Nakala

1


بسم الله الرحمن الرحيم


WIVU KWA MKE MWENZA


Imeandikwa na Abdurahmani Muhina.


Imepitiwa na Yunus Kanuni Ngenda.


Itakapo tokea mumeo kaoa mke mwingine mkawa mko wawili au zaidi ya wawili nasaha zangu kwako ni hizi zifuatazo: Soma kwa makini ewe mwanamke nasaha hizi


1-Unatakiwa ulazimiane na wajibu wako yaani ufanye wajibu wako kwa mumeo na wala usimpe shetani njia, atapata nafasi ya kukushawishi ukaanza kupunguza kutekeleza haki za mumeo kwa wivu wako.


2-Ukifanya hivyo utaukamata moyo wa mumeo na utapendwa na mumeo hata kama mumeo kaoa mke zaidi ya mmoja, na nilazima ujue kwamba mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja ni ruhsa aliyopewa na ALLAH. 3-Elewa Dada yangu kwamba miongoni mwa mambo muhimu ambayo atayachuma mwanamke ambae yupo


2


katika ukewenza ni kumtendea wema mke mwenzie au


wake wenzie na kuwasamehe makosa yao wanayo mfanyia


kwani hakuna mkamilifu isipokuwa ALLAH.


Ili aonekane katika mtazamo wa mwanamke mwenye akili


na heshima asiyekuwa na mambo ya kimaudhi, mwenye


kushikamana na dini yake.


Mwanamke aliye faulu ni yule ambae anampa raha


mumewe vyovyote iwavyo na mwanamke aliye feli na


anaejiadhibu ni yule ambae anayajaza maisha ya mumewe


tabu, malawama, ugomvi na malalamiko, mwanamke huyu


atakosa dunia na akhera na hii ni hasara kubwa.


KUWA HIVI:


Mwanamke aliye swali sala ya alfajir kisha akakaa kwa


ajili ya kumuandalia mumewe kahawa au mlo wa asubuhi


wakati ameshatayarisha mavazi ya mumewe kwa utaratibu


mzuri, mwanamke aliye wapanga vizuri watoto wake na


kuwapatia kifungua kinywa kwa pamoja watoto wakatoka


kwenda zao shuleni hali ya kuwa na furaha tele, na


mumewe akaenda kazini akiwa na furaha, tabasamu,


uchangamfu na nguvu, Mashallah!.


Hayo ni miongoni mwa mambo yanayoleta raha, furaha,


utulivu na burudani katika ndoa.


3


USIWE HIVI:


Mwanamke aliye sali sala ya alfajir mwishoni mwa muda


(kwa kuchelewa) kisha akarudi tena chumbani kwake


kuendelea kulala ili akamilishe usingizi wake:


Mwanamke aliyechelewa kuamka na alipo amka akaanza


kumpiga bint yake kisa hakuchana nywele huku kachelewa


shule na mumewe amekwenda kazini amejaa mawazo ya


ugomvi ulio tokea usiku na kukosa raha kisha akaandaliwa


chai au kahawa na secretary huku akimuuliza vipi boss


mbona umefunga vibaya vifungo na unaonekana hupo


sawa! swali linakosa jibu la ukweli na mumewe anabakia


katika mtihani.


Hayo ni miongoni mwa mambo yanayopelekea maisha ya


ndoa kuwa ya tabu, dhiki, kero, ugomvi na hata kuvunjika


kwa ndoa.


NENO LA MWISHO:


Ewe mwanamke wa kiislam elewa kuwa ndoa ni ibada,


ndoa ni utulivu, ndoa ni raha, ndoa ni furaha, ndoa ni


faraja, ndoa ni amani na upendo. Pia ndani ya ndoa kuna


baraka na kheri nyingi kutoka kwa Allah.


4


Ni vema kuishi kwa kuzingatia hayo na huku ukijitahidi


kumcha Allah subhanahu wa ta'ala.


Tunamuomba Allah ajaalie kheri barka na utulivu katika


ndoa zetu, Ameen!!!!!



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI