Nakala

1


بسم الله الرحمن الرحيم


SIFA ZA MWANAMKE WA KIISLAM Imekusanywa na: Idara ya Wanachuoni.com Imepitiwa na: Yunus Kanuni Ngenda 1- Ni mwenye kushikamana na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mipaka anayoweza juu ya ufahamu wa wema waliotangulia (Salaf-us-Swaalih). 2- Anatakiwa vilevile atangamane na Waislamu wenzake matangamano mazuri, bali hata makafiri [atangamane nao kwa uzuri]. Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema: وَقُولُوا لِلنَّاسِ


"Na semeni na watu kwa uzuri." (02:83) إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الَْْمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا


"Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe." (04:58) وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا


"Na mnaposema [katika kushuhudia] basi semeni kwa uadilifu." (06:152)


2





"Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu mtoapo


ushahidi kwa ajili ya Allaah japokuwa ni dhidi ya nafsi zenu au


wazazi wawili, au jamaa wa karibu. Akiwa tajiri au maskini


Allaah Anawastahiki zaidi. Basi msifuate hawaa [matamanio]


mkaacha kufanya uadilifu. Na mkipotoa [ushahidi wenu] au


mkijitenga [kuepuka au kukataa kutoa ushahidi], basi hakika


Allaah kwa myatendayo ni Khabiyraa (Mjuzi wa vilivyodhahiri


na vilivyofichikana)." (04:135)


3- Anatakiwa kushikamana na mavazi ya Kiislamu na ajiepushe


na kujifananisha na maadui wa Kiislamu. Imaam Ahmad


amepokea kwenye "al-Musnad" yake kupitia Hadiyth ya


´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambapo


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:


"Yule mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao."


Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema kuhusiana na mavazi:





"Ee Nabii! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake


wa Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo kunapeleka karibu


zaidi watambulikane (kuwa ni watu wa heshima, ili)


wasiudhiwe." (33:59)


at-Tirmidhiy amepokea kwenye "al-Jaamiy´" yake kupitia


Hadiyth ya ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) ya


kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:


3


"Mwanamke ni ´Awrah. Anapotoka nje basi matumaini ya


Shaytwaan huwa juu."


4- Tunamnasihi vilevile amtendee mume wake wema ikiwa


kama anataka kupata maisha yenye furaha. Mtume (Swalla


Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:


"Mwanaume akimwita mke wake kwenye kitanda chake na


akakataa, basi Malaika humlaani." (al-Bukhaariy na Muslim)


Kwenye "as-Swahiyh" ya Muslim imekuja:


"... isipokuwa yule aliyeko mbinguni humghadhibikia."


5- Awaangalie watoto zake kwa malezi ya Kiislamu. al-


Bukhaariy na Muslim wamepokea kwenye "as-Swahiyh" zao


kupitia Hadiyth ya ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu


´anhumaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa


sallam) amesema:


"Nyote ni wachungaji na kila mmoja ataulizwa juu ya kile


alichokichunga."


Akasema kuhusu mwanamke:


"Ni mchungaji kwenye nyumba ya mume wake na ataulizwa


kwa kile alichokichunga."


Kwenye "as-Swahiyh" mbili kupitia Hadiyth ya Ma´qil bin


Yasaar (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume wa Allaah


(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:


"Hakuna mchungaji ambaye atachungishwa watu wake kisha


asiwaangalie isipokuwa hatonusa harufu ya Pepo."


4


Da´wah isimshughulishe na kuwalea watoto wake.


6- Inatakiwa kwake kuridhia yale Aliyohukumu Allaah kwa


kumfadhilisha mwanaume juu ya mwanamke. Allaah


(Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema:





"Wala msitamani ambayo Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu


kuliko wengine." (04:32)





"Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah


Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya


[matumizi] wanayotoa katika mali zao. Basi wanawake wema


watiifu, wenye kuhifadhi [hata] wanapokuwa hawapo


[waumezao] kwa Aliyoyahifadhi Allaah. Na wale [wanawake]


ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na [wakiendelea uasi]


wahameni katika malazi [vitanda] na [mwishowe wakishikilia


uasi] wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia [ya


kuwaudhi bure]." (04:34)


Imepokelewa kwenye "as-Swahiyh" mbili kupitia kwa Abu


Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume (Swalla


Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:


"Watendeeni wanawake wema. Hakika mwanamke ameumbwa


kwa ubavu ulopinda. Kiungo kilichopinda zaidi kwenye ubavu


wake ni kile cha juu. Ukienda kutaka kukinyoosha utakivunja,


na ukikiacha kitabaki kimepinda. Hivyo basi, watedeeni


wanawake weama."


5


Inatakiwa kwa mwanamke awe ni mvumilivu kwa yale Aliyomkadiria Allaah kwa kumfadhilisha mwanaume juu yake. Lakini hata hivyo hii haina maana mwanamke amuabudu mwanaume. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema kama ilivo kwenye "al-Jaamiy´" ya at-Tirmidhiy: "Watendeeni wanawake wema. Hakika wao ni kama wafungwa wenu. Hammiliki jengine kwao zaidi ya hilo. Tanabahini! Hakika nyinyi mna haki juu ya wanawake zenu. Tanabahini! Hakika wanawake zenu wana haki juu yenu. Haki zenu juu yao ni wao kutomwacha yeyote yule mnayemchukia akalala kwenye vitanda vyenu na wasimruhusu kwenye manyumba yenu yule mnayemchukia. Haki zao juu yenu ni kuwatendea wema katika kuwalisha, kuwavisha." Kwenye "as-Sunan" na "al-Musnad" ya Imaam Ahmad kupitia Hadiyth ya Mu´aawiyah bin Haydah ya kwamba kuna mtu alimwambia: "Ee Mtume wa Allaah! Ni zipi haki za mke juu ya mmoja wetu?" Akasema: "Ni umlishe pale utapokula. Umvishe pale utapovaa. Usimpige usoni na usimkebehi na usimhame isipokuwa nyumbani." Inatakikana nyote kusaidizana katika kheri. Mwanaume atangamane na mke wake matangamano ya Kiislamu na amsaidie kusoma na kulingania katika Dini ya Allaah. Mwanamke vilevile atangamane na mume wake matangamano ya Kiislamu na amsaidie kusoma na kulingania katika Dini ya


6


Allaah na kuendesha mambo ya nyumbani kwa uzuri. Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema:


"Shirikianeni katika wema na uchaji Allaah na wala msishirikiane katika dhambi na uadui." (05:02) Mzungumzaji: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy Chanzo: "Majmuu´-ul-Fataawaa an-Nisaa-i-yyah"



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI