1
بسم الله الرحمن الرحيم
KWANINI TUNAOGA JANABA?
لماذا نغتسل من الجنابة؟
HALIYAKUWA SIO NAJISI NA WALA HATUOGI KUTOKANA NA MKOJO NA HALI YAKUWA MKOJO NI NAJISI? WAWEZA KUULIZA BAADHI YA WATU KWANINI UISLAM UMEAMRISHA KUOGA JOSHO LA JANABA HALI YA KUENEZA MAJI MWILI MZIMA HALI YAKUWA KIUNGO NI HICHO HICHO KIMOJA KINAHUSIKA KUTOA HAJA NDOGO NA MANII? HEKMA KUBWA AMBAYO MOLA AMEONDOA JOSHO KATIKA HALI BAADA YA KUKOJOA NI KUTAKA KUWAONDOLEA WAUMINI UZITO KATIKA DINI' HAKUNA ATAKAE BISHA KUWA KWA MWANADAMU MWENYE AFYA HAKOSI KWENDA HAJA NDOGO MARA ZISIZOPUNGUA KUMI KWA SIKU, TENA HII NI KWA MAKADIRIO YA CHINI BALI ANAWEZA KWENDA ZAIDI YA HAPO.
2
LAITI SHERIA INGEWEKA JOSHO KWA HAJA NDOGO
INGEKUWA NI UZITO KATIKA DINI KWANI
INGEMLAZIMU KILA ANAEKOJOA HAJA NDOGO BASI
AOGE JOSHO HALI AMBAYO HAJA NDOGO INAWEZA
KUKUSHIKA MAHLA POPOTE WAKATI WOWOTE.
LAKINI JANABA UKIMCHUKULIA MWANANDOA HATA
AFANYE TENDO LA NDOA MARA ATAKAZO WEZA
BASI LINAMTOSHA JOSHO MOJA TU KISHERIA KWANI
HAIJAFUNGAMANISHWA KUWA KILA TENDO LIWE
NA JOSHO LAKE.
UKIMTAZAMA MTU ASIEKUWA KATIKA NDOA KWA
YULE ALIYE BALEGHE JANABA LAKE ANAWEZA
KULIPATA KWA NDOTO KISHERIA HALI AMBAYO SIO
KILA SIKU ATAKUWA ANAOTA,
HIVYO WAWILI HAWA WALIOLAZIMISHWA KUOGA
JANABA UTAONA SIO MZIGO WALA UZITO
KWAKUWA SIO KITU KINACHOJIRUDIA RUDIA MARA
NYINGI KAMA MKOJO HIVYO NDIVYO SHERIA
IKAWEKA KUOGA KWA MWENYE JANABA NA
IKAWEKA KUTAWADHA KWA MWENYE KUKOJOA
KWAKUWA KUOGA JANABA NI MWILI MZIMA HIVYO
KUNAHITAJI TAKLIF KIDOGO HALI YA KUTAWADHA
NI SEHEMU YA VIUONGO HIVYO KUTAWADHA NI
WEPESI KULIKO KUOGA KWAKULE KUJIRUDIA RUDIA
MARA NYINGI KULIKO YANAYOPELEKEA JANABA
KAMA ALIVYOSEMA MOLA KATIKA QURANI:
وما يريد الله ليجعل عليكم من حرج ولكن يريد ليطهركم وليتم نعمته عليكم تشكرون
لعلكم
3
MAANA YA AYA HII:NA HAJAWA MWENYEZI MUNGU
NI MWENYE KUTIA UZITO KWENU NYINYI LAKINI
ANATAKA AKUTWAHARISHENI NA ATIMIZE NEEMA
YAKE KWENU ILI MPATE KUSHUKURU.
ما قاله الإمام ابن القيم ردًا على من عجب من التفرقة بين المني والبول فأوجب
: الغسل من المني دون البول قال
NA YAMENIFURAHISHA SANA MAJIBU YA IBN AL
KAYIM ALJAWZIY ALIPO MJIBU MWENYE
KUSHANGAA TOFAUTI YA JOSHO LA MANII NA
MKOJO IKAWA NI WAJIBU KUOGA JOSHO KUTOKANA
NA MANII HALI YA KUTOKUOGA KUTOKANA NA
MKOJO .
AKASEMA:
هذا من أعظم محاسن الشريعة وما اشتملت عليه من الرحمة والحكمة والمصلحة، "
فإن المني يخرج من جميع البدن . ولهذا أسماه الله " سلالة " لأنه يسل من جميع
.البدن فتأثر البدن بخروجه أعظم من تأثره بخروج البول
NA HAYA NDIO YANAYOONYESHA UZURI WASHARIA
YETU YA UISLAM NA YALIYOKUWEMO NDANI YAKE
MIONGONI MWA HEKMA NA HURUMA PAMOJA NA
MASLAHI,
KWANI HAKIKA YA MANII YANATOKA MWILI MZIMA
NA NDIO MAANA ALLAH AKAYAITA "SULAALA"
KWAKUWA YANA CHOMOZA KATIKA MWILI MZIMA
HALI AMBAYO YANAUWATHIRI MWILI ZAIDI PALE
YANAPOTOKA KULIKO UNAVYO ATHIRI MKOJO
WAKATI UKUTOKA .
4
.وأيضًا فإن الاغتسال من خروج المني من أنفع شيء للبدن والقلب والروح
NA VILE VILE JOSHO LA JANABA NI LENYE
KUUNUFAISHA ZAIDI MWILI, MOYO NA ROHO
KUTOKANA NA ATHARI YA KUTOKA MANII.
فإنها تقوى بالاغتسال،
.والغسل يخلف على البدن ما تحلل منه بخروج المني وهذا أمر يعرف بالحس
KWA HAKIKA MWILI UNAPATA NGUVU KUTOKANA
NA JOSHO
NA JOSHO LINAFUATIA MWILI NA KURUDISHA YALE
YALIO ONDOKA MIONGONI MWA NGUVU KWA
KUTOKA KWA MANII.
NA JAMBO HILI LINAJULIKANA KWA KUHISI TU
BAADA YA KUOGA JANABA NA KABLA PUNDE TU
BAADA YA KUTOKA KWAKUWA KUTOKA KWA MANII
KUNAUTIA MWILI UCHOVU NA UVIVU AMBAPO
KUOGA KUNATIA NISHATI NA UCHANGAMFU,
HALI MKOJO UNAPOTOKA HAULETI UCHOVU WALA
UVIVU HIVYO HAPAHITAJIKI JOSHO KAMA LA
MWENYE JANABA.
اللهم اجعلنا من التوابين ، واجعلنا من المتطهرين
EWE MOLA TUJAALIE NI WENYE KUTUBIA NA
UTUJAALIE KATIKA WATWAHARIFU (WASAFI)
AMEEN!
Imekusanywa na Abubakar shabani Imepitiwa na Yunus kanuni