Nakala

Muhtasari wa misingi minne


]MWANACHUONI MUHAMMAD BIN ABDIL WAHHAB -MWENYEZI MUNGU AMREHEMU [





3


Muhtasari wa misingi minne.


MWANACHUONI MUHAMMAD BIN ABDIL WAHHAB -MWENYEZI MUNGU AMREHEMU


Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu.


Namuomba Mwenyezi Mungu Mkarimu Mola wa Arshi tukufu akusimamie duniani na Akhera.


Na akufanye kuwa mwenye kubarikiwa popote utakapokuwa, na akufanye kuwa ni mtu ambaye ukipewa unashukuru, ukijaribiwa unasubiri, na ukifanya dhambi unaomba msamaha. Kwani mambo haya matatu ndiyo anuani ya furaha.


Tambua, akuongoze Mwenyezi Mungu katika utiifu wake: Yakuwa utakasifu ndiyo dini ya Ibrahim: Nao ni kumuabudu Mwenyezi Mungu, yeye pekee kwa kumtakasia dini, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:





"Na sikuumba majini na binadamu isipokuwa kwa lengo tukufu, nalo niabudiwe mimi peke yangu, na sio asiyekuwa mimi". [A Dhariyati: 56]. Unapotambua kuwa Mwenyezi Mungu kakuumba kwa ajili ya kumuabudu yeye; basi tambua kuwa ibada haiitwi ibada isipokuwa mpaka iwe na tauhidi (yaani kumpwekesha Mwenyezi Mungu) kama ambavyo swala haiitwi swala ila mpaka iwe na twahara, Na pindi inapoingia shirki katika ibada, ibada hiyo inaharibika, kama hadathi (kutokuwa na udhu) kunavyokuwa katika


4


twahara, unapofahamu kuwa shirki ikiingia katika ibada inaiharibu, na inaporomosha amali, na anakuwa mfanyaji wake ni katika watu wenye kukaa milele motoni. Basi hapo utajua kuwa jambo la msingi zaidi kwako ni kulijua hilo (yaani kuifahamu tauhiidi), huenda Allah akakuepusha na mtego huu, nao ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu ambako Mwenyezi Mungu alisema ndani yake:





"Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi Madhambi ya kushirikishwa naye, na husamehe madhambi mengine yote yasiyokuwa ushirikina kwa anayemtaka". [An nisaai: 116]. Na hili ni kwa kuijua misingi minne aliyoitaja Mwenyezi Mungu katika kitabu chake:


5


Msingi wa kwanza:


Nikujua kuwa makafiri aliowapiga vita Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake -walikuwa wakimkubali Mwenyezi Mungu Mtukufu- kuwa ndiye muumbaji, mpangiliaji, na kuwa swala hilo halikuwaingiza katika uislamu; na ushahidi ni kauli yake Mtukufu: "Waambie, ewe Mtume, washirikina hawa, «Ni nani anayewaruzuku kutoka juu kwa mvua anayoiteremsha, na kutoka ardhini kwa mimea na miti aina mbalimbali anayoiotesha kutoka humo, Na ni nani anayemiliki hisia za kusikia na za kuona mnazostarehea nyinyi na wengineo? Na ni nani anayemiliki uhai na kifo, katika ulimwengu wote, akawatoa wenye uhai na wafu, baadhi yao kutoka kwa wengine, katika viumbe mnavyovijua na msivyovijua? Na ni nani anayeyaendesha mambo ya mbinguni na ardhini na yaliyomo ndani yake, (anayeyaendesha) mambo yenu nyinyi na mambo ya viumbe vyote?» Watakujibu kwamba anayefanya yote hayo ni Mwenyezi Mungu. Waambie,





«Basi si muogope mateso ya Mwenyezi Mungu mnapomuabudu mwingine pamoja na Yeye?» [Yunus: 31].


6


Msingi wa pili:


Ni kuwa wao (washirikina) wanasema: Hatukuwaomba wala kuwaelekea isipokuwa ni kwa kutaka ukaribu na utetezi, na ushahidi wa kutaka ukaribu; ni kauli yake Mtukufu:





"Na wale wanaomshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu wakawafanya wasiokuwa Yeye kuwa ni mawalii (wategemewa), wanasema, «Hatuwaabudu waungu hawa pamoja na Mwenyezi Mungu isipokuwa wapate kutuombea kwa Mwenyezi Mungu na ili watukurubishe daraja Kwake.» Hakika Mwenyezi Mungu Atawapambanua, Siku ya Kiyama, baina ya Waumini wenye ikhlasi na wale wenye kumshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, katika yale waliokuwa wanatofautiana juu yake kuhusu vile walivyoabudu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaelekezi kuongoka kwenye njia iliyonyooka wale wenye kumzulia uongo Mwenyezi Mungu, wenye kuzikanusha Aya zake na hoja zake". [Azzumar: 3]. Na ushahidi wa kutaka uombezi, ni kauli yake Mtukufu:





"Na wanaabudu kinyume na Mwenyezi Mungu yale yasiyowadhuru wala kuwanufaisha na wanasema, 'hawa ni watetezi wetu kwa Mwenyezi Mungu'". [Yunus: 18].


7


Na uombezi una aina mbili: Uombezi uliokatazwa, na uombezi uliokubaliwa.


Uombezi uliokataliwa: nao ni ambao una tafutwa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika mambo ambayo hakuna mwenye uwezo nayo ila ni Mwenyezi Mungu; na ushahidi ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:





"Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu toeni Zaka zilizofaradhishwa na mtoe sadaka ya vitu mlivyopewa na Mwenyezi Mungu kabla haijaja Siku ya Kiyama, wakati ambapo hakuna kuuziana ikapatikana faida, wala mali ambayo nyinyi mtajikomboa nayo nafsi zenu kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala urafiki wa rafiki wenye kuwaokoa, wala muombezi anayemiliki kuwafanya mpunguziwe adhabu. Na makafiri ndio madhalimu na wakiukaji mipaka ya Mwenyezi Mungu". [Al baqara: 254]. Na uombezi uliokubaliwa: Ni ule unaoombwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na muombaji awe ni mtu aliyepewa utukufu wa kuombea, na mwenye kuombewa awe ni katika wale ambao Mwenyezi Mungu ameridhia kauli zake na matendo yake baada ya idhini yake; kama alivyosema Mtukufu:





"Ni nani awezaye kuombea kwake maombi yoyote isipokuwa kwa idhini yake" [Al Baqara: 255].


8


Msingi wa tatu:


Ni kuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake alijitokeza kwa watu waliokuwa wametawanyika katika ibada zao, wako miongoni mwao waliokuwa wakiabudu Malaika, na wako waliokuwa wakiwaabudu Manabii na watu wema, na wako waliokuwa wakiabudu miti na mawe, na wako waliokuwa wakiabudu jua na mwezi, na akawapiga vita Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, na wala hakuwatofautisha; na ushahidi ni kauli yake Mtukufu:





"Na piganeni na washirikina, enyi waumini, mpaka usiweko ushirikina na uzuiliaji wa njia ya Mwenyezi Mungu na asiabudiwe isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke yake asiye na mshirika, ili chuki ziwaondokee waja wa Mwenyezi Mungu katika ardhi na mpaka dini, Utiifu na Ibada vitakasiwe Mwenyezi Mungu tu bila mwingine". [Al Anfaal: 39]. Na ushahidi wa kuabudu jua na mwezi; kauli yake Mtukufu:





"Na miongoni mwa hoja za Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake, dalili za upweke wake na ukamilifu wa uweza wake, ni kutofautiana mchana na usiku na kufuatana (kila moja wapo kuufuata mwingine) na kutofautiana jua na mwezi na kufuatana, vyote hivyo viko chini ya uendeshaji wake. Msilisujudie jua wala mwezi, kwani hivyo viwili vinaendeshwa na vimeumbwa; bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba, iwapo nyinyi kwa kweli mnafuata amri yake, mnasikia


9


na mnamtii yeye, basi muabuduni yeye Peke yake Asiye na mshirika". [Suratu Fusswilat: 37]. Na ushahidi wa kuombwa Malaika, ni kauli yake Mtukufu:





"Na haikuwa kwa yeyote katika wao awaamrishe nyinyi kuwafanya Malaika na Mitume kuwa ni miungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu ambao nyinyi mnawaabudu". [Al-Imraan: 80]. Na ushahidi wa kuombwa Manabii; ni kauli yake Mtukufu: "Na kumbuka pindi atakaposema Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Siku ya Kiyama, «Ewe ‘Īssā mwana wa Mariam! Hivi wewe uliwaambia watu, ‘nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni waabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu’?» ‘Īssā akajibu, kwa kumtakasa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na kumuepusha na sifa za upungufu,





«Haipasii kwangu kuwaambia watu yasiyokuwa haki. Nikiwa nimesema hili, basi ushalijua. Kwani hakuna chochote kinachofichikana kwako. Wewe unayajua yaliyomo ndani ya Nafsi yangu, na mimi siyajui yaliyomo ndani ya Nafsi yako. Hakika wewe ndiye Mjuzi wa kila kitu, kilichofichikana au kuwa wazi.» [Al Maaida: 116]. Na ushahidi wa kuombwa watu wema; ni kauli yake Mtukufu:





10


"Hao washirikina wanawaomba Manabii, watu wema na Malaika, wao wenyewe wanashindana kujiweka karibu na Mola wao kwa matendo mema wanayoyaweza, wanatarajia rehema yake na wanaogopa Adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako ndiyo ambayo inatakiwa kwa waja wawe na hadhari nayo na waiogope". [Al Israai: 57]. Na ushahidi wa kuabudiwa miti na mawe; kauli yake Mtukufu: "Mnawaonaje, enyi washirikina, waungu hawa mnaowaabudu: Lāta, 'Uzzā".





"Na mwingine wa tatu ni Manātu, je hao wamenufaisha au kudhuru mpaka wawe ni washirika wa Mwenyezi Mungu?" [An Najmi: 20, 91].


Na imesimuliwa kutoka kwa Abuu Waaqid Al laithiy Amesema Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Tulitoka pamoja na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kwenda katika vita vya Hunain, na sisi tukiwa ni wageni hatuna muda mrefu tangu kutoka katika ukafiri, na washirikina wakawa wana mti wa mkunazi ambao wanauzunguka kwa ibada na wanatundika hapo silaha zao, Mti huo ukiitwa (Dhaata anwaatwi) Yaani mahali pa kutundikia, Tukaupita mti mwingine wa mkunazi nasi tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tuwekee na sisi mahala pa kutundikia kama wao walivyo na mahala pa kutundikia, mpaka mwisho wa hadithi.


11


Msingi wa nne:


Ni kuwa washirikina wa zama zetu wanaushirikina mzito kuliko washirikina wa zamani, kwa sababu wa mwanzo walifanya ushirikina wakati wa raha, na wakimtakasa Mwenyezi Mungu wakati wa matatizo; na ushahidi ni kauli yake Mtukufu:





"Na wanapopanda makafiri kwenye majahazi baharini, na wakaogopa kuzama, wanampwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia dua wakati wa shida yao. Na anapowaokoa akawafikisha nchi kavu, na shida ikawaondokea, wanarudi kwenye ushirikina wao". [Al Ankabut: 65].


Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi. Na Rehema na Amani za Allah ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad na ali zake na Maswahaba zake.


12


Yaliyomo


........................................................................................................ 2


Muhtasari wa misingi minne. ......................................................... 3


Msingi wa kwanza: ..................................................................... 5


Msingi wa pili:............................................................................. 6


Msingi wa tatu: ........................................................................... 8


Msingi wa nne: ......................................................................... 11



Machapisho ya hivi karibuni

Uislamu Ni dini ya ma ...

Uislamu Ni dini ya maumbile na akili na furaha

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL