1
بسم الله الرحمن الرحيم
KINGA YA KILA SIKU DHIDI YA SHETANI, UCHAWI, HUSDA NA KILA UBAYA. Imeandaliwa na :Yunus Kanuni Ngenda. Imepitiwa na :Abubakari Shabani Rukonkwa. Uislam ni dini iliyokamilika katika kila idara miongoni mwa mambo ambayo pia yanapatikana ndani ya uislam ni kinga ya kisheria dhidi ya kila shari kama vile shetani,uchawi, husda, kijicho n.k. Kinga hii ndiyo mujarrab na hupaswi kujikinga kwa hirizi wala chale kama wafanyiwavyo wengi miongoni mwa jamii ya wanaadamu na la kusikitisha zaidi katika kundi la wanaoamini na kufanya ushirikina huu ni waislam! Ndugu zangu shirki ni jambo baya sana na ni miongoni mwa dhambi kubwa ambayo ALLAH amemuambia mtume wake kuwa وَلَقَدۡ أُوحِىَ إِلَيۡكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكَ لَ ٮِنۡ أَشۡرَكۡتَ لَيَحۡبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ
Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a'mali zako zitaanguka, na lazima utakuwa
2
miongoni mwa wenye kukhasiri
Surat Zumar: 65
Huyo ni mtume wa allaah vipi mimi na wewe?
Kwa kuzingatia hilo nimeona ni kheri leo nikawaletea
taratibu sahihi za kujikinga ambazo unatakiwa udumu nazo
kila siku asubuhi na jioni.
Ni matarajio yangu kwamba tutaendelea kuwa pamoja ili
tuweze kufaidika na elimu hii ya bure kabisa kwa ajili ya
kutafuta radhi za ALLAH.
Laa Ilaaha Illa llaahu wahdahuu laa shariika lahu
lahulmulku walahul hamdu wahuwa alaa kulli shai-in
qadiir
mara 100 asubuhi na jioni
Allaahu laa ilaaha illaa huwalhayyul qayyuum laa taakhudhuhuu
sinatun walaa nauum lahuu maa fis
samaawaati wamaafil-ardhwi yashfa'u 'in-dahuu illaa biidhnihii
ya'alamu maa baina aidiihim wamaa khalfahum
walaa yhiitwuuna bishai-in min 'ilmihii illaa bimaa shaa-a
wasi'a kursiyyuhus samaawaati wal-ardhwa walaa yauuduhuu
hifdhuhumaa wahuwal'aliyyul'adhwiim.
mara 1 kila baada ya swala ya fardhi.
3
Qul huwa llaahu ahadu.1) Allaahus Swamadu. 2) Lam yalid
wa lam yuulad. 3) Wa lam yakunlahuu kufuwan ahad. 4)
Mara 3 kila baada ya swala ya fardhi.
Qul a'uudhu birabbil falaq. 1) Minsharri maa khalaq. 2) Wa
minsharri ghaasiqin idhaa waqaba. 3) Wa minsharrin n
affaathaati fil'uqad. 4) Wa minsharri haasidin idhaa
hasada.5)
Qul-a'uudhu birabbin naas.1) Malikin naas. 2) ILaahin
naas.3) Minsharril was-waasil khannaas. 4) Alladhii
yuwas’wisu fii swuduurin naas. 5) Minaljinnati wan naas.6)
Sura hizo tatu za unatakiwa kuzisoma kila baada ya swala
ya fardhi mara 3, na wakati wa kulala.
Isipokua wakati wa kulala ukishazisoma hizo sura mara 3
unapulizia kwenye viganja vyako vya mikono kisha
unajifuta mwili mzima.
4
A'uudhu bikalimaati LLaahi taammaati minsharri maa
khalaqa. mara 3 baada ya Maghribi
Bismi llaahi lladhiy laa yadhurru ma'asmihi shay-un filardhwi
walaa fis samaa-i wahuwas samii'ul-'aliim. mara 3
asubuhi na jioni.
Hizo ni baadhi ya nyiradi za Asubuhi, Mchana, Jioni na
Usiku ambazo kwa nwenye kudum nazo basi mtu huyo
atakua na kinga ya Allah! Kutokana na mambo
tuliyozungumza hapo juu.
Tunamuomba Allah atulinde na kila shari, na atujaalie
mwisho mwema. Ameen!!