بسم الله الرحمن الرحيم
YATUPASAYO KUFANYA KATIKA MIEZI MITUKUFU.
Utangulizi
Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, na rehma na
amani zimwendee Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na watu wake na
Maswahaba wake wote. Amma baad:
Tumeingia Katika Miezi Mitukufu Inatupasa Kuitakasa Kwa Kuacha Maovu Na
Kuzidisha Mema
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
}إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللّهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَات وَالأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ذَلِكَ
الدِّينُ الْقَيِّمُ فَلاَ تَظْلِمُواْ فِيهِنَّ أَنفُسَكُم{
}Hakika idadi ya miezi kwa Allaah ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya
Allaah, tangu Alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko minne mitakatifu.
Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo} [At-Tawbah:
36[.
Miezi minne hiyo imetajwa katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ أَبَى بَكْرَة أَنَّ رَسُول اللَّه - صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ - قَالَ فِي حَجَّة الْوَدَاع:} إِنَّ الزَّمَان قَدْ اِسْتَدَارَ كَهَيْئَتِهِ
يَوْم خَلَقَ اللَّه السَّمَوَات وَالْأَرْض السَّنَة اِثْنَا عَشَر شَهْرًا مِنْهَا أَرْبَعَة حُرُم : ثَلَاث مُتَوَالِيَات ذُو الْق عَْدَة وَذُو
الْحِجَّة وَالْمُحَرَّم وَرَجَب مُضَر الَّذِي بَيْن جُمَادَى وَشَعْبَان{
صَحِيح الْبُخَارِيّ
Kutoka kwa Abu Bakrah ambaye amesema: “Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) amesema alipokuwa katika Hijjah ya kuaga (Hijjah wa
mwisho): {{Mgawanyo wa nyakati umerudi kama ulivyo (wakati) Allaah
Alipoumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili, minne ambayo ni
mitukufu; mitatu inafuatana pamoja (nayo ni) Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na
Muharram, na (wa nne ni) Rajab wa (kabila la) Mudhwar ambao upo baina ya
Jumaada na Sha'abaan)). [Al-Bukhaariy[
YATUPASAYO KUFANYA KATIKA MIEZI MITUKUFU.
3
Hivyo tunaona kwamba ni kuanzia mwezi huu tulioingia wa Dhul-Qa'adah na
miezi miwili ijayo inayofuatia kisha tena hadi tutakapojaaliwa kufika mwezi wa
Rajab In shaa Allaah.
Katika miezi yote kumi na mbili Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameichagua hii
minne na Ameifanya kuwa ni mitukufu na kusisitiza kuitakasa, na kwamba
dhambi zitakazofanyika humo ni zaidi na hali kadhalika thawabu za vitendo
vyema zinakuwa maradufu na zaidi. [Atw-Twabariy 14: 238[
Ni sawa kama Anavyoonya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kufanya maasi
katika sehemu tukufu Alipotaja Masjidul-Haraam (Msikiti Mtukufu Makkah):
}إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ الَّذِي جَعَلْنَاهُ لِلنَّاسِ سَوَاء الْع اَكِفُ فِيهِ وَالْبَادِ
وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيم{ٍ
}Hakika wale waliokufuru na wakazuilia Njia ya Allaah na Msikiti Mtakatifu,
ambao Tumeufanya kwa ajili ya watu wote sawasawa, kwa wakaao humo na
wageni. Na kila atakayetaka kufanya upotofu humo kwa dhulma, basi
Tutamwonjesha adhabu iumizayo{
]Al-Hajj: 25.[
Qataadah amesema kuhusu kauli ya Allaah:
}فَلاَ تَظْلِمُواْ فِيهِنَّ أَنفُسَكُم{
)Basi msidhulumu nafsi zenu humo)
“Dhulma itakayotendeka katika miezi mitukufu ni mbaya na kubwa (au hatari)
kuliko dhulma itakayotendeka katika miezi mingine. Hakika dhulma daima ni
makosa, lakini Allaah Hufanya baadhi ya vitu kuwa ni vizito kuliko vingine
kama Anavyopenda”.
Akaendelea kusema:
“Allaah Amechagua baadhi ya viumbe Vyake na baadhi ya vitu kuwa bora zaidi
kuliko vingine. Amechagua Wajumbe kuwa ni bora kutoka katika Malaika na
kutoka binaadamu. Vile vile Amechagua baadhi ya kauli Zake kuwa ni bora
kuliko nyingine, Misikiti kuwa bora kuliko sehemu nyingine za ardhi,
Ramadhaan na miezi mitukufu kuwa bora kuliko miezi mingine, siku ya Ijumaa
kuwa ni bora kuliko siku nyingine na usiku wa Laylatul-Qadr kuwa ni bora
kuliko nyusiku zingine. Kwa hiyo takasa vile Alivyovitakasa Allaah, kwani
kufanya hivyo ni vitendo vya watu wenye akili na wenye kufahamu.” [Tafsiyr
ya Ibn Kathiyr[.
YATUPASAYO KUFANYA KATIKA MIEZI MITUKUFU.
4
MIONGONI MWA YALIYOKATAZWA KATIKA MIEZI HII MITUKUFU:
Ni kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala:
}يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ اللّهِ وَكُفْرٌ بِهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ
وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِ مِنْهُ أَكْبَرُ عِندَ اللّهِ وَالْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ الْقَتْلِ{
}Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa Lakini kuzuilia watu wasiende katika Njia ya Allaah na kumkanusha Yeye, na kuzuilia watu wasende kwenye Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wake humo, ni makubwa zaidi mbele ya Allaah. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua{
]Al-Baqarah: 217[.
MAASI MENGINE AMBAYO TUNATAKIWA TUJIKUMBUSHE KUYAACHA:
1.Kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kama kwenda kwa wachawi na waganga na kuwaamini wanayoyatabiri kwa watu
2.Kuiba.
3.Kuzini.
4.Kulewa.
5.Kumdhulumu mtu haki yake.
6.Kugombana, kutukanana, kuvunjiana heshima, kudharauliana n.k.
7.Kusengenya (Ghiybah(
8.Kusema uongo, na kila aina ya uovu mwengine.
MAMBO MEMA YA KUKUMBUSHANA KUFANYA KATIKA MIEZI HII MITUKUFU:
1.Kuongeza Sunnah za Swalah,
2.Kufunga Swawm za Sunnah kama Jumatatu na Alkhamiys, Ayyaamul-Biydhw (tarehe 13,14 na 15) na Swawm ya Nabii Daawuwd (kufunga kila baada ya siku moja)
3.Kujielimisha mambo ya dini kwa kusoma vitabu na kusikiliza mawaidha;
4.Kuomba Maghfirah na Tawbah;
YATUPASAYO KUFANYA KATIKA MIEZI MITUKUFU.
5
5.Kufanya kila aina ya dhikr (kumkumbuka na kumtaja Allaah), kwa kusoma Qur-aan kwa wingi, kumshukuru, kumtukuza, kuomba du'aa n.k;.
6.Kuwasiliana na ndugu na jamaa;
7.Kutenda wema kwa jirani, marafiki na watu wote kwa ujumla;
8.Kutoa sadaka;
9.Kulisha masikini;
10.Kupatanisha waliogombana;
11.Kuamrishana mema na kukatazana maovu, na mengi mengineyo katika vitendo vyema.
Allaah Atupe tawfiq tuepukane na maasi na atujaalie tufanye mema katika miezi hii mitukufu na miezi mingine, Ameen.
YATUPASAYO KUFANYA KATIKA MIEZI MITUKUFU.
6