Nakala

1


بسم الله الرحمن الرحيم


NANI KAMA MAMA? Imeandiwa na Yunus Kanuni Ngenda. Imepitiwa na Abubakari Shabani Rukonkwa. Utangulizi: Kwa mara nyingine tena ndugu zangu katika imani tuogelee kwa pamoja katika bahari ya ndefu yenye kina kirefu sana, nayo ni bahari ya wazazi! Na leo hii tutamzungumzia MAMA. MAMA NI NANI? MAMA: ni yule ambae umekaa katika tumbo lake kwa kipindi cha miezi tisa, amekubeba katika tumbo lake shida juu ya shida, akawa ni sababu ya wewe kuwepo katika wigo wa dunia, alipokuzaa MAMA alikulea, alikunyonyesha na ilikua paja lake ndio godoro lako, maziwa yake ndio kinywaji chako na mgongo wake ndio pumziko lako. yuko wapi mwingine kama MAMA?. NAFASI YA MAMA MBELE YA ALLAH. Nafasi ya mama mbele ya Allah ni kubwa sana, na Allah ameusia katika Aya nyingi juu ya kumfanyia wema MAMA, na ni vema kumshukuru Allah kisha kumshukuru MAMA kutokana na majukum mazito aliyoyabeba mpaka ukapatikana. Anasema Allah (S.w)


2


ووصينا الإنسان بوالديه حملته أمه وهنا على وهن و فصاله في عامين أن )


) اشكر لي ولوالديك إلي المصير( )لقمان 41


Na tumemuusia mwanadam kwa wazazi wake wawili,


Mama yake ameichukua (ameibeba) mimba yake kwa


udhaifu juu ya udhaifu (tabu juu ya tabu) na akamwachisha


ziwa baada miaka miwili. (Basi) Nishukuru Mimi (Allah)


na wazazi wako, na kwangu mimi (Allah) ndio marejeo


(yenu).


Qur'an (31:14).


NAFASI YA MAMA KWA MTOTO


MAMA ana nafasi ya pekee kwa mtoto, na mama ni


mlango kaka milango ya Peponi.


الأم باب من أبواب الجنة، من برها دخل الجنة


MAMA ni mlango katika milango ya Peponi mwenye


kumfanyia wema ataingia Peponi.


عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه و سلم:


)رغم أنف رغم أنف رغم أنف، قيل من يا رسول الله؟ قال: من أدرك أبويه


عند الكبر أو أحدهما ثم لم يدخل الجنة( )رواه مسلم(


Kutoka kwa Abiy Hurayra radhi za Allah zimuendee


kaesema: Amesema Mtume (s.a.w) Amepata hasara!


Amepata hasara! Amepata! Pakasemwa nani Ewe Mtume


wa Allah? Akasema: Mtu ambae aliwapata wazazi wake


(Baba na Mama) wakiwa watu wazima (wazee) au mmoja


wao akawa hakuingia Peponi).


(Hadithi hii ameipokea Muslim.)


3


Allahu akbar!! Ndugu zangu katika imani tazameni hiyo


milango ya kuingilia Peponi! Tazama namna ambavyo


Allah ametupendelea sisi ummat Muhammad (s.a.w).


Hii ni fursa adhwim kubwa kwako ewe muislam usiipoteze


kisha ukaenda kujuta mbele ya Allah, jinyenyekeze kwa


wazazi wako kwa kuwafanyia ihsani ili uzipate radhi za


wazazi na upate radhi za Allah (S.w). Kwasababu radhi za


Allah zipo katika radhi za wazazi wawili kama


alivyotufundisha Mtume (s.a.w).


NAFASI YA MAMA KATIKA JAMII.


MAMA ataendelea kuwa na nafasi na hadhi kubwa


katika jamii yoyote hapa dunia kama ilivyokua kubwa


hadhi mbele ya Allah (S.w).


Siku moja aliulizwa Mtume (s.a.w) ni mtu gani! Mwenye


kustahiki kufanyiwa ihsani na wema zaidi kuliko wengine?


Mtume (s.a.w) alijibu kama ifuatavyo:-


عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: جاء رجل إلى رسول الله صلى الله عليه


و سلم فقال: يا رسول الله، من أحق الناس بحسن صحابتي؟ قال: أمك، قال: ثم


من؟ قال: ثم أمك، قال: ثم من؟ قال: ثم أمك، قال: ثم من؟ قال: ثم أبوك(


رواه البخاري و مسلم


Kutoka kwa Abuu Hurayra radhi za Allah zimwendee


anasema: Alikuja mpaka kwa Mtume (s.a.w) (akamuuliza)


akasema: Ewe Mtume wa Allah katika watu ni nani


mwenye haki zadi nimfanyie wema? (ihsani?) Mtume


(s.a.w) (akamjibu) akasema: Ni Mama yako, (akauliza


tena) akasema: kisha nani? Mtume (s.a.w) (akamjibu)


akasema: Kisha Mama yako, (akauliza tena) akasema:


kisha nani? Mtume (s.a.w) (akamjibu) akasema kisha


4


Mama yako, (akauliza tena) akasema: kisha nani? Mtume


(s.a.w) (akamjibu) akasema: kisha Baba yako.))


Hadithi hii ameipoke Bukhar na Muslim.


Katika Hadithi hii Mtume (s.a.w) anabainisha na kuweka


wazi ubora na umuhim wa MAMA na kwamba katika watu


wote duniani MAMA ndio wa kwanza anatakiwa


kufanyiwa wema, ihsani na ukaribu mara tatu ya Baba.


Masikini MAMA!!!! Leo hii MAMA amekua mtu wa


kawaida sana hata kufikia hatu baadhi ya vijana wa zama


hizi wa kiume na wa kike wanamuona MAMA si lolote si


chochote! MAMA hujibiwa vibaya na watoto alio wazaa,


MAMA hasaidiwi na watoto alio wazaa, MAMA


hunyanyaswa na watoto alio wazaa, MAMA wakati


mwingine huambiwa ni mchawi na watoto alio wazaa, kini


MAMA huvumilia yote na mwisho wa siku husema


mwanangu chakula hiki nimekuandalia.


Nani mwingine kama MAMA?


Jinyenyekeze kwa MAMA kwa kumfanyia ihsani ili


upate radhi zake leo na kesho Akherah:


Je unajua kama MAMA akikasirika na Allah


anakasirika?


Je unajua kama MAMA akikulaani na Allah anakulaani?


Je unajua kama MAMA akikutenga na Allah


anakutenga?


Je unajua kama ukifa hali ya kua huna radhi za MAMA


hata harufu ya Pepo huipati?


Basi ogopa kumuasi MAMA kwasababu hakuna kama


MAMA.


5


KWANINI MAMA! Shekh mmoja mwenye hekima alisimlia kisa murua akasema:- Siku moja mtoto alimuuliza mama yake kwa nini unalia? Akajibu kwa sababu mimi ni mwanamke! Mtoto akasema mimi sifahamu, Mama akamkumbatia mtoto wake na kumwambia si rahisi kunielewa! kisha mtoto akamfuata babake na kumuuliza kwanini mama analia? Baba akajibu: Wanawake wengi wapenda kulia bila sababu. Mtoto alipokua akawa bado hajajua sababu hasa ya mwanamke kulia bila sababu kama alivyoambiwa na baba yake, mwisho akamuuliza shekh mwenye hikma: Kwa nini wanawake wapenda kulia bila sababu? Akajibu: Allah alipomuumba mwanamke alimpa mabega yenye nguvu sana kwa ajili ya kubeba mazito ya walimwengu. Na akamjaalia mikono mwiwili milaini na iliojaa upendo kwa ajili ya kuwapa watu raha na akampa nguvu ndani ya mwili wake ili kuweza kubeba mimba hadi kuzaa na vile vile kuvumilia pindi watoto wanapokua kisha wakamkataa. Pia kapewa uwezo wa kubeba aibu za nyumba yake na familia yake pamoja na kuwa na msimamo ktk kila jambo zito bila kutetereka. Na akampa mapenzi juu ya watoto wake yasoisha na wala kubadilika hata wakimkera na kumtukana na kumsababishia maumivu makali bado mapenzi yako pale pale. Na mwisho Allah kampa (machozi)


6


yanayot oka kwa haraka pindi anapopata matatizo, Na huo ndio udhaifu wake. Kwa hiyo chunga na uheshimu machozi ya MAMA katika huu ulimwengu hata ikiwa wanalia bila sababu! Kimekatwa kitovu chako pindi ulipotoka katika hii dunia na hicho kitovu kikaacha athari (alama) kwenye mwili wako ili ukumbuke daima. Mwisho: Ewe mola wetu Tunakuomba kwa kadri ya mapigo ya mioyo yetu wajaalie MAMA ZETU wawe wanamke bora katika wanawake wa Peponi na uwasamehe na uwajaalie wote Pepo ya Firdausi yawe ni makaazi yao. Ameen!!



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI