Nakala





Uislamu unahimiza mchakato mzima wa kujiendeleza na kujitakasa. Mchakato huu ni wa moja kwa moja kati ya Mja na Mola wake - hakuna haja ya dhambi kushirikishwa au “kutubia” kwa mtu mwema/Padri. Vile vile Mungu hahitaji kujitoa muhanga kusamehe madhambi, na hakuna mtu yoyote "anaezaliwa ndani ya dhambi❞. 





6. Uwajibikaji na Hukumu 





siku ya Mwisho 





Uislamu unafundisha kwamba Mungu ni Mwadilifu na kwamba kila mtu atawajibika kwa matendo yake siku ya Kiyama. Kila mtu anawajibika, kwani ana uhuru wa kuchagua na akili ya kupambanua kati ya mema na mabaya. 





Ni hitajio kamili la haki kwamba kuwe na Siku ya Hukumu ambapo kila mtu atapewa thawabu au kuadhibiwa, vinginevyo maisha hayatakuwa ya haki kwani sio kila mtu atapata haki ya kweli katika ulimwengu huu. 





Uislamu unafundisha kwamba mwishowe tutahukumiwa kwa jinsi tulivyotimiza majukumu yetu na kutumia uhuru wetu wa kuchagua. Tutahukumiwa na Mungu, Mjuzi na Mwenye Hekima, ambaye anajua na kuona kila kitu tunachofanya. Hii inahimiza jamii yenye usawa zaidi na inawapa watu ridhaa wakijua kwamba mwishowe haki itatawala. 





7. Njia ya Maisha inayofaa 





na yenye usawa 





Uislamu hutoa usawa kati ya imani na hatua, kwani zote zinahitajika kwa maisha thabiti. Inatoa mwongozo kwa hali zote na mazingira yote. Ni dini ya vitendo yenye kufuata matendo maalum ya ibada hususan kukidhi mahitajio ya kiroho, mwili, saikolojia na mahitaji ya jamii. 





Mifano ya matendo ya ibada yenye faida kubwa ni kama: 





Maombi matano ya kila siku - Yanakinahisha roho kwa kukidhi hitajio la kiroho la kuwasiliana mara kwa mara na Mungu (haswa katika maisha ya leo ya shughuli nyingi); humfanya mtu kuwa mnyenyekevu kwa kumwinamia na kumsujudia Mungu; huondoa vizuizi / kiburi / ubaguzi wowote kati ya waumini wanaosali pamoja; husaidia mtu kujizuia kutenda dhambi kutokana na mtu huyo kusimama mara kwa mara mbele ya Mungu. 





• Zaka - Humtakasa mtu kutokana na ubinafsi; inahimiza huruma kwa maskini; inakumbusha Mja baraka za Mola wake; inasaidia kupunguza umaskini; huziba pengo kati ya . 





• Kufunga Ramadhani - Hukuza kujitakasa kiroho, kujizuia na 





kujiboresha; ni faida kiafya kama ilivyothibitika kisayansi; uelewa na ufahamu wa wale wasio nacho; hufundisha watu kuwa na tabia ya kumtii Mungu. 





• Hija - Huwaunganisha watu wa kila rangi, kabila, hadhi na utaifa, kwani mahujaji huvaa mavazi rahisi na yanayofanana, wakati wakifanya matendo mema kadhaa katika ibada za pamoja. 





Kwa kuwa Uislamu umetoka kwa Mungu, kila amri inayopatikana katika dini hiyo ni nzuri na yenye faida kwa mtu binafsi na jamii wakati inafanywa kwa usahihi. Mifano ya Qur'ani ni pamoja na kuwa waaminifu, mwenye kusamehe, mkweli, mkarimu kwa mke, mvumilivu, mwenye haki, mwenye wastani, mnyenyekevu, mkweli, na anayewaheshimu wazazi, familia na wazee. Pia kuna kanuni nyingi katika mafundisho ya Uislamu zinazozuia au kupunguza mengi ya shida za kibinafsi na za kijamii zinazoikabili dunia hii leo. 





8. Ujumbe kwa Wote 





Wakati wote 





Uislamu una ujumbe ambao 





unatumika kwa watu wote wakati wote, tangu kuumbwa kwa Adam hadi Siku ya kiyama. Unatumika leo kama ilivyokuwa zama za kale. 





Hitimisho 





Mungu yupo kwa kila mtu. Ili kupata radhi 





za Mola wao, Watu wanaweza kujitofautisha wao wenyewe kwa kupitia matendo mema tu - sio kupitia ukabila, utajiri, jinsia, utaifa au tabaka la kijamii. 





Ujumbe mzuri wa Uislamu na usiopitwa na wakati ni ujumbe huo huo wa Manabii wote, pamoja na Nuhu, Ibrahimu, Musa, Issa na Muhammad (amani iwe juu yao wote). Wote waliwalingania watu wao "Kujisalimisha kwa Mungu Mmoja wa Kweli" mana yake kwa Kiarabu, “Muislamu”. Kujisalimisha huku kwa Mungu kunamuwezesha mtu kutimiza kusudio la maisha kwa kutambua ukuu wa Mungu na kumwabudu yeye kwa dhati. Kwa kufanya hivyo, mtu atapata faida nyingi za Uislamu zilizotajwa hapo juu. 





Kwa maelezo zaidi wasiliana na 





Islamic Information Center, Sultan Qaboos Grand Mosque Muscat, Sultanate of Oman 





WhatsApp: +968 99250777 E: support@iicoman.om W: www.iicoman.om 





KWANINI UISLAMU? 





UZURI NA FAIDA 





ZA UISLAMU 





Je Dini zote 





ni sawa? 





Nitajuaje ambayo 





ni sahihi? 





Kwanini nichague 





Uislamu? 





Jifunze 





misingi 





islamicpamphlets.com 





Kijitabu hiki kinalenga kujadili baadhi ya uzuri, faida na mambo ya kipekee ya Uislamu ikilinganishwa na imani na dini zingine. 





1. Uhusiano wa Karibu 





na Muumba 





Kiini cha Uislamu ni mtazamo wa uhusiano wa kibinafsi wa mtu na Mungu, Muumba wao. Inamshawishi muumini kuwa na ufahamu wenye kukinai juu ya Mungu ambao ndio ufunguo wa furaha ya kudumu. 





Uislamu unafundisha kwamba Mungu ndiye 





chanzo cha amani. Kwa kuzingatia 





uhusiano huu muhimu na kufuata mwongozo wa Mungu, waumini 





wataweza kupata amani ya kweli 





na utulivu. Kutafuta furaha ya kudumu kupitia njia zingine, kama vile kufuata matamanio ya mtu au kujilimbikizia mali, kamwe hakutaziba nafasi ya upweke tuliyonayo. Hitaji hili linaweza kujazwa tu na ufahamu wa Mungu. 





Kutoshelezeka kweli 





kweli kunapatikana katika kumtambua na kumtii 





Muumba: "Kwa kweli, katika kumkumbuka Mungu mioyo hupata pumziko." Quran 13:28 





Sababu ya msingi ya uhusiano huu wa karibu ni kwamba Waislamu wanakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Muumba wao. Hakuna mpatanishi, kama vile kuomba kwa, au kupitia wengine katika kumwabudu Mungu. 





2. Mtazamo Mzuri juu ya Maisha 





Uislam unampa mtu mtazamo uliokuwa wazi juu ya matukio mazuri na mabaya yanayotokea maishani mwao, kuwa ni majaribio toka kwa Mungu. Inamtumainisha mtu kuelewa matukio yatokeyayo kuwa ni katika muktadha wa kusudi la jumla la maisha, ambalo ni kumtambua Mungu na kumtii. Aliwaumba wanadamu na akili na hiari ili kuwajaribu kama ni nani atakayeamua kwa maksudi kufuata mwongozo Wake. Maisha tuliyonayo ni uwanja wa mwisho wa majaribu na ingawa hatuwezi kudhibiti kila kitu kinachotokea kwetu, tunaweza kujidhibiti sisi wenyewe jinsi tunavyopokea. Uislamu unamhimiza mtu kuzingatia kile kilicho katika udhibiti wao, kumshukuru Mungu kwa Baraka zake, na kuwa mvumilivu wakati wa shida. Uvumilivu au shukrani - hii ndiyo njia ya maisha ya furaha. 





Uislamu unamhimiza muumini kutovutika na furaha za kupindukia za kidunia inayoweza kumfanya mtu kumsahau Mungu, na pia kuwa na hali ya huzuni kubwa ambayo inaweza kusababisha mtu kupoteza tumaini na kumlaumu Mungu. Kwa kutoshikamana kupita kiasi na tamaa za kilimwengu, Muislamu amepewa mamlaka sio 





tu ya kushughulikia vyema misiba yoyote, bali awe na faida na mkarimu kwa jamii. Hii inasababisha mtazamo sahihi na wenye matumaini juu ya maisha. 





3. Dhana safi na Sahihi ya Mungu 





Tofauti na dini zingine, Uislamu haukupewa jina la mwanzilishi wake au jamii ya uzawa wake. Uislamu ni jina vumishi ambalo linaashiria utii kwa Mungu, Muumba wa Ulimwengu. Moja ya uzuri wake bora kabisa ni kwamba unakubali ukamilifu, ukuu na upekee wa Mungu bila shaka yoyote. Hii inaonyeshwa katika mafundisho safi ya Uislam ya sifa zake Mungu: 





Mungu ni Mmoja na wa kipekee 





• Mungu hana washirika, hana mfano wake na hana mpinzani. 





• Mungu hana baba, mama, wavulana, mabinti au wake. 





• Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa. 





Mungu ni muweza wa kila kitu 





• Mungu ana mamlaka kamili na uweza juu ya vitu vyote. 





• Kumtii Mungu hakumuongezei Nguvu Zake, wala kutotii hakumpunguzii nguvu Zake. 





Mungu ndiye Aliye juu 





• Hakuna kitu juu au kinacholingana na Mungu. 





• Sifa za Mungu hazifanani na zile za uumbaji wake. 





• Hakuna sehemu ya Mungu iliyo ndani ya mtu yeyote au kitu chochote. 





Mungu ni Mkamilifu 





• Mungu hana mapungufu yoyote ya kibinadamu, kama vile kupumzika siku ya saba baada ya kuumba ulimwengu. 





• Mungu siku zote huwa na sifa za ukamilifu na hafanyi chochote kuathiri ukamilifu huu kama vile "kuwa mtu❞ kama inavyodaiwa na dini zingine. Mungu hafanyi vitendo visivyo vya kimungu, kwa hivyo ikiwa Mungu angekuwa mwanadamu na kuchukua sifa za kibinadamu, bila shaka, hatakuwa tena Mungu. 





4. Unasisitiza Ushahidi & Imani 





Uislamu ni dini ambayo imani inategemea uthibitisho ulio wazi. Unahimiza watu kutumia akili waliyopewa na Mungu kufikiri na kutafakari juu ya maisha yao na ulimwengu. Ingawa maisha haya ni mtihani, Mungu ametoa ishara na mwongozo wa kutosha kwa watu walio na nia safi na wanyofu kuweza kuukubali ukweli. 





Kinyume na dini nyengine, Uislam una ushahidi mwingi ulio wazi, ishara na maajabu ndani ya Kitabu kithibitasho kuwa Quran inatoka kwa Mungu. 





Quran: 





• Haina makosa wala mikingamo licha ya kuteremshwa katika kipindi cha miaka 23. 





"Na kwa hakika 





tumeteremsha katika Quran ishara zilizo wazi: na Mungu humuongoza 





amtakaye katika 





• Imehifadhiwa neno kwa neno tangu kuteremshwa kwake katika lugha ya kiarabu, tofauti na vitabu vyengine vya dini vilivyo chakachuliwa, kubadilishwa au kupotea. 





njia sahihi.” Quran 24:46 





• Ina lugha nyepesi, safi na ujumbe kwa watu wote wenye athari kubwa kwa wale wenye kutafuta ukweli. 





• Inayo mtindo wa kipekee wa lugha isiyoweza kuigika ambao unajulikana ulimwenguni kama kilele cha ufasaha wa Kiarabu na uzuri wa lugha - ili hali Quran ilifunuliwa kwa Nabii Muhammad (s.a.w) ambaye alijulikana kuwa hajui kusoma wala kuandika. 





• Inayo ukweli mwingi wa kushangaza wa kisayansi ambao umegunduliwa tu hivi karibuni, licha ya kuteremshwa zaidi ya miaka 1400 iliyopita. 





Hivyo basi, ni wazi, busara na sahihi zaidi kukubali kuwa mambo mengi ya kipekee na ya miujiza ndani ya Quran hayawezi kutoka kwa mwingine isipokuwa Mungu. 





5. Msamaha wa Dhambi 





Uislamu unahimiza uwiano kati ya tumaini katika rehema ya Mungu na hofu ya adhabu Yake - yote mawili haya yanahitajika katika kuishi maisha mazuri na ya unyenyekevu. 





Tumezaliwa hatuna dhambi lakini 





tuna uhuru wa kufanya dhambi. Mungu ametuumba na anajua tuna kasoro na tunafanya dhambi, lakini muhimu kuliko 





chochote ni kile kinachofuatia 





baada ya kufanya madhambi. 





Uislam unafundisha kuwa Mungu ni Mwenye Rehema kubwa na anasamehe na anafuta dhambi kwa wale wenye kujutia madhambi 





ya 





"Msikate 





tamaa na rehema Mwenyezi Mungu, kwa wingi wa madhambi yenu, kwani Mwenyezi Mungu Anasasamehe dhambi zote kwa 





mwenye kutubia." Quran 39:53 





yao. Hatua muhimu za kufutiwa dhambi ni kuwa mkeli, mwenye kujutia, kujizuia kufanya dhambi au nia ya kurudia kufanya dhambi. 



Machapisho ya hivi karibuni

Uislamu Ni dini ya ma ...

Uislamu Ni dini ya maumbile na akili na furaha

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL