Uislamu
Ni dini ya maumbile na akili na furaha
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
Je, umewahi kujiuliza:
Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo miongoni mwa
viumbe vikubwa? Na ni nani aliyetengeneza mfumo huu nyeti wenye
ufanisi mkubwa ndani yake?
Ulimwengu huu mkubwa umepangwaje na kuwa thabiti pamoja na
mifumo yake inayoudhibiti kwa ustadi kwa miaka mingi?
Je, ulimwengu huu ulijiumba wenyewe? Au ulizuka pasina kutokea
mahali? Au umepatikana ghafla?
Nani aliyekuumba?
Ni nani aliyeweka mfumo huu nyeti kabisa katika vifaa vya mwili wako
na katika miili ya viumbe hai wengine?
Hakuna anayeweza kukubali kuwa nyumba hii ilikuja pasina kujengwa
na yeyote! Au mtu akamwambia kuwa kutokuwepo ndiko kuliko ileta
nyumba hii! Ikiwa nyumba unayoishi hukubaliani na hayo inakuwaje
baadhi ya watu wanamuamini mwenye kuwaambia kuwa ulimwengu huu
ulikuja wenye pasina muumbaji? Hivi anakubali vipi mwenye akili kuwa
mpangilio huu wa ulimwengu wa hali ya juu ulitokea ghafla (kama
mlipuko)?
Kwa msisitizo kabisa nikuwa kuna Mola Mtukufu muumbaji na
mpangiliaji wa ulimwengu huu na vyote vilivyomo, naye ni Mwenyezi
Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Na Mola Mlezi Aliyetukuka alitutumia mitume amani iwe juu yao, na
akateremsha vitabu juu yao vya kiuungu (Wahyi), na kitabu cha mwisho ni
Qur'ani alichokiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Muhammadi wa mwisho
katika mitume wa Mwenyezi Mungu, na kupitia vitabu vyake na mitume
wake:
* Ametutambulisha yeye mwenyewe na sifa zake na haki zake juu yetu,
na akatubainishia haki zake juu yetu.
3
* Na akatuelekeza kuwa yeye ndiye Mola Mlezi aliyeumba viumbe
wote, nakuwa yeye yuko hai wala hafi, na viumbe wote wapo mikononi
mwake na chini ya mamlaka yake na maamuzi yake.
Na akatueleza kuwa miongoni mwa sifa zake ni elimu, bila shaka
amekizunguka kila kitu kwa elimu, nakuwa yeye ni msikivu mwenye kuona
hakuna chochote kinachofichikana kwake ardhini wala mbinguni.
Na Mola Mlezi ndiye aliye hai msimamizi wa mambo yote ambaye uhai
wa kila kitu unatoka kwake pekee Aliyetakasika, na kuwa yeye ndiye
msimamizi ambaye yanasimama maisha ya kila kiumbe kupitia yeye
Mtukufu, amesema Mtukufu:ُ
ﱠ
"Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia
mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote
vilivyomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kufanya uombezi
mbele yake isipokuwa kwa idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na
yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui vyema chochote katika vilivyo katika
elimu yake, ila kwa atakalo mwenyewe. kiti chake kimeenea mbinguni na
ardhini; na wala kuvilinda hivyo hakumshindi. Na Yeye ndiye aliye juu mno,
Mkuu". [Suratul Baqara: 255].
* Na akatueleza kuwa yeye ndiye Mola Mlezi anayesifika kwa sifa
kamilifu, na akaturuzuku akili na hisia zinazoweza kufahamu maajabu ya
uumbaji wake na uweza wake, jambo linalotuonyesha utukufu wake na
nguvu zake na ukamilifu wa sifa zake, na akapandikiza kwetu sisi umbile
linalotuonyesha juu ya ukamilifu wake nakuwa yeye haiwezekani asifike
kwa upungufu.
* Na kujua kwetu kuwa Mola Mlezi yuko juu ya mbingu zake
haimaanishi kuwa yuko ndani ya ulimwengu wala ulimwengu hauko ndani
yake.
4
* Na akatueleza kuwa ni wajibu kwetu kujisalimisha kwake Mtukufu
kwani yeye ndiye muumba wetu na muumba wa ulimwengu na mpangiliaji
wake.
Hivyo muumba anasifa za utukufu na wala haiwezekani kamwe asifike
nakuwa na hitajio au mapungufu, Mola Mlezi hasahau wala halali wala hali
chakula, na wala haiwezekani kuwa na mke au mtoto; na kila andiko
ambalo linapingana na utukufu wa muumbaji hilo si katika ufunuo sahihi
waliokuja nao mitume wa Mwenyezi Mungu amani iwe juu yao.
Amesema Allah aliye takasika ndani ya Qurani Tukufu:ۡ
"Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee*
Mwenyezi Mungu ndiye Mkusudiwa *
Hakuzaa wala hakuzaliwa *
Wala hana anayefanana naye hata mmoja." [Al-Ikhlaas: 1-4].
Ukiwa unamuamini Mola Mlezi Muumbaji.... Hivi uliwahi kujiuliza hata
siku moja kuhusu lengo la kuumbwa kwako? Na ni nini anakitaka
Mwenyezi Mungu kwetu sisi, na lipi lengo la uwepo wetu sisi?
Na je, inawezekana kuwa Mwenyezi Mungu alituumba kisha
akatuacha hivhivi? Na je, inawezekana kuwa Mwenyezi Mungu
aliumba viumbe vyote hivi pasina kuwa na lengo wala dhumuni
yoyote?
Uhalisia nikuwa Mola Mlezi Muumbaji Mtukufu (Allah) alitueleza
kuhusu dhumuni la yeye kutuumba sisi, nalo ni kumuabudu Mwenyezi
Mungu pekee, na ni nini anachotaka kutoka kwetu! na akatueleza kuwa
yeye pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa, na akatubainishia kupitia
mitume wake amani iwe juu yake ni namna gani tutamuabudu? Na ni
namna gani tutajiweka karibu kwake kwa kufanya maamrisho yake na
kuacha makatazo yake? na ni namna gani tutapata radhi zake? na
kuhadhari adhabu yake, na akatueleza kuhusu mafikio yetu baada ya kufa?
5
Na akatueleza kuwa maisha haya ya dunia si lolote bali mtihani tu,
nakuwa maisha ya kweli na ya uhakika na yaliyokamilika zaidi yatakuwa
Akhera baada ya kufa.
Na akatueleza kuwa atakayemuabudu Mwenyezi Mungu kama
alivyomuamrisha, na akayaacha aliyomkataza; basi atapata maisha mazuri
duniani, na neema za kudumu Akhera, na atakayemuasi na akamkufuru
basi atapata maisha ya shida katika dunia, na adhabu ya kudumu Akhera.
Na kwakuwa tunajua fika kuwa sisi hatuwezi kuendesha maisha haya
ya dunia pasina ya kila mtu kupata malipo ya yale aliyoyafanya
kuanzia ya kheri au ya shari; kwa hivyo hapatokuwa na adhabu kwa
madhalimu wala kuwalipa watenda wema?
Na ametueleza Mola wetu Mlezi kuwa kufaulu ni kwa kumridhisha
yeye na kuokoka na adhabu zake hakuwi ila ni kwa kuingia katika dini ya
Uislamu, ambao ni kujisalimisha kwake na kumuabudu yeye pekee asiye
na mshirika, na kunyenyekea kwa utiifu, na kutekeleza sheria yake kwa
ridhaa na kukubali, na ametueleza kuwa yeye hakubali kutoka kwa watu
dini isiyokuwa hiyo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Na Mwenye kutafuta dini isiyokuwa dini ya Kiislamu, basi hiyo
haitakubaliwa kwake, na yeye Akhera atakuwa ni miongoni mwa wenye
kupata hasara". [Al-Imran: 85].
Mwenye kutazama vile wanavyoviabudu watu wengi leo hii; atakuta
huyu anaabudu mtu, na mwingine anaabudu sanamu, na mwingine
anaabudu nyota na kadhalika, na haifai kwa mwanadam mwenye akili
timamu aabudu chochote isipokuwa Mola Mlezi wa walimwengu
mkamilifu katika sifa zake, inakuwaje anaabudu kiumbe au chini ya
kiumbe! Muabudiwa hawezi kuwa kiumbe au sanamu au mti au mnyama!
Dini zote wanazozitumia watu kuabudu leo hii -ukiacha Uislamu-
Mwenyezi Mungu hazikubali kwani ni dini zilizotengenezwa na binadam,
au dini ambazo zilikuwa ni za Mwenyezi Mungu kabla kisha zikachezewa
na mikono ya mwanadam, ama Uislamu hiyo ni dini ya Mola Mlezi wa
walimwengu, haitofautiani wala haibadiliki, na kitabu cha dini hii ni
Qur'ani Tukufu, ni kitabu kilichohifadhiwa kama alivyokiteremsha
6
Mwenyezi Mungu na bado kipo mikononi mwa waislamu mpaka leo hii
tena kwa lugha yake kilichoteremshwa kwayo kwa Mtume wa mwisho.
Na miongoni mwa misingi ya Uislamu ni kuwaamini Mitume wote
aliowatuma Mwenyezi Mungu, na wote walikuwa ni binadamu aliowatia
nguvu Mwenyezi Mungu kwa alama na miujiza mbali mbali, na akawatuma
kufikisha ujumbe wa kumuabudu yeye pekee asiye na mshirika wake, Na
wa mwisho katika Mitume ni Mtume Muhammadi rehema na amani ziwe
juu yake, Mwenyezi Mungu alimtuma kwa sheria za mwisho za kiungu
zilizokuja kufuta sheria za Mitume waliokuwa kabla yake, na akamtia
nguvu kwa miujiza mikubwa, na kubwa zaidi ni Qur'ani Tukufu, maneno ya
Mola Mlezi wa walimwengu, kitabu chake kitukufu zaidi wanadamu kuwa
kukijua, ni muujiza katika madhumuni yake na lafudhi zake na mpangilio
wake, na hukumu zake, ndani yake kuna muongozo wa kuipata haki
unaompeleka mtu katika furaha duniani na Akhera, na kilitaremka kwa
lugha ya kiarabu.
Na kuna ushahidi mwingi wa kiakili na wa kielimu (kisayansi) ambao
unathibitisha pasina shaka yoyote kuwa Qur'ani hii ni maneno ya muumba
Aliyetakasika na kutukuka nakuwa haiwezekani kuwa imetengenezwa na
mwanadam.
Na miongoni mwa misingi ya Uislamu ni kuamini Malaika, na kuamini
siku ya mwisho pale Mwenyezi Mungu atakapowafufua watu kutoka
makaburini mwao siku ya Kiyama ili awahesabu kwa matendo yao,
atakayetenda mema hali yakuwa ni muumini basi atapa neema za kudumu
peponi, na atakayekufuru na akatenda maovu basi atapata adhabu kubwa
motoni, na miongoni mwa misingi ya Uislamu ni kuamini yale aliyoyapanga
Mwenyezi Mungu katika mambo ya kheri au shari.
Na dini ya Uislamu ni mtaala ulioyaenea maisha yote, inaafikiana na
maumbile na akili, na nafsi zilizo sawa zinaikubali, ameiweka kuwa sheria
Muumba Mtukufu kwa ajili ya viumbe wake, na ndio dini ya kheri na
furaha kwa watu wote katika dunia na Akhera, haitofautishi kati ya ukoo
na ukoo, wala rangi na rangi, na watu wote ndani ya Uislamu ni sawa,
hakuna mbora katika Uislamu kwa mwenzie isipokuwa kwa kadiri ya
matendo yake mema.
Amesema Allah Mtukufu:ۡ
7
"Mwenye kufanya tendo zuri, akiwa ni mwanamume au ni mwanake,
na huku ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake , basi
tutampa maisha mazuri (yenye utulivu duniani hata kama ni mchache wa
mali), na tutawalipa huko Akhera thawabu zao kwa uzuri zaidi ya
walivyofanya (duniani)". [An Nahli: 97].
Na miongoni mwa mambo anayoyatilia mkazo Mwenyezi Mungu ndani
ya Qur'ani tukufu nikuwa kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola
muabudiwa, na Uislamu ndio dini, nakuwa Muhammadi ni Mtume na
kuingia katika Uislamu ni jambo la lazima ambalo mwanadam hana hiyari
katika hilo; na katika siku ya Kiyama kuna hesabu na malipo; yeyote
atakayekuwa muumini wa kweli basi huyu atafuzu na kufanikiwa
mafanikio makubwa, na atakayekufuru basi atapata hasara ya wazi.
Amesema Allah Mtukufu:
"...na atakayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi atamuingiza
katika pepo zipitazo chini yake mito, ataishi humo milele, na huko ndiko
kufuzu kukubwa,
na atakayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akavuka
mipaka yake, basi atamuingiza motoni, ataishi humo milele na atakuwa na
adhabu yenye kudhalilisha". [Al-Nisaa: 13-14].
Na atakayetaka kuingia katika Uislamu basi anatakiwa kusema:
Ash-hadu anlaa ilaaha illa llaah wa ash-hadu anna Muhammadan
Rasuulullaah (Ninashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa
haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa
Mwenyezi Mungu), kisha ajifunze sheria za Uislamu zilizobakia kidogo
kidogo; ili atekeleze yale aliyowajibishiwa na Mwenyezi Mungu.
Kwa faida zaidi: https://byenah.com/sw
8
9
Uislamu 3
Ni dini ya maumbile na akili na furaha 3
Nani aliyekuumba? 3
Na je, inawezekana kuwa Mwenyezi Mungu alituumba kisha akatuacha
hivhivi? Na je, inawezekana kuwa Mwenyezi Mungu aliumba viumbe vyote
hivi pasina kuwa na lengo wala dhumuni yoyote? 5
Na kwakuwa tunajua fika kuwa sisi hatuwezi kuendesha maisha haya ya
dunia pasina ya kila mtu kupata malipo ya yale aliyoyafanya kuanzia ya
kheri au ya shari; kwa hivyo hapatokuwa na adhabu kwa madhalimu wala
kuwalipa watenda wema? 6
10