Nakala

1


AQIDA NDIO IWE MWANZO KATIKA KILA JAMBO. Imeandikwa na Shaykh Swaalih Al-Fawzaan Imefasiriwa na Abu ‘Abdil-‘Aziyz ‘Abdullaah Imerejewa na Abubakari Shabani Rukonkwa Jambo la kwanza, kubwa, na la msingi katika kulingania watu kumtii Allaah, na nikwa nini Aqiydah iwe mwanzo. Aqiydah ni lazima ije mwanzo kwa sababu, kinachozusha mgawanyiko na maangamizi katika ulimwengu wa Kiislamu ni kukosekana ‘Aqiydah iliyo sahihi. Kwa Nini ‘Aqiydah Liwe Ni Jambo La Mwanzo? Hakika ‘Aqiydah lazima ije mwanzo kwa sababu ni msingi wa Da’wah ya Mitume wote kama Allaah Alivotuma ujumbe Wake kupitia kwa Mitume Wake. Kama Anavyosema Allaah kwa kupitia kwa ulimi wa kila Mtume Aliyemtuma kwa watu wake: “Enyi watu! Muabuduni Allaah, hamna mungu isipokuwa Yeye” (Surat Huud 11: 84) ‘Aqiydah lazima ije mwanzo kwa ajili ya kuepukana na kizuizi cha kubakia motoni (Jahannam) milele na kujiepusha na adhabu hiyo. Hamujasikia maneno ya Allaah Aliyetukuka: “Hakika Allaah hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa” (Suratun Nisaa 4: 48) Kumshirikisha Allaah ni dhambi kubwa ambayo inampelekea mja kutoka kwenye Tawhiyd (kumpwekesha Allaah), na Tawhiyd ni msingi wa usahihi wa ‘Aqiydah. ‘Aqiydah ni lazima iwe mwanzo vilevile kwa ajili kumshirikisha (Shirk) Allaah ni dhambi kubwa ambayo ni dalili ya madhara juu yetu kama Allaah Alivyosema:


2


“Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa” (Suratul Luqmaan 31:13) ‘Aqiydah ni lazima ije mwanzo kwa sababu, kinachozusha mgawanyiko na maangamizi katika ulimwengu wa Kiislamu ni kukosekana ‘Aqiydah iliyo sahihi na watu kufuata ‘Aqiydah zisizo sahihi. Ndio maana ‘Aqiydah nyingi za Waislamu zimejaa ufisadi kwa mambo ambayo ni shirk kubwa kwa mfano utakuta watu wanatufu (wanazunguka) kwenye makaburi na kuwaomba maiti waliomo ndani ya makaburi hayo wawasaidie haja zao na kudhani kufanya hivyo watapata mahitaji yao na kukidhiwa shida zao. Na kwa hali hiyo, watu kama hawa wamerudi nyuma kiwakati, wanajirudisha katika wakati wa Jaahilliyah (zama za ujinga kabla ya Uislamu). Na wanajifanya kama hawajasikia maneno ya Allaah Aliyetukuka: ‘‘Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia hawakujibuni. Na Siku ya Qiyaamah watakataa ushirikina wenu. Na hapana atakayekupa khabari vilivyo kama Yeye Mwenye khabari” (Suurat Faatwir 35: 14) Na sisi tunawakataza kufuata uzushi wa Masufi ambao wameweza kuueneza kwa watu wa kawaida wasio na elimu na hadi taqriban nchi mbalimbali zimekuwa zikiongozwa na kutawaliwa na uzushi wa hawa Masufi na bid’ah zao kama vile Mawlid. Na hata uzushi wa aina mbalimbali kama kuwaiga Makafiri katika sherehe zao na sikukuu zao, achilia mbali uzushi mbalimbali wanaoufanya katika Dini ambao umegawa nchi zao na kuziweka mbali na Qur-aan na Sunnah. Kwa haya machache ndugu yangu mpendwa, tumejaribu kuwaonyesha ukweli ya kwamba ‘Aqiydah ni jambo la muhimu na la mwanzo katika maisha yako na daima ‘Aqiydah inapaswa iwe mwanzo.


3


Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jama’aah Kuhusu Kutokudumu Milele Waislamu Motoni Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah wanaamini kwamba baadhi ya Waislamu wataingia Peponi bila ya kufanyiwa hesabu au kupewa adhabu. Wengine wataingia Peponi baada ya kufanyiwa hesabu, Wengine wataingia Peponi baada ya kuadhibiwa motoni kama Anavyotaka Allaah kisha Atawatoa humo. Kutolewa motoni kisha kuingizwa Peponi hakutawasababishia huzuni au dhiki Peponi kwasababu Pepo ni makazi ya raha tupu. Kama ilivyotajwa katika Qur-aan na Sunnah, watapata kila walichokipata wakaazi wengine wa Peponi. Hakuna dalili inayoashiria kwamba watu hao watakuwa na hisia za majuto baada ya kuingia kwao Peponi kutokana na adhabu watakazozipata motoni. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametutajia hali zao zitakavyokuwa baada ya kutolewa motoni kama ifutavyo: 1. Watatumbukizwa Kwenye Mto Wa Uhai Wabadilike Kuwa Wapya Imesimuliwa kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ))


((Watu wa Peponi watakapoingia Peponi watakapo ingia Peponi na wa motoni watakapoingia Motoni, Allaah Atasema


4


[kuwaambia Malaika]: “Yeyote aliyekuwa na Iymaan moyoni mwake, uzito wa chembe cha atomu, mtoeni!” Watamtoa humo, watatoka kama kwamba ni mifupa iliyounguzwa na watabadilika kuwa makaa. Watatumbukizwa katika mto wa uhai, kisha watakuwa [kimaumbile] humo kama mfano wa mbegu zinapomea katika ufa [mwatuko] wa mafuriko)). Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Je huwaoni wanavyomea [wanavyokuwa kimaumbile] manjano na kupinda?)). [Al-Bukhaariy na Muslim]. 2. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba watabadilika watakapotolewa motoni. Imesimuliwa toka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuhusu Jahannamiyuwn (watu wa motoni):


((Watatolewa motoni baada ya kuweko humo. Kisha watatoka kama kwamba ni matawi ya chembe za ufuta. Kisha wataingia katika Mto miongoni mwa mito ya Peponi ambako wataoga kisha watatoka [weupe] humo kama karatasi)).[Muslim]. Imaam An-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema: “Ufuta imekusudiwa chembe za ufuta maarufu zinazotoa mafuta ya ufuta”. Imaam Abu as-Sa’adaat al-Mubaarak bin Muhammad bin ‘Abdil-Kariym al-Jazariyy anayejulikana kama: Ibn Al-Athiyr (Rahimahu Allaah) amesema: “Inamaanisha - na Allaah Anajua zaidi – kwamba matawi ya ufuta yanapokusanywa na kuachwa juani ili mbegu zake zikusanywe, hubadilika kuwa membamba na meusi kama kwamba zimeunguzwa. Ndio wakafananishwa watu hawa. Kauli yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). ((Kisha watatoka humo kama karatasi))


5


wamefananishwa kama karatasi kwa sababu watakuwa weupe mno baada ya kuoga mtoni na weusi wote waliokuwa nao utaondoshwa.” [Sharh Muslim]. Kadhaalika, imesimuliwa na Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ) )


((Watatoka motoni kwa sababu ya shafa’ah (uombezi) wakiwa kama matango)). [Al-Bukhaariy]. Al-Haafidhw Ibn Hajr al-‘Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema: “Kuhusu matango madogo, makusudio ni, kama kitu cheupe na kidogo” Tanbihi: Sifa ya weupe huu unakusudiwa vile watakavyokuwa baada ya kukua (kumea) [Fat-h al-Baaariy (11/429)]. Lakini mwanzo watakapotoka motoni watakuwa kama makaa kama inavyoelezea Hadiyth ifuatayo: 3. Watakua kama Lulu kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atawaruzuku Radhi Zakke na Hatawaghadhibikia tena. Imesimuliwa kutoka kwa Abu Sa’iyd al-Khudriyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: )) فَيَقُولُ اللََُّّ عَزَّ وَجَلَّ : شَفَ تْ الْمَلََئِوَةُ، وَشَفَعَ النَّبِيُّونَ، وَشَفَعَ


((Allaah Atasema [Peponi]: “Malaika wameshaombea shafa’ah, Mitume wameshaombea shafa’ah, Waumini wameshaombea shafa’ah, hakuna aliyebakia isipokuwa Mwingi wa Rahma, Mwenye Kurehemu kuliko wote wanaorehemu.” Kisha Atateka kutoka motoni na Atatoa watu wasiopata kufanya jema lolote [duniani] na ambao wamebadilika kuwa makaa. Atawatumbukiza katika Mto ulio kingoni kwa Peponi unaoitwa ‘Mto wa Uhai’ watatoka humo kama zinavyotoka mbegu katika ufa wa mafuriko. Kisha watatoka wakiwa kama lulu wakiwa na mapambo shingoni mwao na watu wa Peponi watawatambua. Hawa ni waliofidiwa [waliokombolewa] na Allaah Akawaingiza Peponi bila hata ya kuwa wametenda ‘amali njema au kheri yoyote waliyoitanguliza. Kisha Atasema: “Ingieni Peponi, mtakayoyaona humo ni yenu.” Watasema: “Ee Mola wetu, Umetupa ambayo Hujapatapo kumpa yeyote kati wa walimwengu.” Atasema: “Mtapata kutoka Kwangu yaliyo bora kuliko haya” Watasema: “Ee Mola wetu! Kitu gani tena kitakachokuwa bora kuliko haya?” Atasema: “Radhi Zangu kwani Sitoghadhibika tena nanyi kamwe.”)) [Al-Bukhaariy na Muslim]. Hii ni Hadiyth muhimu ambayo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja daraja ya juu kabisa itakavyokuwa ya watu watakaotolewa motoni ambao Mola wao Atawaruzuku, karama, heshima, na fadhila zikiwemo: Kutumbukizwa katika Mto wa Uhai ili wakuwe (waumbike) kama wapya. Kutoka katika Mto kama kwamba lulu wakiwa wamevaa mapambo shingoni mwao. Kupewa kila watakachokiona Peponi. Kudhania kwao kutokana na kheri na baraka na furaha ya hali ya juu watakayoipata kwamba Allaah Amewakirimu kwa jambo Hajapatapo kumkirimu yeyote mwengine.


7


Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atawaruzuku Radhi Zake na Hatowaghadhibikia tena kamwe. Daraja ambazo Allaah Atawakirimu watu watako ingia Peponi zimethibitika katika usimulizi ufuatao wa Hadiyth: Imesimuliwa kutoka kwa ‘Abdulllaah bin Mas’uwd (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: )) إِنِّي لَََعْلَمُ آخِرَ أَهْلِ النَّارِ خُرُوجًا مِنْهَا وَآخِرَ أَهْلِ الْجَنَّةِ دُخُولًّ،


((Nawajua watu wa mwisho kabisa watakaotoka motoni, na watu wa mwisho kabisa watakaoingia Peponi. Atakuwa ni mtu atakayetoka akitambaa kutoka motoni kisha Allaah Atamwambia: “Nenda na ungie Peponi” Ataifikia lakini atadhania kwamba imejaa. Atarudi na kusema: “Mola wangu! Nimeikuta imejaa!” Allaah Atasema: “Nenda ingia Peponi” Atafikia lakini atadhania kwamba imejaa. Atarudi na kusema: “Mola wangu! Nimeikuta imejaa!” Allaah Atasema: “Nenda ingia Peponi, kwani utapata mfano wa dunia na mara kumi yake”)) Au: ((“Utapata mfano wa mara kumi ya dunia” Atasema [mja]: “Je unanifanyia masikhara?)) Au: ((“Je unanidhihaki na hali Wewe ni al-Malik?”)). Nikamuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akicheka mpaka magego yake yakadhihirika na huku akisema: ((Huyo ndiyo mtu wa daraja ya chini kabisa Peponi)). [Al-Bukhaariy na Muslim]. 4. Watajulikana kama ni Al-Jahannamiyuwn (watu wa motoni) au ‘Utaqaa al-Jabbaar’ (waliokombolewa na Mwenye Ujabari) Kisha wataondoshewa jina hilo.


8


Jina la Al-Jahannamiyuwn ni wingi wa Jahannam yaani moto. Ina maana kwamba Allaah Amewakomboa motoni. Imesimuliwa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: )) يَخْرُجُ


((Miongoni mwa watu watatolewa motoni baada ya miale yake imewagusa [na kuwabadilisha rangi] kisha wataingizwa Peponi. Na watu wa Peponi wataiwa al-Jahannamiyuwn)). [Al-Bukhaariy]. Na pia kauli nyingine kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu): kwa Hadiyth iliyokusanywa na Imaam Ahmad: ))


((…wataingia Peponi na watu wa Peponi watasema: “Hawa ni Al-Jahannamiyuwn lakini Al-Jabbaar [Mwenye Ujabari] Atasema: “Hapana! Bali wao ni waliokombolewa na Al-Jabbaar ‘Azza wa Jalla)). [Imepewa daraja ya Swahiyh na Ibn Mandah katika ‘al-Iymaan’ (2/847), Ibn Khuzaymah (2/710) na Al-Albaaniy katika ‘Hukm Taarik As-Swalaah’ (uk. 33). Ibn Hibbaan amesimulia kutoka kwa Abu Sa’iyd al-Khudriyy (Radhiya Allaahu ‘anhu): ))


 (( . ((Wataitwa humo Peponi: “al-Jahannamiyyuwn” kutokana na weusi katika nyuso zao. Watasema: “Mola wetu! Tuondoshee jina hili!”)) Akasema: ((Kisha Atawaamrisha waoge katika Mto wa Peponi, wataondoshewa hilo [Jina])).[Imepewa daraja ya Swahiyh na Ibn Hibbaan (16/457) na pia Ash-Shu’ayb al-‘Arnauwtw].


9


Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia kwamba mchovyo mmoja tu wa Peponi utamfanya Muislamu asahau tabu zote alizozokabiliana nazo duniani, itakuwaje basi ikiwa Pepo ndio makazi yake ya milele? Imesimuliwa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: )) يُؤْتَى أَنْ مِ أَهْلِ الدُّنْيَا مِنْ أَهْلِ


((Mtu aliyeneemeka kabisa duniani ambaye ni miongoni mwa watu wa motoni ataletwa Siku ya Qiyaamah na atachovywa mara moja motoni kisha ataulizwa: “ee mwanadamu! Umepatapo kuona zuri lolote? Umewahi kupata raha yoyote?” Atasema: “Hapana Mola wangu!” Kisha ataletwa mtu aliyepata shida kabisa duniani akiwa miongoni mwa wa watu wa Peponi atachovywa Peponi ataambiwa: “Ee mwanadamu! Je umepatapo kuona ubaya wowote? Je imekupitia shida yoyote?” Atasema: “Hapana Mola wangu! Sijapatapo kuona ubaya wowote wala haijanipitia shida yoyote.”)) [Muslim]. Dalili nyingine kwamba mchovyo mmoja wa neema za Pepo utamuondoshea tabu zote za awali, mpaka tabu za kuadhibiwa motoni. Hivi ni kuhusiana na yaliyotajwa kuhusu kubadilishwa kwake mtu baada ya kutumbukizwa katika ‘Mto wa Uhai’ ni katika mapokezi yaliyosimuliwa na Imaam Muslim (2836) kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaah ‘anh) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye amesema:


11


((Atakayeingia Peponi atastarehe na hatokuwa na kuhuzunika, nguzo zake hazitochakaa wala ujana wake hautatoweka [hatozeeka])). Neema hiyo inathibitisha kwamba atakayeingizwa Peponi ataondoshewa tabu zote na inamaanisha kwa ujumla kila atakayeingia Peponi, ikiwa ni mwenye kuingizwa motoni kwanza au hakuingizwa. Al-Qaadhwiy amesema: “Kinachomaanishwa hapa ni kwamba Pepo ni makazi ya kuthibiti na neema ambazo hazitobadilika au kuathirika kwa tabu zozote au ufisadi.” [Tuhfat


((Na watasema: “AlhamduliLLah – Himdi Zote ni za Allaah [Pekee] Ambaye Ametuondoshea huzuni [zote]. Hakika Mola wetu bila shaka ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kupokea Shukurani. Ambaye Ametuweka nyumba za makazi kwa Fadhila Zake, haitugusi humo tabu wala haitugusi humo machovu)).[Faatwir: 34-35]. ‘Allaamah As-Sa’diy (Rahimahu Allaah) amesema: “Inamaanisha maskani ya makazi ya milele, maskani ambayo mtu atataka kuishi milele kwa sababu ya mazuri mengi yaliyomo humo na kwa sababu ya starehe zinazodumu na kwa sababu ya kutokuweko cha kuondosha starehe hizo. Na hayo ni kutokana ((kwa Fadhila Zake)) kwetu na Neema Zake, si kwa sababu ya ‘amali zetu, kwani ingelikuwa si Fadhila Zake, tusingelifikia tulivyofikia. ((haitugusi humo tabu wala haitugusi humo machovu)) yaani, hakutakuweko na machofu katika miili yetu, nyoyo au nguvu,


11


wala katika raha nyingi. Hii inaonyesha kwamba Allaah Atafanya miili yao iumbike vizuri upya na Atawafanyia kila sababu za kuwafanyia makazi yao yawe ni yenye raha za kudumu, ili wasiguswe na tabu au wahka wala huzuni.” [Tafsiyr As-’Sa’dy 689]. Na Allaah Anajua zaidi



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI