
kupata izza kwake na cheo.
{Na akawapandisha wazazi wake juu ya kiti cha enzi, na wote
wakaporomoka kumsujudia} [Yusuf:100].
Heri ya kwanza na nuru ya umma huu ilikuwa kupitia ndoto;
Aisha, Allah amridhie, alisema: (Ilikuwa mwanzo wa ufunuo kwa
Mtume wa Allah swala na salamu za Allah zimshukie ni: ndoto ya
kweli katika usingizi, na hakuona ndoto isipokuwa ilikuja kama
mwanzo wa alfajiri) [wameafikiana Bukhari na Muslim kuipokea].
Katika vita vya Badr, Allah alimuonyesha Nabii wake ushindi
katika ndoto, [Mtume] akawahadithia Masahaba zake ndoto hiyo,
basi nyoyo zao zikazidi nduvu, na wakawa wajasiri katika kupigana
na adui wao Pamoja na uchache wao:
{Kumbuka (ewe Nabii) pindi Allah alipokuonyesha uchache wa
maadui zako ukiwa usingizini, na kama angelikuonyesha wingi wa
maadui zako mngeliingiwa na uoga, na mngelizozana kuhusu
kupigana, lakini Allah aliepusha (jambo hilo)} [Al-Anfal:43].
Allah alimuonyesha Nabii wake ndotoni ushindi wa Makkah
akiwa Madina, basi ikawa habari njema kwao:
{Hakika Allah alimtimizia Mtume wake ndoto kwa haki, bila
4
NDOTO NJEMA
shaka mutaingia Msikiti mtakatifu in shaa Allah mkiwa na amani,
hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza. Hamtakuwa na
hofu} [Al-Fath:27], basi Allah akawafutahia [Makkah] baada yam
waka mmoja.
Na Nabii swala na salamu za Allah zimshukie akiona ndoto
huwasimulia Masahaba zake; bali alikuwa anapomaliza kuswali
alfajiri huwakabili masahaba zake kwa uso wake na kuwauliza: (Je,
kuna yeyote kati yenu aliyeona ndoto jana usiku?) [wameafikiana
Bukhari na Muslim kuipokea].
Asili ya kuekwa adhana ni Nabii kuikiri kwa Nabii swala na
salamu za Allah zimshukie ndoto aliyoiona sahaba Abdullah ibnu
Zaid Allah amridhie, alisema: "Nilipoingiliwa na asubuhi
nilimwendea Mtume wa Allah swala na salamu za Allah zimshukie
na nikamhadithia nilichoona. Basi akasema: (Hakika hiyo ni ndoto
ya haki in shaa Allah. Nenda na Bilal, umhadithie kile ulichoona,
ili aadhini [kwa maneno hayo]) [imepokewa na Ahmad]. Ibn
Abdul-Barr alisema: "Imamu wa waongofu, katika masahaba,
tabi'ina, na waliokuja baada yao miongoni mwa wanazuoni wa
waislamu wa madhehebu ya Ahlu Ssunnah wal Jama'a
wamekubaliana juu ya kuiamini [ndoto hii]".
Na ndoto zimegawanyika vigawanyo vitatu; moja yazo ni haki
hapana budi itokee, na mbili [zilizosalia] ima zinatoka kwa Shetani,
ima ni mchangamaniko wa ndoto zisizo na uhakika. Nabii swala na
salamu za Allah zimshukie amesema: (Ndoto ni aina tatu: Ndoto
nzuri ni bishara kutoka kwa Allah, ndoto ya huzuni ni kutoka kwa
Shetani, na ndoto ya kutokana na yale mtu anayojihadithia nafsi
yake) [imepokewa na Muslim].
Ndoto njema humfurahisha muumini wala haimghuri, nayo ni
sehemu katika Unabii. [Mtume] swala na salamu za Allah
zimshukie amesema: (Ndoto ya muumini ni sehemu katika sehemu
arobaini na sita za Unabii) [wameafikiana Bukhari na Musllim
kuipokea], nayo ni mojawapo wa yenye kubashiria yaliosalia baada
ya Unabii. Nabii swala na salamu za Allah zimshukie aliulizwa
a
alqasim.com
NDOTO NJEMA
5
kuhusu kauli yake Allah aliyetukuka:
{wanao bishara katika Maisha ya duniani na Akhera} [Yunus: 64]
Akasema: (Hiyo ni ndoto njema muislamu huiona au ionekane
na wengine) [imepokewa na Ahmad].
Na ndoto ya kweli ni sehemu katika Unabii, na Unabii ni ufunuo
[Wahyi], na mwenye kusema uongo katika usingizi wake huwa
amemsemea uongo Allah kwamba amemwonyesha kile ambacho
hakuona. [Mtume] swala na salamu za Allah zimshukie alisema:
(Hakika katika uongo mkubwa ni kuyaonyesha macho yake kile
ambacho hayakukiona) [imepokewa na Bukhari], na siku ya
Kiyama ataamrishwa kitu ambacho hana uwezo wa kukifanya ili
kuzidisha adhabu, Nabii swala na salamu za Allah zimshukie
alisema: (Atakayedai ndoto ambayo hakuiona; ataamrishwa azipige
fundo tembe mbili za ngano, na hataweza kufanya hilo),
[imepokewa na Bukhari].
Nayo [ndoto njema] ingawa aghalabu ni mahususi kwa watu
wema, ila inaweza kutokea kwa wengineo; kwani Yusuf salamu
zimshukie alifasiri ndoto ya wenzake wa gerezani ikatokea kama
alivyoifasiri, na akafasiri ndoto ya mfalme kafiri ya ng’ombe saba
na ikawa kweli. Bukhari amesema katika kitabu chake cha 'swahih':
“[Huu ni] Mlango wa ndoto za wafungwa, waovu na washirikina”,
na Ibn Hazm Allah amrehemu amesema: “Na ndoto ya kafiri
inaweza kuwa kweli, na wakati huo haitakuwa sehemu katika
Unabii, wala si miongoni mwa yenye kubashiria, lakini ni onyo
kwake na kwa wengine na ni mawaidha”.
Na ndoto ya mchana ni ya haki kama ndoto ya usiku.
Nabii swala na salamu za Allah zimshukie alimtembelea Ummu
Haraam binti Milhaan Allah amridhie akalala kwake wakati wa
mchana, basi akaona ndoto, na akamsimulia [wameafikiana
Bukhari na Muslim kuipokea].
a-alqasim.com
NDOTO NJEMA 6
alqasim.com-a
Inapendekezwa kwa mwenye kuona ndoto anayoipenda
kumhimidi Allah kwa ndoto hiyo, aifurahikie, na amsimulie mtu
anayempenda, ama hasidi na mwenye vitimbi basi asimsimulie,
kama alivyosema Yakub salamu zimshukie:
{Akasema: ewe mwanangu! Usiwasimulie ndugu zako ndoto
yako, wasije wakapanga njama dhidi yako} [Yusuf: 5]
Na atakayeona ndoto anayoichukia ni sunnah kwake kujikinga
na Allah kutokana na shari yake, na shari ya shetani, ateme
kushotoni mwake mara tatu, ageuke kutoka upande aliokuwa
amelala, asimsimulie ndoto hiyo yeyote, na asimame aswali, An
Nawawiy Allah amrehemu amesema: "na akitosheka kufanya
baadhi yake [haya yaliotangulia], yatamtosheleza kukinga shari
yake [ndoto hiyo] kwa idhini ya Allah aliyetukuka kama hadithi
zilivyoweka wazi hilo."
Kutafsiri ndoto ni mojawapo ya elimu za Manabii na watu wa
imani, nayo ni elimu adimu inayochanganya baina ya kipawa na
ujuzi unaochumwa, na ni neema ambayo Allah humpa amtakaye.
[Allah] anasema akielezea kuhusu Yusuf salamu zimshukie:
{Na ili tumfundishe kufasiri ndoto} [Yusuf: 21]
Tafsiri ya ndoto ni fatwa, nayo haijuzu kwa mtu yeyote
kujiingiza ndani yake bila elimu, Yusuf salamu zimshukie
aliwaambia wale vijana wawili:
{limekwisha amuliwa jambo ambalo mnataka fatwa kulihusu},
na Mfalme alisema:
NDOTO NJEMA
7
{Nipeni fatwa katika ndoto yangu} [Yusuf: 43].
na yule Kijana alimwambia Yusufu:
{Nipe fatwa katika [ndoto ya] ng'ombe saba} [Yusuf: 46].
Nayo [tafsiri ya ndoto] inategemea kiasi na kufananisha, na
kuzingatia mambo ya kiakili kwa kutegemea yale ya kihisia. Ibnul
Qayyim Allah amrehemu amesema: "Mifano yote ya Qur'ani ni
misingi na kanuni za elimu ya kutafsiri ndoto kwa yule anayeielewa
vizuri kuitolea hoja. Vivyo hivyo, yule anayeelewa Qur'ani ana
uwezo wa kutafsiri ndoto kwa njia bora zaidi, na misingi sahihi ya
tafsiri ya ndoto imechukuliwa katika shubaka la Qur'ani".
Mtu yeyote anayetaka kutafsiri ndoto yake asiitafsiri isipokuwa
kwa mtaalamu wa kufasiri ndoto, kwani si kila anayejitokeza
anaweza kutafsiri vizuri, wala aliyetosheka na vitabu vya ndoto, ni
mfasiri, kwani inayo [ndoto] hali tofauti kulingana tofauti za watu,
wakati na sehemu; [imamu] Malik Allah amrehemu aliulizwa: "Je,
kila mtu anaweza kutafsiri ndoto?" Akajibu: "Je, Unabii
huchezewa?!"
Yule aliyepewa na Allah uzuri wa kutafsiri ndoto inamlazimu
kuwa na uchaji Allah, ajiepushe na riya na kupenda kutangaa,
amuombe Mola wake msaada na kusibu, ajihadhari na majivuno
kwani yanapoteza neema, na amshukuru Allah kwa neema hii.
Yusuf salamu zimshukie alishukuru neema za Allah kwa kusema:
{Ewe Mola wangu! Hakika umenipa ufalme na umenifunza
tafsiri ya ndoto} [Yusuf: 101]
Mufti, mfasiri ndoto, na daktari huona siri na aibu za watu
ambazo wengine hawaoni. Kwa hivyo, ni lazima wawe ni wenye
kusitiri yale yasiopendeza kudhihirishwa.
Hapana budi ndoto ya kweli kutokea, iwe imetafsiriwa au la,
a-alqasim.com
8
NDOTO NJEMA
kwani Yakub alimwambia Yusuf salamu ziwashukie:
{Usisimulie ndoto yako} [Yusuf: 5], wala hakuitafsiri, lakini
bado ilitokea.
Hakika mfasiri anafichua uhakika wa maana ya ndoto, lakini
anaweza kusibu na anaweza kukosea, Nabii swala na salamu za
Allah zimshukie alimwambia Abu Bakr Allah amridhie baada ya
kutafsiri kwake ndoto: (Umepata baadhi na umekosea baadhi)
[wameafikiana Bukhari na Muslim kuipokea].
Ama wakati wa kutokea kwake [ndoto] basi inaweza kutokea
papo hapo, au inaweza kuchelewa kidogo au sana, Abdullah ibn
Shaddaad Allah amrehemu amesema: "Ndoto ya Yusuf salamu
zimshukie ilitokea baada ya miaka arobaini, na kufikia mda huo
ndio upeo wa ndoto", na kila Muislamu anapaswa kujua ya kwamba
kile ambacho Allah amemkadiria ni kheri kwake, sawa itokee kwa
haraka au katika siku zijazo.
[Wa ba'du, Ayyuhl muslimuun] Baada ya hayo, enyi
Waislamu:
Basi pindi zama za Unabii na athari zake zilipoisha; Allah
aliwapa waislamu badala yake ndoto. Nabii swala na salamu za
Allah zimshukie amesema: (Pindi Kiyama kitakapokurubia, ndoto
ya muumini haitokosea) [wameafikiana Bukhari na Muslim
kuipokea].
Ama katika zama za nguvu ya nuru ya Unabii; basi mna katika
kudhihiri kwa nuru yake na nguvu yake yenye kutosheleza kuhitajia
ndoto. Mtu mwenye ndoto ya kweli zaidi ni aliye mkweli zaidi
katika kuzungumza wakati yu macho, Nabii swala na salamu za
Allah zimshukie amesama: (Mkweli wenu zaidi katika ndoto ni
mkweli wenu zaidi katika kuzungumza) [imepokewa na Muslim].
Ibnu Hajar Allah amrehemu amesema: "Yule ambaye mara nyingi
husema kweli wakati yumacho, atakuwa hivyo pia katika usingizi
a
alqasim.com
NDOTO NJEMA
9
wake, basi hataona isipokuwa ukweli, na hili ni kinyume na
mwongo na mwenye kuchanganya; kwani moyo wake unaharibika
na kuwa na giza, basi haoni [ndotoni] isipokuwa kuchanganyikiwa
na ndoto za ovyo".
Basi Jilazimishe ukweli katika mazungumzo, na shikamana na
uchaji Allah; utafanikiwa kupata kheri za duniani na Akhera.
[Audhu billahi mina sh-shaitwani rrwajiim] Najilinda na
Allah kutokana na shetani aliyelaaniwa
{Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi. Na wote
wakaporomoka kumsujudia. Na akasema: Ewe baba yangu! Hii
ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani, Allah ameijaalia kuwa
kweli} [Yūsuf: 100]
Allah anibarikie mimi na nyinyi katika Qur-ani tukufu...
a-alqasim.com
10
NDOTO NJEMA
HOTUBA YA PILI
Sifa njema zote astahili Allah kwa wema Wake [kwetu], na
shukrani zote astahili Yeye kwa kutuafikia na kutuneemesha, na
nashuhudia ya kwamba hakuna apasaye kuabudiwa ila Allah peke
yake hana mshirika; ili kuadhimisha shani yake, na nashuhudia ya
kwamba Nabii wetu Muhammad ni mja Wake [Allah] na Mtume
wake, swala na salamu nyingi za Allah zimshukie yeye, watu wa
nyumba yake na Masahaba wake.
[Ayyuhal muslimuun] Enyi Waislamu!
Dini imekamilika kwa kifo cha Nabii swala na salamu za Allah
zimshukie, na ndoto njema haithibitishi chochote katika hukumu
[za sheria], Ash-Shatibi Allah amrehemu amesema: "Faida yake -
yaani: ndoto – ni kutoa tu habari njema au onyo, ama kutoa
hukumu, basi hapana".
Allah amemlinda Nabii wetu Muhammad swala na salamu za
Allah zimshukie kutokamana na Shetani kujifananisha naye, basi
aliyemuona katika ndoto, atakua amemuona kweli. Nabii swala na
salamu za Allah zimshukie amesema: (Anayeniona katika ndoto,
basi ameniona [kweli]. Kwani Shetani hawezi kujifananisha na sura
yangu) [wameafikiana Bukhari na Muslim kuipokea], na
atakayemuona Nabii katika ndoto haimaanishi kuwa ni mtu mwema
kuliko wengine, na atakayemuona katika ndoto kwa sura
isiyolingana na ile iliyotajwa katika Sunnah na Seera yake, au
akamuona akimuamrisha batili, basi hizo ni ndoto za ovyo
[zinazotokana na Shetani au mawazo ya mtu mwenyewe]. Na heri
ipo katika kumfuata Nabii swala na salamu za Allah zimshukie.
Kisha jueni kuwa Allah amewaamrisha kumswalia na
kumsalimu Mtume wake...
a
alqasim.com
NDOTO NJEMA
1
a-alqasim.com