
Swali : Nilipi jambo la kwanza la wajibu kwa kiumbe?
Jawabu: Jambo la wajibu la kwanza kwa viumbe ni lile ambalo viumbe
wanalinganiwa kwalo, na amelibainisha Mtume (s.a.w) kwa Muadhi bin Jabal
(r.a) wakati alipomtuma kwenda Yemen, alimwambia: "Hakika unawaendea
watu ambao ni mayahudi na manaswara, basi liwe jambo la kwanza utakalo
walingania ni kutoa shahada ya Laa Ilaha ila Allah Muhamada rasulu Allah".
Imepokelewa na Imamu Bukhari (1496) na Imamu Muslim (19).
Hili ndilo jambo la kwanza ambalo ni wajibu kwa kila mja ashahidilie kuwa
hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haqi ila ni Mwenyezi Mungu na Mtume
(s.a.w) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni wajibu kwa waja wampwekeshe
Mwenyezi Mungu, na waukubali na kukiri utume wa Muhamad (s.a.w), kwa
kufanya hivyo ndio inapatikana Ikhlas na kufuata mambo hayo mawili ndio
sharti ya kukubaliwa ibada.
Haya ndiyo mambo ya kwanza ambayo ni wajibu kwa kila mja kuyafanya,
ampwekeshe Mwenyezi Mungu na akiri Utume wa Muhamad (s.a.w) na
kutamka shahada ya (La ILLaha ila Allah Muhamada rasulu Allah) ndani yake
ndiyo kunaTawhiidi yote.c