1
بسم الله الرحمن الرحيم
Fadhila Za Tawhiyd. Imeandaliwa na alhidaaya.com Imepitiwa na Yunus Kanuni Ngenda. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa):
Basi elewa kwamba laa ilaaha illa-Allaah (hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Allaah)[Muhammad: 19] Maana ya Tawhiyd kama alivyosema ‘Allaamah ‘Abdir-Rahmaan Naaswir As-Sa’dy katika “Al-Qawlus-Sadiyd Fiy Maqaaswidit-Tawhiyd - Sharh Kitaab At-Tawhiyd” “Tambua kwamba maana ya Tawhiyd haina mipaka. Ni maarifa na kukiri kumpwekesha Ar-Rabb (Mola) kwa Swifa za ukamilifu, na kuthibitisha kwamba Anapwekeshwa katika Sifa Zake Adhimu na Tukufu, na kumpwekesha katika ‘ibaadah zote”. Kinyume cha Tawhiyd ni ‘Shirk’ ambayo ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) katika hayo yaliyotajwa yote yanayomuhusu Yeye Pekee. ‘Ulamaa wameigawanywa Tawhiyd katika sehemu tatu: 1 – Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah
2
Nayo ni kumpwekesha Allaah katika Uumbaji,
Uendeshaji wa mambo yote katika Ulimwengu, Utoaji
rizki, Uletaji uhai na Ufishaji, kwa kuamini kwamba
Yeye Ndiye Aliyeumba kila kitu, Anayeruzuku na
kuendesha mambo yote ni Allaah (Subhaanahu wa
Ta’alaa). Hana mshirika, na kuamini kwamba Ufalme
wote ni wake:
Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) Anasema:
Sema: "Ni nani Mola wa mbingu na ardhi?" Sema: "Ni
Allaah" [Ar-Ra’d:16]
Na Anasema:
Sema: “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na
ardhini. Au nani anayemiliki kusikia na kuona; na nani
anayemtoa (aliye) hai kutoka mfu, na anayemtoa mfu
kutoka (aliye) uhai; na nani anayedabiri mambo (yote)?
Watasema: “Ni Allaah”; basi sema: “Je basi hamuwi na
taqwa?” (Hamumkhofu Allaah?) [Yunus: 31]
2-Tawhiyd Al-Uluwhiyyah
Maana yake ni kumwepekesha Allaah katika 'ibaadah
na kuzielekeza ‘ibaadah zote kwa Allaah (Subhaanahu
wa Ta’alaa).
3
Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) Anasema:
Sema: “Hakika Swalaah yangu, na nusukiy (kuchinja
kafaara na ‘ibaadah zangu) na uhai wangu na kufa
kwangu ni kwa ajili ya Allaah (Pekee) Mola wa
walimwengu.” Hana mshirika, na kwa hayo ndio
nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza
(waliojisilimisha kwa Allaah). [Al-An’aam: 162-163]
3-Tawhiyd Asmaa wasw-Swifaat
Kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) kwa
Sifa Zake Tukufu, na Majina Yake mazuri, bila
kuzigeuza Sifa hizo maana zake, au kuzipinga, au
kuzifananisha na viumbe au kuzipa unamna. Yeye
Amejipa Majina mazuri mazuri na Sifa nzuri nzuri na
Akawataka waja Wake wamuombe na kumtukuza kwa
Majina na Sifa hizo.
Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) Anasema:
Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni
kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa (kwa kuharibu
utukufu, kukanusha, kugeuza maana, kushabihisha)
katika Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa
wakiyatenda. [Al-A’raaf: 180]
4
Qur-aan nzima imedhihirisha Tawhiyd ya Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala); mfano Suwratul-Faatihah
ambayo tunaisoma kila siku mara kumi na saba katika
Swalaah zetu za fardhi na pia katika Swalaah zote
nyinginezo, imejumuisha aina tatu zote za Tawhiyd.
Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaanir-Rahiym (Mwingi wa
Rahmah - Mwenye kurehemu). AlhamduliLLaahi (Sifa
njema zote ni za Allaah) Mola wa walimwengu. Ar-
Rahmaanir-Rahiym (Mwingi wa Rahmah-Mwenye
kurehemu). Maalik (Mfalme) wa siku ya malipo. Wewe
Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba
msaada [Al-Faatihah: 1-5]
Na pia kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
Mola wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake; basi
mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah
Yake. Je, unamjua (mwengine) mwenye Jina Lake? (Bila
shaka hakuna aliyefanana Naye kwa lolote, vyovyote, na
wala hana mshirika!). [Maryam: 65]