Nakala

SHARTI ZA SWALA NA NGUZO ZAKE NA WAJIBU WAKE


KIMETUNGWA NA SHEIKHUL ISLAM AL MUJADDID IMAMU MUHAMMADI BIN ABDIL WAHHAB -MWENYEZI MUNGU AMREHEMU-


MWAKA 1115-1206 H


AMEKIHAKIKI NA AKASHUGHULIKA NACHO NA AKAZICHAMBUA HADITHI ZAKE FAKIRI KWA MWENYEZI MUNGU MTUKUFU


DR. SAIDI BIN ALLY BIN WAHFU AL QAHTWAANIY





3


Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema na Mwenye kurehemu.


Utangulizi wa Muhakiki.


Hakika kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, tunamhimidi yeye na tunamtaka msaada yeye, na tunamuomba msamaha, na tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari ya nafsi zetu, na ubaya wa matendo yetu, aliyemuongoza Mwenyezi Mungu hakuna wa kumpoteza, na aliyempoteza hakuna wa kumuongoa, na ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, na juu ya watu wake, na maswahaba zake, na ampe amani na salamu nyingi. Baada ya hayo:


Hakika kitabu cha "Sharti za swala, na nguzo zake, na wajibu wake", cha Imamu Muhammadi bin Abdil Wahhab, ni katika vitabu vyenye faida kubwa, na hasa kwa wanaoanza kujifunza, na watu wote kwa ujumla, bali Mwenyezi Mungu kamnufaisha mtu mmoja mmoja na hata wengi kupitia kitabu hiki, kama alivyonufaisha Mtukufu kwa vitabu vyake (Sheikh) vingine nchi zote za Ardhi, na hii ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu juu yake na kwa watu.


Na alikisherehesha sheikh wetu imamu Abdul Azizi bin Abdallah bin Baazi -Mwenyezi Mungu amrehemu- kitabu hiki kitukufu katika msikiti wake ulio karibu na nyumbani kwake, alikuwa akimsomea imamu wa msikiti wake Sheikh Muhammadi Ilyasa Abdul Qaadir, na


4


hiyo ilikuwa takribani mwaka 1410 H, Akakisherehesha Mheshimiwa Sheikh kwa wenye kuswali ndani ya siku tano katika vikao vitano kati ya adhana na iqama ya swala ya ishaa, ukawa ni ufafanuzi wa kipekee, ulio hakikiwa, tena mfupi, wenye faida, na manufaa, na ilikuwa jumla ya muda alioutumia katika darsa hizi tano ni dakika tisini (90) tena katika kanda ya kaseti moja, na ikabakia kwangu muda wa miaka ishirini na tano takribani mpaka mwezi Muharram 1435H, Mwenyezi Mungu akanifanyia wepesi wa kuichambua kanda hiyo.


Na ilikuwa kazi yangu katika utaratibu ufuatao:


1- Nimeyachukua maneno ya Sheikh -Mwenyezi Mungu amrehemu- ya sauti yaliyorekodiwa katika kanda ya kaseti, sawa sawa yawe ya kitabuni ambayo hayajafafanuliwa au yaliyo fafanuliwa neno kwa neno kwa umakini mkubwa namshukuru Mwenyezi Mungu.


2- Nimekiweka kitabu ambacho hakikufafanuliwa cha sharti za swala na nguzo zake na wajibu wake katika chapa nne: Katika chapa ya msomaji ambayo alikuwa akimsomea Sheikh kama alivyoisoma, na Sheikh akisikiliza, na nikaifanya kuwa ndio asili (Original), Na katika chapa mbili nilizoziandika: Chapa ya kwanza: Ikiwa imekamilika kwa mwandiko wa wazi, na mchapaji wake ni Ibrahim bin Muhammadi Al Dhwauyan, Tarehe: 6/5/11307H, Nayo ilichukuliwa na kituo cha Mfalme Faisal cha utafiti na masomo ya kiislamu, cha Microfilm No: 5258, na nakala ya asili iko Maktaba ya msikiti Mkuu wa Unaiza huko Qassiim, Na nakala hii imekusanya machapisho matatu nayo ni: Thalathatul Usuuli, (Misingi mitatu), Na Al qawaaidil Arba'a (Kanuni nne) Na kitabu cha Kashfu shubuhaati (Kuondoa utata), Na vyote hivi ni vya mtunzi -Mwenyezi Mungu


5


amrehemu-, Na nakala ya pili iliyoandikwa katika kituo cha Mfalme Faisal, chini ya Namba: Microfilm 5265, na sehemu asilia ya nakala hii ni Maktaba ya Msikiti Mkuu wa Unaiza huko Qassiim, nayo imekusanya machapisho matatu, ni: Thalathatul Usuuli, (Misingi mitatu), Na Arba'u qawaaidi (Kanuni nne) Na kitabu cha tauhidi, na Aadabul Mashyi ila sswalaa (Adabu za kwenda katika swala), na vyote hivi ni vya mtunzi -Mwenyezi Mungu amrehemu-, Na ziko pamoja pia na kijitabu cha Aqiidatul Waasitwiya, cha Sheikhul Islaam bin Taimiya -Mwenyezi Mungu amrehemu-, Na hii nakala ya pili ni nakala ya mwaka 1338H, na mchapaji hakuandika jina lake, nayo imeandikwa kwa mwandiko wa wazi, na mzuri, lakini ina kukatikakatika kwa ibara kiasi kidogo, kuanzia katika kauli ya mtunzi: Na ushahidi ni kauli yake Mtukufu: "Na atakayefuata dini isiyokuwa ya uislamu basi hatakubaliwa. mpaka mwisho wa kauli yake Mtume ziwe juu yake amani katika nyakati mbili." Na hii nakala nimeiunganisha na nakala zingine, na nakala ya nne: ilichapishwa na chuo kikuu cha kiislamu cha Imamu Muhammadi bin Soud ambacho kilisimamia zoezi la kukisahihisha, na kuilinganisha kwake na nakala ya kimaandishi (ya mkono) 269/86: Sheikh Abdul Azizi bin Zaidi Al Rumiy, na Sheikh Swaleh bin Muhammadi Al Hasan.


3- Ninazithibitisha tofauti kati ya nakala katika maelezo ya chini.


4- Nimeziambatanisha Aya katika sura zake.


5- Nimeziwekea marejeo hadithi zote na Athari (maneno ya wanachuoni) yote.


6


6- Nimeweka dibaji za Aya, na hadithi, na athari (maneno ya Maswahaba).


7- Ufafanuzi (sherehe) hii nimeiita: "Ash sharhul Mumtaaz Lisamaahati sheikhi ibn Baazi (Ufafanuzi mzuri zaidi wa muheshimiwa Sheikh Ibn Baazi", na baada yakuwa nimemaliza ufafanuzi huo mzuri, uliotajwa hivi punde, na ukachapishwa: nimependelea niweke pekee sharti za swala, na nguzo zake, na wajibu wake katika kitabu chake pekee, na kutokana na juhudi zote alizozitumia mfafanuzi katika ufafanuzi huu mzuri; Tunataraji huenda Mwenyezi Mungu Mtukufu akaunufaisha umma; Na huenda kukifanya peke yake kikawa chepesi kukihifadhi, hasa hasa kwa wanaoanza kujifunza na wengineo, na anayependa kurejea katika sherhe (ufafanuzi) mzuri uliotajwa anarejea pia.


Na Mwenyezi Mungu Mtukufu namuomba aifanye kazi hii kuwa takasifu kwaajili ya kutaka radhi zake Mtukufu, na amnufaishe kwa kazi hii mtunzi wake Imamu Muhammadi bin Abdil Wahhab -Mwenyezi Mungu amrehemu- na mfafanuzi wake sheikh wetu Bin Baazi -Mwenyezi Mungu amrehemu-, na aifanye kwao ni katika elimu yenye manufaa, na aninufaishe nayo pia mimi katika maisha yangu, na baada ya kifo changu, na amnufaishe pia kitakayemfikia, kwani yeye Mtukufu ndiye mbora wa kuombwa, na Mwenyezi Mungu ampe rehema na ambariki Nabii Muhammadi, na watu wake na maswahaba zake wote.


7


Amekiandika Abuu Abul Rahman.


Saidi bin Ally bin Wahfu Al Qahtwaaniy


Kimehaririwa baada ya Adhuhuri siku ya juma tano 25/5/1435H.


Ukurasa wa sita katika kitabu cha kwanza namba 5258 cha kituo cha Mfalme Faisal, nacho kimehifadhiwa katika maktaba ya msikiti mkuu wa Unaiza huko Qassiim.


Ukurasa wa tano katika kitabu cha pili namba 5265 cha kituo cha Mfalme Faisal


Nacho kimehifadhiwa katika maktaba ya msikiti mkuu wa Unaiza huko Qassiim.


[Amesema mtunzi Sheikhul Islam Al Mujaddid Imamu Muhammadi bin Abdil Wahhab -Mwenyezi Mungu amrehemu-]:


8


Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema na Mwenye kurehemu.


Sharti za swala ni tisa:


Uislamu, Akili, Kupambanua, Na kuondoa hadathi (uchafu), na kuondosha najisi, na kusitiri uchi, na kuingia wakati, na kuelekea kibla, na nia.


Sharti ya kwanza: Ni uislamu na kinyume chake ni ukafiri, na kafiri amali yake haikubaliki hata kama atafanya amali gani 1, Na ushahidi ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Si katika mambo ya washirikina kuziimarisha Nyumba za Mwenyezi Mungu huku wao wanautangaza ukafiri wao wa kumkanusha Mwenyezi Mungu na wanamfanya kuwa Ana washirika. Washirikina hawa, Siku ya Kiyama, vitendo vyao vyote vitaharibika na mwisho wao ni kukaa milele Motoni}. Na kauli ya Allah Mtukufu: {Na tutayaleta yale waliyoyafanya (yanayoonekana kuwa ni mazuri na ya kidini), tuyafanye ni yenye kubatilika na kupotea}. 2.3


[Sharti]4 la pili: Akili na kinyume chake ni wendawazimu, na mwendawazimu kalamu kwake imenyanyuliwa mpaka


1 Katika nakala mbili za mkono, ya kwanza na ya pili: "Na kafiri amali yake haikubaliki, na haikubaliki swala isipokuwa kwa muislamu, na ushahidi ni kauli yake Mtukufu: "Na mwenye kutafuta dini isiyokuwa dini ya kiislamu, haitokubalika kwake naye akhera atakuwa ni miongoni mwa watu waliopata hasara", na kafiri amali yake haikubaliki, hata kama atafanya amali gani yoyote".


2 Hapa ni mwanzo wa kukatika katika baadhi ya maneno katika nakala ya pili ya mkono, na inaishia katika sharti ya tisa.


3 Al Tawba: Aya: 17.


4 katika nakala ya msomaji, na nakala ya chuo: "ya pili" hakuna neno sharti.


9


atakapojitambua, na ushahidi ni hadithi5: "Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Aliyelala mpaka aamke, na mwendawazimu mpaka ajitambue, na mtoto mpaka abalehe"6.


Ya tatu: Kupambanua na kinyume chake ni utoto, na kikomo chake ni miaka saba kisha anaanza kuamrishwa7 kuswali kwa kauli


5 Katika nakala ya msomaji, na nakala ya chuo: "Hadithi", na katika nakala ya mkono ya kwanza: "Mpaka ajitambue kwa hadithi ya".


6 kaitoa Abuudaudi, katika kitabul huduud, mlango unaomuhusu mwendawazimu anapoiba au kumjeruhi mtu, kwa namba 4405, na tamko lake: Kutoka kwa Ally -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu, kwa aliyelala mpaka aamke, na mtoto mpaka ajiotee, na mwendawazimu mpaka apate akili", na kwa mwanachuoni asiyekuwa Abuudaudi imekuja kwa lafudhi tofauti ila zinakaribiana kimpangilio kati ya aliyelala, na mwendawazimu, na mtoto, na riwaya zote ni kutoka kwa Ally -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Imamu Tirmidhiy, katika kitabul Huduudi kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, mlango wa yaliyokuja kuhusu ambaye si wajibu kwake kusimamishiwa sheria, kwa namba 1423, na Ahmadi 2/461, kwa namba 1362, na Haakim, 2/59, na akaisahihisha na akaafikiana naye imamu Dhahabiy, na wakaisahihisha kwa hadithi nyingine wahakiki wa kitabu cha Al Musnad, 2/461, na akaisahihisha mwanachuoni Al Albaaniy katika kitabu chake cha Irwaaul Ghalil, 2/5, na kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwa tamko: ya kwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema-: "Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu, kwa aliyelala mpaka aamke na kwa aliyepewa mtihani mpaka apone na kwa mtoto mpaka akue", Abuudaudi, katika kitabul Huduudi, mlango wa mwendawazimu akiiba au akamdhuru mtu, kwa namba, 4400, na Ahmadi, 42/51, kwa namba 25114, na kwa wanachuoni wengineo imekuja kwa lafudhi inayokaribiana, na wakaifanya kuwa nzuri isnadi yake wahakiki wa kitabu cha Al Musnad, 42/51, na akaisahihisha Al Albaaniy katika kitabu chake Irwaaul Ghalil, 2/4.


7 katika kijitabu cha kwanza: "Amaamrishwa kuswali" bila kuwepo neno kisha.


10


yake -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba, na muwapige kwa ajili yake wakiwa na miaka kumi, na muwatenganishe kati yao katika malazi"8.


Sharti la nne9: Ni kuondoa hadathi (uchafu), nao ni udhu unaojulikana, na sababu yake ni hadathi (uchafu usioonekana).


Na sharti zake ni kumi: Uislamu, Akili, kupambanua, na nia, na kuambatanisha hukumu zake kuwa asinuie kuikatisha mpaka twahara ikamilike10, na kumalizika kinachowajibisha (haja), na kustanji kwa maji na kwa mawe kabla yake, na utwahara (usafi) wa maji, na uhalali wake, na kuondoa yanayozuia kufika maji katika ngozi, na


8 Ameitoa Abuudaudi katika kitabu cha swala, mlango wa ni wakati gani mtoto anaamrishwa kuswali, kwa namba, 495, kwa tamko: "Waamrisheni watoto wenu kuswali nao ni wakiwa ni watoto wenye umri wa miaka saba, na muwapige kwaajili yake, nao wakiwa ni watoto wenye umri wa miaka kumi, na muwatenganishe kati yao katika malazi" Na Ahmad, 11/369, kwa namba 6756, na lafudhi yake ni: "Waamrisheni watoto wenu kuswali kwa umri wa miaka saba, na muwapige kwaajili yake kwa umri wa miaka kumi, na muwatenganishe kati yao katika malazi, na atakapomuozesha mmoja wenu mtumwa wake au muajiriwa wake, basi hakika asitazame chochote katika uchi wake, kwani kuanzia chini ya kitovu chake mpaka katika magoti yake ni katika uchi wake", na kaipokea Ahmad pia kwa namba 6689, na lafudhi yake: "Waamrisheni watoto wenu kuswali, watakapofikisha miaka saba, na muwapige kwaajili yake, watapaofikisha miaka kumi, na muwatenganisha kati yao katika malazi" kutoka kwa Amri bin Shuab kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, na wameifanya kuwa hadithi Hasan wahakiki wa kitabu cha Al Musnad, 11/369, na akaisahihisha Imamu Albaaniy katika kitabu cha Irwaaul Ghalil, 1/266.


9 Katika kitabu cha kwanza: (Ya nne) "bila kutajwa sharti", nayo iko katika nakala ya msomaji na chapa ya chuo kikuu.


10 Katika kitabu cha kwanza: imeandikwa "utwahara wake" bila kuwekwa alif na lam, na katika nakala ya msomaji kuna alif na lam, pia na katika chapa ya chuo kikuu.


11


kuingia kwa wakati11 kwa yule ambaye hadathi yake ni ya kudumu kwaajili ya kutekeleza faradhi yake.


Na ama faradhi (mambo ya wajibu) yake ni sita: kuosha uso pamoja na kusukutua na kupandisha maji puani, na mpaka wake; urefu ni kuanzia katika maoteo ya nywele za kichwa mpaka katika kidevu, na upana mpaka katika ncha za masikio, na kuosha mikono mpaka katika viwiko viwili, na kufuta kichwa kizima pamoja na masikio mawili, na kuosha miguu miwili mpaka katika fundo mbili, na kufuata utaratibu na kufululiza12, na ushahidi ni kauli yake Mtukufu: {Enyi mlioamini pindi mtakaposimama kutaka kusali, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka katika vifundo na pakeni maji vichwa vyenu (na muoshe) miguu yenu mpaka katika fundo mbili}. 13 mpaka mwisho wa Aya 14.


Na ushahidi wa kufuata utaratibu ni hadithi: "Anzeni na kile alichoanzanacho Mwenyezi Mungu"15.


11 katika kitabu cha kwanza: "Na kuingia kwa wakati".


12 katika kitabu cha kwanza ametaja baada ya kufululiza: "Na wajibu wake ni kusema Bismillah na kufanya dhikri (kusoma dua)".


13 . Maida, mpaka mwisho wa Aya 6.


14 "Aya": hii haiko katika nakala ya mkono ya kwanza wala ya pili.


15 Kaipokea An Nasaai, kitabu manaasikil Hajji, kauli baada ya rakaa mbili za twawafu (yaani kuzunguka Alka'ba), kwa namba 2962, ni katika hadithi za Jaabir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, na akaisahihisha Al Albaaniy katika kitabu Tamaamul Minna, uk.88, na kaipokea Muslim katika Hajji, mlango wa hija ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa namba 1218, kwa lafudhi ya: "Anza kwa kile alichoanzanacho Mwenyezi Mungu".


12


Na ushahidi wa kufululiza ni hadithi ya yule bwana mwenye mng'ao kutoka kwa Mtume- Rehema na Amani ziwe juu yake-: yakwamba yeye alipomuona mtu mmoja katika kisigino chake16 kuna mng'ao kiasi cha Dirhamu (yaani kiduara kidogo) hakijafikiwa na maji 17 akamuamrisha arudie18.


Na wajibu wake ni kusema Bismillaahi pamoja na kumtaja Mwenyezi Mungu19.


Na vitenguzi vyake ni vinane: Kinachotoka katika njia mbili, na kinachotoka chenye najisi mbaya 20 kutoka katika mwili, na kumgusa mwanamke kwa matamanio21, na kugusa tupu kwa mkono iwe ya


16 Katika kitabu cha kwanza: imekuja kwa neno "katika mguu wake".


17 Katika kitabu cha kwanza imekuja kwa neno: "Alimuamrisha kurudia".


18 Abuudaudi, kitabu ttwahara, mlango wa kuachanisha udhu, kwa namba 175, na Ahmad, 24/251, kwa namba 15595, kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa lafudhi: yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alimuona mtu akiswali na nyuma ya kisigino chake kuna mng'ao kiasi cha Dirham (pesa ya sarafu) haijafikiwa na maji, akamuamrisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- arudie udhu pamoja na swala, na wameisahihisha kwa hadithi nyingine wahakiki wa kitabu cha Al Musnad, 24/252, na Albaaniy katika sahihi sunani Abiidaudi, 1/310, kwa namba 168, na amenukuu bin Daqiiq Al iidiy katika kitabu Al Ilmaami, uk. 15 kutoka kwa Imamu Ahmad kwa Isnadi Jayyid, na ameipokea mfano wa hiyo Ibni Maajah katika sunani yake, kitabusswalaa, mlango wa atakayetawadha akaacha sehemu haijafikiwa na maji, kwa namba, 666, kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-.


19 Katika nakala ya mkono ya kwanza imetangulizwa sentensi hii baada ya kauli yake: "Kufululiza".


20 "Najisi" neno hili haliko katika nakala ya mkono ya kwanza.


21 Amesema Sheikh wetu bin Baazi -Mwenyezi Mungu amrehemu-: katika kitabu Al Sharhul Mumtaaz, uk.68: katika kumgusa mwanamke kwa matamanio


13


mbele22 au ya nyuma, na kula nyama ya ngamia, na kuosha maiti23, na kuritadi (kutoka katika) uislamu atukinge Mwenyezi Mungu na hilo.


Sharti ya tano24: kuondoa najisi katika sehemu tatu: mwilini, na katika nguo, na mahala pa kuswalia, na ushahidi ni kauli yake Mtukufu: "Na nguo zako zisafishe"25


Sharti ya sita: ni kusitiri uchi: Wamekubaliana wanachuoni juu ya kuharibika kwa swala ya atakayeswali uchi hali yakuwa anaweza kujisitiri, na kikomo cha uchi wa mwanaume ni kuanzia kitovuni mpaka magotini, na mjakazi pia hivyo hivyo, na aliyehuru mwili wake wote ni uchi isipokuwa uso wake, na ushahidi ni kauli yake


atakapokuwa hajatoa chochote katika madhi, au kinginecho: "Na kilicho sahihi nikuwa hilo halitengui; kwasababu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akiwabusu baadhi ya wake zake kisha wala hatawadhi" [kaipokea Ahmad katika Musnad, 42/499, kwa namba 25766, na Abuudaud, kwa namba 179, na Tirmidhiy, kwa namba 86, na wengineo, na wameisahihisha Isnadi yake wahakiki wa kitabu cha Al Musnad, 42/499, na akaisahihisha Al Albaaniy katika sahihi Abiidaud, 1/322], na ama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu "Au mkawagusa wanawake". [An Nisaai:43], Makusudio yake ni Jimai -tendo la ndoa.


22 "Alikuwa" neno hili haliko katika kitabu cha kwanza.


23 Na kilicho sahihi nikuwa kuosha maiti hakutengui udhu, ila kama utagusa mkono wa muoshaji tupu ya maiti, na akalitia nguvu hilo Sheikh wetu bin Baaz katika kitabu Sharhul Mumtaaz, uk 70.


24 Katika kitabu (kilichoandikwa kwa) mkono cha kwanza, kumeandikwa "Ya tano" bila kutajwa neno sharti.


25 . Al Furqaan: 4.


14


Mtukufu: {Enyi wanadamu chukueni pambo lenu, kila muwapo msikitini}. 26, Yaani: katika kila swala.


Sharti la saba: Kuingia wakati, na ushahidi ni kutoka katika mafundisho ya Mtume katika hadithi ya Jibril -Amani iwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- aliswalisha mwanzo wa wakati na mwisho wa wakati27, akasema: "Ewe Muhammad swala ni kati ya nyakati hizi mbili"28.


26 suratul A'raf Aya ya: 31.


27 Katika kitabu (kilichoandikwa kwa) mkono cha kwanza, kumeandikwa "Na mwisho wake" bila kutajwa neno "katika".


28 Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: Aliniongoza mimi katika ibada Jibril katika Alka'ba mara mbili, akanisalisha adhuhuri lilipopinduka jua, na lilikuwa kiasi kama cha ncha ya kiatu, na akanisalisha laasiri pale kilipokuwa kivuli chake mfano wake (kilipolingana sawa), na akanisalisha -yaani magharibi- wakati anaostahiki kufungua aliyefunga, na akanisalisha ishaa yalipopotea mawingu, na akanisalisha Alfajiri muda anaoharamishiwa kula na kunywa mwenye kufunga, ilipofika kesho yake alinisalisha Adhuhuri kivuli kilipofikia mfano wake, na akanisalisha Laasiri kivuli kilipofikia mfano wake mara mbili, na akanisalisha Magharibi wakati anaofuturu aliyefunga, na akanisalisha Ishaa mpaka theluthi ya usiku, na akanisalisha Alfajiri mpaka kukawa kwa njano, kisha akanigeukia akasema: Ewe Muhammadi, huu ndio wakati wa manabii kabla yako, na wakati wa baina ya nyakati hizi mbili", kaipokea Abuudaudi katika maudhui ya swala, mlango wa faradhi za swala, kwa namba 393, na Tirmidhiy, kitabu cha swala, mlango uliokuja kuelezea nyakati za swala, kwa namba 149, na Imamu Shafiy katika Musnad wake, 1/26, na Ahmad, kwa namba 5/202, kwa namba 3081, na Ibn Khuzaimah, 168/6, kwa namba 325, na Al haakim, 1/193, na tamko ni la Abuudaudi, na akaisahihisha Al haakim, na wakaifanya kuwa Hasan Isnad yake wahakiki wa kitabu cha Al Musnad, 5/202, na akaihakiki ibn Abdil Barri katika utangulizi, na akamjibu aliyeisema vibaya, 8/28, na akaisahihisha Al Albaaniy katika Sahihi Abiidaud, kwa namba 377. Na imethibiti katika hadithi aliyoipokea Muslim, katika kitabul masaajid wa mawaadhiu swala, mlango wa nyakati za swala


15


Na kauli yake Mtukufu 29: {Hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyowekewa wakati maalumu}. 30. Yaani: Imefaradhishwa kwa nyakati, na ushahidi wa nyakati 31 ni kauli yake Mtukufu: {Simamisha Swala itimie kuanzia kipindi cha kupinduka jua wakati wa mchana mpaka kipindi cha usiku. Na simamisha Swala ya Alfajiri na urefushe kisomo chake, kwani Swala ya Alfajiri inahudhuriwa na Malaika}. 32.


Sharti la nane: kuelekea kibla, na ushahidi ni kauli yake Mtukufu: {Hakika Tunauona 33 mzunguko wa uso wako upande wa mbinguni


tano, kwa namba 612, kuwa wakati wa swala ya Ishaa ni mpaka nusu ya usiku, na kutoka kwa Abdillahi bin Amri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtakaposali Alfajiri; basi huo ndio wakati wake mpaka inapochomoza pembe ya jua ya kwanza, kisha mtakaposali Adhuhuri; basi huo ndio wakati wake mpaka itakapofika Laasiri, mtakaposali Laasiri basi huo ndio wakati wake mpaka jua linapokuwa la njano, mtakaposali Magharibi; basi huo ndio wakati wake mpaka yatakapotoweka mawingu, mtakaposali Ishaa basi huo ndio wakati wake mpaka nusu ya usiku", Hivyo wakati wa swala ya Ishaa ni mpaka nusu ya usiku, na ndio kauli yenye nguvu zaidi na yenye kutegemewa.


29 Mwanzo wa kumalizika kwa mapungufu katika nakala ya pili iliyoandikwa kwa mkono.


30 . Al Nisaa: Aya ya: 103.


31 Katika nakala ya kwanza ya mkono kumeandikwa neno "Wakati".


32 . Israa: Aya ya: 89.


33 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Basi elekeza uso wako upande wa msikiti mtukufu" basi, na ikaondolewa sehemu ya Aya iliyobakia, ama katika nakala ya pili iliyoandikwa kwa mkono akafupisha katika kauli yake: "{Hakika


16


mara kwa mara, Basi hakika Tukuelekeze kwenye kibla unachokiridhia, Basi, elekeza uso wako upande wa msikiti Mtukufu. Na popote mtakapokuwa, (na mkataka kuswali), elekezeni nyuso zenu upande wake (Msikiti Mtukufu). 34.


Sharti la tisa ni: Nia, na mahala pake ni moyoni, na kuitamka ni uzushi, na ushahidi ni hadithi 35: "Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia" 36.


Na nguzo za swala ni kumi na nne: kusimama kwa mwenye uwezo, na takbiratul ihramu (takbira ya kuanza swala), na kusoma suratul faatiha, na kurukuu, na kunyanyuka, na kusujudu juu viuongo saba 37, na kunyooka kukiwemo, na kukaa 38 kati ya sijida mbili, na kutulizana katika nguzo zote, na kufuata mpangilio 39, na tahiyatu ya mwisho, na kukaa kwaajili ya tahiyatu, na kumswalia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-,na salamu mbili.


Tunauona [34] mzunguko wa uso wako upande wa mbinguni mara kwa mara, Basi hakika Tukuelekeze kwenye kibla unachokiridhia". mpaka mwisho wa Aya}.


34 . Al Baqara: Aya ya: 144.


35 katika nakala ya mkono ya kwanza: "Hadithi ya Omar, amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:", Ama nakala ya mkono ya pili, Akasema: "Na ushahidi: "Hakika matendo yote huzingatiwa nia".


36 Al Bukhariy, kwa namba1, na Muslim, kwa namba 1907, na imetangulia kutajwa.


37 katika nakala ya mkono ya kwanza na ya pili imekuja "Na kusujudu katika viungo saba".


38 Katika nakala ya mkono ya pili: "Na kukaa baina ya sijida mbili".


39 Katika nakala ya mkono ya pili kuna ziada: "Na kufululiza".


17


Nguzo ya kwanza: kusimama uwezo ukiwepo, na ushahidi ni kauli yake Mtukufu: {Zihifadhini, Swala (tano zilizofaradhiwa) Na muhifadhi swala iliyo katikati ya swala hizo, (nayo ni Swala ya Alasir) Na simameni katika Swala zenu hali ya kumtii Mwenyezi Mungu, kumnyenyekea na kumdhalilikia].40.41


Ya pili 42: Takbiratul Ihram, na ushahidi ni hadithi 43: "Kuihirimia kwake (kuifunga kwake) ni kusema Allahu Akbar 44, na kuifungua kwake ni salamu" 45. Na baada yake ni dua ya ufunguzi wa swala -


40 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na nakala ya mkono ya pili kumeandikwa "Na msimame kwaajili ya Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu", na ikaondolewa sehemu ya Aya iliyobakia.


41 . Al Baqara: Aya ya: 238.


42 "Ya pili": neno hili haliko katika nakala ya mkono ya kwanza.


43 Katika nakala ya chuo kikuu neno: "Hadithi", na lilisomwa kwa sheikh Hadithi, na katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili, na ushahidi katika hadithi ni kauli yake -Rehema na Amani ziwe juu yake-.


44 "Na kuifungua kwake ni kutoa salamu" Haliko katika nakala ya mkono ya kwanza, na katika nakala ya mkono ya pili: "Inafungwa kwa takbira na inafunguliwa na salamu".


45 Kaitoa Abuudaud, kitabu swalaa,mlango wa imamu akitengua udhu baada ya kunyanyua kichwa chake katika rakaa ya mwisho, kwa namba 618, na lafudhi yake: Kutoka kwa Ally -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Ufunguo wa swala ni twahara (usafi), na kuiharamisha (kuifunga) kwake ni kwa takbira, na kuifungua kwake ni kwa salamu", Na Tirmidhi, milango ya twahara kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, Mlango wa yaliyokuja kuwa; ufunguo wa swala ni twahara, kwa namba 3, Na akasema: "Hadithi ndio sahihi zaidi katika mlango huu", na bin Maajah, kitabu cha twahara na sunna zake, mlango wa ufunguo wa swala ni twahara, kwa namba 275, na Imamu Shafiy katika Kitabu chake cha Al


18


Nayo ni sunna- ni kusema 46: (Sub-hanakallahumma wabihamdika,wa tabaarakasmuka ,wa taalajadduka walaa ilaha ghairuka) -kutakasika ni kwako ewe Mola na kushukuriwa ni kwako, limetukuka jina lako, na umetukuka utukufu wako na hakuna mola mwingine zaidi yako-. Na maana ya umetakasika ewe Mwenyezi Mungu, Yaani: ninakutakasa utakaso unaolingana na utukufu wako 47. Na sifa njema ni zako, yaani: Sifa juu yako. Na limetakasika jina lako 48 Yaani: Baraka hupatikana kwa kukutaja wewe. Na umetukuka


Musnad, 34/1, na bin Abii Shaiba, 208/1,kwa namba 2378, na Ahmad, 2/292,kwa namba 1006, na Daaru Qutniy, 360/1, na Dhiyaa Al Maqdisiy katika kitabu Al Mukhtaar, 341/2, na akasema: "Isnad yake ni Hasan", Kutoka kwa Ally -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Na wakaisahihisha kwa hadithi nyingine wahakiki wa kitabu cha Al Musnad, 2/292, na Amesema Sheikh Al Albaaniy katika sahihi Abiidaud, 1/102, kwa namba 55: "Isnad yake ni Hasan Sahihi, na akaisahihisha Al Hakim na bin Sakan na vile vile Al Haafidh, Na akaifanya kuwa Hasan Imamu Nawawi, na aliiandika Al Maqdisy katika Hadithi Al Mukhtar".


46 Katika nakala ya mkono ya pili : "kauli yake".


47 Kaitoa Abuudaud, kitabu cha swala, mlango wa anayeona kuwa inafaa kufungua swala kwa Dua ya Sub-haanaka llaahumma wabihamdika, kwa namba, 775, na Tirmidhiy, kitabu cha swala, mlango wa anayoyasema mtu wakati wa kufungua swala, kwa namba 243, na bin Maajah, kitabus swalaa, mlango wa kufungua swala, kwa namba 806, kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akaisahihisha mwanachuoni Al Albaaniy katika kitabu cha sahihi Abiidaud, 3/361, na kaitoa Muslim, kitabus swalaa, mlango wa hoja ya atakayesema bismillahi haidhihirishwi, kwa namba 399, ikiwa ni Hadithi Mauquf kwa Omar kwa lafudhi ya: Kutoka kwa Abdata, yakwamba Omar bin Khattwab, alikuwa akiyadhihirisha maneno haya akisema: Sub-haanaka llaahumma wabihamdika, watabaaraka smuka, wata'ala jadduka walaa ilaaha ghairuka".


48 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: kuna neno "kwa utukufu wako ewe Allah".


19


Utukufu wako, Yaani: Utukufu wako 49. Na hapana Mola zaidi yako: Yaani: Hakuna muabudiwa Ardhini wala mbinguni kwa haki 50 zaidi yako ewe Mwenyezi Mungu.51


"Ninajikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa" 52 Maana ya ninajikinga: Yaani ninakimbilia na ninaomba hifadhi, na ninashikamana nawe ewe Allah kutokana na shetani 53: Aliyelaaniwa, aliyefukuzwa, aliwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu 54, Hanidhuru katika dini yangu, wala katika dunia yangu 55.


49 Katika nakala ya mkono ya pili kuna neno: "Na limetakasika jina lako, na umetukuka ufalme wako: Yaani: iko juu heshima yako, na limetukuka jambo lako".


50 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Na umetakasika utukufu wako: Iko juu heshima yako".


51 katika nakala ya mkono ya pili: "Haki" bila herufi baa mwanzoni.


52 Katika nakala ya mkono ya pili: ""Ninajikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa, aliyefukuzwa, aliwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu".


53 Katika nakala ya mkono ya kwanza kuna neno: "kutokana na shetani huyu".


54 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Aliwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu".


55 Kuanzia katika kauli yake: "Maana ya ninajilinda: Ninajisogeza kwake, mpaka katika kauli yake: "katika dunia yangu" haya hayako katika nakala ya mkono ya pili".


20


Na kusoma suratul faatiha ni nguzo katika kila rakaa, kama ilivyo katika hadithi 56: "Hakuna swala kwa ambaye hatosoma ufunguzi wa kitabu (suratul faatiha)" 57, nayo ndiyo mama wa kitabu.


{Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu}. 58: Baraka na kutaka msaada.


{Shukurani zote}., ni sifa, na herufi alif na lam, zinamaanisha kukusanya sifa zote, ama mzuri ambaye hana alichotengeneza mfano ubora na mfano wake, sifa kwake 59 huitwa sifa za kawaida na si shukurani.


{Mola mlezi wa walimwengu}., Mola: ni 60 Muabudiwa,Muumba, Mgawa riziki 61, Mmiliki, Mwenye maamuzi, Mlezi wa viumbe vyote kwa kuvipa neema 62.


56 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na nakala ya mkono ya pili, na chapa ya chuo: "kama ilivyo katika hadithi".


57 Kaipokea Bukhariy, kitabul Adhana, mlango wa ulazima wa kusoma kwa imamu na maamuma, kwa namba 756, kitabu cha swala, na Muslim, kitabu cha swala, mlango wa ulazima wa kusoma suratul fatiha katika kila rakaa, na kwamba mtu asipoweza kuisoma vizuri suratul faatiha, na akawa hajaweza kujifunza, atasoma kitakachokuwa chepesi kwake isiyokuwa suratul faatiha, kwa namba 394.


58 Katika nakala ya msomaji, na nakala ya mkono ya kwanza: "kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu" ama katika nakala ya mkono ya pili: ndani yake kuna: "Kauli yake: kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu".


59 "Kwalo": neno hili haliko katika nakala ya mkono ya pili.


60 "Yeye" neno hili haliko katika nakala ya mkono ya kwanza.


61 "Muumba, mgawa riziki" haliko katika nakala ya mkono ya kwanza, wala ya pili.


21


{Walimwengu}.: kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu hicho ni kilimwengu, na yeye ndiye Mola wa wote.


{Ar Rahman-mwingi wa rehema}.: Rehema za kiujumla [kwa] viumbe wote 63.


{Ar rahiim -mwenye kurehemu}.: huruma maalumu kwa waumini, na ushahidi ni kauli yake Mtukufu: "Na amekuwa kwa waumini ni Mpole mno" 64.


{Mmiliki wa siku ya malipo}.: siku ya malipo na hesabu, siku 65 ambayo kila mmoja atalipwa kwa mujibu wa matendo yake, kama yatakuwa ya kheri atapata kheri, na kama yatakuwa ya shari basi atapata shari, na ushahidi ni kauli yake Mtukufu: "Ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu?" "Kisha ni kipi kinachokujuza ni ipi siku ya malipo?" 66 Siku (ya Hesabu), hatoweza yeyote kumnufaisha yeyote. Na amri zote Siku Hiyo ni za Mwenyezi Mungu (Peke yake)". 67, Na kalizungumzia hilo Mtume Rehema za


62 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: "Mlezi wa walimwengu wote kwa neema".


63 Katika chapa ya chuo kikuu, na katika nakala ya mkono ya pili: "ni viumbe vyote", na vile vile katika nakala ya aliyekuwa akimsomea sheikh, ama nakala ya mkono ya kwanza, ndani yake: "Kwa viumbe wote".


64 . Al Ahzaab: 43.


65 "Siku": neno hili haliko katika nakala ya mkono ya kwanza.


66 Katika nakala ya mkono ya pili hakuikamilisha Aya, bali amesema: "Mpaka mwisho wa Aya".


67 Suratul Infitwaar Aya: 17-19.


22


Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Mwenye akili ni yule atakaye itathmini nafsi yake, na akafanya yale yanayofuata baada ya kifo, 68 na mpumbavu ni yule mwenye kufuata matamanio ya nafsi yake, na akawa na matumaini mengi kwa Mwenyezi Mungu" 69.


{Wewe tu tunakuabudu}. Yaani: Hatumuabudu asiyekuwa wewe, hii ni ahadi kati ya mja na Mola wake kuwa hatoabudu isipokuwa yeye 70.


{Na wewe tu tunakuomba msaada}.: Hii ni ahadi baina ya mja na 71 Mola wake kuwa asitake msaada kwa yeyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu.


{Tuongoze njia iliyonyooka}. Maana ya {Tuongoze}: Tujulishe, na tuelekeze, na utupe uthubutu 72, Na {Njia}: Ni uislamu, na


68 Katika nakala ya mkono ya pili hakuikamilisha hadithi, bali amesema: "Mpaka mwisho wake".


69 Attirmidhiy, kitabu swifatil Qiyama war raqaaiq, mlango 25, kwa namba 2459, na bin Maajah, kitabu zzuhdi, mlango wa kifo na maandalizi yake, kwa namba 4260, na Ahmad katika Musnad, 28/350, kwa namba 17123, na Haakim. 1/57, na akaisahihisha, kutoka kwa Shaddad bin Ausi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, na akaifanya kuwa Hasan Tirmidhiy, na akaitolea ushahidi Sheikhul Islami bin Taimiya, Na akaafiki kuifanya kuwa Hasan Tirmidhiy pale aliposema katika kitabu Maj-mu'ul fataawa, 8/285: "Kaipokea bin Maajah na Tirmidhiy, na akasema ni hadithi Hasan".


70 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "kuwa asimuabudu yeyote zaidi yake", na katika nakala ya mkono ya pili: "Yakuwa asimtake msaada yeyote zaidi yake".


71 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Ni ahadi baina ya mja na Mola wake", Na katika nakala ya mkono ya pili: "Ni ahadi baina ya mja na baina ya Mwenyezi Mungu kuwa asimtake msaada zaidi yake".


72 "Tuongoze: Tujulishe, na utuelekeze, na utudumishe" Ibara hii haiko katika nakala ya mkono ya pili.


23


inasemekana: Ni Mtume 73, Na inasemekana: Ni Qur'ani, na yote yako sawa. Na {Iliyonyooka}.: Ambayo haina kupinda ndani yake.


{Njia ya wale uliowaneemesha}: Njia ya walioneemeshwa juu yao, na ushahidi 74 ni kauli yake Mtukufu: {Na mwenye kukubali amri za Mwenyezi Mungu (Aliyetukuka) na uongofu wa Mtume Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, basi hao watakuwa pamoja na wale waliopewa neema na Mwenyezi Mungu miongoni mwa Mitume na wakweli wa Imani, (ambao kuamini kwao yaliyoletwa na Mitume kulikamilika kiitikadi, kimaneno na kivitendo) na mashahidi (katika njia ya Mwenyezi Mungu) na Waumini wema. Na wazuri wa marafiki wa mtu kuwa nao Peponi ni hao}.75


{Si ya wale waliokasirikiwa}.: Nao ni Mayahudi, wana elimu lakini hawakuifanyia kazi 76, Hapa unamuomba Mwenyezi Mungu akuepushe na njia yao.


{Wala waliopotea}.: Nao ni wakristo wanamuabudu Mwenyezi Mungu 77 kwa ujinga na upotovu, Hapa unamuomba Mwenyezi


73 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: "Na njia, inasemekana ni Mtume, na inasemekana ni Uislamu, na inasemekana ni Qur'ani".


74 Kuanzia katika kauli yake: "Na ushahidi -mpaka katika kauli yake: si ya wale waliokasirikiwa, na" Hili haliko katika nakala ya mkono ya pili.


75 . Al Nisaa: Aya ya: 69.


76 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: kuna neno "Wala hawakuifanyia kazi".


77 Katika nakala ya mkono ya pili limekosekana jina Mtukufu "Allah".


24


Mungu akuepushe na njia yao, na ushahidi wa waliopotea ni kauli yake Mtukufu: "Sema, hivi tukujulisheni waliopata hasara katika matendo" "Wale ambao matendo yao yalipotea katika maisha 78 ya ulimwengu- (nao ni washirikina wa watu wako na wengineo kati ya wale waliopotea njia ya sawa wasiwe kwenye uongofu wala usawa- ) na hali wao wanadhania kuwa wanayatengeneza matendo yao". 7980, Na kalizungumzia hilo Mtume Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu, kiwango cha unyoya wa mshale (Yaani: taratibu taratibu), hata watakapoingia katika shimo la kenge mtaingia. Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, (Unakusudia) Mayahudi na Manaswara? Akasema: Akina nani wengine (kama si hao!)" wameitoa maimamu wawili (Bukhari na Muslim 81.82


78 Katika nakala ya mkono ya pili: "Amefupisha akasema: "Wale amabo zilipotea (bure) juhudi zao katika maisha ya dunia"Mpaka mwisho wa Aya. mpaka katika kauli yake: "Hatuto wajali chochote siku ya kiyama (katika matendo yao)".


79 Suratula kahf, Aya mbili: 103-104.


80 Katika chapa ya chuo kikuu, na nakala ya kwanza kuna ziada: {Hao ndo ambao waliokufuru Aya za Mola wao, na kukutana naye, hivyo yakaporomoka matendo yao hatuto wajali chochote siku ya kiyama (katika matendo yao)" Suratul kahf: 105, na ndio iliyothibiti katika kisoma cha msomaji wa Mhe. Sheikh.


81 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Na katika hadithi kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ya kwamba yeye amesema" ama katika nakala ya mkono ya pili, kuna: "Na katika hadithi kutoka kwake -Rehema na Amani ziwe juu yake-".


82 Al Bukhariy, kitabul I'tiswam, Mlango wa kauli ya Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Hakika mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu", kwa namba 7320, na Muslim, kitabul Ilmi, mlango wa kufuata nyenendo za mayahudi na wakristo, kwa namba 2669, na tamko lake ni: Kutoka kwa Saidi Al khudriy kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Hakika


25


Na hadithi 83 ya pili "Wamegawanyika mayahudi katika makundi sabini na moja, na wamegawanyika wakristo katika makundi sabini na mbili, na utagawanyika umma huu katika makundi sabini na tatu, yote motoni isipokuwa moja, tukasema: ni la akina nani Ewe 84 Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: yeyote atakayekuwa katika mfano wa yale niliyonayo mimi 85 na maswahaba zangu" 86.


mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu shibri kwa shibri, dhiraa kwa dhiraa, hata wakiingia shimo la kenge mtawafuata, tukasema; Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Mayahudi na wakristo? Akasema: Ni akina nani? (kama si hao)" Na imamu Ahmad, 18/322, kwa namba, na wakaisahihisha Isnad yake wahakiki wa kitabu cha Al Musnad, 8/322, na Al Albaaniy katika silsilatul Ahaadiithi sswahiiha, 6/999.


83 Katika nakala ya mkono ya kwanza kuna: "hadithi ya pili" bila herufi wau yaani kiunganishi cha 'Na'.


84 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni la akina nani hilo" hapa kuna kutanguliza na kuchelewesha baadhi ya maneno.


85 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "yeyote atakayekuwa mfano wa yale niliyonayo na maswahaba zangu", na katika nakala ya mkono ya pili: "Yeyote atakayekuwa katika mfano wa yale ambayo mimi niko nayo na maswahaba zangu leo hii".


86 Kaipokea bin Maajah, kitabul fitan, mlango wa kugawanyika umati, kwa namba 3992, na tamko lake ni: kutoka kwa Auf bin Maaliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Wamegawanyika mayahudi katika makundi sabini na moja, kundi moja litaingia peponi, na sabini motoni, na wamegawanyika wakristo katika makundi sabini na mbili, makundi sabini na moja motoni, na kundi moja peponi, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hakika utagawanyika umma wangu katika makundi sabini na tatu, kundi moja peponi, na makundi sabini na mbili motoni" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni akina


26


Na kurukuu, na kunyanyuka kutoka katika rukuu, na kusujudu juu ya viungo saba, na kunyooka wima, na kukaa kati ya sijida mbili, na ushahidi ni kauli yake Mtukufu: {Enyi mlioamini rukuuni na msujudu}. 8788, Na kalizungumzia hilo 89 Mtume Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Nimeamrishwa nisujudu juu ya mifupa saba" 9091, Na kutulizana 92 katika vitendo vyote 93 na kufuata


nani hao? Akasema: "Ni jamaa". Na hadithi hii ina ushuhuda wa hadithi nyingine kwa Tirmidhiy, kitabul iiman, mlango uliokuja katika kugawanyika umma huu, kwa namba 2641, na tamko lake: Kutoka kwa Abdillahi bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Yataufikia umma wangu yale yaliyowafikia wana wa Israeli kiasi cha kiatu kwa kiatu (hatua kwa hatua), mpaka ikiwa miongoni mwao alikuwepo aliyekuwa akimuingilia mama yake hadharani, pia hilo atapatikana katika umma wangu mwenye kulifanya hilo, na hakika wana wa Israeli waligawanyika katika mila sabini na mbili, na utagawanyika umma wangu katika mila sabini na tatu, mila zote motoni isipokuwa mila moja", wakasema: Ni ya akina nani ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? akasema: "Ni wale watakaokuwa katika yale niliyo nayo mimi na maswahaba zangu", na ushahidi wa pili kwa Abuudaud katika hadithi za Abuu Huraira, kwa namba 4596, na tamko lake: "wamegawanyika mayahudi katika makundi sabini na moja au mbili, na wamegawanyika wakristo katika makundi sabini na moja au mbili, na utagawanyika umma wangu katika makundi sabini na tatu", nayo iko kwa Tirmidhiy, kwa namba 2640, na kwa bin Maajah, kwa namba 3991. Na akaifanya kuwa Hasan Al Albaaniy katika Kitabu Mishkatil Maswaabiih, kwa namba 171 (Uhakiki wa pili), na katika Silsilatu sswahiiha, kwa namba 1348, na katika sahihi bin Maajah, kwa namba 3982.


87 Al Haji: 77.


88 Katika nakala ya mkono ya pili kuna ziada: "Na muabuduni Mola wenu na mfanye ya kheri ili mpate kufaulu".


89 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: "Na katika hadithi kutoka kwake -Rehema na Amani ziwe juu yake-".


90 Katika nakala ya mkono ya pili: {juu ya mifupa saba}.


27


utaratibu baina nguzo, na ushahidi ni hadithi ya aliyekuwa akikosea katika swala yake, kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Wakati sisi tukiwa tumekaa kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ghafla aliingia mtu mmoja 94 akaswali, [akanyanyuka] 95, akamsalimia Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema 96: "Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali", Alifanya hivyo mara tatu kisha 97 akasema: Namuapa


91 Al Bukhariy, kitabul adhana, mlango wa kusujudu juu ya mifupa saba, kwa namba 810, na Muslim, kitabu swala, mlango wa viungo vya kusujudu na katazo la kufunga nywele na nguo, na kufunga kichwa ndani ya swala, kwa namba 490, na lafudhi yake: kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu-, kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Tumeamrishwa kusujudu juu ya viungo saba, na wala tusikunje nguo wala nywele".


92 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Na kuipangilia kila nguzo kabla ya nyingine, na kutulizana katika nguzo zote", na katika nakala ya mkono ya pili: "Na kufuatanisha baina ya nguzo, kila nguzo kabla ya nyingine, na kutulizana katika nguzo zote".


93 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: "Na kutulizana katika nguzo zote".


94 Na katika nakala ya mkono ya pili: "Ghafla aliingia kwetu sisi mtu mmoja akaswali".


95 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili, na chapa ya chuo kikuu kuna ziada: "Akasimama" na neno hili haliko katika nakala ya msomaji.


96 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Akasema Mtume kumwambia -Rehema na Amani ziwe juu yake- swali tena kwani wewe hujaswali", na katika nakala ya mkono ya pili: "Akamwambia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Rudi kaswali kwani wewe huja swali".


97 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Akasema: Namuapa yule aliyekutuma kwa haki".


28


yule aliyekutuma kwa haki kuwa Nabii, sina namna nyingine ya kufanya vizuri zaidi 98 ya hapo, basi nifundishe, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kumwambia- 99: "Utakaposimama katika swala basi toa takbira, (sema Allaahu Akbaru), kisha soma kitakachokuwa chepesi kwako katika Qur'ani, kisha rukuu mpaka utulizane ukiwa umerukuu, kisha nyanyuka mpaka ulingane sawa 100 ukiwa umesimama, kisha usujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umekaa, kisha fanya hivyo katika swala yako yote" 101, Na tahiyatu ya mwisho ni nguzo ya lazima 102, kama ilivyo katika hadithi kutoka kwa bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: tulikuwa tukisema kabla hatujafaradhishiwa tashahudi, Amani iwe juu ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa waja wake, Amani iwe juu ya Jibril, na Mikail, Na akasema 103 Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Msisema: Amani iwe juu ya Mwenyezi Mungu kutoka 104 kwa waja


98 Katika nakala ya mkono ya pili: "Siwezi kufanya vizuri tena zaidi ya hapo".


99 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Amesema: Utakaposimama katika swala", na katika nakala ya mkono ya pili: "Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Utakaposimama katika swala".


100 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: kuna neno "Mpaka utulizane wima".


101 Kaipokea Bukhariy, kwa namba 6251 kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, na kwa Muslim, kwa namba 397, na imetangulia kuelezwa.


102 "Ya wajibu": hii haiko katika nakala ya mkono ya kwanza wala ya pili.


103 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: "Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-".


104 Katika chapa ya chuo kikuu: "Kwa waja wake". Na huenda likawa ni kosa la kiuchapaji.


29


wake, kwani Mwenyezi Mungu yeye ndiye Amani 105, Lakini semeni: "Attahiyyaatulillahi, 106 Wasswalawaatu watwayyibaatu, Assalaamu Alaika Ayyuhan Nabiyyu Warahmatullahi Wabarakaatuhu, Assalaamu Alaina wa'alaa ibaadillahi swaalihiina, Ash-hadu an-laailaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullahi" 107, Tafsiri yake:


105 Katika nakala ya mkono ya pili: "Msiseme: Amani iwe juu ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa waja wake, lakini semeni: Amani ni ya Mwenyezi Mungu".


106 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili imeondolewa kuanzia katika kauli yake: "Na swala, na vilivyo vizuri, mpaka katika kauli yake: "Na kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake".


107 Kaitoa Bukhariy kitabul Adhan, mlango wa dua anazochagua mtu baada ya tahiyatu na siyo wajibu, kwa namba 835, na lafudhi yake: kutoka kwa Abdillahi bin Mas'ud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Amesema: "Tulikuwa tunapokuwa na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake katika swala, tunasema: Amani iwe juu ya Mwenyezi Mungu toka kwa waja wake, Amani iwe juu ya fulani na fulani, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: ""Msisema: Amani iwe juu ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa waja wake, kwani Mwenyezi Mungu yeye ndiye Amani, Lakini semeni: "Attahiyyaatulillahi, Wasswalawaatu watwayyibaatu, Assalaamu Alaika Ayyuhan Nabiyyu Warahmatullahi Wabarakaatuhu, Assalaamu Alaina wa'alaa ibaadillahi swaalihiina" Tafsiri yake: Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri, amani iwe juu yako ewe nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, kwani mtakaposema hivyo zitampata kila mja aliyeko mbinguni au kati ya mbingu na ardhi, na ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, kisha achague dua inayopendeka zaidi kwake, na aombe" na Muslim, kitabus swalaa, mlango wa tashahudi katika swala, kwa namba 402, na tamko lake: ni kutoka kwa Abdillah, Amesema: Tulikuwa tukisema katika swala nyuma ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: Amani iwe juu ya Mwenyezi Mungu, Amani iwe juu ya fulani, akasema kutuambia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- siku moja: "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Amani, atakapokaa mmoja wenu katika swala


30


Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri, amani iwe juu yako ewe nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, nashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mjumbe wake. Na maana ya "Tahiyyatu" (Amani): Yaani aina zote za kutukuzwa ni za Mwenyezi Mungu 108, kiufalme na kwa kuzistahiki, mfano: kuinama na kurukuu 109 na kusujudu, na kubakia, na kudumu, na yote 110 anayotukuzwa kwayo Mola Mlezi wa walimwengu hayo ni yake Mwenyezi Mungu, atakayehamisha chochote kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu basi huyo kafanya shiriki bali ni kafiri 111, na Swala maana yake: ni dua zote. Na inasemekana maana yake ni swala tano, Na vitu vizuri ni vya Mwenyezi Mungu 112: Mwenyezi Mungu ni mzuri, na wala hakubali


basi aseme: Amani ni ya Mwenyezi Mungu, na swala ni vilivyo vizuri, Amani iwe juu yako iwe Nabii na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake, Amani iwe juu yetu, na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, akisema hivyo zitamfikia kila mja mwema wa Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini, Na ninashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, kisha achague katika maombi ayatakayo".


108 "Allah": haliko katika nakala ya mkono ya kwanza wala ya pili.


109 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: kuna neno "Na kunyenyekea na kurukuu, na kusujudu".


110 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: "vyote vinavyotumika kumtukuza navyo Mola wa walimwengu".


111 "Kafiri": hili haliko katika nakala ya mkono ya kwanza wala ya pili.


112 "Ya Mwenyezi Mungu": hii haiko katika nakala ya mkono ya kwanza wala ya pili.


31


katika maneno na matendo ila mazuri yake 113, Amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake: Unamuombea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amani, na rehema 114, na baraka 115, na anayeombewa, hawezi kuombwa pamoja na Mwenyezi Mungu, Amani 116 iwe juu yetu na juu ya waja wa Mwenyezi Mungu wema: hapa unaisalimia nafsi yako na kwa kila mja mwema 117 mbinguni na ardhini, na waja wema wanaombewa, na wala hawaombwi pamoja na Mwenyezi Mungu, nashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee 118 asiye na mshiriki wake 119: Hapa unashuhudia ushuhuda wa yakini kuwa asiabudiwe katika


113 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "katika matendo na maneno isipokuwa yaliyo mazuri", na katika nakala ya mkono ya pili: "katika matendo na maneno na vitendo isipokuwa vilivyo vizuri".


114 "Rehema" neno hili haliko katika nakala ya mkono ya kwanza.


115 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Na kunyanyuliwa daraja nyingi", na katika nakala ya pili: "Na kunyanyuliwa daraja moja" ziada katika baraka.


116 Katika nakala ya chuo kikuu: "Na amani iwe juu yetu" kwa kuongezewa herufi kiunganishi 'Wau' Yaani 'Na'.


117 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: "Katika wakazi wa mbinguni na ardhini".


118 "Yeye pekee asiye na mshirika" haliko katika nakala ya mkono ya kwanza, wala ya pili.


119 Katika nakala ya mkono ya kwanza na ya pili, na chapa ya chuo kikuu kuna ziada: "Na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake".


32


ardhi 120 wala katika mbingu kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kushuhudia kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nikuwa yeye 121 ni mja wala haabudiwi, na ni Mtume hivyo hakanushwi, bali anatiiwa na anafuatwa, kamtukuza Mwenyezi Mungu kwa uja, na ushahidi ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ametakasika yule Ambaye Ameiteremsha Qur’ani, (yenye kupambanua baina ya ukweli na ubatilifu), kwa mja Wake (Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie), 122 ili awe kwa walimwengu ni muonyaji}. 123, Ewe Mwenyezi Mungu mswalie Muhammadi, [Na watu wa familia ya Muhammad] 124 kama ulivyomswalia Ibrahim [Na watu wa familia ya Ibrahim] 125 Hakika wewe ni mwingi wa kushukuriwa na mkarimu 126. Swala ya


120 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Asiabudiwe mbinguni, wala ardhini", na katika nakala ya mkono ya pili: "Asiabudiwe mbinguni na ardhini".


121 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: "Na kushuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake, na ni Mtume wake ni mja wala haabudiwi".


122 Katika nakala ya mkono ya pili hakuikamilisha Aya, bali amesema: "Ametakasika yule aliyeteremsha kipambanuzi (Qur'ani) kwa mja wake". Mpaka mwisho wa Aya.


123 . Al Furqaan, Aya: 10.


124 "Na juu ya watu wa Muhammadi" neno hili haliko katika nakala ya msomaji, nalo liko katika chapa ya chuo kikuu, na katika nakala mbili za mkono ya kwanza na ya pili.


125 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "kama ulivyotia rehema juu ya watu wa Ibrahim" ama katika nakala ya mkono ya pili kuna: "kama uvyotia rehema juu ya Ibrahim", na katika nakala ya chuo kikuu, na katika nakala ya msomaji: "Kama ulivyompa rehema Ibrahim".


126 Bukhariy, kitabu Ahaadithul Anbiyaa, mlango wa 10, kwa namba 3370, na Muslim, kitabu swalaa, mlango wa kumswalia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu


33


kutoka kwa Mwenyezi Mungu: Ni kumsifia kwake 127 mja wake kwa viumbe walioko juu, kama alivyosimulia imamu Bukhari -Mwenyezi Mungu amrehemu- katika sahihi yake kutoka kwa Abil Aaliya Amesema: swala ya Mwenyezi Mungu ni kumsifia kwake mja wake kwa viumbe walioko juu 128129, na inasemekana maana yake ni rehema, na sahihi ni hiyo kauli ya mwanzo, na swala kutoka kwa Malaika ni: ni kumuombea msamaha, na kutoka kwa wanadamu: ni


yake- baada ya tahiyatu, kwa namba 406, na tamko lake: Kutoka kwa Ka'bu bin Ujza -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Tulimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni namna gani tutawaombea rehema nyinyi watu wa nyumba yako, kwani Mwenyezi Mungu ametufundisha ni namna gani tutawasalimia, Akasema: "Semeni: Ewe Allah shusha rehma juu ya Muhammadi na ali zake (familia yake) Muhammadi kama ulivyo shusha juu ya Ibrahim na watu wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye sifa tukufu, na mwenye utukufu, na shusha baraka juu ya Muhamad na watu wa Muhammadi kama ulivyo shusha baraka juu ya Ibrahim na watu wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye sifa tukufu na mwenye utukufu".


127 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Ni sifa kwa mja wake mbele ya walioko juu", na katika nakala ya mkono ya pili, na chapa ya chuo kikuu: "Ni kumsifia kwake mja wake".


128 Katika nakala ya mkono ya kwanza, na ya pili: "Kutoka kwa Abul Aaliya: Ni kumsifia Mwenyezi Mungu mja wake kwa walioko juu".


129 Bukhariy, kitabut Tafsiir, mlango wa kauli yake Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake humswalia Nabii (Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake-) Enyi mlioamini mswalieni na mumtakie amani juu yake kwa wingi". kabla ya namba: 4797, na tamko lake: "Amesema Abul Aaliya: "Swala ya Mwenyezi Mungu: ni kumsifia juu yake mbele ya Malaika, na swala ya Malaika ni kumuombea dua".


34


dua, na neno umbariki na yale yanayofuata baada yake 130 ni sunna ya maneno na vitendo.


Na mambo ya wajibu ni manane: Ni takbira zote isipokuwa ile ya kuhirimia (kuanza swala), na kauli: Sub-haana Rabbiyal A'dhwiim, (Ametakasika Mola wangu Mtukufu) katika rukuu, na kauli: Samiallaahu liman hamidah (kamsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi) kwa Imamu na mwenye kuswali peke yake, na kauli ya Rabbanaa walakal hamdu (Mola wetu sifa njema ni zako) kwa wote, na kauli: sub-haana Rabbiyal A'laa (Ametakasika Mola wangu aliye juu) katika sijida, na kauli: Rabbighfirlii (Mola wangu nisamehe) baina ya sijida mbili, na tahiyatu ya kwanza, na kikao kwaajili yake.


Hivyo nguzo 131 ni ile ambayo ikikosekana kwa kusahau au kwa makusudi, swala inabatilika kwa kuiacha kwake, na mambo ya wajibu, ni yale ambayo yakikosekana kwa makusudi, swala itaharibika kwa kuyaacha kwake, na kwa kusahau yanafidiwa na sijida ya kusahau 132. Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi. [Na rehema na amani za Allah ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad na ali zake na Maswahaba zake, na ampe amani nyingi] 133.


130 Katika nakala ya mkono ya kwanza: "Na yale yanayofuata baada yake katika dua".


131 Katika nakala ya mkono ya pili : "Na nguzo".


132 Ibara ya nakala ya mkono ya kwanza na ya pili: "Na mambo ya wajibu ni yale yatakayokosekana kwa kusahau, yakafidiwa na sijida ya kusahau, na kwa makusudi swala inabatilika", na katika nakala ya mkono ya pili kuna ziada "Kwa kuyaacha kwake".


133 Na maneno yaliyowekwa katika mabano ni ziada katika nakala ya mkono ya pili.


35


Yaliyomo


SHARTI ZA SWALA NA NGUZO ZAKE NA WAJIBU WAKE .............. 1


Utangulizi wa Muhakiki. ..................................................... 3


Na ilikuwa kazi yangu katika utaratibu ufuatao: ............. 4


Sharti za swala ni tisa: ........................................................ 8



Machapisho ya hivi karibuni

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI

KWANINI UISLAMU? UZU ...

KWANINI UISLAMU? UZURI NA FAIDA ZA UISLAMU