Nakala

1


بسم الله الرحمن الرحيم


IJUWE ITIKADI YA AHLU SUNNAH WALJAMAA Imeandikwa na Muhammad Faraj Salim As-Sa’y imepitiwa na Abubakari Shabani Rukonkwa Iikadi ya Ahlu Sunnah ni sahili na nyepesi, haina tabu kufahamika wala haina mikanganyo. Haina tabu kuisherehesha. Bali inafahamika na mtu wa kawaida kama inavyofahamika na mtaalamu. Mtu yeyote anaweza kuifahamu kwa wepesi kabisa. Vitabu vyao vya Hadiyth kama vile Al-Bukhaariy na Muslim na vingine, pamoja na mafundisho ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) yaliyonukuliwa ndani ya vitabu hivyo na kuenezwa kila mahali ulimwenguni kwa njia ya isnadi yenye kufuata mfumo na elimu ya hali ya juu, vitabu hivyo vinakubaliwa na sehemu kubwa sana ya umma huu na vinatumiwa katika kuitimiza na kuisherehesha sheria ya Allaah. Maulamaa wake kama vile Imam Abu Haniyfah na Imam Maalik na Imam Shafi na Imam Ahmad bin Hanbal na Ibnul Mubaarak na Ibnu Taymiyah na wenzao wengi wengine wanapendwa na kufuatwa na asilimia zaidi ya 95 ya Waislamu ulimwenguni, kutokana na elimu yao kubwa na masharti yao mepesi. Walikuwa daima wakisema: “Ukikuta katika mafundisho yetu yanayokubaliana na Qur-aan au Sunnah sahihi, basi yafuateni. Na kama hayakubaliani na hayo basi yapigeni na ukuta.” Watu wamedurusu sira zao na mwenendo wao na elimu yao heshima yao, wakawakubali kama ni Maimamu wao walioisherehesha Qur-aan tukufu na mafundisho ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwa njia ya kitaalamu na kwa uhodari mkubwa.


2


Viongozi wao walipambana na maadui wa Waislamu, wakaweza


kuzifungua nchi nyingi sana na nyoyo nyingi. Walitayarisha


majeshi na wapiganaji walioweza kuziteka nchi kubwa kubwa


kuanzia Uturuki, sehemu kubwa ya Uchina na Urusi. Afghanistan


na Afrika na Asia na sehemu kubwa ya Ulaya, na kwa njia hiyo


mamilioni kwa mamilioni ya watu waliingia katika dini hii tukufu.


Walifanikiwa kote huko kuwatoa watu katika giza la kumkufuru


Allaah na kuwaingiza katika nuru ya Uislamu, kuwatoa katika


jeuri ya watawala wao, na kuwaingiza katika uadilifu wa Uislamu,


kuwatoa katika kuipenda dunia, na kuwaingiza katika kuipenda


akhera yao, na juu ya kuwa wao ndio walioziteka nchi hizo, lakini


wananchi wake wanaendelea mpaka leo kuwapa watoto wao


majina ya wafunguzi wale wa Kiislamu.


Utamkuta mtoto wa Kirusi au wa Kituruki au wa Ki Africa au


Asia au Ulaya au hata Marekani akipewa jina la Abu Bakr au


‘Umar au ‘Aliy au ‘Uthmaan au Mu’aawiyah au Khaalid (Khaalid


bin Waliyd) au Haarun au Salaahud-Diyn, n.k.


Kutokana na mafundisho ya Maulamaa wao yaliyo mepesi


yanayokubalika na akili ya mwanadamu yeyote wa kawaida,


madhehebu haya yalipendwa na kufuatwa na asilimia kubwa sana


ya Waislamu duniani.


Kuthibitisha Sifa Za Allaah:


Kwa mfano katika kuzithibitisha sifa za Allaah, Ahlus Sunnah


wanakubali na kukithibitisha kila Alichokubali na Kukithibitisha


Allaah bila ya kuchelewesha wala kubadilisha.


Allaah Anaposema kuwa Anao Uwezo, na sisi tunaamini kuwa


Anao Uwezo. Anaposema kuwa Anaona, na sisi tunaamini kuwa


Anaona Subhaanahu wa Ta’ala.


Anaposema kuwa Anasikia, na sisi tunaamini kuwa Anasikia.


Na anaposema kuwa Anayo macho, na sisi tunaamini kuwa Anayo


Macho, Subhanahu wa Taala, na Anaposema kuwa Anayo Mikono


na sisi tunaamini kuwa Anayo Mikono, na Anaposema kuwa Anao


Wajihi, na sisi tunaamini kuwa Anao Wajihi Subhaanahu wa


Ta’ala. Lakini macho Yake na mikono Yake na Wajihi wake na


3


Kuona Kwake na kusikia Kwake hauna mfano wowote na kitu


chochote.


Maulamaa wetu wametufundisha kuzikubali sifa zote za Allaah


bila ya kukisia kwa akili zetu namna yake au mfano wake. Kwa


sababu kuzikataa sifa ambazo Mwenyewe Amejipa Subhaanahu


wa Ta’ala, ni makosa, na kuzifananisha sifa hizo pia ni makosa.





“Hapana kitu kama mfano Wake. Naye ni Mwenye kusikia


Mwenye kuona” Ash-Shuuraa: 10


Maulamaa wetu wametufundisha kuzikubali sifa zote za Allaah


bila ya kukisia kwa akili zetu namna yake au mfano wake. Kwa


sababu kuzikataa sifa ambazo Mwenyewe Amejipa Subhaanahu


wa Ta’ala, ni makosa, na kuzifananisha sifa hizo pia ni makosa.


“Hapana kitu kama mfano Wake. Naye ni Mwenye kusikia


Mwenye kuona”


Allaah Anaposema:





“Mkono wa Allaah Uko juu ya mikono yao” Al-Fat-h: 10


Sisi tunaamini kuwa Allaah Anao Mkono. Kwa sababu Yeye


Mwenyewe Subhaanahu wa Ta’ala Amesema hivyo. Lakini


hatuufananishi Mkono Wake na vijikono vyetu.


Tutoe tu ushahidi katika vitabu wa wapinzani, anasema


mwanachuoni wa Kishia As-Sayed Muhammad Al-Husayniy Ash-


Shiraziy katika tafsiri yake inayoitwa; Taqriyb al Qur’an fil


Adh’haan katika kuifasiri Aayah hii: “Mkono wa Allaah Uko juu


ya mikono yao.” “Aya hii inazungumza juu ya Maswahaba


(Radhiya Allaahu ‘anhum) waliofungamana na Mtume wa Allaah


(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) (chini ya mti), na katika


kufungamana, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa


sallam) alikuwa akiutandaza mkono wake huku matumbo ya


4


vidole yakielekea juu, na wanapokuja wenye kufungamana naye


walikuwa wakiweka mikono yao juu ya mkono wa Mtume wa


Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).”


Aayah hii iliteremshwa baada ya Maswahaba kufungamana na


Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) walipokuja


chini ya ule mti na kuiweka mikono yao juu ya mkono wa Mtume


wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ndipo Allaah


Aliposema;


“Mkono wa Allaah Uko juu ya mikono yao” Al-Fat-h: 10


Maulamaa wanasema: ‘Mguu wa meza hauwezi kufanana na


mguu wa Seremala aliyeichonga meza hiyo na kutengeneza miguu


yake, kama vile mkono wa fundi aliyetengeneza simu hauwezi


kuwa sawa na mkono wa simu. Siku zote sifa za mtengenezaji


haziwezi kufanana na sifa za bidhaa yake.


Na Allaah Ndiye Mwenye mifano mikubwa. Kwa hivyo


Anaposema Subhaanahu wa Ta'ala kuwa Anao Mkono, na sisi


tunakubali kuwa Anao Mkono lakini hatuufananishi na mkono


wetu, kwa sababu sifa za Muumba haziwezi kufanana na sifa za


viumbe


Na katika Aayah nyingine Allaah Anamuuliza Ibilisi:





Ewe Iblisi! Kipi kilichokuzuia kumtii yule niliyemuumba kwa


mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika


wakuu kweli? Swaad: 75


Sisi tunaamini kuwa; kwa vile Allaah Amesema kuwa


Amemuumba Aadam kwa mikono yake basi haiwezekani kuwa


Amekusudia kuwa Amemuumba kwa njia nyingine.


Ndani ya Qur-aan tukufu Allaah Anazungumza na watu wa kila


aina, wenye elimu na wasiokuwa na elimu. Na kusudi Lake


Subhaanahu wa Ta’ala ni kuwafundisha watu hao waijuwe dini


yao, juu ya hitilafu ya ufahamu wao. Kwa hivyo haiwezekani


Azungumze nao kwa njia ya mafumbo au majazi akawa Anasema


neno huku Akikusudia jambo au neno lingiine.


5


Allaah Angelitaka kusema kuwa Amemuumba mwanaadamu kwa Kudra Yake, kwa mfano; basi Angelisema tu, pasingekuwa na haja ya kuutaja mkono. Na katika Aayah nyingine pia Allaah Anasema: أوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا خَلَقْنَا لَهُمْ مِمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَا أَنْعَامًا فَهُمْ لَهَا مَالِكُونَ


“Je! Hawaoni kwamba Tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono Yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki.” Yaasin: 71 Na hivi ndivyo ilivyo katika sifa Zake zote Allaah Subhaanahu wa Ta’ala, kila Anapozitaja, ni juu yetu kusema: ‘Samiina wa twaana, tuzikubali bila kubabaisha maana yake wala kubadilisha wala kufananisha sifa hizo na sifa za viumbe. Kwa mfano Allaah Anaposema:


“Hakika amri Yake Anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.” Yaasin: 71 Tunapoisikia kauli hiyo ya Allaah Subhaanahu wa Ta’ala, hatuna budi kuikubali na kuiamini. Kwa nini? Kwa sababu Allaah Mwenyewe Amesema hivyo. Ikiwa Allaah Subhaanahu wa Ta’ala Hasemi, kwa nini basi alisema kuwa; hukiambia tu: Kuwa! Na kikawa? Na katika Aayah nyingine Allaah Anasema: 


“Na Allaah Alinena na Muusa kwa maneno.” An-Nisaa: 164


6


Bali hata Qur-aan Tukufu ni maneno ya Allaah Subhaanahu wa Ta’ala. Allaah Anasema: وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّى يَسْمَعَ كَلاَمَ ه اللَِّ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ذَلِكَ





“Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Allaah. Kisha mfikishe pahala pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua kitu.” At Tawbah: 6


Wengine wanasema kuwa Allaah hakusudii hivyo, bali hayo ni majazi tu. Na maana yake ni kuwa Anaposema kuwa Anasikia, hakusudii kuwa Anasikia kweli bali hayo ni majazi tu, na Anaposema kuwa Anaona hakusudii kuwa Anaona kweli bali hayo ni majazi tu, na Anaposema kuwa Anayo macho, hakusudii kuwa Anayo macho, bali hayo ni majazi tu, na Anaposema kuwa Anayo mikono hakusudii kuwa Anayo mikono bali hayo ni majazi tu, na anaposema kuwa Anao wajihi hakusudii kuwa Anao wajihi kikweli bali hayo ni majazi tu… Subhaana-Allaah!!! Sisi tunasema; Majazi yapo, lakini majazi ni kwa mfano mtu shujaa akaitwa Simba, au mtu muovu akaitwa nyoka nk. Haya ni majazi. Lakini maneno ya Allaah Aliyotuletea waja wake kwa ajili ya kutufundisha dini yetu na kutujulisha sifa Zake Subhanahu wa Ta'ala , hayawezi kuingia katika mfumo huu. Ni maneno ya Kiarabu yasiyokwenda upande. Lugha ya Kiarabu safi kabisa. Allaah Anasema: قُرآنًا عَرَبِيهًا غَيْرَ ذِي عِوَجٍ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ


“Qur-aan ya Kiarabu isiyo na upogo (isiyokwenda upande), ili wamche Allaah” Az-Zumar: 28 Allah ndio mjuzi zaidi.


Kwa haya machache tumuombe Allah atupe imani madhubuti, Atufishe katika Aqiyda ya Ahlu sunna waljmaa, Amiin!!


7



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI