Nakala

1436


UBORA WA KUAMRISHANA MEMA NA KUKATAZANA MAOVU.


KISWAHILI.


IMEANDIKWA NA: SHEKH YUNS KANUNI NGENDA.


IMEPITIWA NA :


ABUBAKARI SHABANI RUKONKWA


---------------------------------------------------------


1


Utangulizi


Ndugu waislamu hakika Allaah [Subhaanahu wa Ta’ala] anatuamrisha tuamrishane mema na tukatazane maovu ili tuweze kufanikiwa.


" Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri [Uislamu] na unao amrisha mema [Tawheed na maamrisho yote ya Uislamu] na unakataza maovu [Ushirikina na ukafiri na makatazo yote ya Uislamu]. Na hao ndio walio fanikiwa.


]Qur'an,3:104[


Mtume (s.a.w) amesema:“Yule ambaye atakae uona uovu basi aubadilishe kwa mkono wake;kama hawezi kufanya hivyo,basi akemee kwa ulimi wake;na kama hawezi kufanya hivyo basi na achukie moyoni mwake na huko ndio udhaifu zaidi wa imani”.


] Muslim,2/22-25; Tirmidhi,9/18-19; Dawud,1128; Nasa'i’,8/111; Majah,4013 .[


Ummah wetu umekuwa ni ummah bora juu ya ummah zote zilizopita kwa sababu tuamrishana mema na tunakatazana mabaya.


" Nyinyi [Waumini wa kweli wa Tawheed] mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema [Tawheed na maamrisho yote ya Uislamu] na mnakataza maovu [Ushirikina na ukafiri na makatazo yote ya Uislamu], na mnamuamini Allaah"..


]Quran 3:110[


Kuamrishana mema na kukatazana mabaya ni sifa za


2


'Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu'


] Qur'an,9:71]


Ama wanafiki wao huamrisha maovu na huyakataza mema.


'Wanaume wanaafiki na wanawake wanaafiki, wote ni hali moja. Huamrisha maovu na huyakataza mema [Qur'an,9:67]


Ndugu waislamu kama hatutoamrishana mema na kukatazana mabaya,basi tupo hatarini kupata adhabu kali kutoka kwa Allaah,kama zifuatazo.


}1{Tutapata adhabu kali na dua zetu hazitojibiwa.


Mtume (s.a.w) amesema: “Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, Ni lazima muamrishane mema na kukatazana mabaya,au[kama hamkufanya hivyo] Allaah hakika muda mchache tu atawaletea adhabu kutoka Kwake,na kisha mumuombe Yeye na asiwajibu du’aa zenu.


] Tirmidhee (2169) Shaikh al-Albaanee amesema ni hadeeth 'Hassan]'


Mtume (s.a.w) amesema: “Ikiwa maasi yatafanyika katika watu wowote wale,na wasiyabadilishe ingawa wanauwezo wa kufanya hivyo [kuyabadilisha ,kuyaondoa] ,basi Allaah muda mfupi tu atawaadhibu wote[wanaotenda maasi na wasiotenda ]


”.


(Abu Dawud, 4316; Ibn Majah, 4005; Ahmed, 1/16).


}2{Kupata hasira na laana ya Allaah kama ilivyotokea kwa wana wa Israel.


"Walilaaniwa walio kufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi[Allaah na Mitume yake] na wakawa


3


wanapindukia mipaka.Walikuwa hawakatazani maovu waliyo kuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyo kuwa wakiyafanya !


]Quran 5:78- 79[


Ndugu muislamu kuamrishana mema na kukatazana mabaya ni miongoni mwa matendo ya Jihad kwa ajili ya Allaah kwani kuna ugumu ndani yake na tunatakiwa tuwe na subra kwa matusi na madhara katika hili.Kama Luqmaan alivyomshauri mwanawe


" Ewe mwanangu! Shika Sala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa."[Qur'an, 31:17[


Tunapoamrishana mema na kukatazana mabaya,basi tusijisahau wenyewe katika utendaji kama Allaah anavyo tuonya vikali katika aya hizi.


Je! Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii ?


] Qur'an,2:44]"Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda?Yanachukiza vikubwa mno kwa Allaah kuwa mnasema msiyo yatenda.


]Qur'an,61:2-3 "[


Ndugu waislamu kuamrishana mema na kukatazana mabaya ni kazi tukufu,hivyo wanaofanya kazi hii ni lazima wawe na elimu sahihi ya wanachokiamrisha au kukitataza,na wawe na matendo mema,na pia wawe na busara na kauli njema ili in shaa Allaah watu waongoke kupitia mikono yako.Allaah anasema:


" Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi [Uislamu] kwa hikima[kwa Qur'an na Sunnah] na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola


4


wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka.


]Qur'an,16:125[


Basi ndugu waislamu ni wajibu wetu kuendelea kuamrishana mema na kukatazana mabaya.Tunamuomba Allaah atufanyie wepesi katika hili,Aamyn



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI