بسم الله الرحمن الرحيم
MAMBO 10 YATAKAYOKUFANYA UWE MUME BORA Imeandikwa na Kabuga Kanyegeri Imepitiwa na Abubakari Shabani Rukonkwa. Utangulizi: Kila sifa kamilifu nizake Allah mtukufu alie fanya maisha yasiwe mazuri mpaka mtakapo kuwa wawili mke na mume kasha akamfanya mume ndie msimamizi wa mambo yoote katika nyumba,kasha akawaumba wanawake ili wawe pomziko na starehe kwa waume zao,anasema Allah Mtukufu: {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri }Ar-Rum 21. Sala na amani zimuendee Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juuyake mtume ambae alikuwa nimfano mwema kwa waume bora na alikuwa nimwalimu wa waalimu, na ziwe juu ya maswahaba zake na woote watakao mfuata kwa wema mpaka siku ya Qiyama. Mada hii inazungumzia sababu ya kuwa mume bora nimada muhimu sana hasa katika zama hizi za utanda wazi na zama za
fitna ambazo watu wameifanya halali kuwa haramu mabaya
kuwa nimazuri ,NK
Leo tunakuletea mambo haya ili uwe mume bora kwa familia
yako,sababu hizi niningi sana ila tuta kuelimisha haya mambo
kumi tulio kuchagulia.
1. Vaa vizuri kwa ajili ya mkeo, uonekane nadhifu na mwenye
kunukia vizuri. Kama ambavyo mume anapenda mke wake
aonekane maridadi kwa ajili yake, naye pia anapenda mume
wake avae vizuri kwa ajili yake. Kumbuka kwamba Mtukufu
Mtume (s.a.w) daima alikuwa akianza kupiga mswaki pindi
anaporudi nyumbani na daima alikuwa akipenda harufu nzuri.
2. Muite mkeo kwa majina mazuri. Mtukufu Mtume (s.a.w)
alikuwa akiwaita wakeze kwa majina mazuri ambayo hata wao
wenyewe walikuwa wakipenda kuyasikia. Muite mkeo kwa jina
zuri analolipenda zaidi kulisikia, na epuka kutumia majina
yatakayoumiza hisia zake.
3. Usiamiliane na mkeo kama nzi. Mara zote katika maisha yetu
ya kila siku huwa hatukumbuki kuwa kuna nzi mpaka pale
wanapotuudhi. Angalia, mkeo hukufanyia mambo mengi mema
kwa siku nzima ambayo huwa huyaangalii, ila pale
anapokufanyia kosa kidogo unamtazama. Usiishi naye kwa
namna hii; yatambue mambo mema yote anayokufanyia.
4. Ukiona kosa kutoka kwa mkeo, jaribu kutohamaki au
kumkaripia, muongoze kwa hekma na busara, atakuelewa! Hivi
ndivyo Mtukufu Mtume (s.a.w) alivyokuwa pale anapoona
jambo lisilokuwa muafaka kutoka kwa wakeze. Ni njia ambayo
ni wanaume wachache wa Kiislamu wameimudu.
5. Onyesha tabasamu kwa mkeo pindi unapomuona na daima
zidisha kumkumbatia. Kutabasamu ni sadaqah na mkeo naye
anastahili hiyo sadaka kwa namna ya kipekee. Fikiria maisha
yatakavyokuwa pale mkeo anapokuona unatabasamu kwa ajili
yake! Kumbuka pia zile hadith zinazosema kuwa Mtukufu
Mtume (s.a.w) alikuwa akimbusu mkewe kabla ya kwenda
kuswali, hata kama akiwa amefunga.
6. Mshukuru kwa kila analokufanyia. Kisha mshukuru tena na
tena! Angalia, mkeo anakuandalia chakula, anasafisha nyumba
na anafanya kazi nyingine nyingi mno. Wakati mwingine hata
kumpongeza hufanyi! Usiwe hivyo, mshukuru na useme:
“Ahsante mke wangu!”
7. Muombe akuandikie mambo kumi uliyomfanyia na
yakamfurahisha. Kisha mfanyie mambo hayo tena. Mara nyingi
huwa ni vigumu kujua mambo yanayomfurahisha mkeo. Huna
haja ya kubahatisha, muombe akwambie na kisha uyafanye hayo
na mengine pia katika kipindi chote cha maisha yenu.
8. Usiyapuuze na kuyabeza matakwa yake. Mfariji. Wakati
mwingine wanaume huyadharau maombi ya wake zao. Mtukufu
Mtume (s.a.w) hakuwa hivyo.
9. Uwe mwenye kunyumbulika na fanya michezo na mkeo.
Mtukufu Mtume (s.a.w) alikuwa akishindana na mkewe bibi
Aisha katika mchezo wa kukimbia. Mara ya mwisho
umemfanyia lini mkeo jambo kama hilo?
10.Daima kumbuka maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w): “Mbora
wenu ni yule anayeitendea mambo bora familia yake. Nami ni
mbora wenu kwa familia yangu.” Jaribu kuwa bora!
Usisahau kumuomba Mwenyezi Mungu aifanye ndoa yako
kuwa bora.
Mwisho:Ninaamini kuwa umefaidika vyakutosha na utayafanyia
kazi kwa idhini ya Allah.
Ninamuomba Allah azijaze nyumba na nyoyo zetu utulivu,
upendo na kuhurumiana sasa na hata milele!!!.