Nakala




UBORA WA TAWHIYD





IMEANDIKWA: SHEKH: YASINI TWAHA HASAN


IMEPITIWA:


ABUBAKARI SHABANI RUKONKWA.





بسم الله الرحمن الرحيم


Utangulizi:


Shukrani zote ni zake Mola wa ulimwengu wote, na mwisho


mwema nikwawamchao Allah, na hapana uadui isipokuwa


kwa madhalimu.


Nashuhudia kuwa hapana anayestahiki kuabudiwa isipokuwa


Allah Peke yake Asiye na mshirika Mwenye Ufalme na haki


iliyo wazi. Na nashuhudia kuwa Muhammad (s.a.w) ni


mjumbe wake na Mtume wake nawa mwisho wa wajumbe


wake na ni kiongozi wa wacha Mungu. Mola wetu mswalie na


msalimie Mtume wako huyu pamoja na Masahaba wake na


kila atakayemfuata kwa wema na uongofu mpaka Siku ya


Qiyama.


Tawhiyd Ni Bora kuliko Mali Na Starehe Za Duniani Na


Neno La Tawhiyd litakuwa Zito Siku ya Qiyaamah


Makafiri wa Kiquraysh wa Makkah walitaka kumpa Rasuli


(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mali na starehe


za dunia, walitaka kumpa cheo ili aache kulingania Tawhiyd


lakini Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)


hakufadhilisha hayo, bali alijikita katika da’wah yake kwa


kuwa aliamini kulingania Tawhiyd ndio haki na ndio


itakayomfaa bin Aadam Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo mtu


atatamani kufidia kwa mali yake yote aliyokuwa nayo duniani


ili aepukane na adhabu ya Moto kwa kukanusha Tawhiyd.





Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri,


basi haitokubaliwa kutoka kwa mmoja wao (fidia ya) dhahabu


ya kujaza dunia nzima lau wakitaka kujikombolea nayo. Hao


watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye


kuwanusuru. [Aal-‘Imraan: 91]


Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)


amesema katika Hadiyth iliyosimuliwa na Anas bin Maalik


(Radhwiya Allaahu ‘anhu):





((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Atamwambia mtu


atakayekuwa na adhabu nyepesi kabisa Motoni “Je, ungekuwa


una dunia nzima na yaliyomo ndani yake [mali n.k.]


ungeitolea fidia?”)) Atajibu ((Ndio)) Atasema Allaah:


((Nilikutaka kwa jambo jepesi zaidi kuliko hayo, ulipokuwa


katika uti wa mgongo wa Aadam kwamba usinishirikishe))


Nadhani Akasema: (na sitokuingiza motoni lakini umekataa


isipokuwa kunishirikisha)). [Muslim]


Ni dhahiri kwamba Tawhiyd ambalo ni jambo jepesi kabisa


itakuwa na thamani zaidi kuliko dunia na yaliyomo duniani,


3


3


bali neno la Tawhiyd; laa ilaa illa Allaah litakuwa zito kabisa katika Miyzaan ya ‘amali Siku ya Qiyaamah: ْ  Imepokewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudhriyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muwsaa alisema: Ee Mola wangu! Nifundishe kitu ambacho kwacho nikudhukuru na nikuombe du’aa. Akasema [Allaah]: Ee Musa: Sema: “Laa ilaaha illa-Allaah”. Muwsaa akasema: Ee Mola wangu! Kila mja anasema hivi. Akasema [Allaah]: Ee Musa, lau kama mbingu saba na kila kilichokuwemo isipokuwa Mimi, na ardhi saba zikiwekwa katika kiganja cha mizani, na laa ilaaha illa-Allaah imewekwa katika kiganja kingine cha mizani, basi laa ilaaha illa-Allaah itazishinda hizo)). [Ibn Hibaan na Al-Haakim, na ameikiri kuwa ni Swahiyh].


FAIDA ZA TAWHIID:


Tawheed inafaida nyingi sana miongoni mwa faida hizo:


1.Nisababu ya kuondoshewa matatizo ya kidunia na Akhera na kuziwiya adhabu zake.


2.Inamziwiya mwanadamu kuishi milele motoni ikiwa katika moyo wake kuna kiasi cha imani kinacho lingana na tembe


4


4


ndogo ya khaldali, na anapokua na imani kamili tawheed inamziwiya kuingia motoni.


3.Mwenye tawheed anapata uongofu ulio kamilika na amani ilio timia katika dunia na akhera.


4.Tawheed nisababu ya kupata radhi za Allah na thawabu zake, hakika atakae fanikiwa na uombezi wa mtume (s.a.w) siku ya qiyama niyule alie sema : (la ilaha ila Allah ) akitaraji malipo kwa Allah.


5.hakika matendo ya mwanadamu ya dhahiri na yasiri hayawezi kukubaliwa pindi anapokuwa mtu hana Tawheed.


6.Tawheed inamrahisishia mja kufanya kheri nakuacha mambo machafu, na inamlewaza pale penye misiba na masononeko.


Tunamuomba Allah mtukufu atupe imani zilizo thabiti na atufutie madhambi yetu na atupe mwisho mwema.



Machapisho ya hivi karibuni

Uislamu Ni dini ya ma ...

Uislamu Ni dini ya maumbile na akili na furaha

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL