Nakala

1


بسم الله الرحمن الرحمن الرحيم


VIPI ANATAKIWA AWE MWANAMKE MWEMA? Imeandaliwa na: Yunus Kanuni Ngenda Imepitiwa na: Abubakari Shabani Rukonkwa. Mwanamke mwema huimarisha ndoa yake kwa kutekeleza haki za mumewake, na hayo ndio maamrisho ambayo ameamrishwa na Allah mtukufu. Chukua tahadhari ewe mwanamke wa kiislamu ili usiingie motoni! Anasema Mtume s.a.w:- عن عبد الله ابن أبي أوفى أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:"لو كنت آمراً


أحداً أن يسجد لغير الله تعالى لأمرت المرأة أن تسجد لزوجها، و الذي نفس


محمد بيده لا تؤدي المرأة حق ربها حتى تؤدي حق زوجها كله حتى لو


) سألها نفسها وهي على قتب لم تمنعه" )السلسلة الصحيحة 3021


Kutoka kwa Abdullah bin abii awfaa Radhi za Allah ziwe juuyake, hakika Mtume (Swalla Allaahu alayhi wasallam) alimesema:- ((Ningekuwa nimwenye kuamrisha mmoja wenu amsujudie asie kuwa Allah basi ningemuamrisha mwanamke amsujudie mumewe, Ninaapa kwa Allah ambae nafsi ya Muhammad iko mikononi mwake mwanamke hawezi kutekeleza haki za mola wake mpaka atekeleze haki zote za mume wake kwanza, hata akimuomba mumewe nafsi yake (akimuhitaji) akiwa jikoni mke hana haki yoyote yakukataa".


2


Subhana Allah! !


Subhana Allah! !.


Muogopeni Allah enyi wanawake Allah hakuwapa


wanaume daraja hiyo ila nibaada yakuona shida na taabu


ya majukumu ya kuitunza familia tulieni majumbani na


muwatii waume zenu.


Mwanamke kukaa nyumbani na kumtii mumewe kwa


kila jambo la halali basi mwanamke huyo analipwa


thawabu za sawa na mtu aliyepigana jihadi.


Na miongoni mwa haki za mume kwa kwa mkewe:-


1-Ni mwanamke kuwa radhi pindi mumewe atakapo


muhitaji (falagha) kitandani.


Anasema Mtume s.a.w:-


عن عبدالرحمن بن عوف رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه


وسلم:إذا دعا الرجل امرأته إلى فراشه فأبت فبات غضبان عليها لعنتها


.الملائكة حتى تصبح " البخار ومسلم


Kutoka kwa Abdurahmani bin Aufi Radhi za Allah ziwe


juu yake alisema:-


Alisema Mtume rehma na amani zewe juu yake: ((Pindi


mume atakapo muita (atakapo muhitaji) mkewe


kitandani kisha mwanamke akakataa, mwanaume akalala


hali ya kua amekasirika kwa kitendo kile basi malaaika


wanamlaani yule mwanamke mpaka asubuhi))


(Bukhari na muslim).


Inna lillahi wainna ilayhi rajiuna! Niwanawake wangapi


walioko kwenye ndoa na kila siku wanalaaniwa na


malaika?


3


Enyi kina mama wa kiislam hivi mnajua maana ya laana?


Maana ya laana ni mtu kufukuzwa (kutolewa) katika


Rehma za Allah.


Sasa ukitolewa katika rehma za Allah utakuwa katika


rehma za nani!?


Basi ni vema enyi kina mama wa kiislam kumuogopa


Allah na kujitahidi kuzitekeleza haki za waume zenu


kwani wao ni sababu kubwa ya nyinyi kuingia Peponi.


Anasema mtume (S.a.w):





Imekuja kutoka kwa Abiy Said Alkhudriy Radhi za Allah ziwe


juu yake: Alikuja mtu kwa Mtume (s.a.w) na binti yake,


akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Huyu binti yangu


amekataa kuolewa. Mtume s.a.w akamwambia Yule binti (ewe


binti) mtii baba yako. Yule binti akasema ninaapa kwa


Mwenyezi Mungu ambae amekutuma kwa haki siolewi mpaka


unieleze haki za mume kwa mkewe. Akasema Mtume S.a.w:


haki za mume kwa mke wake nikwamba laiti angekuwa mume


wako ana kidonda chenye usaha kisha mke akakilamba kile


kidonda kwa ulimi wake basi asingekuwa ametekeleza mke haki


yake kwa mumewe)


4


Wameongeza baadhi ya wapokezi :(laiti usaha au damu


ingetapakaa kwenye midomo ya mke kisha akameza usaha au


damu ya mume asingekuwa ametekeleza haki ya mume wake).


Akasema Yule binti: ninaapa kwa Mwenyezi Mungu ambae alie


kutuma kwa haki kamwe sita olewa,


Akasema mtume S.a.w: Basi msiwaozeshe mabinti zenu ila kwa


idhini yao).


(Ameipokea ibn Abii Shayba na Anasaai).


2-Mwanamke kutomuweka katika kitanda chake


mwanaume asiekua mumewe.


Alisema Mtume s.a.w katika khutbatul-wadaa, khutba ya


kuaga:-


((....أما بعد: أيها الناس إن لنسائكم عليكم حقا ولكم عليهن حق، لكم أن لا


يواطئن فرشهم غيركم...))


Ama baada: Enyi watu hakika wake zenu wana haki


kwenu na nyinyi mna haki kwao, (katika haki zenu kwao


wake zenu) wasiwaweke katika vitanda vyao wanaume


wasiokua nyinyi.


3-Mwanamke asimuingize ndani mtu yeyote ambae


mumewe anamchukia.


Anasema Mtume s.a.w:-


((..ولا يدخلن أحدا تكرهونه بيوتكم إلا بإذنكم...))


Na wala wasiingize katika nyumba zenu mtu yeyote


(katika watu) mnaowachukia.


4-Kutokufanya mambo machafu, (na maovu) kwani


kufanya hivo kutapelekea kuhamwa kitanda nk.


5


Anasema Mtume s.a.w:- )ولا يأتين بفاحشة، فإن الله قد أذن لكم أن تعضلوهن و تهجروهن في


المضاجع و تضربوهن ضربا غير مبرح(


Na wala wasifanye mambo machafu (maovu kwasababu wakifanya hivo) hakika Allah ametoa idhini (amewaruhusu wanaume) kuwahama (wanawake hao) katika vitanda na kuwapiga kipigo kisichoumiza. Hizo ni baadhi ya haki za mume juu ya mkewe, zipo haki nyingi sana za mke na mume ambazo kama wana ndoa watazizingatia kwa umakini basi misukosuko katika ndoa itakwisha na kutashamiri upendo, huruma, upole na ihsani. Tambih, (Uzinduo) Enyi wanawake wa kiislam mlio katika ndoa na nyinyi kina dada mnaotarajia kuingia katika ndoa, ni vema mkajitahidi kuzisoma ndoa zenu ili muweze kuzijua haki zenu kwa waume zenu na haki za waume zenu juu yenu hiyo itakua rahisi kwako kuzitekeleza. Qur'ani iko wazi sana katika kuzielezea khabari hizi, na Sunna za Mtume s.a.w ziko wazi! Pia mnashauriwa akina mama wa kiislam kusoma vitabu na kusikiliza mawaidha mbalimbali yanayohusu mambo ya ndoa, maana mmekua wepesi kumtunza bibi harusi vyombo vya kupikia kuliko kumzawadia vitabu vya hukum za ndoa. Ndoa ni nusu ya dini Ndoa ni ibada yaqini


6


Ndoa ni utulivu makini Ndoa hujaza mapenzi rohoni Ndoa hueneza huruma moyoni Anasema Allah s.w:- )و من آياته أن خلق لكم من أنفسكم أزواجا لتسكنوا إليها و جعل بينكم مودة


و رحمة(


((Na katika alama zake Allah (s.w) ni kwamba amewaumbia kutokana na nafsi zenu wake ili mpate utulivu utulivu kwao, na akajalia baina yenu mapenzi na huruma)) Tumuomba Allah ajaalie katika majumba yetu upendo, huruma, furaha na ucha Mungu. Ewe Allah tunakuomba wajaalie wanawake wa kiislamu walio katika ndoa waweze kutekeleza haki za waume zao, na wao watekelezewe haki zao na waume zao. Ameeen!



Machapisho ya hivi karibuni

Uislamu Ni dini ya ma ...

Uislamu Ni dini ya maumbile na akili na furaha

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL