1
بسم الله الرحمن الرحيم
UMMATI MUHAMMAD UTAKUWA WA KWANZA KUINGIA PEPONI. Imeandaliwa na alhidaaya.com Imepitiwa na Yunus Kanuni Ngenda Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((Watu wote walikuwa ni Umma mmoja. Allaah Akapeleka Manabii wabashiri na waonyaji. Na pamoja nao Akateremsha Kitabu kwa Haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale waliokhitalifiana. Na wala hawakukhitalifiana ila wale waliopewa Kitabu hicho baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina yao. Ndipo Allaah kwa idhini Yake Akawaongoa walioamini kuiendea haki katika mambo waliyokhitalifiana. Na Allaah Humwongoa Amtakaye kwenye Njia Iliyonyooka)) [Al-Baqarah: 213] Ibn 'Abbaas amesema kuhusu kauli hii: "Kulikuweko na vizazi (karne) kumi baina ya Aadam (‘AlayhisSalaam) na Nuuh (‘Alayhis Salaam), wote wakiwa katika dini ya haki. Kisha tena wakakhitilafiana, hivyo Allah Akatuma Mitume kama waonyaji na wabashiriaji" [Tafsiyr Ibn Kathiyr].
2
Idadi ya Mitume ni 124,000 wakiwemo Wajumbe
313 kama ilivyo kauli ya wengi wa Maulamaa wa Ahlus-Sunnah
wal Jama’ah. Mitume 25 wametajwa majina yao katika Qur-aan.
[Aysarut-Tafaasiyr – Abu Bakr Al-Jazaairy 1:191]
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) alisema kuhusu kauli:
((Ndipo Allaah kwa idhini Yake Akawaongoa walioamini
kuiendea haki katika mambo waliyokhitalifiana))
Akasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) amesema:
((Sisi ni (Ummah) wa mwisho lakini ni wa kwanza siku ya
Qiyaamah. Sisi ni wa kwanza kuingia Peponi ingawa wao
(Mayahudi na Manaswara) walipewa Kitabu kabla yetu nasi
tumepewa baada yao. Allaah Ametuongoza katika haki katika
waliyokhitilafiana kwa idhini Yake. Hii ni siku (Ijumaa)
waliyokhitilafiana, nasi Allah Ametuongoza nayo Hivyo watu
wanatufuata kwani kesho (Jumamosi) ni siku ya Mayahudi na
inayofuatia (Jumapili) ni ya Manaswara)) [Al-Bukhaariy, Muslim,
Musnad Ahmad na wengineo]
3
Ibn Wahb amesema kwamba 'Abdur-Rahmaan bin Zayd bin
Aslam amesema kuwa baba yake amesema kuhusu Aayah hii:
)) ا ف ا ه ا دى الُلّه الََِّّي ا ن آ ا منُواْ لِ ا ما اخْتالافُواْ فِيهِ مِ ا ن الْْاقِّ بِإِذْنِهِ ((
((Ndipo Allaah kwa idhini Yake Akawaongoa walioamini
kuiendea haki katika mambo waliyokhitalifiana))
Wamekhitilafiana kuhusu siku ya Jamaa (Ijumaa); Mayahudi
wamesema ni Jumamosi, Manaswara wamesema ni Jumapili,
Allaah Akaongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) kufuata Ijumaa.
Wamekhitilafiana kuhusu Qiblah; Manaswara wameelekea
Mashariki na Mayahudi wameelekea Baytul-Maqdis (Palestina),
Allaah Akaongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Qiblah sahihi (Ka'bah
iliyoko Makkah).
Wamekhitilafiana kuhusu Swalah; wengine wanarukuu lakini
hawasujudu, wengine wanasujudu lakini hawarukuu, wengine
wanaswali huku wakizungumza na wengine huku wanatembea.
Allaah Amewaongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) katika haki.
Wamekhitilafiana pia katika kufunga (Swawm); wengine
wanafunga sehemu tu ya siku, wengine wanafunga kujizuia tu
baadhi ya vyakula (vingine wanakula). Allaah Ameongoza
Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) katika haki.
4
Wamekhitilafiana pia kuhusu Nabii Ibraahiym; Mayahudi
wamesema "Alikuwa ni Myahudi" na Wakristo wakidai ni
Mnaswara. Allaah Amemfanya ni Haniyfam-
Musliman (Muongofu Muislamu) Allaah Ameongoza Ummah wa
Muhammad katika haki.
Wamekhitilafiana pia kuhusu Nabii 'Iysaa; Mayahudi
wamemkanusha na kumzulia mama yake kuwa kafanya madhambi
makubwa (ya zinaa), Manaswara wamemfanya ni Mungu na mtoto
wa mungu. Allaah Amemfanya kwa maneno Yake ni roho kutoka
Kwake (Kwa Alivyoviumba) Allaah Ameongoza Ummah wa
Muhammad katika haki"
Kisha (muelezeaji) akamalizia maelezo hayo kwa kusema (Kwa
idhini Yake [Allaah]) (kamailivyoendeleza Aayah hiyo tukufu
kuwa sisi Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) tumeongozwa na Allaah kwa Idhini Yake).
((Ndipo Allaah kwa idhini Yake Akawaongoa walioamini
kuiendea haki katika mambo waliyokhitalifiana))
Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anhaa) amesimulia kuwa
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa
anapoamka usiku akisoma duaa ifuatayo:
Allaahuuma Rabbi Jibraaiyl wa Miykaaiyl, wa Israafiyl,
Fatwiras-Samawaati wal-ardhw, 'Aalimal-Ghaybi wash-
Shahaadah, Anta Tahkumu bayna 'Ibaadika fiymaa kaanu fiyhi
yakhtalifuun. Ihdiniy lima-khtulifa fiyhi minal-Haqq Biidhnika,
Innaka Tahdiy man Tashaau ilaa Swiraatwim Mustaqiym.
Ee Allaah Mola wa Jibriyl na Mikaaiyl na Israafiyl, Muumba
wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo yaliyojificha na yaliyowazi,
Wewe Unahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo
walikuwa wakitofautiana, niongoze mimi kwenye haki katika yale
waliotofautiana kwa ruhusa Yako. Hakika Wewe Unamuongoza
Umtakae kwenye Njia Ilionyoka.
Zaidi ya du'aa hiyo inatupasa pia tuombe du'aa ifuatayo daima ili
tubakie katika haki,
Allaahumma Arinal-Haqqa Haqqan War-Zuqnat-tibaa'ah. Wa
Arinal-Baatwila baatwilan War-Zuqnaj-tinaabah. Wa laa taj'alhu
mutalabbisan 'alaynaa Fanadhwilla Waj-'alnaa Lil-Muttaqiyna
Imaama.
Ee Allaah, Tuonyeshe yale yaliyo haki, Uturuzuku tuweze
kufuata (na kutekeleza).
Na Tuonyeshe yaliyo batili (maovu) na Utuongoze tujiepushe
nayo.
Usituchanganye (usitufunike tusiiujue) hakika ya uovu ili
tusipotee kuufuata, na Tujaaliye tuwe viongozi wa Wamumini))
[Takhiryj Al-Ihyaaa 3: 1318].