
1
FADHILA YA SUNNA ZA MTUME (S.A.W)
Imeandaliwa na: Abubakari Shabani Rukonkwa
Imepitiwa na: Yunus Kanuni Ngenda
Utangulizi:
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote, na rehma na amani zimwendee kiongozi wa umma huu Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na watu wake na Maswahaba zake wote,! Amma baad.
Ni wazi kwamba Sunna za Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ndio kielelezo na uhimili katika dini yetu ya kiislam, pia ndio tafsiri ya mwongozo mzima wa maisha ya mwislam kidini na kijamii kwa ujumla, hivyo mwislam hawezi kuwa na imani thabiti kama hajafuata sunna za Mtume Muhammad (s.a.w).
Hii inamaana kwamba yeyote aliye mbali na sunna basi yuko mbali na dini, na aliyekaribu na sunna yupo karibu na dini, Mwenyezi Mungu mtukufu anatilia mkazo na kuamrisha katika Qur’an pale alipo sema:
2
Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni
jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika
Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
[Surat Hashri: 7.
Ayah hii tukufu imekusanya sunna zote alizokuja nazo Mtume
wetu Muhammad (s.a.w) ya kwamba hatuna budi kuzipokea na
kuzifanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kuzilinda, kuzinusuru na
kuzieneza ulimwenguni kote.
Hili ni jambo kubwa lenye fadhila nyingi kwa yeyote mwenye
kujishughulisha nalo, na ni sababu ya pata mwisho mwema na
kuipata Jannah (Pepo).
Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe
juu yake:
Uislam ulianza ni mgeni na utarudi ni mgeni kama ulivyoanza,
lakini habari njema ni kwa wale wanao onekana ni wageni
(maghurabaa). (Pia inasemekana kwamba “TWUUBAA” ni mti
katika miti ya peponi.
3
Na katika riwaya nyingine akaulizwa Mtume (s.a.w): Ewe
Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kina nani hao wanao onekana
wageni (maghurabaa)? Akasema Mtume (s.a.w):
Ni watu ambao wanatengeneza (palipo haribika) wanapoharibu
watu (Dini).
Na katika lafdhi nyingine: Hao ni watu ambao wanatengeneza
yaliyo haribiwa na watu kutokana na sunna zangu.
Chanzo: Majumuu fatawa Ibun Baaz namba 3/158.
Na katika Hadithi nyengine.
Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe
juu yake: “Umati wangu wote wataingia Peponi isipokua atakae
4
kata”, wakasema (Maswahaba): Ewe Mjumbe wa Mwenyezi
Mungu ni nani basi atake kata? Akasema: “Mwenye kunitii
ataingia Peponi na mwenye kuniasi basi huyo amekataa.”
Ameipoke Imamu Bukhari, katika Hadhithi iliyotokana na Abuu
Hurayra.
Kitabu ni: Swahihi Bukhari ukurasa namba 7280.
Hivyo shime ndugu zngu katika imani tushikamaneni na sunna
za bwana Mtume Muhammad (s.a.w) hata kama jamii itakuona
umekuja na mambo mageni, au hata ukipewa majina yasofaa
hilo usijali bali hata Mtume (S.A.W) aliitwa mchawi a kaitwa
mwendawazimu lakin aliendelea kuitangaza dini na kueneza
Sunna zake (s.a.w).
Mfano ulio hai ni wanislam wanaoifanyia kazi kauli ya bwana
Mtume (s.a.w) ya kupunguza nguo iliyozidi katika kongo mbili
za miguu kwa wanaume utakuta baadhi ya watu wana watukana
na kuwabeza kwa kuwapa majina yasiyofaa kama : njiwa, au
kavaa nguo ya mtoto, au kavaa kimini sketi nk.
Hayo yakikukuta basi usikate tama unatakiwa kushikamana na
sunna tu bila kujali matusi na kebehi za maadui wa haki.
Au kauli za baadhi ya watu kuwa eti huu sio wakati wa
kuambiana kuhusu ndevu, kukata nguo inayozidi chini, na
mfano wa hayo.
5
Hizi zote ni sauti za shari zinazokurudisha nyuma katika kufata
maamrisho ya Mtume wetu Muhammad swallah llah alayhi
wasalam.
Bali juwa kuwa ukifanya bidaa moja basi umeuwa suna
iliyostahiki kuwa mahala hapo.
Na ukishika sunna basi juwa umefanya juhudi kubwa ya kuzuia
bidaa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu mshindi na mtukufu
atudumishe katika Sunna za Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na
atukutanishe nae katika Pepo ya Firdausi, pamoja na wema
waliokuja baada yake, Ameen!!.