NI UPI USIKU WA LAYLATUL QADR
Swahili
Imeandikwa na:
Daudi Abubakari
Imepitiwa na :
Abubakari Shabani Rukonkwa
بسم الله الرحمن الرحيم
Utangulizi:
Hadiyth kadhaa zimetaja kuhusu usiku wa
Laylatul-Qadr. Imetajwa kuwa ni katika masiku
kumi ya mwisho; siku ya ishirini na moja, au
ishirini na tatu, au ishirini na tano au ishirini na
saba kwa dalili zifuatazo:
عن عائشة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ))تحروا ليلة
القدر في الوتر من العشر الأواخر(( رواه البخاري
Hadiyth ya 'Aiashah (Radhiya Allaahu 'anhaa)
kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) amesema: ((Utafuteni usiku wa
Laylatul-Qadr katika siku za witiri kwenye siku
kumi za mwisho)) [Al-Bukhaariy[
حديث ابن عباس رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم
قال: ))التمسوها في العشر الأواخر من رمضان ليلة القدر في
تاسعة تبقى ، في سابعة تبقى ، في خامسة تبقى(( رواه البخاري
Hadiyth ya Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu
'anhumaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa sallam) amesema: ((Utafuteni usiku
wa Laylatul-Qadr katika siku kumi za mwisho
za Ramadhaan; katika (usiku wa) tisa, saba, na
wa tano utakaobakia [mwisho wa Ramadhaan]))
[al-Bukhaariy[
Imaam Ahmad amepokea kutoka kwa 'Ubaydah
bin As-Swaamit kwamba alimuuliza Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kuhusu
usiku wa Laylatul-Qadr akasema:
) ) Katika Ramadhaan, utafuteni siku kumi za mwisho, hakika umo katika siku za witiri; siku ya ishirini na moja, au ishirini na tatu, au ishirini na tano, au ishirini na saba, au ishirini na tisa, au usiku wa mwisho)) [Ahmad[
Alama Zinazobainisha Laylatul-Qadr:
1. Usiku huo unakuwa na mwanga zaidi.
2 . Upepo siku hiyo hutulia, yaani siku hiyo hautokei upepo mkali.
3. Hali ya hewa huwa nzuri.
4 . Nyoyo za Waumini usiku huo huwa zina utulivu kuliko siku nyingine.
5 . Baadhi ya watu wema huoteshwa usiku huo kama walivyokuwa wakioteshwa Maswahaba na Salafus-Swaalih (wema waliotangulia(
Asubuhi Yake:
حديث أبي بن كعب رضي الله عنه أنه قال: "أخبرنا رسول الله
صلى الله عليه وسلم أنها تطلع يومئذ لا شعاع لها" رواه مسلم
Hadiyth ya ‘Ubay bin Ka'ab (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ametuambia kuwa, jua siku hiyo hutoka likiwa halina mishale (mikali)" [Muslim[
Pia:
ليلة القدر ليلة طلقة لا حارة ولا باردة ، تُصبح الشمس يومها
حمراء ضعيفة(( صحيح ابن خزيمة
) ) Laylatul-Qadr ni usiku ulio katika hali ya ukunjufu, usio na baridi wala joto, asubuhi yake jua huwa jekundu na dhaifu)) [Swahiyh Ibn Khuzaymah[
ليلة القدر ليلة بلجة )أي مضيئة( لا حارة ولا باردة ، لا يرمى
فيها بنجم(( )أي لا ترسل فيها الشهب( رواه الطبراني ومسند
أحمد
))Laylatul-Qadr usiku wa kung'aa [yaani wenye mwanga] sio joto wala baridi, na vimondo
(nyota za kufyatuliwa) havitotumwa)) [At-Twabaraaniy na Ahmad]
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atuwezeshe kukesha masiku kumi ya Ramadhaan ili tujaaliwe kuupata usiku huu mtukufu, tutoke katika Ramadhaan tukiwa tumeghufuriwa madhambi yetu yote. Aamiyn