1
بر الوالدين
ULAZIMA WA KUWATENDEA WEMA WAZAZI WA WILI NA TAHADHARI YA KUWAUDHI
IMEANDALIWA NA: YASSINI TWAHA HASSANI
IMEPITIWA NA: YUNUS KANUNI NGENDA
2
بسم الله الرحمن الرحيم
Utangulizi:
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake
Nyingi ambazo hazina Idadi na Rehma na Amani
zimuendee Mtume Muhammad, pamoja na Familia
yake na Maswahaba zake na Waislamu wote watakao
fuata Mwenendo wake mpaka siku ya Mwisho Mungu
atujaalie nasi tue Miongoni Mwahao AMIN.
Amesema mwenyezi mungu mtukufu. israi: 23-24
wazazi wawili, utawajuaje wazazi wawili? wazazi
wawili, ambao nisababu ya kupatikana kwako
duniani, wema wao juu yako, huduma zao kwako,
yaliompata mama wakati wa kujifungua kwa ajili
yako.
Sifa zote kamilifu anastahiki Mwenyezi Mungu
ambae alie nasifa ya kuumba na kukuleta duniani,
baada ya hapo ni wazazi wawili, kwa neema ya
kukuzaa na kukulea. Anasema mtaalamu wa kutafsiri
qour-ani Abdullah Bin Abbas radhi za Allah ziwe juu
yao: Aya tatu ndani ya qour-an zimekamatana na vitu
vitatu, hakikubaliwi kimoja bila ya kingine.
1-yeyote atakae mtii mwenyezi mungu na hakumtii
mtume hatokubaliwa. Taghabuni: 12.
2-yeyote atakae swali na hakutoa zakkah hato
kubaliwa (akiwa na uwezo wakutoa zakkah).
Baqara: 43.
3-yeyote atakae mshukuru allah na hakuwashukuru
wazazi wake wawili hato kubaliwa. Luqman: 14.
3
Kwa sababu hiyo jambo la kuwatendea wema
wazazi wa wili lime zungumzwa sana ndani ya qor-an
na mwenyezi mungu akatoa usia juu ya hilo na onyo
ikatolewa kwa wenye kuwaudhi na kuto waheshimu
wazazi kwa njia yoyote ile. Amesema mwenyezi
mungu mtukufu atika Surat Nisaai: 36.
Katika Surat Ankabuut: 8.
Na katika Surat Luqmani: 14.
Aya zote hizi zimeweka wazi ubora wa wazazi, na
walio pata kwa ajili yako, hasa mama, kwa yale yalio
mfika kwaajili yako, matatizo ya mimba, uchungu,
uchovu, kubwa zaidi wakati wa kujifumgua, mzazi
huwa karibu na kifo kuliko uhai, hakuna anaejua uzito
wa uchungu ila Yule alie wahi kujifungua miongoni
mwa wakina mama.
Na katika hadithi za mtume Muhammad rehma na
amani za Allah ziwe juu yake, zina himiza kuwatendea
wema wazazi wa wili kwa hili yoyote ile, na makemeo
makali sana yakuto waudhi.
Miongoni mwa hadithi hizo ime thibiti kutoka kwa
mtume Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu
yake yakwamba: (radhi za allah zina patikana katika
kuwatendea wema wazazi wa wili, na adhabu zake
zinapatikana katika kuwaudhi kwao, Kapokea hadithi
hii imam twabrani , na kaisahihisha Shekh Albany.
kapokea Imam Nasai na Ibnu Maaja na Abuudaudi,
kwa upokezi sahihi kutoka kwa Abdullah Bin Amru
Binul Aswi radhi za Allah ziwe juu yake, amesema:
kaja bwana mmoja kwa mtume Muhammad rehma
na amani za Allah ziwe juu yake, akasema: nimekuja
kukuunga mkono kwa kufanya hijra -kuhama, kutoka
4
makkah kuelekea madina- na nimewaacha wazazi
wangu haliyakua wan alia!, akasema mtume
Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake:
rejea kwao, uwachekeshe kama ulivyo waliza)
Kapokea Imam ahmad katika musnadi wake na Ibnu
Majah kutoka kwa Muawiya Bin Jaahimati assulamy
kwamba yeye alimtaka idh'ni mtume Muhammad
rehma na amani za Allah ziwe juu yake, akasema:
kwenda jihadi pamoja nae, akamuamrisha arejee na
amfanyie wema mama yake, jamaa alipo kazana,
mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake,
akasema: (olewako! Lazimiana na miguu yake
utaipata pepo).
Na katika sahihi Bukhari na Muslim kutoka kwa
Abahuraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
alikuja mtu kwa mtume Muhammad rehma na amani
za Allah ziwe juu yake, akasema: ewe mtume wa
Allah: nani mwenye haki zaidi kwangu miongoni mwa
wanaadamu? Akasema: mama yako, jamaa akasema:
kisha nani? Akasema: mama yako, jamaa akasema
tena kisha nani? Mtume akasema: mama yako, jamaa
akazidi kusema kisha nani? Mtume akasema:
baba yako.
Hadithi yaonyesha nafasi ya mama zaidi ya baba,
mama yatakiwa afanyiwe wema zaidi ya mara tatu
kuliko baba, kutokana na mambo alio yapata mama,
kuanzia uzito wa mimba, kujifungua, wengine mpaka
opareshen ndio mtoto anatoka, kunyonyesha, haya
nibaadhi ya mambo ambayo yanamuhusu mama
pekeyake, kisha baba anashirikiana na mama katika
malezi, na mwenyezi mungu ame ashiria hali hii ndani
ya qour-an Surat Luqman: 14.
5
Na imethibiti kutoka kwa Mtume Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake, amesema: wenye sifa aina tatu mwenyezi mungu hato watazama siku ya qiyama:
1- mwenye kuwa asi wazazi wake. 2- mwanamke mwenye kujiachia -hajistiri- mwenye kujifananisha na mwanamume. 3- mwanamume ambae anaona uovu unafanwa na familia yake akaridhika.
Akasema tena mtume rehma na amani za allah ziwe juu yake: wenye sifa aina tatu hawatoingia peponi:
1-mwenye kuwa asi wazazi wao. 2- na mwenye kudumu katika ulevi. 3- kumsengenya mtu ambae umempa kitu.
Kapokea hadithi hii imam nasaai na ahmad na hakim. mfano: umempa mtu kanzu au hijabu baadae waanza kusema kwa watu: unamuona yule jamaa mimi ndio nimempa ile kanzu, mimi ndio nimempa ile hijabu… kapokea imam ahmad kwa upokezi mzuri kutoka kwa muadhi bun jabal radhi za Allah ziwe juu yake amesema: aliniusia mtume Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake maneno kumi, akasema: usimshirikishe Allah na chochote hatakama ukiuliwa na kuchomwa moto, nawala usithubutu kuwaudhi wazazi wako hatakama wakikuamrisha kumtoa mke wako na mali zako.
kama inavyo julikana kuwatendea wema nimiongoni mwa tabia ya mtume Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake na tabia ya manabii walio tangulia kabla yake, kwa maneno na vitendo.
6
Kuhusu kuongozo wa mtume Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwa maneno tumekwisha tangulia kuyasema, ama katika vitendo vya Mtume Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake kuhusu kuwatendea wema wazazi, siku moja alipita kwenye kaburi la mama yake mzazi amina bintu wahabi alipo zikwa sehemu iitwayo abawai kati ya makkah na madina akiwa pamoja na maswahaba zake -1000- mwaka wa hudaibiya, akasimama akenda kulizuru kaburi la mzazi wake, akalia sana Mtume wetu Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na maswahaba alio kua nao wakalia, na akasema: nilimtaka idhni mwenyezi mungu ili nimuombee msamaha mama yangu hakunipa idhni hiyo! Na nikamtaka idhni ya kuzuru kaburi lake akaniruhusu, yazuruni makaburi kwa sababu yata kukumbusheni akhera.
Kapokea hadithi hii imam baghwiy katika sherhe sunna, na asili ya hadithi hii inapatikana katika sahihi Muslim. wazazi wa Mtume wetu Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake walifariki haliyakua sio waislamu.
Angalia kipenzi cha mwenyezi mungu nabii Ibrahim rehma na amani za Allah ziwe juu yake, baba wa Mitume, anaongea na baba yake mzazi kwa upole wa hali yajuu hata kama mzazi wake hakua muislamu ni kafiri!, akasema: (ee baba yangu) haliyakua akimlingania katika ibada ya kumuabudu mwenyezi mungu pekeyake na achane na shirki, baba alipo kanda juu na kupanik na kusema ukiendelea kunikumbusha mungu wako mmoja ntakupiga na kukufukuza hapa kwangu na kukutolea radhi! Nabii
7
Ibrahim akasema: (amani iwe juu yako nita kuombea msamaha kwa mola wangu.) maryam: 47.
Na mwenyezi mungu kamsifu nabii yahya bin zakariyya rehma na amani za allah ziwe juu yao, akasema mwenyezi mungu: (na alikua mwema kwa wazazi wake na wala hakua heuri wala mkosa adabu) maryam: 14.
Kuna maneno mengi ya manabii ambayo yamesajiliwa ndani ya kitabu cha Allah. hivyo hivyo ndivyo walivyo kua wema walio tangulia katika umati huu, walikua na pupa zaidi katika kuwatendea wema wazazi wao.
Miongoni mwao ni swahaba mtukufu abahuraira radhi za Allah ziwe huu yake, alikua akitaka kutoka nyumbani kwake anasimama mlangoni kwa mama yake akisema: amani ya Allah iwe juu yako ewe mama yangu na rehma zake na Baraka zake, mama anasema: nawewe amani ya Allah iwe juu yako na rehma zake na Baraka zake, anasema abahuraira: Allah akurehem kama ulivyo nilea nilipo kua mdogo, mama anasema: Allah nawe akurehem kama unavyo nifanyia wema katika hali ya utuuzima.
Abdullah bin mas'udi radhi za Allah ziwe juu yake, usiku mmoja mama yake mzazi alitaka maji, akenda kuleta maji, alipo rudi kamkuta mama kalala, akasimama na maji upande wa kichwa cha mzazi wake mpaka asubuhi, hakumuamsha kuhofia kumuudhi, na wala hakuondoka kuchelea, atapo amka akitafuta maji asiyakose.
Na huyu motto wa Hassan tamimy Allah amreheh siku moja alikua anakata kua nge, hakufaanikisha
8
mpaka nge kaingia kwenye tundu ndani ya nyumba yao, akaziba tundu kwa vidole vyake, nge akamgongaa, akaulizwa kwa nini umefanya hivyo, akasema: nimekhofia asije akatoka ndani ya shimo hili akamgonga mama yangu.
Ama mtoto wa auni al'muzany, siku moja aliitwa na mama yake, akamuitika kwa sauti ya juu ili amsikie, akajuta kwa hilo, akawaacha huru watumwa wa wili. wema walio tangulia walikua wakiwafanyia wazazi wao wema aina tofauti tofauti, hatuwezi kumaliza mifano yote, ila tumeeleza kwa ufupi tu.
Tukiangalia halizetu tutakuta upungufu mkubwa saana kuhusu kuwatendea wema wazazi wa wili, wakati mwengine wanaudhiwa kufokewa kutukanwa wengine wafikia kuwapiga wazazi wao.
Allah atulinde kutokana na hali kama hizo.
K uwaudhi wazazi wawili kuna aina tofauti tofauti, wengine wanakua hawajui, mfano: mtoto kujinyanyua mbele ya wazee wake na kuwafanyia kiburi kwa sababu tofauti tofauti, ikiwemo mtoto kua na pesa zaidi ya wazai, kua na elimu zaidi yao, au mtoto kua na cheo sehem fulani na mfano wamambo kama hayo.
Na miongoni mwa kuto watendea haki wazazi wawili nikuwatelekeza na kuto wahudumia kuwaacha wakawa omba omba.
Na miongni mwa kuto watendea haki wazazi nikuwatanguliza watu baki kabla yao, kama baadhi ya watu wanavyo fanya, kumtanguliza rafiki au mke au hata namsi yake, usimtangulize rafiki kabla ya mzazi au kumfadhilisha mke kuliko mzazi au hata kuitanguliza nafsi yako kabla ya mzazi haifai, lakini
9
wapo wapi wafanyao haya? Na miongoni mwa kuto watendea wema wazaziwawili ni kuwaita kwa majina yao ikiwa watahisi kuto waheshim, mfano wamwita mzazi wako: Juma, Said, Ally, au Mariam, Salma, Asha nk. wakati mwengine mtu anasahau haki ya wazazi juu yake anajifanya yupo bize na maisha, anasahau ya kwamba haki ya wazazi ni kubwa juu yake, yawezekana milango ya kheri na baraka ikafungwa kwake, kwa sababu ya wazazi.
Mama ambae kabeba mimba yako mwezi tisa kwa tabu ya hali yajuu, hakuna anacho pata zaidi ya batu na mashaka na uzito, baadae kajifungua kwatabu, kifo kipo mbele yake, mzazi anakubali ale kisu ili utoke salama, baada ya kujifungua anakuhudumia kwa kila kitu, huduma ambazo hata mke wako/ mume wako hawezi kufanya lakini mama yote kayafanya kwa furaha usiku na mchana bila kuchoka wala kuchukia, maziwa wake chakula chako, mapaja yake nyumba yako, mikono yake kipando chako, anakaa nanjaa ili ushibe, anakesha ili upate usingizi, mama kwako nimwenye huruma, mwenye mapenzi yasio namfano, unapo fikwa na matatizo hukosa raha.
Yote haya walio yafanya wazazi malipo yake kuto waheshimu, kuwadharau, kuwanyanyasa, na hata kufikia kuwapiga, Allah atunusuru nahali hiyo.
Ama Baba! anatoka kwenda kutafuta rizki kwaajili yako upata malezi bora, anapo rejea anakubeba, watu wana kuokopa kwa kujua ni mtoto wamzee fulani, haya namengineo anayo yafanya baba kwaajili yako malipo yake, kumnyanyasa, kuto muheshimu, kumdharau, kumsimanga, nakufikia kumpigaa, hasara hasara hasara kwa yule atakae wafanyia ubaya
11
wazazi haliyakua walimfanyia wema wakati akingaliki tumboni, hadi kujifungua, chaajabu kijana au binti ana wadharau wazazi, anasahau udhaifu wake na utoto wake.