NYUMBA KATIKA PEPO
MTUNZI SHEKH: YASINI TWAHA
KIMEREJEWA NA SHEKH: ABUBAKARI SHABANI RUKONKWA
2
بسم الله الرحمن الرحيم
Ndugu yangu Duniani kuna Nyumba nyingi za kila aina Lakini Nyumba
zote hizo zimejengwa na Miti au Udongo au Tofari au Mawe au Mchanga
au Simenti……Nk.
Nyumba zote hizo zina Vyoo vya ndani na vya nje Wenye kuishi ndani
ya Nyumba hizo hakupiti Siku wala Mwezi au Mwaka ila Utasikia
Matatizo ndani ya Nyumbahizo, Utasikia Mtu Kaumwa, Mwengine
Mnyonge, Mwengine Ana huzuni, au Nyumba ime Bomoka,Wengine
Wana fukuzwa kwenye Nyumba za kupanga kwa Ajili ya kodi,Wengine
Chakulatabu,Wengine Mpaka Waseme Uongo ndio wapate Kula! Yaani
Matatizo Juu ya Matatizo, Hii ndio Hali ya Nyumba za Duniani na watu
Wake.
Lakini Ndugu Yangu Waweza kujenga Nyumba katika Pepo Ukiwa Hapa
Hapa Duniani, Nyumba Ya ajabu kabisa, Nyumba Ambayo Tofari zake
za Dhahabu na Fedha, Simenti ni Miski, ndani ya Nyumba hiyo kuna
Wanawake wanaitwa Hurul-aini, Laiti Mwanamke wa Peponi
Akichungulia kwenye Mbingu ya Dunia basi Dunia yote itajaa Nuuru na
Harufu nzuri!!, Ndani ya Nyumba hiyo Pamejaa Neema zisizo katika, za
kila Aina, Neema Ambazo Macho hayajawahi kuona, wala Masikio
hayajawahi kusikia, sihivyo tu Hata Moyo kuwaza Namna ya Neema hizo
zilivyo bado!, Watu Wanyumba hiyo Watakula na Kunywa Wataishi
hawatokufa.
3
Ndugu yangu Ukitaka Kuipata Nyumba hiyo Fanya Hili jambo:
Kapokea Imam Muslim Mungu Amrehemu katika Swahihi yake:
(Mlango unaoelezea Ubora wakuswali Sala za Sunna zilizo pangiliwa
kabla ya Faradhi na baada yake).
Kanihadithia Muhammad bin Abdullahi bin Numairi, Kanihadithia Baba
yake na Khalid ambae ni Suleiman bin Hayyan' kutoka kwa Daaud bin
Abiihindi, kutoka kwa Nuuman bin Saalim, kutoka kwa Amru bin Ausi,
Amesema: Amenihadithia Ambasa bin Abii Sufyan katika Maradhi
alioFishwa nayo, Mazungumzo Ambayo Ukiyasikia yanafurahisha,
Amesema: Nilimsikia Mama Habiba Akisema: Nilimsikia Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) Akisema:
{Yeyoto Atakae Swali Rakaa kumi na mbili kwa Usiku na Mchana
Hujengewa Nyumba Katika Pepo kutokana na Rakaa hizo}.!!!
Akasema Ummu Habiba: Sikuacha kuswali Rakaa hizo toka nilipo
Msikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani za Allah ziwe
juu yake).
4
Na Akasema Ambasa: Sikuacha kuswali Rakaa hizo toka nilipo msikia
Mama Habiba.
Na Akasema Amru bin Ausi: Sikuacha kuswali Rakaa hizo toka nilipo
msikia Ambasa.
Na Akasema Nuuman bin Saalim:Sikuacha kuswali Rakaa hizo toka
nilipo msikia Amru bin Ausi.
Ndugu zangu tukimbilieni kheri hizi na tujitahidini katika hali hii na
tuwaamrishe tunaowamiliki akiwemo mke, motto, nawengineo.
Ndugu yangu Jaribu kuiuliza Nafsi yako Maswali machache:
1/ Miaka mingapi imepita katika Umri wangu Sijaswali Rakaa hizi?.
2/ Thawabu ngapi zimenipita kwa sababu ya Mambo ya Kipuuzi?.
3/ Mambo gani Mema Ambayo Nimekwisha yatanguliza mbele ya
Mwenyezi Mungu?.
4/ Lini nitaacha Kumuasi Mwenyezi Mungu?.
5/ Nitaanza lini Kufanya Ibada?.
6/ Kwa nini Nafsi yangu ni nzito Katika Mambo ya Kheri?.
7/ Kwa nini Nafsi yangu ni nyepesi Katika Mambo ya Shari?.
Mwisho kabisa:
Ndugu yangu Muislam kuwa na pupa katika kutekeleza Sunna tulizo
zitaja, Faida yake Utaikuta Mbele ya Allah pia Usisahau Kufanya Mambo
ya Kheri kwa wingi kama vile: Kuswali Swala tano kwa Jamaa Muskitini,
Funga za Sunna: J/tatu na Al-khamis na zile ayyaamulbiidh (Masiku
meupe) Tarehe (13-14-15) Kila Mwezi ,na Funga ya Ashuraa, na Funga
ya Arafaa, na Nyenginezo. Pia Katika Mambo ya Kheri kutoa Zaka na
kutoa Sadaka kufanya Ibada ya Hija naUmra. Ndugu yangu Milango ya
Kheri ni Mingi sanaTushindane Katika hilo, Mungu Atufanyie Wepesi.
5
NَAMNA YA KUTEKELEZA IBADA ZA SUNNA TULIZO ZITAJA:
َ
Ishaaَ Maghrebَ Laasiriَ Adhuhuriَ Al-fajri
BَAADIAَ KABLIAَ BAADIAَ KABLIAَ BAADIAَ KABLIAَ BAADIAَ KABLIAَ BAADIA KABLIA
2 2 2 4 2
Kuna Swala za Sunna Nyingine Tofauti na Tulizo zitaja:
1/ Rakaa 2 Wakati Wa kuingia Mskitini.
2/ Rakaa 4 Kabla ya Swala ya Laasiri 2unatoa Salam 2 unatoa Salam.
3/ Rakaa 2 Kabla ya Maghreb kwa Mwenye Kutaka.
4/ Rakaa 2 Baada ya Kumaliza Kutawadha. Nk….
Tuna Muomba Mwenyezi Mungu Atupe Kila la Kheri, na Atuepushe
na Kila la Shari, Atupe Mwisho Mwema Wakati Wa kufa kwetu,
Atuepushe na Adhabu za Kaburini, Atufufue Siku ya MwishoTukiwa
Nyuma ya Mtume wetu Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe
juu yake) ,Atupe Kitabu chetu Kwa Mkono wa Kulia.
Rehma na Amani za Allah zimuendee Nabii Muhammad Pamoja na
Watu wa Nyumbani kwake na Maswahaba zake na Waislamu wote
watakao Fuata Mwenendo wake Mpaka Siku ya Mwisho, Mwenyezi
Mungu Atujaalie Tue Miongoni Mwa watu wema. Ameen!!
AMIN.