Nakala




UMUHIMU WA KUKIMBILIA KUTEKELEZA NGUZO YA HIJJA.





بسم الله الرحمن الرحيم


UMUHIMU WA KUKIMBILIA KUTEKELEZA


NGUZO YA HIJJA.


Utangulizi


Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, na rehma na


amani zimwendee Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na watu wake na


Maswahaba wake wote. Amma baad:


Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala:


))وَ هّ لِلّ عَلَى النَّاسّ حّجُّ الْبَيْتّ مَنّ اسْتَطَاعَ إّلَيْهّ سَبّيلاً وَمَن كَفَرَ فَإّنَّ الله غَنّيٌّ عَنّ الْعَالَمّ ينَ((


))Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze Hajj katika Nyumba


hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni Ghaniyy


(Mkwasi) kwa walimwengu))


[Al-'Imraan: 96-97[.


Na kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam(


))بني الإسلام على خمس شهادة أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمِّداً رسولُ الله وإقام الصلاة ، وإيتاء الزكاة،


وصوم رمضان، وحج البيت(( متفق عليه


)Uislamu umejengeka kwa matano; Kushuhudia kwamba hakuna ilaah


(Muabudiwa wa haki) isipokuwa Allaah, na Muhammad ni Rasuli wa Allaah,


kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan, na kuhijii katika


Nyumba (tukufu))


[Al-Bukhaariy na Muslim[


Tunatambua kutokana na kauli hizo za utangulizi kuwa kutekeleza ‘ibaadah ya


Hajj ni fardh kwa kila mwenye uwezo. Hivyo asiyeharakisha kutekeleza


‘ibaadah hii atakuwa amemuasi Mola wake na Mtume Wake (Swalla Allaahu


'alayhi wa aalihi wa sallam) na itakuwa ni dhambi kubwa kwake ikiwa kuacha


huko ni kwa makusudi na hali alikuwa ana uwezo wa mali, siha n.k., sababu


atakuwa amekanusha amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kama


Anavyosema:


 3 


))وَمَا كَانَ لّمُؤْمّ نٍ وَلَا مُؤْمّنَةٍ إّذَا قَضَى اللهَُّ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخّيَرَةُ مّنْ أَمْرّهّمْ وَمَن يَعْصّ اللهَ


وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبّينًا((


Na haiwi kwa Muumini mwanamme na wala kwa Muumini mwanamke, ((


Anapohukumu Allaah na Rasuli Wake jambo lolote, iwe wana hiari katika


jambo lao. Na anayemuasi Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amepotoka


upotofu bayana)) [Al-Ahzaab: 36


KWANINI MUISLAM AHARAKISHE KUTEKELEZA HAJJ?


1. Huenda Akafikwa Na Masaibu:


Muislamu mwenye uwezo wa fedha na siha inampasa afanye hima kutimiza


fardhi hii kabla ya kufikwa na masaibu kwani huenda ukawa humiliki tena siku


za mbele.


Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuhimiza na


kutuonya hayo:


))مَنْ أَرَادَ الْحَجَّ فَلْ يَتَعَجَّلْ(( . رواه الإمام أحمد وأبو داود وابن ماجه.


وفي رواية أحمد وابن ماجه: )) فَإّنَّهُ قَدْ يَمْرَضُ الْمَرّيضُ ، وَتَعْرّضُ الْحَاجَةُ((


حسنه الألباني في صحيح ابن ماجه.


Mwenye kutaka kufanya Hijjah basi aharakize.


[Imaam Ahmad, Abu Daawuud na Ibn Maajah]


Na katika riwaayah ya Ahmad na Ibn Maajah ((Kwani huenda akapata maradhi


au akafikwa na haja)).


Maajah[[Kaipa daraja ya Hasan Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh-Ibn .


Vile vile amesema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa


)sallam


))تعجلوا إلى الحج )يعني الفريضة( فإن أحدكم لا يدري ما يعرض له(( أخرجه الإمام أحمد رحمه الله


وحسَّنه الألباني في إرواء الغليل.


Harakizeni Hajj, (yaani kutekeleza fardhi ya Hajj) ((kwani hajui mmoja wenu ((


nini kitamsibu)). [Imaam Ahmad na kaipa daraja ya hasan Shaykh Al-Albaaniy


]katika Irwaaul-Ghaliyl


2.Hatuna Dhamana Na Umri Mrefu


Waislamu wengi hawaifanyii hima ibada hii na aghalabu ya sababu ni:


 4 


a)Wengine huona kuwa ni bado vijana hivyo wanasubiri wawe na umri mkubwa ndio watimize. Hao wajiulize; je, wana uhakika gani kuwa wataruzukiwa umri mrefu? Bali wana dhamana gani kama wataishi hata mwaka mmoja zaidi? Au mwezi mmoja zaidi? Au wiki moja zaidi? Au hata siku moja zaidi? Hawasomi kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala:)


))وَمَا تَدْرّي نَفْسٌ مَّاذَ ا تَكْسّبُ غَدًا وَمَا تَدْرّي نَفْسٌ بّأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ إّنَّ اللهََّ عَلّيمٌ خَبّير((


))na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni ‘Aliymun-Khabiyr (Mjuzi wa yote - Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana)) [Luqmaan: 34[.


b)Wengine wameshughulika na anasa za dunia na kujisahau kabisa kama huenda wakaondoka duniani wakiwa katika hali hizo za mapenzi ya dunia huku wameacha kutenda yaliyo muhimu kama ‘ibaadah hii ya fardhi. Nafsi inayojidhulumu kama hivi hujuta wakati wa kutolewa roho yake, na hutamani arudi atende yale aliyoyakosa kutenda lakini haiwezekani tena kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):


))حَتَّى إّذَا جَاء أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجّعُونّ(( )) لَعَ لِّي أَعْمَلُ صَالّحًا فّيمَا تَرَكْتُ كَلَّا إّنَّهَا كَلّمَةٌ هُوَ


قَائّلُهَا وَمّن وَرَائّهّم بَرْزَخٌ إّلَى يَوْمّ يُبْعَثُونَ((


))Mpaka itakapomfikia mmoja wao mauti, atasema: “Rabb wangu! Nirejeshe (duniani).” Ili nikatende mema katika yale niliyoyaacha.” (Ataambiwa) “Wapi!” Hakika hilo ni neno (tu) yeye ndiye msemaji wake. Na nyuma yao kuna barzakh (maisha baada ya kufa) mpaka Siku watakayofufuliwa)) [Al-Mu-minuwn: 99-100.[


3. Ni ‘Amali Bora Kabisa


سئل النبي صلى الله عليه وسلم أي العمل أفضل؟ قال: ))إيمان بالِل ورسوله(( قيل: ثم ماذا؟ قال:


))الجهاد في سبيل الله((" قيل ثم ماذا؟ قال: ))حج مبرور(( متفق عليه


Aliulizwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Ipi amali njema kabisa? Akasema: ((Kumuamini Allaah na Rasuli Wake)) Akaulizwa: "Kisha nini"? Akasema: ((Jihaad katika Njia ya Allaah)) Akaulizwa: "Kisha nini"? Aakasema: ((Hajj yenye kukubaliwa)). [Al-Bukhaariy na Muslim.[


 5 


4. Hufutiwa Madhambi Yote


عن أبي هريرة رضي الله عنه قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ))من حج، فلم يرفث ولم


يفسق، رجع كيوم ولدته أمه(( متفق عليه


Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayefanya Hajj, kisha asiseme maneno machafu wala asitende vitendo vichafu atarudi akiwa kama siku aliyozaliwa na mama yake)) [Al-Bukhaariy na Muslim[


5. Jazaa Yake Ni Jannah


عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: "))العمرة إلى العمرة كفارة لما


بينهما، والحج المبرور ليس له جزاء إلا الجنة(( متفق عليه


Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (('Umrah hadi 'Umrah ni kafara (kufutiwa dhambi) baina yao, na Hajjul-Mabruwr [yenye kukubaliwa] haina jazaa isipokuwa ni Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim.[


Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atujaalie Waislamu sote uwezo wa kutekeleza nguzo hii muhimu na atukutanishe Peponi pamoja na Mtume wetu Muhammad (s.a.w), Ameen.


 6 



Machapisho ya hivi karibuni

Uislamu Ni dini ya ma ...

Uislamu Ni dini ya maumbile na akili na furaha

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL