1
NI YUPI RAFIKI MWEMA? الصديق الصالح
IMEANDALIWA NA: YUNUS KANUNI NGENDA IMEPITIWA NA: ABUBAKARI SHABANI RUKONKWA
2
بسم الله الرحمن الرحيم
Utangulizi
Ndugu zangu katika imani ni kawaida kwa binadam na ni
muhim kuwa na rafiki, Lakini kwa Muislam kuchagua
rafiki mzuri ni lazima kwa ajili ya kuhifadhi Dini yetu.
Kufanya urafiki na watu wema wenye tabia nzuri, wenye
dini na heshima ni moja ya mambo yanayotufanya sisi
Waislam kuwa katika njia iliyonyooka, na kuwa mfano
bora katika jamii.
Mtume (Swalla Allahu Alaihi Wa Sallam) amesema:
"Mtu yamkini (inawezekana) kufuata dini ya rafiki yake,
kwa hivyo muangalie unayemfanya rafiki." {Abu Dawud
na Tirmidhiy}
Ukiona rafiki yako ana matendo maovu, jaribu
kumkumbusha,kumpa nasaha na mawaidha, asipobadilika
na akaendelea kufanya maovu, ni vema kumuepuka kwa
sababu unaweza ukaiga tabia zake ambazo zinakwenda
kinyume na Dini yako (ya kiislam). Lakini pamoja na
kumuepuka inakupasa kumfanyia wema na kumuombea
kwa Allah uongofu.
Allah (Subhanahu Wa Ta'ala) amesema:
"Na Siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono
yake, na huku anasema: 'Laiti ningelishika njia pamoja na
3
Mtume (S.a.w) Ee Ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani
kuwa rafiki! Amenipoteza nikaacha Ukumbusho, baada ya
kwisha nijia, (kunijia) na kweli shetani ni khaini (mwenye
khiyana) kwa mwanaadamu."
{Surat Al-Furqaan 25:27-29}
Allah (Subhanahu Wa Ta'ala) tena Anasema:
"Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui, wao kwa wao,
isipokuwa wachaji Allah (wacha Mungu)" {Surat Az-
Zukhruf 43:67}
Muumini ni kioo cha ndugu yake muumini, akiona makosa
ya mwenzake inampasa amueleze kwa uzuri na kumsaidia
kurekebisha kosa hilo.
Huo ndio urafiki unaotakiwa katika Uislam, na muumini
wa kweli lazima ataangalia nani wa kumfanya rafiki.
Lakini kwa masikitikiko makubwa vijana wa kiislam wa
leo hawana habari na jambo kama hili, imefikia hatua
marafiki wa zama hizi wanatumia muda mwingi kusaidiana
katika mambo yasiyofaa, badala ya kusaidiana katika
mambo ya dini na ya kheri.
Tunamuomba Allah atuongoze pamoja na marafiki zetu.
Ameen!!!