Nakala

1


حُسن الخلق


TABIA NJEMA





MTUNZI: ABDULMALIK AL'QAASIM


MFASIRI NI SHEIKH. HAMZA RAJABU SEIF


KIMEREJEWA NA SHEKH: YASSINI TWAHA


NA SHEKH YUNUS KANUNI NGENDA


2


بسم الله الرحمن الرحيم


Utangulizi


Kila sifa njema zinamstahikia Allah Ambaye Ameumba


kila kitu na akakitengeneza vizuri na kukipangilia, na


akamfundisha adabu Nabii wetu Muhammad Rehma na


Amani za Allah ziwe Juu Yake, kisha akazifanya kuwa ni


nzuri zaidi.


Ama baada ya utangulizi huo:


Hakika Tabia njema ni sifa miongoni mwa sifa za


Manabii na Wakweli na Wema, kwa Tabia hizo


hupandishwa Daraja ya juu kabisa, na hupandishwa


Heshima/vyeo.


Na kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu


Amemuhusisha Nabii Muhammad Rehma na Amani za


Allah ziwe juu yake kwa Aya ambayo imekusanya sifa


zenye kusifika (na uzuri) na adabu nzuri, Akasema


Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na hakika wewe una tabia


njema).(Alqalam: 4).


Na tabia njema hupelekea kupendana na kushikamana


(katika mambo ya kheri), na (kinyume chake) tabia mbaya


huzaa kubughudhiana na kuhusudiana na kupeana


nyongo/kupeana mgongo.


Na kwa hakika amehimiza Mtume Rehma na Amani za


Allah ziwe Juu Yake, juu ya tabia nzuri na kushikamana


nayo, na akaunganisha kati ya Ucha Mungu na tabia njema


aliposema: (Mambo mengi yatakayo waingiza watu wengi


Peponi ni kumcha Allah na kuwa na tabia njema). Hadithi


imepokelewa na Imam Tirmidhi na Alhaakim).)


Na maana ya tabia njema: Ni kuuachia uso/kutabasamu,


na kutoa mambo mazuri, na kujizuia kuwafanyia watu


3


uovu, haya ni pamoja na yale anayo shikamana nayo


Muislamu katika kuongea maneno mazuri, na kujizuia na


ghadhabu na kuvumilia maudhi.


Na Mtume Rehma na Amani za Allah ziwe Juu Yake


alimuusia Abaa huraira Radhi za Allah ziwe juu yake usia


mkubwa sana aliposema: (Ewe Abaa Huraira! Ni juu yako


kushikamana na tabia njema, akauliza Abuu Huraira: na ni


ipi hiyo tabia njema ewe Mtume wa Allah? Akasema:


"Muunge aliyekata undugu, na umsamehe aliyekudhulumu,


na umpe aliyekunyima"). Hadithi ameipokea Imam


Al'baihaqi.


Na hebu zingatia kwa makini –ewe ndugu yangu


mkarimu- Athari kubwa na malipo makubwa ya hili tendo


zuri lililosifika, na tabia nzuri, kwa hakika amesema


Mtume Rehma Na Amani za Allah ziwe Juu Yake: (Hakika


mtu atafikia daraja ya Aliyefunga, na Aliyesimama usiku


kwa tabia yake nzuri).Hadithi ameipokea Imamu Ahmad).)


Na hakika Mtume Rehma na Amani za Allah ziwe Juu


Yake Ameihesabu tabia njema kuwa ni katika ukamilifu wa


imani ya mtu Aliposema: (Mkamilifu zaidi wa imani katika


waumini ni yule Mwenye tabia njema kati yao). (Hadithi


ameipokea Imam Ahmad na Abuu Daud).


Na ni juu yako kushikamana na kauli ya Mtume Rehma


na Amani za Allah ziwe Juu Yake: (Watu wanao pendwa


zaidi na Allah ni wale wenye manufaa kati yao, na matendo


yapendezayo mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni


furaha unayo iingiza katika moyo wa Muislamu, au


kumuondolea Tabu/Shida/Matatizo, au kumlipia Deni, au


kumkimbizia/kumuondoshea Njaa, na kuwa


sambamba/pamoja na Nduguyangu Muislamu katika shida


zake inapendeza zaidi kwangu Mimi kuliko kukaa Itikafu


4


Msikitini Mwezi Mzima). Hadithi ameipokea Imam


Twabaraaniy).)


Na Muislamu ameamrishwa kusema neno dogo laini


(zuri) ili liwe hilo neno ni katika mizani ya mema yake,


Amesema Mtume Rehma na Amani za Allah ziwe Juu


Yake: (Na Neno zuri ni sadaka). (Hadithi


imepokelewa na Imam Bukhari na Muslin).


Bali hata kutabasamu ambako hupungukiwi na chochote


unapata malipo: (Na tabasamu yako mbele ya ndugu yako


ni sadaka).


(Hadithi ameipokea Imam Tirmidhi).


Na maelekezo ya Mtume Rehma na Amani za Allah ziwe


juu yake katika kuhimiza tabia nzuri na kuvumilia maudhi


ni mengi sana na yanajulikana, na mwenendo wake ni


mfano wa kufatwa katika tabia njema pamoja naye, na


pamoja na wakeze, na jirani zake, na madhaifu katika


Waislamu na pamoja na wajinga wao bali hata pamoja na


kafiri, kwani Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Wala


kuchukiana na watu kusikupeleeni kutofanya uadilifu (watu


hao msiowapenda) Hivyo ndio kuwakaribu mno na ucha


Mungu). (Almaaidah: 8).


Na hakika zimekusanywa alama nyingi sana za tabia


njema/nzuri katika sifa nyingi, basi zitambue –ewe


nduguyangu- na ushikamane nazo, kwa ufupi nikama


ifuatavyo: " Ni Mtu kuwa na haya/Aibu nyingi, Maudhi


machache, Mwenye kufanya Mazuri mengi, Mkweli wa


Maneno, Mwenye maneno machache, Mwenye matendo


mengi (ya kheri), Mwenye kuteleza kidogo, Mchache wa


mambo yasiyo na faida, Mwenye kufanya wema na kuunga


ujamaa/udugu, Mwenye heshima, Mwenye subira, Mwenye


kushukuru, Mwenye kuridhia, Mpole, Laini, Mwenye


5


kujiheshimu, Mwenye huruma, si Mwenye kulaani hovyo, wala si mtusi/mwenye kutukana, wala si


m'beya/mfitinishaji,wala asiwe ni sengenyaji/kuwazungumza watu vibaya, na wala asiwe ni Mwenye pupa, wala asiwe ni Mwenye hiqdi/kinyongo, wala asiwe Bakhili/Mchoyo, wala asiwe Mwenye kuhusudu wenziwe, bali awe mkunjufu wa Uso/Moyo, Mwenye furaha kwa watu, Anapenda kwa ajili ya Allah na Anaridhia kwa ajili ya Allah na Anachukia kwa ajili ya Allah.


ASILI YA TABIA MBAYA ZOTE HUTOKANA NA: KIBURI, DHARAU/UDHAIFU NA UDHALILISHAJI. NA ASILI YA TABIA NZURI ZOTE HUTOKANA NA: UNYENYEKEVU NA HIMA YA JUU KABISA.


Ama ufakhari na kiburi/kupinga na kujiona na husda na dhulma na kujisikia na ugumu na kutakabbari/kujikweza na kupuuza na kukataa kukubali haki na kuwapendelea wengine na kutafuta ukubwa na kupenda cheo na uongozi na kusifiwa kwa yale ambayo hakuyafanya na mfano wa hayo, yote hayo yanatokana na KIBURI.


Ama uongo na dharau na khiyana na kujionyesha/riyaa na hila/udanganyifu na tamaa na kufadhaika na uogana ubakhili na kushindwa kwa jambo Fulani na uvivu na udhalili kusiko kwa Allah na kutaka kubadilisha lile ambalo ni la chini/dhalili kabisa kwa lile ambalo ni la kheri na mfano wake, hakika yote hayo yanatokana na Dharau Udhaifu na Udhalili na Udogo wa Nafsi.


6


SHAIRI: Utakapomtafuta Mcha Mungu utamkuta Mtu mkweli wa maneno yake na vitendo vyake


Na mtu atakapomcha Allah na akamtii, Basi mikono yake ipo baina ya mazuri na matukufu


Na kwa Mcha Mungu atakapo shikamana na Ucha MunguAna mataji mawili: taji la utulivu na taji la uzuri.


Na watakapo nasibiana watu basi sioni Nasabu inayokuwa ni nzuri kama matendo mema


EWE NDUGUYANGU MUISLAMU:


Hakika huu ni mnasaba mzuri/mtukufu wa kutaraji ujira/malipo kwa kujipamba na sifa nzuri, na kuipeleka nafsi yako kwenda kuyachukua (matendo mazuri) na kutoa juhudi katika hayo, na jihadhari juu ya kuyaacha kwa hiqdi/kinyongo na kuyachukia na kwa kusema maneno mabaya na kutofanya uadilifu na kusengenya watu na kufitinisha watu na uchoyo na kukata udugu.


Na ninashangazwa na yule aoshae uso wake mara tano kwa siku hali ya kuwa ni Mwenye kumuitikia Allah, na wala haoshi moyo hata mara moja kwa mwaka mzima ili aondoshe yale yaliyofungamana naye katika uchafu wa duniani na uweusi wa moyo(moyo mchafu) na tabia mbaya!


Na fanya pupa katika kuizoesha nafsi kuficha ghadhabu ili wafurahi walio pembeni mwako katika: wazazi wawili, mke, watoto, marafiki, na wanaojulikana/wema katika waishio nawe na kwa maneno yako matamu na ukunjufu wa sura yako na utarajie ujira/malipo katika yote hayo.


Na ni juu yako ewe nduguyangu Muislam, kushikamana na wasia wa Mtume Rehma na Amani za Allah ziwe Juu Yake uliokusanya: (Mche Allah popote ulipo, na fuatisha baya ulilofanya kwa kufanya jema, (hilo jema) litafuta hilo


7


baya, na changanyika/ishi na watu kwa tabia njema). (Ameipokea ImamTirmidhiy).


Alla atujaalie sisi na nyie tuwe miongoni mwa wale ambao amewasema Mtume Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake: (Hakika atakayekuwa karibu yangu zaidi siku ya Qiyama ni yule mwenye tabia nzuri zaidi miongoni mwenu).


Ameipokea Imam Ahmad na Tirmidhiy na Ibnu Hibbaan).)


Ee Mola wetu hakika sisi twakuomba msamaha na afya usalama wa milele. Ewe Mola wetu tutengenezee tabia zetu na utupendezeshee matendo yetu, Ewe Mola wetu kama ulivyoyatengeneza vizuri maumbile yetu, basi kwa neema zako/Ihsani yako zitengeneze vizuri pia tabia zetu, Ewe Mola wetu tusamehe madhambi yetu sisi na wazazi wetu na waislamu wote. Na Rehma na Amani za Allah zimuendee nabii Muhammad pamoja na watu wa Nyumbani kwake na Maswahaba zake na Waislamu wote watakao fuata Mwenendo wake mpaka siku ya Qiyama. Aamiin!!!



Machapisho ya hivi karibuni

Uislamu Ni dini ya ma ...

Uislamu Ni dini ya maumbile na akili na furaha

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL