1
KUWA NA TAWHID YA KWELI NI SABABU YA KUPATA MWISHO MWEMA
Imeandaliwa na: Yunus Kanuni Ngenda
Imepitiwa na: Abubakari Shabani Rukonkwa
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote, na rehma na amani zimwendee kiongozi wa umma huu Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na watu wake na Maswahaba zake wote,! Amma baad.
Muislamu anapokuwa na msimamo katika tawhid, na imani, na ucha Mungu, hubashiriwa Pepo wakati anapofikwa na mauti. Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:
Hakika wale waliosema: “Rabbuna (Mola) wetu ni Allaah.” Kisha wakanyooka (wakawa na msimamo); Malaika huwateremkia
2
(wakati wa kutolewa roho kuwaambia) kwamba: “Msikhofu, na
wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo
mlikuwa mkiahidiwa (kwayo). “Sisi ni marafiki walinzi wenu
katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale
yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale
mnatayoyaomba. “Ni mapokezi kutoka kwa Ghafuwrir-Rahiym
(Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu).” [Fusw-Swilat: 30-
32].
Na amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:
Hakika walio sema: “Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu;
kisha wakatengenea (wakawa na msimamo), hawatakuwa na
khofu, wala hawatahuzunika. Hao ndio watu wa Peponi,
watadumu humo, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa
wakiyatenda.” [Surat Ahqaaf: 13-14]
Ukitafakari kwa umakini Aya hizo tukufu, utatambua ya
kwamba mtu kusema “RABBUNA LLAH” pekee! haitoshi kwake
yeye kupata bishara njema, isipokuwa lazima neno hilo
liambatane na:
1.Tauhid ya dhati.
2.Imani ya kweli.
3
3-Msimamo ulio madhubuti.
5.Na matendo yaliyo mema.
Ndiyo maana Mwenyezi Mungu mtukufu mwisho wa Aya
anasema:
“Hao ndio watu wa Peponi, watadumu humo, kuwa ni malipo
kwa waliyo kuwa wakiyatenda.” [Surat Ahqaaf: 13-14]
Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atujaalie tuwe na
tauhid ya kweli katika nyoyo zetu, na atufishe hali ya kuwa ni
waislam wenye imani thabiti, na atuwezeshe kwa rehma zake
tuweze kutenda matendo yaliyo mema ili tupate mwisho
mwema, na atufufue Mola wetu pamoja na Mtume wetu
Muhammad (s.a.w) siku ya Kiyama, Ameen!