Nakala

1


MATINI YA AKIDA YA TWAHAWIYA


Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; Mwanazuoni mkubwa Huja Al-Islaam Abuu Jafar Al-Waraaq Al-Twahawiyu wa Misri Allah amrehemu amesema: Nyaraka hizi ni ukumbusho unaobainisha itikadi ya Ahlu Sunna wal-jamaatu, na yale wanayoyaamini na kuyatekeleza kwa Mola wa viumbe vyote, miongoni mwa misingi ya dini kwa mujibu wa madhehebu ya wanazuoni wa Kiislamu wafuatao: Abuu Hanifa Al-Nuumani bin Thaabit Al-Kuufiyu, Abuu Yusufu Yakubu bin Ibrahim Al-Answaariyu na Abuu Abdallah Muhammad bin Al-Hassan Al-Shaybaaniyu Allah awawie radhi wote. Juu ya tauhidi Katika kumpwekesha Munguu tunasema (1) kwa kujiamini


1 Mwandishi aliposema: (Katika kumpwekesha Munguu tunasema… hadi mwisho wake). Fahamu kuwa upwekeshaji aliouleta Allah kwa mitume na akateremsha kwa ajili hiyo vitabu, kwa mujibu wa utafiti wa maandiko ya Quran na Suna na kwa mujibu wa hali halisi ya wanadamu, unagawanyika kwa aina tatu.


Aina ya kwanza: Tauhidi ya Rububiya (Mola Mlezi na Muumba): Nayo ni kumpwekesha Allah Mtukufu kwa matendo yake. Nayo ni kumwamini Allah, kuwa yeye ndiye Muumba, Mpaji riziki, Mpangaji wa mambo ya viumbe vyake, Yeye ni Mpangaji wa vitu vya viumbe duniani na akhera hana mshirika katika hayo kama alivyosema Allah Mtukufu: “Allah ni Muumba wa kila kitu” Surat Zumar aya ya 62, pia Allah mtukufu akasema: “Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambayeameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha mambo yote…” Surat Yunus aya 3. Na aina hii ya tauhidi, wameikiri washirikina wanaoabudu masanamu na kama wengi wao watapinga kufufuliwa na kukusanywa basi kukiri kwao huku hakutowaingiza katika Uislamu. Kwa kuwa wanamshirikisha Allah katika ibada pia wanaabudu masanamu pamoja na Allah mtukufu, pia hawamwamini Mtume Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake.


Aina ya pili: Tauhidi ya Ibada kukiri uungu wa Allah, pia huitwa Tauhidi ya Uungu: Nayo ni kuabudu, aina hii ndiyo iliyopingwa na washirikina pale Allah Mtukufu alipowataja kwa kusema: “Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anayetokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo. Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu. Surat Swaadi 4 – 5. Kuna aya nyingi kama hizi. Aina hii za tauhidi inajumuisha kutakasa nia katika kumwabudu Allah peke yake, kuamini kuwa Allah pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa na ibada ya kuabudu visivyokuwa yeye ni batili. Na hii ndio maana ya La Ilaha Illa Llaha, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah, kwani maana yake ni kuwa hakuna mwabudiwa ila Allah kama alivyosema Allah Mtukufu aliyetukuka: “Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Wa Kweli, nakwamba wale wanao waomba badala yake, ni baat'ili, nahakika Mwenyezi Mungu ndiye Aliye Juu na ndiye Mkubwa.” Al-Haji 62.


Aina ya tatu: Tauhidi ya Majina na Sifa za Allah: Nayo ni kuamini kila kilichokuja katika kitabu cha Allah Mwenye nguvu na hadithi sahihi za Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa majina na sifa za Allah, kuzithibitisha kuwa ni za Allah Mtukufu kwa namna inayostahiki kwake bila ya kupotosha wala kuzisitisha, bila


2


ya kuwa Allah atatuwezesha. Hakika Allah ni mmoja hana Mshirika, hakuna kinachofanana naye, hakuna kinachomshinda na hakuna Mungu kinyume na yeye.


Wa tangu na tangu bila ya kuwa na mwanzo ( 2 ) . Ni wa daima bila kikomo, hamaliziki wala hatoweki, na hakitokei chochote ila akitakacho, hafikwi na fikra potofu wala hatambuliki undani wake kwa milango ya fahamu, na Hashabihiani na viumbe / wanadamu, Yu hai hafi, Yu macho


kumjaalia Allah kuwa ana namna wala mfano, kama alivyosema Allah Mtukufu: “Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja.” Surat Al-Ikhlaswi. Pia Allah Mtukufu amesema: “Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” Al-Shura 11. Pia Allah Mtukufu amesema: “Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo.” Surat Al-Aarafu 180. Pia Allah Mtukufu amesema katika surat : “…na MwenyeziMungu ndiye Mwenye sifa tukufu. Naye ni Mwenye nguvuna Mwenye hikima.” Surat Al-Nahli 60. Aya zenye maana hii ni nyingi sana. Na sifa tukufu ndio sifa ya hali ya juu kabisa isiyo na upungufu. Na hii ndio kauli ya Ahlu sunna waljamaatu kuanzia Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yao na wale waliowafuata kwa wema wanazipitia aya na hadithi za sifa kama zilivyokuja. Na wanathibitisha maana zake kwa Allah Mtukufu kwa uthibitisho ambao ameepukana na kumfananisha, huku wakimtakasa Allah Mtukufu na kufanana na viumbe vyake, na hao Ahlu sunna waljamaatu ndio wale waliotajwa katika kauli ya Allah Mtukufu: “Na wale walio tangulia, wa kwanza, katikaWahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema,Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhikanaye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake,wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” Sura At-Tawbah 100. Allah ametujaalia sisi kwa kutupatia neema na karama zake kutokana na wao, na Allah ndio wa kuombwa msaada.


2 Aliposema (Wa tangu na tangu bila ya kuwa na mwanzo) Tamko hili halijakuja katika majina matukufu ya Allah kama ilivyobainishwa na mshereheshaji Allah amrehemu, na wengineo. Hakika si jinginelo tamko hili limetajwa na wanazuoni wengi wa elimu ya Tauhidi ili wathibitishe uwepo wa Allah kabla ya kuwepo vitu vyote kwa kutumia tamko hili, kwa hakika majina ya Allah ni ya kimapokeo na haifai kuthibitisha chochote miongoni mwa majina yake ila kwa maandiko ya Kitabu kitukufu au Hadithi sahihi. Na haifai kuthibitisha chochote miongoni mwa majina yake kwa kutumia rai kama walivyosema wanazuoni wa zama za njema. Na tamko Wa tangu na tangu halijulishi maana iliyokusudiwa na wanazuoni wa tauhidi, kwa kuwa lenyewe kwa lugha ya Kiarabu linakusudia mtu aliyemtangulia mwingine ijapokuwa ametanguliwa na kutokuwepo kama ilivyo katika kauli ya Allah Mtukufu: “…mpaka unakuwa kamakarara kongwe”. Yasini 39. Na hakika si jinginelo tamko hili linajulisha maana ya haki kwa ile ziada iliyotajwa na mwandishi pale aliposema (Wa tangu na tangu bila ya kuwa na mwanzo). Lakini hata hivyo halipaswi kuhesabiwa kuwa ni miongoni mwa majina matukufu ya Allah, kwa kuwa halijathibiti katika maandiko pia kuna jina la Allah Mtukufu lenye maana hiyo, kama alivyosema Allah Mtukufu aliyetukuka: “Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho …” Surat Al-Hadidi 3 Na Allah ndiye anayetawalia kuwafikisha.


3


halali, Ni Muumba bila ya kuwa na haja, na Mwenye kutoa riziki bila Kusaidiwa, Anafisha bila kuhofia, Anafufua bila tabu, Ni mwenye kuwa na sifa zake hizo hizo tangu na tangu kabla ya viumbe vyake, hakuna sifa iliyozidi kwa Allah kwa kuwepo viumbe – sifa ambayo haikuwapo kabla ya kuwepo viumbe, kama alivyo na sifa zake ni za tangu na tangu, vivyo hivyo zitaendelea kuwa za milele, baada ya kuumba viumbe hajafaidika kulipata jina la (Muumba), na kwa kuanzisha viumbe hajafaidika kulipata jina la (Mwanzilishi / Muumba), Ana maana ya kuwa ni Mola Mlezi bila ya kuwepo kwa viumbe wa kuwalea, na Ana maana ya kuwa Muumba bila ya kuwepo kwa viumbe alivyoviumba. Yeye ni mfufuaji wa maiti baada ya kuwahuisha. Amestahiki jina hili kabla ya kuwahuisha, pia amestahiki jina la Muumba kabla ya kuwaumba, na haya ni kwa kuwa yeye ni Muweza wa kila kitu huku kila kitu ni fakiri mbele ya Allah.


Kila jambo ni lepesi kwake, haitaji kitu (Hafanani na …) Ameumba viumbe kwa elimu yake, na kuwakadiria makadirio yao, na kuwawekea miisho yao, hakuogopa chochote kabla ya kuwaumba, ameyajua watakayoyafanya kabla hajawaumba, akawaamrisha wamtii, akawakataza wasimuasi, kila kitu kinaenda kwa makadirio na matakwa yake, matakwa yake yanatekelezwa, hakuna matakwa kwa waja zake, ispokuwa yale aliyoyataka yawe kwa viumbe miongoni mwa alivyovitaka na vikawa, na vile asivyovitaka viwe havikuwa.


Humwongoza amtakaye, na kumkinga na kumponya kwa ukarimu wake, humpoteza amtakaye, anadhalilisha na kutoa mitihani kwa uadilifu, na wote wamo katika mabadiliko mabadiliko kwa matakwa yake, baina ya fadhila na uadilifu wake, ametakasika na vinyume pamoja na washirika, hakuna wa kuzirejesha hukumu zake, hakuna wa kuzitolea maelezo hukumu zake, wala mwenye kuzishinda amri zake. Tumeamini haya yote na tumeyakinisha kuwa haya yote yanatoka kwake na Hakika Muhammadi ni Mja wake Mteule, ni nabii wake alimujtaba na ni nabii wake mwenye kuridhiwa. Naye ni nabii wa mwisho miongoni mwa manabii, imamu (kiongozi) wa wachamungu, bwana wa mitume, kipenzi cha Mola wa viumbe wote, na madai yote ya kupewa utume baada yake ni upuuzi na kuangamia, yeye ni mwenye kutumwa kwa majini na wanadamu wote kwa haki na uongofu, kwa nuru na mwangaza, na kwa hakika Qurani ni maneno ya Allah, yameanza kwake bila ya kuwa na namna nayo ni kauli, ameiteremsha kwa mjumbe wake ikiwa ni ufunuo, na waumini wakaisadiki hivi ilivyo kwa haki kabisa, wameyakinisha kuwa Qurani ni maneno ya Allah ya hakika, haijaumbwa kama yanavyoumbwa maneno ya wanadamu, na atakayeyasikia na akadai kuwa


4


hayo ni maneno ya mwanadamu ameshakufuru, Allah ameshamkemea, mkosoa na kumwahidi adhabu ya moto wa Saqari, pale aliposema: ‘Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.” Quran 74:26 kwa kuwa Allah amwahidi moto wa Saqari yule anayesema: “Haya si chochote ila kauli ya binaadamu”. Quran 74:25 kwa kuwa Allah amesema hivi tumejua na kuyakinisha kuwa Qurani ni kauli ya muumba wanadamu na haifanani na kauli za viumbe.


Atakayemsifu Allah kwa maana miongoni mwa maana za wanadamu kwa hakika amekufuru. Aliyeyaona/aliyeyatambua haya amezingatia, na ameshaacha kauli zilizo kama za makafiri, na ameshajua kuwa Allah na hata sifa zake hazifanana na za wanadamu. Na watu wa Peponi ni kweli watamwona Mungu, bila ya kumhitwu wala namna na hivyo ni kama vile kilivyotamka kitabu cha Mola wetu: “Nyuso siku hiyo……) Quran 75:22-23 na tafsiri yake ni kwa mujibu wa alivyotaka Allah Mtukufu na ujuzi wake, yote yaliyokuja katika hadithi sahihiza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, kuhusu tafsiri yake ni haki na ndivyo hivyo hivyo na maana zake ndivyo kama alivyozikusudia, hutuingilii katika jambo hilo, kwa kutaawili (kutoa fasili) kwa rai zetu, wala hatujisemei kwa matamanio yetu, kwani hakika mambo yalivyo, hakuna kilichosalimika katika dini yake ila kwa yule aliyekisalimisha kwa Allah Mtukufu aliyetukuka pamoja na mtume wake Rehema na amani ziwe juu yake, pia ujuzi wa yale yanayomtatiza anaurudisaha kwa mjuzi wake.


Mguu wa Uislamu hausimami ila kwa mgongo wa kujisalimisha (kwa Allah), hivyo atakayeikusudia elimu ya vilivyoharamisha kuvijua, na hajakinaika na kuisalimisha fahamu yake, basi makusudio yake yatamzuia asifikie tauhidi halisi, maarifa safi na imani sahihi kwa hiyo atayumbishwa baina ya ukafiri na imani, kusadikisha na kupinga, kukiri na kukana, ana wasiwasi akihangaishwa na shaka si muumini mwenye kusadikisha wala si si mpingaji mwenye kukadhibisha.


Imani ya kumwona Allah haisihi kwa watu wa Peponi kwa yule aliyelichukulia swala hilo kuwa ni imani potofu, au aliyelifasili kwa ufahamu wake, kwani fasili ya kumwona Mungu – na fasili ya kila maana iliyoegemezwa kwa Uunguzi Ulezi wake – fasili yake inaachwa na kupaswa kuisalimisha kwake na hii ndio dini ya Waislamu. Na asiyejihadhari na kumkana na kumfananisha Allah atatereza na hatapatia kumtakasa Allah.


Kwa hakika Mola wetu Mtukufu aliyetukuka amesifika kwa sifa za upweke, umoja, na maana zake hana mtu yeyote miongoni mwa


5


wanadamu. Ametakasika ( 3 ) na mipaka na vikomo, nguzo na viungo, nyenzo, hazungukwi na pande sita kama wanavyozungukwa viumbe vingine vilivozuka


Na Miraji (Ngazi aliyopandia mbinguni) ni haki, kwa hakika Nabii Rehema na amani ziwe juu yake, amepelekwa usiku kwa usiku, (hadi msikiti wa Aqsaa huko Palestina) kisha akapandishwa akiwa yu macho hadi mbinguni, kisha akafika hadi pale alipopataka Allah. Allah akamkirimu kwa alivyovitaka, na akamfunulia alivyomfunulia, “Moyo


3 Pale mwandishi aliposema Ametakasika na mipaka na vikomo, nguzo na viungo, nyenzo, hazungukwi na pande sita kama wanavyozungukwa viumbe vingine vilivyozuka”. Maneno haya yanaeleza kiujumla na huenda yakatumiwa na watu wa kutaawili (kutoa maoni yao) na wapinga majina ya Allah na sifa zake hali ya kuwa hawana hoja ya kweli katika jambo hilo. Kwa kuwa makusudio ya mtunzi Allah amrehemu ni kumtakasa Muumba Mtukufu asifanane na viumbe. Lakini akatumia ibara ya ujumla inayohitaji ufafanuzi ili kuondoa utata. Makusudio yake aliposema mipaka ni ile mipaka inayojulikana na wanadamu. Allah yeye ni Mtukufu na hakuna ajuaye mipaka yake ila Yeye mwenyewe. Kwa sababu viumbe hawana elimu ya kjua kila kitu chake kama Allah Mtukufu alivyosema katika Surat Twaha: “Yeye anajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyumayao. Wala wao hawawezi kumjua Yeye vilivyo.” Surat Twaha 110. Na yeyote miongi mwa Salafi atakayesma kuthibitisha mpaka wa istiwaai yaani kuwa juu ya kiti cha enzi au mengineyo, makusudio yake ni mpaka unaojulikana na Allah Mtukufu na haujulikani na viumbe. Na aliposema Ametakasika na vikomo, nguzo/kona viungo na nyenzo) makusudio ya mtunzi Allah amrehemu ni kmtakasa Allah asifanane na viumbe katika hekima zake na sifa za dhati yake miongoni mwa kuwa ana uso, mkono, mguu, na nyinginezo. Yeye Allah Mtukufu anasifika na sifa hizo lakini sifa zake hazifanani na za viumbe na hakuna ajuaye zilivyo hizo sifa zake zaidi yake yeye mwenyewe. Na watu wa Bidaa (uzushi) wanatamka matamko kama haya ya mtunzi ili wayatumie kukanusha sifa bila kutumia yale matamko aliyoyatumia Allah na kujithibitishia yeye mwenyewe ili wasifedheheshwe na kushutumiwa na watu wa haki. Na mtunzi Twahawiyu Allah amrehemu hakukusudia kama wanavyokusudia wao kwa kuwa yeye ni miongoni mwa watu wa suna wanaozithibitisha sifa za Allah, na maneno yake katika itikadi hii yanajifafanua yeyewe kwa yenyewe na kujisadikisha yeyewe kwa yenyewe na kufafanua maneno yenye utata kwa kutumia yasiyo na utata, na hivyo hivyo aliposema: (hazungukwi na pande sita kama wanavyozungukwa viumbe vingine vilivozuka) makusudio yake ni zile pande sita zilizoumbwa na sio kukanusha uwepo juu wa Allah na kukalia kiti chake cha enzi, kwa kuwa hilo haliingii katika pande sita ispokuwa Allah yupo juu ya ulimwengu na umeuzunguka ulimwengu wote. Na Allah amewajaalia waja zake wawe na maumbile ya imani ya kuwa Allah Mtukufu yupo juu na kwamba Allah yupo upande wa juu na Ahlu sunna waljamaatu wote kuanzia Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yao na wale waliowafuata kwa wema wamekubaliana juu ya hilo. Na ushahidi kutoka katika kitabu na suna sahihi zilizopokea kwa njia ya mutawaatiri (wengi) zote zinajulisha kuwa Allah Mtukufu yupo juu. Kwa hiyo ewe msomaji mtukufu zindukana na jambo hili kubwa na ujue kuwa hili ndilo jambo la haki na mengineyo kinyume na hili ni batili. Na Allah ndiye anayetawalia kuwafikisha.


6


haukusema uwongo uliyoyaona.” ‘8’ Quran 53: 11 Nabii Rehema na amani ziwe juu yake Akhera na duniani. Na Hodhi alilokirimiwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, ni haki nayo ni kinywaji cha uma wake, na Shafaa (ponyo la kuwaombea watu watolewe motoni) Allah alilowawekea nalo ni kweli, kama lilivyopokelewa katika hadithi.


Na ile ahadi aliyoiweka Allah Mtukufu kwa Adam na kizazi chake ni ya kweli, kwa hakika Allah alijua idadi ya watakaoingia peponi na idadi ya watakaoingia motoni kwa jumla moja, na idadi hiyo haitozidi wala kupungua. Pia alijua matendo yao watakayoyafanya, na yote hayo yamewezeshwa kwa yalichoumbiwa, na matendo yanazingatiwa mwisho wake, na mwenye furaha ni yule aliyepewa furaha na hukumu ya Allah na mwenye tabu ni yule aliyepewa tabu na hukumu ya Allah.


Asili ya kadari (makadirio ya Allah) ni siri ya Allah kwa viumbe wake, hajamuonesha siri hiyo malaika aliyekaribu na Allah wala mtume aliyemtuma, na kujikita na kulitafiti sana jambo hili ni sababu ya kudhalilika, ngazi ya kunyimwa mazuri na ni daraja la kuchupa mipaka. Jihadhari sana na kulichunguza, kulifikiria na kuwa na shaka nalo. Kwa hakika Allah ameiziba elimu ya kadari kwa viumbe wake, na amewakataza kuilenga/kuikusudia kama alivyosema Allah Mtukufu katika kitabu chake: “Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanaohojiwa kwa wayatendayo.” Quran Al-Anbiyaai 23 Na atakayeuliza kwa nini amefanya hivi? Mtu huyo ameikataa hukumu ya kitabu, na anayeikataa hukumu ya kitabu ashakuwa miongoni mwa makafiri.


Haya ndio jumla ya mambo anayoyahitajia mtu mwenye nuru ya moyo miongoni mwa mawalii (wapenzi) wa Allah mtukufu. Hii ni daraja ya wale walibobea katika elimu kwa kuwa elimu zipo aina mbili: elimu waliyonayo viumbe na elimu wasiokuwa nayo viumbe ( 4 ) kwa hiyo


4 Makusudio ya mtunzi Allah amrehemu aliposema elimu wasiyokuwa nayo viumbe: ni elimu ya ghaibu (vilivyofichikana) na elimu hii ni maalumu kwa Allah Mtukufu. Na mtu yeyote atakayedai kuwa ana elimu hii ameshakufuru kwa mujibu wa maneno ya Allah Mtukufu: “Na zipo kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu…” Surat Al-Anaam 59. Na maneno ya Allah Mtukufu: “Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye yaghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu.” Surat An-Namli 65.


Na maneno ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake: (Fungo za ghaibu ni tano hakuna azijuaye ispokuwa Allah kisha akasoma kauli ya Allah Mtukufu: “Hakika kuijua Saa (ya Kiyama) kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anayeiteremsha mvua…” Surat Luqman 34.


Na hadithi zilizokuja katika mlango huu zote zinajulisha kuwa Mtume mwenyewe, Rehema na amani ziwe juu yake hajui ghaibu licha ya kuwa yeye ndiye kiumbe bora kuliko wote na ni bwana wa mitume, kwa hiyo viumbe wengine ndio hawajui kabisaa. Na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake hajua chochote miongoni mwa mambo


7


kupinga elimu uliyopo ni kukufuru. Na kujidai kuwa una elimu isiyokuwepo pia ni kukufuru. Imani haithibiti ispokuwa kwa kukubali elimu iliyopo na kuacha kuitafuta elimu isiyokuwepo.


Tunaamini ubao na kalamu na yote yaliyokuwemo na kuandikwa humo, lau kama viumbe wote wataungana juu ya jambo lililoandikwa na Allah kuwa liwepo na hao viumbe wakataka walifanye lisiwepo hawataweza. Pia lau kama viumbe wote wataungana juu ya jambo lisiloandikwa na Allah kuwa liwepo na hao viumbe wakataka walifanye liwepo hawataweza. Kalamu imeshakauka kwa vilivyopo hadi siku ya Kiama. Kisichomkosa mja hakikuwa cha kumpata pia kile kilichompata nacho hakikuwa cha kumkosa.


Mja lazima aelewe kuwa kwa hakika Allah kwa elimu yake ametangulia kukijua kila kiumbe miongoni mwa viumbe vyake na akavikadiria makadirio mazuri kabisa hayana upungufu, hayana wa kuyatilia maelezo, wa kuyaondosha, wa kuyageuza, wa kupunguza, wala kuzidisha miongoni mwa viumbe walioko katika mbingu na ardhi zake. Haya ni kifungo cha imani na misingi ya maarifa na kuikiri tauhidi ya Allah mtukufu pamoja na umola ulezi wake. Kama Allah mtukufu alivyosema katika kitabu chake: “Na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo”. Surat Al-Furqaan 2 Pia Allah amesema: “Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kudura iliyo kwisha kadiriwa.” Surat Ahzaabu 38.


Ole wake yule atakayekuwa adui wa Kudura za Allah, na kuhudhurisha katika hili mtazamo wake wa moyo mgonjwa, kwa hakika mtu huyo kwa imani yake potofu amejitafutia siri ya kiza ya kutafiti undani wa yaliyofichikana mtokeo yake kwa hayo aliyoyasema atakuwa amerejea katika ufasiki na madhambi.


Arshi na Kiti cha enzi ni haki, na Allah ni mwenye kujitosheleza hana shida na Arshi wala vilivyo chini yake au juu yake, amekizunguka kila kitu, huku amevifanya viumbe vyake kuwa vimeshindwa kuizunguka.


Tunasema: Kwa hakika Allah amemjaalia Ibrahimu kuwa kipenzi chake, na akasema na Musa haki ya kusema naye, haya tunayamini,


ya ghaibu ispokuwa kile alichofundishwa na Allah Mtukufu. Wakati watu wa uzushi waliposema katika suala la Aisha, Allah amuwie radhi, Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hakuujua usafi wa Aisha ila baada ya kuteremshiwa ufunuo. Na wakati mkufu wa Aisha, Allah amuwie radhi, ulipopotea katika moja ya safari za Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alikituma kikundi cha watu kwenda kuutafuta na yeye hakujua upo wapi hadi walipomsimamisha ngamia na kuukuta chini yake. Alhamdu lillahi, ushahidi wa haya upo mwingi katika kitabu na Suna.


8


kuyasadikisha na kujisalimisha kwayo. Tunaamini Malaika, Mitume, Vitabu vilivyoteremshwa kwa mitume, tunashuhudia kuwa Mitume ilikuwa katika haki ya wazi. Watu wa kibla chetu tunawaita Waislamu waumini, muda wa kuwa wanayakubali yale aliyokuja nayo Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, pia wanayasadikisha yale yote aliyoyasema na kuyaeleza, wala hatujitumbukizi katika dhati ya Allah wala hatuipuzi dini ya Allah, wala hatuijadili Quran. Tunashuhudia kuwa Quran ni maneno ya Mola wa viumbe wote iliyoteremshwa na Malaika mwaminifu akamfundisha bwana wa mitume Muhammad Rehema na amaini ziwe juu yake, Quran ni maneno ya Allah mtukufu hayapo sawa na maneno yoyote miongoni mwa maneno ya viumbe, hatusemi kuwa Quran ameiumbwa wala hatuendi kinyume na jamaa ya waislamu wala hatumkufurishi yeyote miongoni mwa watu wa kibla kwa dhambi asiyoihalalisha. ( 5 )


Wala hatusemi kuwa “Mwenye imani akitenda dhambi haidhuru”.


Tunataraji kwa Allah awasamehe wale wema miongoni mwa waumini na kuwaingiza peponi kwa rehema zake. Hatuna dhamana nao wala atushuhudii kuwa wataingia peponi ( 6 ) . Pia tunawaombea msamaha wale


5 Mtunzi aliposema (wala hatumkufurishi yeyote miongoni mwa watu wa kibla kwa dhambi asiyoihalalisha). Makusudio ya mtunzi Allah amrehemu ni kuwa Ahlu sunna waljamaatu hawamkufurishi muislamu kumwenye kumpwekesha na kumwamini Allah na siku ya mwisho kwa kutenda dhambi. Kama kuzini, kunywa pombe, kula riba, kuwaasi wazazi na engineyo muda wa kuwa hajastahalalisha hilo, na kama ataliihalalisha atakufuru kwani kwa kufanya hivyo atakuwa anasema kuwa maneno ya Allah ni Mtume wake ni uongo (anamkadhibisha) kwa hiyo atakuwa amejitoa katika dini yake ama kama hatohalalisha mtu huyo hatakufuru kwa Ahlu sunna waljamaatu, lakini atakuwa mdhaifu wa imani. Na anastahiki hukumu ya maasi aliyoyatenda ikiwemo kuitwa fasiki na kufanyiwa hadi (kupewa adhabu) na mengineyo kama yalivyokuja katika sheria takatifu. Na hii ndio kauli ya Ahlu sunna waljamaatu nayo ni kinyume na Makhawariji, Muutazila na wale waliopita mapito yao ya batili. Makhawariji wanawakufurisha watu kwa kutenda dhambi na Muutazila wanamjalia mtua atendaye dhambi kuwa atakuwa katika sehemu ya katikati baina ya sehemu mbili yaani atakuwa baina ya Uislamu na ukafiri duniani na ahera wanakubaliana na Makhawariji kuwa mtu huyo ataingizwa motoni milele. Na kauli ya makundi haya mawili ni batili kwa mujibu wa kitabu, suna na makubaliano ya salafi wa umma. Kwa hakika mambo yao yamewatatiza baadhi ya watu kwa sababu wana ufinyu wa kulijua. Lakini tunamshukuru Allah kuwa, jambo lao lipo wazi kwa watu wa haki kama tulivyolibainisha na Allah ndiye mwenye kuwafikisha.


6 Makusudio ya mtunzi Allah amrehemu: Ispokuwa wale waliobashiriwa pepo na na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kama wale maswahaba kumi na wengineo. Kama yatakavyoelezwa haya mwishoni mwa maneno ya mtunzi. Pamoja na kujua kuwa itikadi ya Ahlu sunna waljamaatu ni kuwa waumini na wachamungu kwa ujumla wote ni watu wa peponi. Na makafiri, washirikina na wanafiki ni watu wa


9


waovu miongoni mwa waumini, tunaogopa wasidhurike na hatuwakatishi tama.


Dhamana na kukata tamaa vinatoa mtu kutoka katika Uislamu. Kwa hiyo, njia ya haki kwa watu wa kibla yetu ipo baina ya mawali haya. Mja hatoki katika imani ispokuwa kwa kukanusha yale yaliyomuingiza katika Uislamu 7 ) ). Imani ni kukiri kwa ulimi na kusadikisha kwa matendo ( 8 ) .


motoni. Kama unavyojulisha ushahidi wa aya tukufu na suna zilizopokelewa kwa tawaaturi (na wengi) kutoka kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwa ushahidi huo ni kauli ya Allah Mtukufu: Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na neema” Surat Al-Tuuri 17. Na kauli ya Allah Mtukufu: “Mwenyezi Mungu amewaahidi Waumini wanaume naWaumini wanawake Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo…” Surat Tawbah 72. Kuna aya nyingi zinazojulisha maana hii. Kauli ya Allah kwa makafiri: “Na walio kufuru watakuwa na Moto wa Jahannamu,hawahukumiwi wakafa, wala hawatapunguziwa adhabu yake. Hivyo ndivyo tunavyo mlipa kila mwenye kuzidi ukafiri.” Faatiri 36. Na kauli ya Allah Mtukufu: “Hakika wanaafiki watakuwa katika t'abaka ya chini kabisa Motoni, wala hutompata yeyote wa kuwanusuru. An-Nisaa 145. Kuna aya zingine zinazojulisha maana hii hii. Na Allah ndiye mwenye kuwafikisha.


7 Na huku kuyafunga maneno kuna walakini kwani kafiri anaingia Uislamu kwa shahada mbili ikiwa hazitamki, na akizitamka ataingia Uislamu kwa kutubia kile kilichomlazimu awe kafiri. Huenda mtu akatoka katika Uislamu bila kuupinga kwa vigezo vingi vilivyobainishwa na wanazuoni katika mlango wa hukumu ya mwenye kuritadi (kutoka Uislamu) miongoni mwa vigezo hivyo ni Kuushambulia Uislamum, au Mtum, Rehema na amani ziwe juu yake au kumchezashere Allah na Mtume wake au kitabu chake au chochote katika sheria ya Allah Mtukufu kwa mujibu wa maneno ya Allah Mtukufu. Na ukiwauliza, wanasema: Sisi tulikuwa tukipigaporojo na kucheza tu. Sema: Mlikuwa mkimfanyiamaskhara Mwenyezi Mungu na Ishara zake na Mtume wake? 66. Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuaminikwenu!..” Surat Al-Tawbah 65 - 66 Na miongoni mwa vitu vinavyomtoa mtu Uislamu ni kuabudu sanamu, kuwaomba maiti na kuwataka msaada na kuwataka wamwokoe na wamsaidie na yaliyo kama hayo. Kwa kuwa mambo haya yanapingana na kauli ya hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah kwa kuwa kauli hii inajulisha kuwa ibada ni haki ya Allah peke yake. Na miongoni mwa vitu vinavyomtoa mtu Uislamu ni kuomba dua, kuomba msaada, kuinamia (kurukuu), kusujudia, kuchinja, kuweka nadhiri, na kama haya. Atakayetenda chochote katika hayo kumfanyia asiyekuwa Allah miongoni mwa masanamu, malaika, majini, walio makaburini na wengineo miongoni mwa viumbe, mtu huyo atakuwa ameshamshirikisha Allah na wala hajaithibitisha kauli ya Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah. Mambo yote haya yanamtoa mtu kutoka katika Uislamu kwa mujibu wa makubaliano ya wanazuoni. Na hayo si mambo ya kupinga. Na ushahidi wa hili unajulikana kutoka katika kitabu na suna. Pia kuna mambo mengine mengi yanayomtoa mtu kutoka katika Uislamu na yenyewe hayaitwi kuwa ni kupinga/kukana na yenyewe yametajwa na wanazuoni katika katika mlango wa hukumu za mwenye kutoka katika Uislamu, ukipenda pitia mlango huo. Na Allah ndiye mwenye kuwafikisha.


11


Yote yaliyoswihi kutoka kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, miongoni mwa Sheria na Ubainifu wa yote ni haki. Imani ni moja ( 9 ) na wenye imani kwa asili wapo sawasawa. Na tofauti za ubora miongoni mwao ni kwa kumcha na kumwogopa Mungu, kupingana na matamanio ya nafsi na kushikamana na yaliyomema. Waumini wote ni mawalii wa Mungu wa Rehema, na mbora wa Waislamu ni mtiifu sana miongoni mwao na mfuasi mzuri wa Quran.


Imani ni kumwani Allah, malaika zake, vitsbu vyske, mitume yake, siku ya Kiama na Kadari ya heri yake na shari yake, tamu yake na chungu yake zote zinatoka kwa Allah Mtukufu. Sisi tunaamini yote hayo, hatumtofautishi yeyote miongoni mwa mitume yake. Tunawasadikisha wote kwa yale waliokuja nayo.


Wenye madhambi makubwa (katika uma wa Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake) watakapokufa huku wakiwa wanampwekesha Allah wataingia motoni bila kuishi humo milele na watu hao wapo katika matakwa na hukumu ya Allah. Allah akipenda atawaghufiria na kuwasamehe kwa fadhila zake, kama ilivyotajwa na Allah Mtuku aliyetukuka katika kitabu chake: “…na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye… ”. Surat Al-Nisaa 48 na 116.


Ewe Mola, ewe Mlinzi wa Uislamu na watu wake tuthibitishe katika Uislamu hadi tukutane nawe kwa Uislamu. Pia tunaona kuwa inafaa kuswali nyuma ya mwema au mwovu miongoni mwa watu wa kibla pia kumsalia yeyote miongoni mwao. Wala hatumuingizi peponi au motoni yeyote miongoni mwao. Wala hatuwashuhudii wao kwa ukafiri,


8 Fasili hii ina walakini na upungufu na iliyosawa kwa Ahlu suna waljamaatu ni kuwa imani ni maneno na vitendo na kwamba itikadi inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi. Na ushahidi wa hilo upo mwingi sana katika kitabu na suna. Mshereheshaji bwana Abul Izzi ametaja idadi kubwa ya huo ushahidi rejea kipenda. Na kuyatoa matendo katika imani ni kauli ya Murjia, na tofauti kati yao na Ahlu suna si ya matamshi tu bali ni ya matamshi na maana na kwa imani hii kunapatikana hukumu nyingi anazijua yule anayezingatia maneno ya Ahlu suna na maneno ya Murjia, na Allah ndio wa kuombwa msaada.


9 Kauli ya mtunzi (na imani ni moja na wenye imani kwa asili wapo sawasawa). Maneno haya yana walakini pia na ni batili. wenye imani wenye imani hawapo sawa ispokuwa wapo tofauti kubwa. Imani ya manabii si sawa na watu wengine. Kama ilivyo kuwa imani ya makhalifa waongofu na maswahaba wengine Allah awawie radhi si sawa na imani ya wengine. Na hivyo hivyo imani ya waumini si sawa na imani ya mafasiki. Na tofauti hii ni kwa mujibu wa yale yaliyomo moyoni miongoni mwa kumjua Allahu, majina yake, sifa zake na sheria alizowapangia waja zake. Na hii ndio kauli ya Ahlu suna waljamaatu ikiwa ni kinyume na Murjia na wanaosema kama wao, na Allah ndiye wa kuombwa msaada.


11


ushirikina wala unafiki kama hakijadhihiri kwao chochote katika hayo, na siri zao tunaziacha kwa Allah Mtuku.


Hutoenelei kuwa kuna mtu yeyote katika uma wa Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake kuwa anayestahiki kukatwa panga ispokuwa yule aliyewajibikiwa kupigwa panga. Wala hatuonelei kutoka katika kuwatii maimamu na watawala wetu hata kama watachupa mipaka, wala hatuwaombei laana, wala hutoi mkono wa kuwatii. Tunaonelea kuwa kuwatii wao ni lazima na ni miongoni mwa twaa kwa Allah Mukufu, ikiwa hawajaamrisha maasi. Tunawaombea uongofu na kusamehewa. Tunafuata Sunna na jamaa na kujiepusha michepuko, kwenda kinyume na kufarikiana. Tunaapenda waadilifu na waamini. Tunawabughudhi waovu na wahaini.


Tunasema: Allah anajua yale yenye kututatiza kuyajua, tuaonelea kuwa kupaka juu ya Khofu mbili safarini na sio safarini kama ilivyokuja katika hadithi. Hija na Jihadi vinaendana na wenye mamlaka miongoni mwa Waislamu wema wao na waovu wao hadi kusimama kwa Kiama vitu hivyo havibatilishwi wala kutanguliwa na chochote.


Tunaamini ukarimu wa Malaika waandishi kwa hakika Allah amewajaalia wao kwetu sisi wawe ni watunzaji (kumbukumbu), tunamwamini malaika wa mauti aliyepewa jukumu la kutoa roho za viumbe wote, tunaamini adhabu ya kaburi kwa mwenye kuistahiki, pia tunaamini maswali ya malaika waitwao Munkari na Nakiiri huko kaburini kuwa yapo, watauliza juu ya mungu wake, dini yake, nabii wake, nahabari zilizomfikia kuhusiana na mtume wa Allah, rehema na amani ziwe juu yake, pia kuhusu maswahaba, Allah awawie radhi.


Kaburi ni kiwanja miongoni mwa viwanja vya peponi au ni shimo miongoni mwa mashimo ya moto. Tunaamini kufufuliwa na kulipwa matendo siku ya Kiyama, kufufuliwa na kuhesabiwa na kusoma kitabu, thawabu na adhabu. Njia nyembamba na mizani. Pepo na moto vimeumbwa havitoweki milele wala haviangamii. Na kwa hakika Allah Mtukufu ameumba pepo na moto kabla ya kuumba na akaviumbia watu wake, atakayemtaka miongoni mwao ataingia peponi kwa fadhila toka kwa Allah, na atakayemtaka miongoni mwao ataingia motoni kwa uadilifu wa Allah, na kila kimoja anatenda kwa mujibu wa alichowekea, pia atakuwa katika yale aliyoumbiwa.


Heri na shari zimekadiriwa kwa mja, na kule kuweza ambapo kwa ajili yake kitendo kinalazimika mfano kuafikishwa ambapo hakuwezi kujuzu kusifiwa kiumbe jambo hilo lipo pamoja na kitendo. Ama kuweza kwa


12


upande wa kusihi na ukunjufu na kuweza na kusalimika kwa vifaa hivyo vinakuwa kabla ya tendo. Na kwa kuweza huku ndiko kunakofungamana mahubiri kama alivyosema Allah Mtukufu: “Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwakadiri ya iwezavyho…: Surat Baqara 286.


Matendo ya waja yameumbwa na Allah, kuchuma ni kwa waja. Allah Mtu hajawakalifisha ispokuwa yale wanayoyaweza. Na hakuna wanachokiweza ( 10 ) zaidi ya kile walichokalifishwa kwacho na hii ndio fasili ya (hapana hila wala nguvu ila ni za Allah) tunasema: hakuna hila kwa yeyote wala harakati wala kubadilika kwa yeyote kuacha kumuasi Allah ila kwa msaada wa Allah. Na yeyote hana nguvu ya kuanza kumtii Allah na kuthibiti katika jambo hili ila kwa taufiki (kuwezeshwa) ya Allah.


Kila kitu kinaende kwa matakwa ya Allah Mtukufu, elimu yake, hukumu zake na kadari yake. Matakwa yake yameshinda matakwa yote. Hukumu zake zimeshinda hila zote. Anafanya atakavyo naye ni dhalimu milele, ametakasika na kila baya na HIIN na ametakasika na kila dosari na upungufu. “Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanaohojiwa kwa wayatendayo". Surt Al-Anbiyaau 23.


Dua za walio hai na sadaka ni manufaa kwa waliokufa, Allah Mtukufu anapokea dua, anakidhi haja haja na anamiliki kila kitu. Hamilikiwi na chochote. Haiwezekani kujitosheleza pasi na Allah Mtukufu hata kwa kupepesa jicho. Na atakayejifanya ametosheka hana haja ya Allah hata kwa kupepesa jicho ameshakufuru na kuwa kafiri na kuwa miongoni mwa watu wa HIINI. Allah anaghadhibika na kuridhia lakini si kama yeyote miongoni mwa wanadamu.


Tunawapenda Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wala hatchupi mipaka katika kumpenda yeyote miongoni mwao. Hatumbagui yeyote miongoni mwao. Tunawachukia wanaowachukia Maswahaba na kuwataja kwa yasiyo ya heri. Hatuwataji Maswahaba ila kwa heri. Kuwapenda wao ni dini, imani na ihsani. Kuwabughuzi wao ni kufuru, unafiki na kuchupa mipaka.


Tunathibitisha Ukhalifa baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake kuwa wa kwanza ni Abu Bakri Al-Swidiiqi, Allah amuwie radhi, na


10 Hili si sahihi, lakini makalafuuna (walioamrishwa) wanayaweza mengi zaidi ya walioamrishwa na Allah Mtukufu. Lakini Allah Mtukufu amewahrumia na kuwafanyia wepesi waja zake na hajawatilia uzito katika dini yao na hizo ni fadhila na wema wake, na Allah ndiye mwenye kutawalia kuwafikisha.


13


huku ni kufadhilisha na kumuweka mbele ya umma wote. Kisha Omar bin Al-Khatwaabi, Allah amuwie radhi, kisha Othmani, Allah amuwie radhi, kisha Ali, Allah amuwie radhi. Hawa ndio makhalifa waongofu na maimamu waongofu.


Kwa hakika Maswahaba kumi waliotajwa na kubashiriwa Pepo na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, tunawashuhudia kuwa wao ni watu wa Peponi kwa kuwa wameshuhudiwa hivyo na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, na kauli yake ni kweli. Nao ni Abu Bakari, Omari, Othumani, Ali, Twalha, Zuberi, Saadi, Said, Abdulrahman bin Aufi na Abu Ubaida bin Al-Jaraah na huyu ndiye mtunza siri wa umma huu. Allah awawie radhi wote.


Atakayetoa kauli nzuri juu ya Maswahaba, wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wake zake walioepukana na kila chafu, kizazi chake kilichotakaswa na kila chafu, Mtu huyo ameepukana na unafiki.


Wanazuoni wa Kisalafi waliotangulia, na waliokuja baada yao miongoni mwa Mataabiina ni watu wa heri, athari nzuri, fiqihi (ufahamu wa dini) na mtazamo mzuri. Hawataji ila yaliyomazuri, na atakayewataja kwa uovu mtu huyo yupo nje ya njia ya haki.


Hatumfadhilishi walii yeyote kuliko mtume yeyote miongoni mwa mitume, Rehema na amani ziwe juu yao na tunasema: Mtume mmoja ni mbora kuliko mawalii wote.


Tunaamini karama walizokuja nazo kuwa ni sahihi zikiwa zimetoka kwa wapokezi wa kuaminika.


Tunaamini alama za Kiama: miongoni mwazo ni kutokea kwa Dajali, kuteremka kwa Issa ibni Maryam, amani iwe juu yake, tunaamini kuwa jua litachomoza upande wa magharibi, kutokea kwa mnyama wa ardhini katika sehemu yake.


Hatumsadikishi kuhani wala muagua nyota (mpiga ramli) wala anayelingania kitu kilichokinyume na Kitabu na Sunnah na Ijimai ya umma.


Tunaamini kuwa Jamaa lipo katika haki, na kufarikiana nayo ni kupotea na kuadhibika.


Dini ya Allah ardhini na mbinguni ni moja, nayo ni Uislamu. Allah Mtukufu amesema: “Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni


14


Uislamu…” Surat Al-Imrani 19. Na amesema tena: “…Mimi, leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini…” Surat Al-Maaida 3.


Na Uislamu ni dini ya kati na kati baina ya ziada potofu na upungufu mbaya, baina ya kumfananisha Allah na kumuondolea sifa zake, baina ya imani ya (Ajabri na Alqadari) kulazimishwa na kukadiriwa, baina ya kujiamini mno na kukata tamaa. Hii ndio dini yetu na itakadi yetu kwa wazi na kwa siri. Sisi tunajitakasa kwa Allah na kila anayeenda kinyume na haya tuliyoyataja na kuyabainisha.


Tunamuomba Allah Mtukufu atuthibitishe katika imani, na atufikishe mwisho wetu na imani hiyo, atukinge na matamanio ya nafsi yaliyo mbalimbali, pia atuepushe na rai za kufarikisha na madhehebu mabaya kama vile madhehebu ya Al-Mushabiha (ya kumfananisha Allah), Muutazila, Al-Jahamiya, Al-Jabriya, Al-Qadariya na wengineo miongoni mwa wale ambao wameenda kinyume na Sunnah Waljamaa. Wakaungana na upotevu. Sisi tunajitenga nao, na madhehebu hayo kwetu sisi yanazingatiwa kuwa ni upotovu na ubaya. Na kwa Allah ndipo tunapotarajia kulindwa na kuwafikishwa.


Mwisho wa akida ya Twahawiya, Allah amsamehe mtunzi wake na awanufaishe waja zake kwa utunzi huu.


[Akida ya Attwahawiya imeisha, Allah amsamehe mtunzi wake na awanufaishe kwayo waja zake]



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI