Nakala




زيارة المدينة


ZIARA YA MADINA MUHAMMAD FARAJ SAALIM AS-SAIYL


MFASIRI SHEKH: YASSINI TWAHA KIMEREJEWA NA SHEKH: ABUBAKARI SHABAN





بسم الله الرحمن الرحيم


Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, na Rehma na


Amani za Allah zimuendee Nabii Muhammad pamoja


na Ahli zake na Swahaba zake na Waisilamu wote


wataofuata Mwenendo wake mpaka siku ya Mwisho.


Ziara ya Madina ni jambo linalopendeza sana, Kwa


kawaida Mahujaji na wafanyao ‘Umra huuzuru Mji


huu Mtukufu wa Mtume wa Allah (Rehma na Amani


za Allah ziwe juu yake) kabla au baada ya kwenda


Makkah.


Hata hivyo kuna baadhi ya watu wanaojaribu


kupunguza umuhimu wa ziara ya Mji huu Mtukufu


kwa kuwaambia watu kwa mfano:


“Ukihiji bila ya kwenda Madina Hija yako


inakubaliwa", au


“Ziara ya Madina haihusiki na Hija", au


“Haina lazima kwa Mwenye kuhiji kwenda


Madiynah", n.k.


Ingawaje maneno kama hayo ni ya kweli, na kwamba


mtu akienda Makkah na kutimiza shughuli za Hija bila


ya kwenda Madina, Hija yake huwa imekamilika, na


haina shaka yoyote, na inakubaliwa, lakini maneno


hayo yanaleta maana ya kuwakimbiza watu mbali na


mji huo Mtukufu ambao Mtume wa Allah (Rehma na


3


Amani za Allah ziwe juu yake) alikuwa akiupenda


sana na kuutukuza.


Mtume wa Allah (Rehma na amani za Allah ziwe juu


yake) amesema:


(Madina ni Mji Mtukufu kuanzia (Jabali) Ayrin mpaka


(Jabali) Thawr).


Haya ni majabali mawili, mojawapo lipo Mwanzo wa


Madina na la pili lipo Mwisho wa Madina.


Na akasema:


(Hakika Ibrahim ameutukuzaMji wa Makkah na


akauombea dua, na Mimi na utukuza Mji wa Madina


kama alivyoutukuza IbrahimMji wa Makkah. Mola


wangu Mimi naitukuza Ardhi (yote ya Madina) iliyo


baina ya majabali yake (Ayrin na Thawr), usikatwe


mti wake na pasitendeke maasi, Atakayetenda maasi


katika Mji huu, atapata laana ya Allah na ya Malaika


wake na ya watu wote kwa ujumla). [Imepokewa na


Bukhari na Muslim].


Wakati fulani palikuwa na shida kubwa sana hapo


Madina na vitu vikapanda bei na kuwa ghali kupita


kiasi, Mtume wa Allah (Rehma na Amani za Allah ziwe


juu yake)


akasema kuwaambia watu wa Madina:


(Nakupeni bishara njema. Mimi nimekubarikieni


katika vibaba vyenu na katika magao yenu, chakula


cha (mtu) mmoja kitawatosha wawili, na cha wawili


kitawatosha wanne, watano au sita. Kwa hivyo


jikusanyeni katika chakula kwa sababu baraka imo


katika mkusanyiko wa jamii. Atakayesubiri katika


shida za Mji huu (Madina) nitamuombea shifaa siku


4


ya Qiyama, na atakayeweza kufa katika Mji huu, basi


afe, kwani Mimi nitakuwa Mwenye kumuombea


shafa’a siku ya Qiyama).


[Imepokewa na Twabaraaniy].


Hii ndiyo sababu iliyomfanya ‘Omar bin al-Khattwaab


(Radhi za Allah ziwe juu yake) apende kuomba dua


ifuatayo:


“Mola wangu, Mimi nakuomba nife Shahidi katika njia


yako na katika Mji wa Mtume wako (Rehma na Amani


za Allah ziwe juu yake)”. [Imepokewa na Bukhaari].


Dua zote mbili hizo za ‘Omar (Radhi za Allah ziwe juu


yake) zimekubaliwa, maana aliuliwa shahidi akiwa


anaswalisha Swala ya Alfajiri ndani ya Msikiti wa


Mtume wa Allah (Rehma na Amani za Allah ziwe juu


yake), na akazikwa Madina tena karibu na kaburi la


Sahibu yake Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe


juu yake).


Hizi ni baadhi tu ya sifa mbali mbali za Mji huu


Mtukufu ambao Mtume wa Allah (Rehma na Amani za


Allah ziwe juu yake) alikuwa akiupenda sana.


Pana kundi jengine ambalo hupindukia mipaka katika


kuitukuza ziara ya Mji huu Mtukufu, Kundi hili


huwatuhumu wasiouzuru Mji huu Mtukufu kuwa


wamemuasi Mtume wa Allah (Rehma na Amani za


Allah ziwe juu yake), wakitegemea Hadithi zisizo


sahihi (Hadithi Maudhu’i).


5


(Hadithi Maudhu’i - ni zile ambazo Maulamaa wa fani hii wamezigunduwa kuwa ni Hadithi zilizopachikwa, zisizo za kweli na hazina asili wala msingi wowote). Mfano wa Hadithi wanazozitegemea ni hizi zifuatazo: Wanasema kwamba eti Mtume wa Allah (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) amesema: “Atakayehiji na asinizuru ameshaniasi.” au “Atakayehiji na akalizuru kaburi langu baada ya kufa kwangu anakuwa mfano wa aliyenizuru nilipokuwa hai”. Zipo Hadithi nyingi za mfano huu. Ni haramu kumsingizia Mtume wa Allah (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) uongo, na Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) ametoa onyo kali kwa kila anayemsingizia uwongo aliposema: (Atakayenisingizia uongo makusudi, basi keshajitayarishia makazi yake Motoni). Hapana sababu yoyote ya mtu kutumia hoja kama hizo katika kuithibitisha Ibada ya aina yoyote ile. Isitoshe zipo hoja zenye nguvu kuliko hizo zinazotegemea Hadithi zilizo sahihi zinazotilia nguvu ziara ya mji huu mtukufu wa Madina.


ZIARA YA MISIKITI Kwanza kabisa itabidi tusahihishe itikadi yetu kuhusu ziara ya Mji huu Mtukufu katika kutia nia ya Ziara. Nia ya ziara ya Mji wa Madina, inatakiwa iwe ni kuuzuru Msikiti wa Mtume wa Allah (Rehma na


6


Amani za Allah ziwe juu yake) na isiwe kulizuru kaburi lake!!!, kama wanavyotia nia hiyo baadhi ya watu. Ingawaje kuzuru makaburi kwa nia ya kuwaombea maiti na kujikumbusha Akhera ni jambo jema, lakini kufunga safari ndefu kwa ajili hiyo haijuzu. Mtume wa Allah (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) amesema: (Isifungwe safari ndefu (kwa ajili ya ibada) isipokuwa kwenda katika Misikiti mitatu; Al-Masjidul Haraam (Makkah), na Msikiti wangu huu (Madina), na Msikiti wa Ilyaa (Baytul Maqdis),). [Imepokewa na Bukhari, Muslim, Tirmidhi na wengineo]. Na akasema: (Swala katika Msikiti wangu ni bora kuliko Swala elfu katika Misikiti mingine, (isipokua msikiti wa makkah) na Swala katika Msikiti wa Makkah (Masjidul Haraam) ni bora mara Laki kuliko Misikiti mingine). [Imepokewa na Imam Ahmad bin Hanbal]. Allah huumba na kuchagua atakavyo, Ametuchagulia sayari ya Ardhi miongoni mwa sayari zote kuwa ni mahali petu pa kuishi, na Akamchagua Mwanadamu miongoni mwa viumbe vyote Akamtukuza, kisha Akawachagua Mitume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yao) miongoni mwa Binadamu wote na kuwatukuza, na Akamchagua Nabii Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kuwa ni Imamu wa Mitume wote, na Akaichagua Misikiti katika Ardhi kuwa ni mahali patukufu kuliko sehemu zote, kisha Akaichagua Misikiti hii mitatu kuwa ni Mitukufu zaidi miongoni mwa Misikiti yote, na Yeye


7


ndiye Anayeumba na kuchagua na sisi jukumu letu ni kufuata tu. Kwa sababu Anayeumba ndiye Mwenye kujua na si aliyeumbwa. Allaah Anasema: {Na Mola wako huumba atakavyo na huchagua (atakavyo); Hawana (viumbe) khiyari; Allah Ameepukana na upungufu, na Ametakasika na hao wamshirikishao (naye).} [Al-Qasas: 68].


BUSTANI KATIKA BUSTANI ZA PEPONI Hapana Hadithi sahihi isemayo; "Baina ya Kaburi langu na mimbari yangu bustani katika bustani za Peponi." Bali Hadithi iliyo sahihi ni ile iliyopokelewa na Imam Bukhari na Muslim na Tirmidhi na An-Nasaai na Imam Ahmad inayosema kuwa Abu Hurayrah (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema, kuwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) amesema: (“Baina ya Nyumba yangu na Mimbari yangu, bustani katika bustani za Peponi”). (Bayna BAYTIY wa mimbariy, na sio Bayna Qabriy wa Mimbary). Kwa hivyo itikadi iliyo sahihi ni kutia nia ya kuuzuru Msikiti wa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) na sio kaburi lake, na hii ni kwa sababu unapofika pale kaburini na kumswalia na kumsalimia Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), wewe na aliyopo popote duniani thawabu zenu ni sawa sawa, maana aliye mbali pia Swala na Salam


8


zake zinafikishwa kwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). Lakini ulichofaidika wewe ni kule kusali kwako ndani ya Msikiti wake (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), na hasa katika Ar-Rawdhah Ash-Shariyf, na pia unafaidika na ziara yako katika sehemu nyingine Takatifu za Madina. Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) amesema: (Niswalieni, kwani popote mlipo Swala zenu nina fikishiwa). [Imepokewa na Abu Daawud, Imam Ahmad na Twabarani]. Na akasema: (Allah Ana Malaika wanaotembea Ardhini, wananifikishia salam kutoka kwa umma wangu). [Imepokewa na An-Nasai, Ad-Daramiy na Ibni Hibban].


9


ZIARA YA MSIKITI Inapendeza mtu aoge na kuvaa nguo safi, kisha aende Msikitini na kuingia kwa mguu wa kulia kwa utulivu na unyenyekevu na kusema pale anapoingia: “A’udhu biLlahi mina Shaytwaani rrajiym, BismiLlahir Rahmanir Rahiym Allahumma Swaliy ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa sallim Allahumma gh-firliy dhunuubiy wa ftah liy ab’waaba rahmatika.” Na maana yake ni: Baada ya kusema A’udhu biLLahi na BismiLLahi, kisha unamswalia Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) na ‘Aali zake na unamuomba Allah maghfirah (msamaha) na Akufungulie milango yake ya Rehma. Ni vizuri unapoingia Muskitini kwanza uelekee Ar-Rawdhah (sehemu iliyopo baina ya nyumba yake na mimbari yake ndani ya Msikiti), na kuswali hapo Tahiyyatul Masjid rakaa mbili, ukishindwa kwa sababu ya zahma, basi swali sehemu yoyote ile ndani ya Msikiti, na ukishaswali elekea penye kaburi la Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kwa utulivu na kwa moyo mkunjufu, na unapofika penye kaburi lake sema; “Assalamu Alayka ya RasuulaLLaah wa RahmatuLLahi wa Barakaatuh! Na unaweza kuzidisha kwa kusema: “Swalla Allahu wa sallam ‘alayka wa ‘alaa asw-haabika, wa jazaaka Allahu ‘an ummatika khayra, Allahumma Aatihi al-wasiylata wal fadhwiylata wa b’ath-hul maqaamal mahmuudal lladhiy wa’adtahu”.


11


Na maana yake ni: “Amani iwe juu yako ewe Mtume wa Allah, na Rehma za Allah na Barakah zake.” “Rehma za Allah na Amani ziwe juu yako na juu ya Maswahaba zako, na akulipe Allah kheri Wewe na Umma wako, Ee Allah mpe wasiylah na fadhila na mnyanyue katika makazi matukufu ambayo umemuahidi. Kisha unasogea mbele kidogo na unamsalimia AbuBakar (Radhi za Allah ziwe juu yake), aliyezikwa umbali wa dhiraa moja na kaburi la Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), kisha hatua moja nyingine unamsalimia ‘Omar (Radhi za Allah ziwe juu yake). Kwa sababu Maswahaba wawili hawa (Radhi za Allah ziwe juu yao) wamezikwa karibu na Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). Kisha unaelekea Qibla na kujiombea Mwenyewe Dua na kila unayempenda na unawaombea Ndugu zako Waisilamu, kisha unaondoka. Si vizuri kunyanyua sauti na kuomba kwa sauti kubwa, unatakiwa uombe kwa sauti ndogo na kwa moyo mkunjufu, kiasi cha kuweza kujisikia Mwenyewe tu. Iwapo utasoma juu ya ukuta wa nyumba yake (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), ambayo kwa sasa ni kaburi lake, utaona kuwa imeandikwa Aayah isemayo; {Ya ayyuha lladhiyna aamanuw Laa tarfa’uw aswaatakum fawqa swawti Nnabiy}. Na maana yake ni:


11


(Enyi mlioamini!Msinyanyue sauti zenu zaidi ya sauti ya Nabii). [Suratul-Hujurat: 2]. ‘Omar (Radhi za Allah ziwe juu yake) aliwahi kuwasikia watu wawili wakipaza sauti zao mahali hapo, akawaambia: “Mungelikuwa nyinyi ni watu wa hapa hapa Madina, basi ningelikupigeni bakora”. Haijuzu mtu kupangusa Mikono yake kwenye kuta za Kaburi kisha akajipangusia Mwilini kwake, au kubusu yale Mapambo ya Kaburi, kama wanavyofanya Baadhi ya watu kwa kutegemea eti wanapata Baraka za Mahali hapo. Haya ni katika mambo aliyokataza Mtume (Rehma na amani za Allah ziwe juu yake) aliposema: (Musigeuze kaburi langu kuwa mahala pa Ibada, na Mniswalie popote mlipo, kwa sababu Swalah zenu nina fikishiwa). Kumbuka - Tulivyoamrishwa ni kumswalia na kumsalimia Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), na sio kumuomba yeye akuondolee shida zako. Dua ni Ibada, na ibada zote zinaelekezwa kwa Allah peke Yake. Unapomaliza kulizuru kaburi, omba Dua ukiwaumeelekea Qiblah na umelipa mgongo Kaburi la Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) - Usielekee kaburini, huku ukiomba Dua.


12


MAKABURI YA BAQIY Hakuna ulazima ila akipenda mtu vizuri kwa Wanamume tu, kuyazuru makaburi ya Baqiy’, mahala walipozikwa Maswahaba wengi sana (Radhi za Allah ziwe juu yao), pamoja na wake za Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yao), wajukuu zake (Radhi za Allah ziwe juu yao), na wengi katika waliofuata baada yao, kama vile Imam Maalik na wengineo (Allah Awarehemu). Kumbuka kuwa waliozikwa hapo wote ni ndugu zako Waisilamu, kwa ajili hiyo unatakiwa unapoyafikia makaburi hayo, ufanye kama alivyokuwa akifanya Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), kwani Mtume wetu Mtukufu (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) alikuwa mara anapoyafikia makaburi hayo akiwasalimia na kuwaombea Dua wote waliozikwa humo bila ya kubagua. Alikuwa akisema: “Assalaamu Alaykum ahl ddiyaari minal muuminin wal muslimiyn, wainnaa in shaa Allahu bikum laahiquwn. Yarhamu llahul mustaqdimina minna wa min-kum wal-muta-akhiriyn. Nas-alu Allaha lanaa


13


walakumul ‘aafiyah. Allahumma laa tuh-rimnaa ajrahum walaa tuftinnaa ba’adahum, waghfir lanaa walahum”.


ZIARA YA MSIKITI WA QUBAA Hakuna ulazima mtu anapokuwa Madina kwenda Msikiti wa Qubaa (Masjid Qubaa), lakini akiwa na nafasi baada ya 'ibada zake, akitaka anaweza kuzuru Msikiti wa Mwanzo ulojengwa na Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), ambao Allah Amesema juu yake: {Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa kumcha Allah tangu siku ya kwanza (ya kufika kwa Mtume Madina) unastahiki zaidi wewe usimame humo. Humo wamo watu wanaopenda kujitakasa. Na Allah Anawapenda wajitakasao}. [At-Tawbah: 108]. Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) alikuwa akipenda kwenda hapo kila Jumamosi, Akiwa amepanda Mnyama, na kuswali rakaa mbili. Na alikuwa akisema: (Mtu akijitwaharisha Nyumbani kwake, kisha akaenda Msikiti wa Qubaa na Akaswali hapo rakaa mbili, huandikiwa thawabu za Aliyefanya Umra). [Imepokewa na Imam Ahmad, An-Nasai, Ibni Majah na Al-Hakim[


MASHAHIDI WA UHUDI


14


Hakuna ulazima japo Mtu anaweza kuzuru Mashahidi wa Uhudi na kuwaombea, na hapo lipo kaburi la ‘Ammi yake Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) Hamza, (Radhi za Allah ziwe juu yake) ‘Kiongozi wa Mashahidi’ pamoja na Maswahaba wengine (Radhi za Allah ziwe juu yao) waliokufa mashahidi. ‘Ammi yake Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) aliuliwa hapo alipopigwa mkuki katika vita vya Uhudi na kuzikwa pale pale alipouliwa. Kwa vile mahali hapo pana Makaburi mengine, kwa hivyo ni vizuri mtu kuwatolea Salam waliozikwa hapo kwa kutamka yale yale uliyotamka pale ulipoyazuru Makaburi ya Baqiy’. Twamuomba Allah Mtukufu, aturuzuku Elimu yenye Manufaa, na Atujaalie kuwa katika wenye kuutembelea Mji huo, na kuswali katika Raudhwa Tukufu. Ameen!!.



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI