Lengo la kuumbwa Mwanadamu
Sheikh: Binadamu ameumbwa kwa malengo gani?.
JAWABU: Kwajina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye
kurehemu, Namshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa ulimwengu mzima, na
Rehma na Amani zimshukie Nabii Muhammad (s.a.w), pamoja na Familia yake
na Maswahaba zake, Baada ya hayo.
Kwa hakika kabla ya kujibu swali hilo napenda kutoa zinduo kuhusu kanuni
muhimu sana katika mambo anayo yaumba Mwenyezi Mungu Mtukufu na yale
aliyo yapanga.
Na kanuni hiyo imechukuliwa kutoka katika kauli yake Mwenyezi Mungu
Mtukufu: (Na Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye hikima). Tahrim (2).
Na kauli yake: (Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima).
Ahzab (1).
Na aya nyingi tofauti na hizo zinazo onyesha na kuthibitisha hikma ya uumbaji
wa Mwenyezi Mungu na yale aliyo yapanga.
Maana yake: katika mambo ya kidunia na yakisheria, kwa sababu hakuna jambo
lolote analo liumba Mwenyezi Mungu Mtukufu isipokuwa ndani yake kuna
hikma, sawa sawa katika kuwepo jambo hilo au katika kuliondoa, na hakuna
jambo analo lipanga Mwenyezi Mungu Mtukufu isipokuwa kwa hikma vile vile,
sawa sawa iwe katika ulazima au katika kuharamisha au kuhalalisha.
Lakini hikma zinazo fungamana na mambo ya kidunia au ya kisheria,
yawezekana tukayajuwa na yawezekana tusiyajuwi, na yawezekana baadhi ya
watu wakayajua na wengine wasiyajue, hii nikutokana na elimu na ufahamu
anao wapa Allah waja wake.
Ikiwa ndivyo hivyo tunasema ya kwamba: Hakika Mwenyezi Mungu
Mtukufu kaumba Majini na Binadamu kutokana na hikma kubwa na malengo
mazuri nayo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Lengo la kuumbwa Mwanadamu
2
Kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu:(Nami sikuwaumba majini na
watu ila waniabudu Mimi). Adhariyati: (56).
Na kauli yake: ( Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba
nyinyi kwetu hamtarudishwa). Al-Muminun: (115). Na akasema: (Ati anadhani
binaadamu kuwa ataachwa bure). Al-Qiyama: (36).
Na aya nyingine tofauti na hizo zinazo julisha ya kwamba Mwenyezi Mungu
anayo malengo maalum katika kuumba binadamu na majini, nako ni kufanya
ibada.
Na ibada ni kudhalilika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kupenda na
kutukuza kwa kufanya amri zake na kujiepusha na makatazo yake katika njia
iliyo elekezwa na sheria zake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Nao
hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini,
wawe waongofu). Al-Bayyina: (5).
Hii ndio hikma ya kuumbwa majini na binadamu.
Kwa maana hiyo yeyote atakae fanya jeuri na kiburi kwa Mwenyezi Mungu kwa
kuacha kufanya ibada, kwa hakika atakuwa ni mwenye kupuuza hikma ambayo
viumbe wameumbwa kwa sababu hiyo.
Na kitendo chake hicho kinaonyesha ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu
kaumba viumbe kwa mchezona bila ya majukumu yoyote, na yeye japo
hajatamka lakini vitendo vyake vina ashiria hivyo kutokana na jeuri yake na
kupinga kwake ibada ya Mola wake.
Nini maana ya Ibada? Je, ina maana ya ujumla na maana maalumu?.
JAWABU: Ibaada ina maana mbili:
A.Maana ya ujumla.
B.Maana maalumu.
Maana yake kwa ujumla nikama tulivyo eleza katika swali la kwanza ya
kwamba: ni kudhalilika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kupenda
na kutukuza kwa kufanya amri zake na kujiepusha na makatazo yake katika njia
iliyo elekezwa na sheria zake.
Hii ndio maana yake kwa ujumla.
Maana yake maalum - nakusudia kwa urefu- Amesema Sheikhul-Islam Ibnu
Taimiyya (r.h): Ni jina lililo kusanya kila anacho kipenda Mwenyezi Mungu na
kukiridhia kutokana na maneno na vitendo vya siri na dhahiri,
Mfano: Khofu, Unyenyekevu, Kutegemea, Swala, Zaka, Funga, na ibada
nyinginezo tofauti na hizo zilizopo katika sheria ya Uislamu.
Na ukiwa unakusudia maana ya ibada kwa ujumla au kwa maana maalum kama
walivyo taja badhi ya wanachuoni ya kwamba Ibada yawezekana ikawa ya
kidunia au ya kisheria.
Kwa maana ya kwamba yawezekana binadamu akadhalilika kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu Mtukufu lakini ikawa kwa sababu ya dunia, na yawezekana
ikawa kudhalilika kwa sababu ya kisheria.
Ibada za kidunia ni kwawote, Muislamu, Kafiri, Mwema, Muovu. Kwa kauli
yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Hapana yeyote aliomo
mbinguni na ardhini ila atafika kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni
mtumwa wake). (Maryam: 93).
Maana ya Ibada
2
Vyote vilivyopo mbinguni na duniani ni vyenye kunyenyekea kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yale aliyo ya panga, haiwezekana kiumbe
akaenda kinyume na matakwa ya Allah katika mambo aliyo ya kadiria.
Lakini Ibada maalum nazo ni ibada za kisheria ni kudhalilika kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kisheria, ibada hizi ni maalumu kwa waumini
wenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, wenye kusimama katika amri
zake.
Kisha miongoni mwa ibada kuna ibada maalum zaidi. Zile ibada maalumu nizile
za Mitume (s.a.w), mfano kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Ametukuka
aliye teremsha Furqani kwa mja wake). (Al-Furqan: 1).
Na kauli yake: (Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu).
(Al-Baqara: 23.)
Na kauli yake: (Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa'qubu).
)Swad: 45.)
Na dalili nyingine tofauti na hizo zinazo wasifia Mitume (s.a.w), kuonyesha
kama na wao ni waja wake.
Je, wanalipwa thawabu wale wanao dai kufanya ibada kwa kuamini
matendo ya Mwenyezi Mungu kama kuumba na kufisha na kuhuyisha, bila
kufanya ibada alizo zifaradhisha Mwenyezi Mungu kama kutoa shahada na
kuswali na kufunga …nk. ?
JAWABU: Hao hawalipwi, kwasababu wanadamu wote wameubwa na
Mwenyezi Mungu wakiwa katika maumbile ya kukiri ukubwa wa Mwenyezi
Mungu na vitendo vyake katika ulimwengu na hilo nilazima kwa watu wote,
mwanadamu anauguwa na anakuwa masikini, na anampoteza kipenzi chake bila
yeye kupenda, bali halipendi jambo hilo, lakini ni lazima iwe hivyo kwa sababu
nimatashi ya Mwenyezi Mungu.