Nakala

“Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo” (Kurani 7:12)





         Mwanzo wa historia ya ubaguzi.  Shetani alijiona mkubwa kwa Adam kwasababu ya asili yake. Kuanzia siku ile, Shetani amekipoteza kizazi cha Adam katika kuwaaminisha kuwa wao ni bora kwa wengine, iliyo wasababishia kutesa na kuwanyonya wengine. Mara nyingi, dini imekuwa ikitumiwa kuhalalisha ubaguzi.  Uyahudi, kwa mfano, licha ya kuwa na asili ya Mashariki ya Kati, uchukuliwa kama dini ya Kimagharibi; Ila kuingia kwa wayaudi kwenye viwango vyote vya jamii ya kimagharibi hakika inasaliti ukweli wa mafundisho ya kiyaudi.  Maandiko matakatifu ya aya ya biblia:


“Akuna Mungu duniani kote ila ndani ya Israel.” (2 Kings 5:15)





…Ingependekezwa kuwa katika siku hizo za Mungu, au Mungu, akuabudiwa ila tu kwa waisraeli.  Ila, leo Uyaudi umebaki katikati ya kujisifu kuwa 'wateule' wa asili kwa ubora .





“Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasipo kuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa mnasema kweli.’” (Kurani 62:6)





Kwa upande mwingine, Wakristo wengi sio wayaudi, Yesu, kama mtume wa mwisho wa waisraeli, hakutumwa kwa watu wengine bali wajaudi.[1]





“Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad[2]...’” (Kurani 61:6)





Na kadhalika, kila Mtume alitumwa mahususi kwa watu wake,[3]  Kila Mtume, kwa maana hiyo, isipokuwa Muhammad.





“Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote…’” (Kurani 7:158)





Kwa Muhammad kuwa Mtume wa mwisho wa Mungu na Mjumbe, misheni yake ilikuwa ya ulimwengu wote, alikusudiwa sio tu kwa watu wa taifa lake, Waarabu, ila kwa watu wa ulimwengu wote.  Mtume amesema:





“Mitume mingine walitumwa mahususi kwa watu wao, bali mimi nimetumwa kwa watu wote.” (Saheeh Al-Bukhari)





“Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui.” (Kurani 34:28)





Bilal Muhabeshi


Mmoja wa watu wa kwanza kuukubali Uislamu alikuwa mtumwa wa Kiabeshi aliyeitwa Bilal.  Kikawaida, Waafrika weusi walikuwa watu wa chini katika mtazamo wa Waarabu ambao waliwaona kuwa na matumizi madogo ya burudani na utumwa.  Pindi Bilal aliukubali Uislamu, bwana wake wa kipagani alimfanya ateswe vibaya kwenye joto kali la jangwani hadi Abu Bakr, rafiki wa karibu wa Mtume, alimwokoa kwa kununua uhuru wake.





Mtume alimchagua Bilal kuwaita waumini kwenye sala.  Athan ilisikika kutoka kwenye kila kona ya ulimwengu toka wakati huo, mwangwi wa maneno sawa sawa yaliyosomwa na  Bilal.  Hivyo, hapo mwanzoni mtumwa alipata heshima kama muezzin wa kwanza katika Uislamu.





“Na hakika Tumewatukuza Wanaadamu...” (Kurani 17:70)





Utukufu wa magharibi unasifu Ugiriki ya kale kuwa eneo la uzao wa demokrasia.[4]  Ukweli ni kwamba, kama watumwa na wanawake, idadi kubwa ya Waatheni walinyimwa haki ya kuchagua watawala wao.  Ila, Uislamu uliamuru kuwa mtumwa anaweza kuwa mtawala! Mtume Aliamuru:





“Mtii mtawala wako hata kama atakuwa mtumwa wa Kiabeshi.” (Ahmad)





Salman Muajemi


Kama watu wengi wa taifa lake, Salman alilelewa katika dini ya Majusi.  Ila, baada ya kukutana na Wakristo katika kuabudu, aliukubali Ukristo kama ‘kitu bora’.  Kisha Salman alisafiri mara nyingi akitafuta maarifa, kutoka kwa mtawa mmoja wa huduma hadi mwingine, wa mwisho alisema: ‘Mwanangu! simjui mtu yoyote mwenye (imani) sawa na sisi . Ila, wakati wa kuja kwa Mtume umewadia.  Mtume huyo yupo ndani ya dini ya Abrahamu.’  Mtawa kisha akaendelea kumwelezea Mtume huyo, wasifu wake na wapi atatokea.  Salman akaenda Uarabuni, ardhi ya utabiri, na alipomsikia na kukutana na Muhammad, haraka sana akamtambua kutokana na wasifu walioutoa walimu wake na akaukubali Uislamu.  Salman alijulikana kutokana na maarifa yake na alikuwa mtu wa kwanza kutafsiri Kurani kwenda kwenye lugha nyingine, Kiajemi.  Katika kipindi kimoja, Mtume alipokuwa na Maswahaba wake, alifunuliwa yafuatayo:





“Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma... Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao...” (Kurani 62:2-3)





Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kisha akaweka mkono wake kwa Salman na kusema:





“Hata kama Imani ingekuwa karibu na (nyota ya) Kilimia, mtu kutoka (Wahajemi) hakika ataipata.” (Saheeh Muslim)





Suhayb Mrumi


Suhayb alizaliwa katika upendeleo ndani ya nyumba ya kifahari ya baba yake, ambaye alikuwa gavana kwaajili ya utawala wa Kiajemi.  Alipokuwa bado mdogo, Suhayb alikamatwa na watembezi wa Byzanti na kuuzwa utumwani ndani ya Konstantinopoli.





Hatimaye, Suhayb alitoroka kutoka utumwa na akakimbilia Makka, sehemu maarufu ya hifadhi, ambapo karibuni atakuwa mfanyabiashara tajiri kwa jina lingine ‘ar-Rumi’, Mrumi, kwasababu ya ulimi wake wa Byzantini na malezi. Pindi Suhayb aliposikia Muhammad anafundisha, mara moja akashawishiwa na ukweli wa ujumbe wake na akaukubali Uislamu.  Kama Waislamu wote wa mwanzo, Suhayb aliteswa na wapagani wa Makka.  Hivyo, aliuza utajiri wake wote kwaajili ya kuungana na Mtume huko Madina, Ambapo Mtume, alifurahi kumuona Suhayb, akamsalimu mara tatu: ‘Biashara yako imezaa, Wewe [Suhayb]!  Biashara yako imezaa!’  Mungu alimtaarifu Mtume kitendo cha Suhayb’s kabla ya kukutana na ufunuo huu:





“Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.” (Kurani 2:207)





Mtume alimpenda Suhayb kuwa jambo kubwa na alimwelezea kuwa Mrumi mwanzilishi wa kuingia kwenye Uislamu.  Uchamungu wa Suhaybthat na kusimama pamoja na Waislamu wa mwanzo ulikuwa juu pindi Caliph Umar alipokuwa kwenye kitanda cha mauti, alimchagua Suhayb kuwaongoza hadi atakapopatikana mrithi.





Abdullah Myahudi


Wayahudi walikuwa nchi nyingine ambayo iliwadharau Waislamu Wakiarabu wa mwazo.  Wayahudi wengi na Wakristo walikuwa wakimsubiri Mtume mpya kutokea ndani ya Uarabuni katika kipindi cha Mtume Muhammad.  Wayahudi haswa kabila la Walawi walikuwa kwa idadi kubwa katika mji wa Medina.  Ila, Pindi Mtume aliyetarajiwa alipofika, Sio Myahudi mwana wa Israeli, ila Muarabu mzao wa Ishmaeli, Wayahudi wakamkataa.  Isipokuwa, haikuwa, kwa wachache kama Hussein ibn Salam.  Hussein alikuwa Mrabbi msomi sana na kiongozi wa Wayahudi Madina ila  alishutumiwa na kudhalilishwa na wao alipoukubali Uislamu.  Mtume alimpa jina Husayn, ‘Abdullah’, likiwa na maana ya ‘Mtumishi wa Mwenyezi Mungu’, na kumpa ubashiri wa kuingia peponi.  Abdullah aliwaambia watu wa kabila lake:





‘Enyi mayahudi!  Mjueni Mwenyezi Mungu na kubalini alicholeta Muhammad.  Kutoka Kwa Mungu!  Kwa hakika mnajua ni Mjumbe wa Mungu na mnaweza kupata utabiri wake kuhusu yeye na utajo wa jina lake na wasifu wake ndani ya Torati.  Mimi ninakubali ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.  ninaimani nae na ninamuamini ni mkweli.  Mimi (peke yangu) nimemtambua.’  Mungu anafunua yafuatayo kuhusu Abdullah:





“na akashuhudia shahidi miongoni mwa Wana wa Israili juu ya mfano wa haya, na akaamini, na nyinyi mnafanya kiburi?.” (Kurani 46:10)





Hivyo, katika vyeo vya Maswahaba wa Mtume Muhammad wanapatikana  Waafrika, Waajemi, Warumi na Waisraili; wawakilishi wa kila bara linalojulikana.  Kama Mtume alivyosema:





“Hakika, marafiki zangu na wahirika wangu sio kabila hili wala lile.  Ila, marafiki zangu na washirika wangu ni wachamungu, Popote walipo.” (Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim)Undugu huu wa kilimwengu unaohubiriwa na uislamu ulitetewa na maswahaba wa mtume baada yake. Pindi Sahaba, Ubada ibn as-Samit,  alibeba ujumbe kwenda  Muqawqis, askofu mkuu wa Kikristo wa Alexandria, barua ilisema: ‘Mtoe mwanaume huyu mweusi kwangu na mlete mwingine badala yake azungumze na mimi! ...  Mnawezaje kukubali mtu mweusi awe bora zaidi yenu?  Je, haifai zaidi awe chini yenu?’  ‘Kwa hakika hapana!’, Ndugu wa Ubada wakajibu, ‘Japokuwa yeye ni mweusi kama unavyoona, yeye bado ni wa kwanza kati yetu kwenye uongozi, akili na hekima; kwa weusi haudharauliki kati yetu.’





“Hakika, waumini ni ndugu...” (Kurani 49:10)





Ni Haji, au safari ya Makka, ambayo inabaki kuwa ishara ya msingi ya umoja na undugu kwa mwanadamu.  Hapa, tajiri na masikini kutoka nji zote husimama na kuinama kwa umoja mbele ya Mungu katika makutano makubwa ya mwanadamu; kushuhudia maneno ya Mtume aliposema:





“Hakuna mbora kwa Mwarabu juu ya asiyekuwa Mwarabu; au asiyekuwa mwarabu juu ya Mwarabu; au kwa mtu mweupe juu ya mtu mweusi; au mtu mweusi juu ya mtu mweupe; Ila tu kwa njia ya uchamungu.” (Ahmad)





Na hii inasadikisha Kurani, inaposema:





“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi.…” (Kurani 49:13)





Kuhusu utaifa, na mgawanyiko kwa Waislamu kulingana na mstari wa utaifa na kabila, inachukuliwa na uvumbuzi mbaya.





“Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.” (Kurani 9:24)





Mtume anasema:





“... Yeyote mwenye kupigana chini ya bendera ya vipofu, anakuwa na hasira juu ya utaifa, akiuita utaifa, au kusaidia utaifa, na akafa: basi amekufa kifo cha jahiliyya (mf. ujinga kabla ya uislamu na asiyeamini).” (Saheeh Muslim)





Ila, Kurani inasema:





“Pale walio kufuru walipo tia katika nyoyo zao hasira, hasira za kijinga-hasira na hasira za kijinga za jahiliyya, Mwenyezi Mungu aliteremsha utulivu juu ya Mtume wake na juu ya Waumini…” (Kurani 48:26)





Hakika, waislamu ndani yao na wenyewe wanaunda mwili mmoja na taifa kuu,kama ilivyoelezwa na Mtume:





“Mfano wa Walioamini katika upendo wao na huruma ni kama wa mwili ulio hai: kama sehemu moja ikisikia maumivu, mwili wote utateseka kwa kutokulala na homa.” (Saheeh Muslim)





Kurani inathibitisha umoja huu:





“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani...” (Kurani 2:143)





Labda moja wapo cha kikwazo kikubwa cha kutoukubali Uislamu kwa Wamagharibi wengi ni uzushi kuwa msingi wa dini ni kwaajili ya Wamashariki au watu wenye ngozi nyeusi.  Hakuna shaka, ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi wengi,  kuwa watumwa wa Abyssinia Waarabu kabla ya Uislamu, au karne ya 20 Waafrika wa kimarekani, waliwataarifu wengi kuukubali Uislamu.  Ila hii ni nje ya mada.  Mtume Muhammad alikuwa ni mweupe, alivyoelezewa na maswahaba zake kuwa ‘mweupe na mwekundu’ - wasifu wa mamia na mamilioni ya Waarabu, Berber na Waajemi wnafanana.  Hata blondi wenye macho ya bluu sio nadra sana kwa watu wa Wamashariki.  Zaidi, Ulaya ina Waislamu wenye asili nyeupe zaidi ya waamiaji weusi’ .  Wabosnia, kwa mfano, ambao idadi yao ilipunguzwa katika karne ya 20 ila, kwasababu ya ushujaa wao na uvumilivu, imechangia Balkan kuwa yenye utulivu na amani.  Waalbania pia, waliotokana na WaaIllyrian wa ulaya, pia wengi wao ni Waislamu.  kwa hakika, Moja ya wasomi wa Kiislamu wa karne ya 20, Imam Muhammad Nasir-ud-Deen al-Albani, alikuwa, kama jina linavyojieleza, Mualbania.





“Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.” (Kurani 95:4)





Watu weupe wamekuwa wakiitwa ‘Wazungu’ tangu wana anthropojia walipotangaza milima ya wazungu, nyumbani mwa vilele vya juu zaidi vya Uropa, kuwa ‘Chimbuko la Asili Nyeupe.’  Leo, wenyeji wa milima hii ni Waislamu.  Moja ya makabila ya uchache sana  ni wafuasi wa milimani na wasichana wa Kizungu wanaojulikana kwa ujasiri na uzuri na ambao, kama mtawala wa Mamluke wa Syria na Egypt, alisaidia kutetea ulimwengu ulioendelea na kulinda ardhi yake takatifu kutokana na uharibifu wa vikosi vya Wamongoli.  Pia kuna Wachenchen walio tendewa ukatili bila shaka ni watu dhaifu kuliko viumbe vyote wa Mungu, ambao kwa ushupavu na upingaji wamesaidia hatma ya Wazungu.  Muda huo huo, zaidi ya Wamarekani 1,000,000 na Wazungu weupe wa Ulaya ya Kaskazini - Waanglo-Wasaxon, Franks, Wajerumani, Wascandinavia na Wacelt wakiwemo - sasa wanaukubali Uislamu.  Hakika, Uislam umeingia kiamani sehemu ya Ulaya kabla ya Ukristo, tangu: ‘Muda wingi uliopita, tangu Slav wa Kirusi hajaanza kujenga makanisa ya Kikristo Oka au kuchukua maeneo haya kwa jina la Ulaya, Bulgar ilikuwa inasikiliza Kurani kwenye benki za Volga na Kama.’ (Solov’ev, 1965) [mnamo 16 Mei 922, Uislamu ukawa dini rasmi ya taifa la Volga Bulgars, ambapo leo Wabulgaria wanashirikiana kwa asili hii.]





Kila imani ila Uislam inataka ibada ya uumbaji wa aina flani,umbo au taswira.  Zaidi, asili na rangi ina jukumu kubwa la kugawanya karibu katika mifumo yote ya imani isiyo ya Kiislamu.  Ukristo maana ya Yesu na santi au Buddist  katika maana ya Buddha na Dalai Lamas wana watu wa jamii flani na rangi huabudiwa katika kumdharau Mungu.  Ndani ya Uyahudi, ukombozi unazuiliwa na mtu asiye Myahudi.  Mfumo wa tabaka wa Kihindu vivyo hivyo huangalia matarajio ya kiroho, kijamii na kisiasa na kiuchumi dhana ya 'uchafu’ tabaka la chini.  Uislamu, hivyo hivyo, unatafuta kuwaonganisha na kuwafanya kiumbe mmoja wa ulimwengu katika ushirikiano na umoja wa Muumba wao.  Hivyo, Uislam pekee ndio unaokomboa watu wote, asili na rangi katika kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke yake.





“Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi.” (Kurani 30:22)



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI