Nakala




FUNGA YA RAMADHANI.


Swahili.





Utangulizi


Kwajina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma mwenye kurehemu, tunamshukuru sana Allah kwa neema zake nyingi sana juu yetu, na tukijaribu kuzihesabu neema zake kwetu hatuwezi kuzimaliza,


Mwenyezi Mungu amabae ni Mmoja katika Uungu wake Mfalme wa siku ya qiyama hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hafananishwi na chochote katika viumbe vyake, Rehma na Amani za Allah zimuende Nabii Muhammad (s.a.w), pamoja na familia yake na Maswahaba zake na Waislamu wote watakaofuata mwenendo wake mpaka siku ya qiyama, amma baad.


MAANA YA SWAUMU


Kuna maana mbili za neno Swaum.


.1KILUGHA


.2KISHERIA


Katika lugha ya kiarabu neno "Swaumu" lina maana ya - :


Kujizuilia kufanya jambo lolote la kawaida mtu


alilozoea kulifanya.


Qur-ani inatufahamisha kuwa Bi Mariyam baada ya kumzaa Nabii Issa (Alayh Salaam) alijizuilia kusema na Mtu yeyote juu ya Mtoto


فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ الْبَشَرِ أَحَدًا فَقُولِي إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَنِ صَوْمًا فَلَن


أُكَلِّمَ الْيَوْمَ إِنْسِيًّا


Na kama ukimuona mtu yeyote (akauliza habari za


mtoto huyu) Sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa


mwingi wa rehma ya swaumu(kufunga) kwa hiyo leo sitosema na mtu" (19:26)


.2KISHERIA


Katika sheria ya Kiislam neno Swaum lina maana ya -:


Kujizuia kwa nia ya kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kuacha kula kunywa,kufanya tendo la ndoa,na maaswia mengine kuanzia kuchomoza kwa Alfajri mpaka kuzama kwa jua.


Swaum kwa Muislam wa kweli ni zaid ya kujizuilia na hayo tuliyoyataja hapo juu.


Kwa Muislam wa kweli Kufunga/swaum ni pamoja


kujizuilia kutenda maovu yote yaliyokatazwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Ili Swawm ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu- pamoja na fikra na hisia zake na matendo aliyokataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala.)


Kwa kufanya hayo ndipo mfungaji ataweza kulifikia lengo la Swaum ambalo ni ili kuweza kupata cheo cha Uchamungu. Kama Allah anavyosema katika Qur'an kuwa -:


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ


مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ


"Enyi mlio amini mmefaradhishiwa kufunga kama


walivyo faradhishiwa waliokua kabla yenu ili mpate


kumcha Allah" (2:183)


Na kinyume na hapo mtu atajizuia na kula na kunywa na hata kufanya jimai wakati wa Swaum lakini bado


Swaum kisheria na dalili ya hili tunaipata katika Hadith hii. Abu Hurayrah amesimulia kuwa Mtume wa Allaah


amesema: “Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allaah hana haja na kuona kuwa anaacha chakula chake na kinywaji


chake (yaani Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hana haja na funga yake.” (Al-Bukhaariy.)


HISTORIA YA FUNGA YA RAMADHANI


Kwa mujibu wa Qur-ani tukufu tunaona kuwa kufunga si jambo lililoanzishwa na Mtume Muhammad(Swalah Llahu Alahy Wasalaam) bali


ni ibada iliyotekelezwa na Nyumati za Mitume wa Allah walio pita kabla ya Mtume wetu Muhammad. Allah anasema : -


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ


مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ


"Enyi mlio amini mmefaradhishiwa kufunga kama


walivyo faradhishiwa waliokua kabla yenu ili mpate


kumcha Allah" (2:183(


Na tukio hili la kufardhishwa funga katika Umma huu lilikuwa katika mwaka wa pili mwezi wa Sha‘abaan siku ya Jumatatu baada ya Hijra. Ila kama tulivyoona hapo mwanzo kuwa Funga/Swaum haikuanza ktk Ummah wa Mtume wetu Muhammad(Swallah Llahu Alayh Wassalam) bali hata kwa Mitume wengine waliopita kabla yake walikuwa wanafunga. Hebu tutizame ni vipi waliokuwa kabla walikuwa wanafunga.


Watu wa Nabii Ibrahiym(Alayh Salam) Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) aliinuliwa katika jamii ya washirikina.


Walikuwa wakiabudu jua, mwezi, nyota na masanamu chungu nzima waliyoyachonga


wenyewe .


Pamoja na ushirikina wao huo walikuwa


wakifunga siku 30 mfululizo katika kila mwaka kwa


heshima ya mwezi. Mayahudi (Judaism) Dini ya Kiyahudi ni dini waliyoibuni Mayahudi baada ya


Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) ambapo walimfanya


Uzairi mwana wa Mungu. Pamoja na hivyo Waumini wa Kiyahudi walikuwa wakifunga Alhamisi na Jumatatu kama kumbukumbu ya kwenda na kurudi


kwa Nabii Mussa (‘Alayhis Salaam) katika safari yake ya Sinai kwenda kuchukua Taurati. Kutokana na kumbukumbu ya historia, Nabii Musa alikwenda kwenye mlima Sinai siku ya Alhamisi na kurejea


siku ya Jumatatu baada ya siku arobaini kupita.


Pia Mayahudi hufunga kwa saa 24 katika kila mwezi 10 Muharamu, kwa kumbukumbu ya siku ambayo Wanaisraili (Mayahudi) walipookolewa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kutokana na udhwalimu wa Firauni. Siku hii ambayo hata Waislamu wamesuniwa kufunga huitwa siku ya ‘Ashuuraa.


Ukiacha siku ya ‘Ashuuraa ambapo funga huchukua saa 24, funga za Mayahudi huanza alfajiri na huishia pale inapojitokeza nyota ya kwanza usiku.


Wakristo Hawa wanajnasibisha na Nabii Isaa (Alayhis Salaam. Katika dini hii Nabii ‘Iysaa (‘Alayhis Salaam) amefanywa mwana wa Allaah


(Subhaanahu wa Ta’ala) na kwamba yeye ndiye


mkombozi wa Wakristo. Pamoja na hivyo, Wakristo wanakiri kuwa kufunga ni Ibada kubwa miongoni mwa Ibada zao. Wakristo wa mwanzo walikuwa wakifunga siku 40 mfululizo kasoro siku za Jumapili kama kumbukumbu ya siku zile


alizofunga Yesu (Nabii ‘Iysaa ‘Alayhis Salaam) kama inavyobainishwa katika kitabu chao(Biblia(


UBORA WA SWAUMU NA FADHILA ZAKE


Linalo julisha ubora na fadhila za Funga ni maneno ya Mtume (Swallah Llahu Alayh Wassalam) haya yafuatayo : -


"الصوم جنة من النار كجنة أحدكم من القتال "


. ) 1 ( Kufunga ni kinga ya Moto kama vile kinga ya mmoja wenu katika vita".(Ahmad, Nasaiy)


من صام يوما في سبيل الله باعد الله بذلك اليوم حر جهنم


عن وجهه سبعين خريفا


. ) 2 ( Atakae funga siku moja katika njia ya Allah, Allah atamwepusha kwa utukufu wa siku hiyo uso wake na joto la moto wa Jahannam umbali wa miaka sabiin" (Ahmad, Nasaiy,Ibn Majah,Tirmidhi(


أن في الجنة باب يقال له الريان يقال يوم القيامة أين


الصائمون هل لكم إلى الريان من دخله لم يظمأ أبدا فإذا


دخلوا أغلق عليهم فلم يدخل فيه أحد غيرهم


" 3Hakika peponi kuna mlango unaitwa Rayyan,


pata semwa siku ya Qiyama; wako wapi waliokuwa


wakifunga waingie katika mlango huu? Watakapo ingia hawatohisi kiu tena na utafungwa mlango wake hatoingia humo ila aliyedumu na ibada ya Funga" (Bukhari,Muslimu,Nasaiy) Na hadithi nyinginezo. Na mlango huu umepewa jina hilo kunasibiana na sifa ya Swawm ambayo inampa


mtu kiu kutokana na athari ya kufunga. Mara


nyingi mtu anapofunga hatamani chakula kama


anavyotamani maji.


FADHILA ZA MWEZI WA RAMADHANI


Ameeleza Mtume (Swallah Llahu Alayh Wasalam) ubora/fadhila za mwezi wa ramadhani


katika hadithi zifuatazo : -


الصلوات الخمس والجمعة إلى الجمعة ، ورمضان إلى رمضان


مكفرات لما بينهن ، إن اجتنبت الكبائر ( ] رواه مسلم


- " 1 swala tano, swala ya Ijumaa hadi Ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani (yote hayo) ni yenye kufuta dhambi zilizo baina yake, maadamu madhambi makubwa yataepukwa." (Muslimu)


من صام رمضان إيماناً واحتساباً غفر له ما تقدّم من ذنبه(( ))


] متفق عليه "


- " 2 Atakaefunga Ramadhani hali ya kuamini na kutaraji thawabu atasamehewa dhambi zake zilizo


tangulia" (Bukhari na Muslimu)


إذا كان أول ليلة من رمضان صفدت الشياطين ومردة الجان ،


وغلقت أبواب النار فلم يفتح منها باب ، وفتحت أبواب الجنة


فلم يغلق منها باب ، ونادى منادٍ : يا باغي الخير أقبل ، ويا


باغي الشرّ أقصر ، ولله عتقاء من النار ،


وذلك كل ليلة (


- " 3Inapokuwa usiku wa kwanza wa Mwezi wa


ramadhani Masheitwani hufungwa na Majini wakorofi,nao hufungwa pia Milango yote ya moto,na hufunguliwa milango yote ya pepo.Hutangaza mtangazaji (malaika) kwa kusema: Ewe unaetaka kheri elekea katika kheri hiyo,na Ewe mwenye


kutaka shari acha shari hiyo, Allah huwa anawaacha huru na moto.Na maneno haya


husemwa kila usiku" (Tirmidhi . (


Pia ndani ya mwezi huu ndimo Qur'an iliteremshwa kutoka ktk Lawhum Mahfuudh ilaa samaai dduniya (Kutoka Lawhim-Mahfuudh mpaka mbingu ya


kwanza. Hivyo kwa ubora wa Qur'an basi inaunyanyua mwezi huu na kuwa bora kama Allah alivyosema katika Qur'an kuwa -:


"Mwezi wa Ramadhaan ni mwezi ambao imeteremshwa Qur-aan ili iwe uongozi kwa


watu na hoja na upambanuzi (Baina ya haki na batil)” (Qur'an Baqarah:185(


Kitu kingine kinachoupa ubora mwezi huu ni Usiku wa Cheo/Laylahtul qadr kwani ktk usiku huu ndimo Qur'an ilishuka na usiku huu ukafanywa kuwa bora zaidi ya miezi elfu moja. Kama Allah alivyosema -:


" Huo ni usiku wa hishima ni bora kuliko miezi elfu.Huteremka Malaika na roho (za viumbe watakatifu) katika (usiku) huo kwa idhini ya Mola kwa kila jambo.Ni amani (usiku) huo mpaka


mapambazuko ya alfajiri" (Qur'an 97:3-5(


Yaan mtu akifanya Ibada ndani ya usiku huo basi ibada ile huandikwa/hulipwa sawa na mtu aliyefanya ibada hiyo kwa miezi elfu moja.


Pia ndani ya mwezi huu Dua zetu hupokelewa kwa kila mwenye kuomba na haya tunayapata Katika hadiyth iliyopokewa na Imaam Ahmad: "Kutoka kwa Jaabir (radhiya Allaahu 'anhu) kwa isnadi iliyo nzuri kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Amesema: "Kila Muislam du'a zake ni zenye kukubaliwa atapomuomba Allah katika mwezi wa Ramadhaan". Kuna Fadhila nyingi katika mwezi huu ambazo zimeufanya mwezi huu kuwa na ubora ndani yake na ikawa ni furaha kubwa kwa Muumini kupitikiwa/kufikiwa na


mwezi huu na akaudiliki huku akiwa na afya nzuri akawa ni mwenye kutekeleza Ibada zinazopatikana ndani ya mwezi huu.


UBORA WA AMALI NJEMA NDANI MWEZI WA RAMADHANI.


Thawabu za amali njema huongezwa kwa sababu


nyingi miongoni mwazo ni utukufu na ubora wa zama,kama mwezi wa Ramadhani. Zifuatazo ni baadhi tu ya amali njema zinazoongezewa thawabu katika Mwezi wa Ramadhani:


.1 Kusimama usiku kwa Ibada Mtume(Swallah Llahu Alayh Wassalam) kasema:


من قام رمضان إيماناً واحتساباً غفر له ما تقدم من ذنبه (


] متفق عليه [


Atakae simama Ramadhani ilhali ya kuamini na kutaraji thawabu Allah atamsamehe dhambi zake zilizo tangulia" (Bukhari na Muslimu)


. 2 Kufanya Umra.Mtume(Swallah Llahu Alayh Wassalam) anasema:


) عمرة في رمضان تعدل حجة معي ( ] متفق عليه [


Umrah katika mwezi wa Ramadhani hulingana na Hijja pamoja nami" (Bukhari na Muslimu)


.3Kusoma Qur-ani tukufu.


Kwa kuwa Qur'an imeshushwa ndani ya mwezi huu basi kila mwenye kukithilisha kuisoma ktk mwezi huu basi anaujira mkubwa zaidi na baada ya kulitambua hilo Maswahaba walikithirisha sana kuisoma Qur'an ndani ya mwezi huu na mifano yao tunaiona hapa chini.


'Uthmaan bin 'Afaan (Radhiya


Allaahu 'anhu) kila siku akisoma Qur-aan yote


yaani anakhitimisha mara moja kwa siku, kwa


maana, msahafu mzima anausoma kwa siku moja. Na walikuwa baadhi yao katika wema wakisoma Qur-aan yote kwa siku tatu,wengine kwa wiki moja na wengine kwa siku kumi.Walikuwa wakisoma Qur-aan ndani ya Swalah na nje ya Swalah.



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI