1
بسم الله الرحمن الرحيم
MAONI YA BAADHI YA MAIMAMU KUHUSU MASHIA NA ITIKADI POTOFU. Imekusanywa na kuiratibiwa na Abubakari Shabani Rukonkwa Imepiriwa na Yasini Twaha Kila sifa kamilifu nizake Allah mtukufu alie tuumba na kuruleta katika dunia hii kasha akatuletea muongozo sahihi wa Quraan na Sunna,amefaulu atakae fuata muongozo huo wa Quraan na sunna,sala na amani za Allah ziwe juu ya Mtume Muhamad na Ali zake na maswahaba zake watukufu. 1- IMAAM ASH-SHAAFI'IY Imam Shafi’iy alisema siku moja kuhusu Mashia, ‘Sijawahi kuona miongoni mwa makafiri watu wanaojulikana kwa kusema uongo kuliko Mashia.’ [Minhaaj as-Sunnah an-Nabawiyyah, 1/39] Wakati mwingine alisema, ‘Simulia elimu kutoka kwa yeyote yule utakayekutana naye isipokuwa Mashia, kwani wao hutunga Hadyith na kuzifanya sehemu ya Dini yao.’ [Minhaaj as-Sunnah an-Nabawiyyah, 1/38]. 2- IMAAM ABU HANIYFAH Imesimuliwa kuwa Imaam Abu Haniyfah alikuwa akikariri kauli ifuatayo kuhusu Mashia, ‘Yeyote mwenye mashaka kuhusu ukafiri wao basi nae pia ni kafiri.’ 3- IMAAM MAALIK
2
Siku moja Imaam Maalik aliulizwa kuhusu wao (Mashia)
akajibu, ‘Usiongee nao wala kupokea hadithi zao, kwani hapana
shaka wao ni waongo.’ [Minhaaj as-Sunnah, 1/37] Ilitajwa
katika darsa yake kuwa Mashia wanawatukana Maswahaba.
Katika kujibu akataja ayah: ‘‘Muhammad ni Mtumwa wa Allaah
na waliokuwa naye ni wakali dhidi ya makafiri na wenye
kurehemeana wenyewe kwa wenyewe. Ili kuwachukiza
makafiri…’’ Kisha akasema, ‘Basi yeyote anayebughudhiwa
wakati Maswahaba wanapotajwa basi na yeye kakusudiwa pia
na ayah hii.’ (Yaani yeyote anayechukizwa kwa kutajwa
Maswahaba basi amekusudiwa katika Aayah hii kwa sababu
Allaah Anasema, ‘‘Ili kuwachukiza makafiri…’’)
4- IMAAM IBN AL-MUBAARAK
Imaam Ibnul Mubaarak amesimuliwa akisema, ‘Dini hupatikana
kwa Watu wa Hadiyth (Ahlul Hadiyth), falsafa na udhuru wa
kijanjajanja unapatikana kwa watu wa rai (Ahlur Rai ) na uongo
unapatikana kwa Mashia.’ [Al-Muntaqaa min Minhaaj al-
I`tidaal, uk. 48]
5-IMAAM ABU ZUR’AH RAAZI
Mwanachuoni huyu mkubwa amenukuliwa akisema, ‘Ukimuona
mtu yeyote anayewadharau Maswahaba, basi jua ya kuwa yeye
ni kafiri. Hiyo ni kwa sababu Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam. alikuwa mkweli na alituletea ukweli ambao
umetufikia kwa njia ya Maswahaba. Hao makafiri (Mashia)
lengo lao ni kutia shaka katika wasimulizi wa ukweli huo
(Maswahaba) ili kutia shaka pia katika Qur-aan na Sunnah. Basi
3
makafiri ndio wanaostahiki zaidi kudharauliwa.’
6- IMAAM AL-QAADHIY ABU YA’ALAA
Imesimuliwa kuwa Imaam Abu Ya’alaa alisema, ‘Msimamo wa
Wanachuoni wa Fiqhi kuhusu mtu anayewalaani Maswahaba,
ilhali akiamini kuwa kufanya hivyo inajuzu, ni kwamba
amekufuru. Kama anawalaani ilhali akiamini kuwa kufanya
hivyo haijuzu, basi atakuwa ametenda kosa la ufasiki, na sio
kosa la ukafiri.’ [As-Swaarim al-Masluul, uk. 569].
7- IMAAM ATW-TWAHAAWIY
Katika kitabu chake kuhusu itikadi za Uislamu, al-`Aqiydah
atw-Twahaawiyyah, anasema, ‘Tunawapenda Maswahaba wa
Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam bila kupituka
mipaka katika mapenzi yao au kujiweka mbali na yeyote katika
wao. Tunawachukia wale wanaowachukia na hatusemi ila kheri
kuhusu wao (Maswahaba). Kuwapenda ni kitendo cha kidini, na
dalili ya Imani na ucha Mungu na (kwa upande mwingine)
kuwachukia ni kitendo cha ukafiri, unafiki na ufasiki.’ [Sharhul-
`Aqiydah atw-Twahaawiyyah, uk. 528]
IMAAM IBN HAZM AL-ANDALUSIY
Siku moja, wakati wa utawala wa Waislamu katika nchi ya
Hispania Imaam Abu Muhammad Ibn Hazm alikuwa
akijadiliana na Mapadri Wahispania wa Kikatholiki kuhusu
baadhi ya maandiko ya dini yao. Aliwaletea dalili na hoja
kuhusu kubadilishwa sehemu nyingi katika Biblia na kupotea
kwa maandiko ya asili. Walipomjibu kwamba Mashia pia
4
wanadai kuwa Qur-aan ilibadilishwa na hii tuliyonayo sio ile ya
asili, akajibu, ‘Mashia hawawezi kutumiwa kama hoja dhidi ya
Qur-aan na Waislamu kwani wao wenyewe si Waislamu.’ [Ibn
Hazm, al-Fiswaal fiy al-Milal wa an-Nihal, 2/78 na 4/182]
Madai hayo yao (Mashia) yamejibiwa na wanachuoni wengine
wengi wa zamani kama Ibn Taymiyah katika Minhaaj us
Sunnah, adh-Dhahabiy katika Muntaqaa min Minhaaj al-I`tidaal,
Ibn Kathiyr katika kitabu chake mashuhuri cha historia Al-
Bidaayah wan-Nihaayah, Ibn al Jawziy katika Talbiys Ibliys, na
al-Qaadhiy Ibn al-‘Arabiy katika al-`Awwaasim min al-
Qawaasim]
8-IMAAM AL-ALUUSIY
Mwanachuoni huyu aliwatangaza Mashia kuwa ni makafiri kwa
sababu ya kutukana kwao Maswahaba. Msimamo wake ulikuwa
umechukuliwa kutoka kwenye kauli za Imaam Maalik na
wanachuoni wengine waliokuwa wakiwafikiana nae katika suala
hilo.
Kuhusu madai yao kuwa wao ni katika Ahlul Bayt (familia ya
Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema,
‘Hapana, ukweli ni kwamba wao (Mashia) ni wafuasi wa
Shaytwaan, na Ahlul Bayt hawana uhusiano wowote na wao
(Mashia).
Mwisho:Mashia nimadhehebu machafu na niwaovu kushinda
makaviri imani ya kishia niimani potovu na niimani ya kikafiri.
tumuombe Allah atuepushe na imani za kishia na upotevu
wao,atufishe tukiwa wafuasi wa Mtume Rehma na amani za
Allah ziwe juu yake.