Imeandaliwa na Alhidaya.
Imepitiwa na Abubakari shabani Rukonkwa.
Ingia Katika Milango Mingi Ya Kheri
Ramadhaan
Mwezi mtukufu wa Ramadhaan unakaribia kutufikia.
Chukua fursa ya kujichumia thawabu nyingi kwa sababu
malipo ya amali inayotekelezwa humo yanaanzia mara kumi
mpaka mara mia saba. Juu ya hivyo, kuna malipo maalum
yatokayo kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) kama
ilivyothibiti katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam):
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu
‘anhu): ((Kila amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara
kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba,
na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema: Isipokuwa Swawm,
2
kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye
Nitakayemlipa.
Ameacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili
Yangu. Kwa aliyefunga swawm atapata furaha mbili; furaha
anapofuturu na furaha atakapoonana na Mola wake, harufu
inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri mbele ya
Allaah kuliko harufu ya misk))
[Muslim na Ahmad]
Kwanza kabisa inatupasa kutia niyyah ya ikhlasi moyoni (si
kuitamka) kwa sababu ni sharti mojawapo la kutakabaliwa
amali yoyote, na ili kupata Radhi za Allaah (Subhaanahu wa
Ta’aala) kama Anavyosema:
Na hawakuamrishwa (chochote kile) isipokuwa wamwabudu
Allaah mukhliswiyn (wenye kumtakasia) Dini, hunafaa1 na
wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini
iliyosimama imara.
Wakielemea haki na kujiengua na upotofu -١
3
[Al-Bayyinah:5]
Weka azimio la nguvu kutekeleza amali zifuatazo katika
mwezi wa Ramadhaan.
1-Kufunga Swawm kwa imaani na matarajio ili kufutiwa
madhambi
Amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam): ((Atakayefunga Ramadhaan kwa iymaan na kutaraji
malipo ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia ))
Al Bukhaariy na Muslim.
2-Qiyaamul-Layl (Kusimama usiku katika Swalah);
Tarawiyh na Tahajjud
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallaam)
amesema: ((Atakayesimama [kwa Swalah ya usiku] kwa
4
iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake
yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
3-Kutoa sadaka
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallaam)
amesema:
((Sadaka bora kabisa ni ile inayotolewa katika mwezi wa
Ramadhaan))
[At-Tirmidhiy kutoka kwa Anas]
4-Kumfuturisha aliyefunga Swawm:
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallaam)
amesema: ((Atakaye mfuturisha aliyefunga Swawm, atapata
5
ujira kama ujira wake bila ya kupungua chochote katika ujira
wa yule aliyefunga))
[Ahmad, An-Nasaaiy – Ameipa daraja ya Swahiyh Shaykh
Al-Albaaniy]
Na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:
Na wanalisha chakula juu ya mapenzi yao (kwa hicho
wanacholisha) masikini na mayatima na mateka. “Hakika
sisi tunakulisheni kwa ajili ya Allaah, hatutaki kwenu jazaa
na wala shukurani. “Hakika sisi tunakhofu kwa Mola wetu
siku inayokunjisha uso ngumu nzito. . Basi Allaah
Atawakinga na shari ya siku hiyo, na Atawakutanisha na
mng’ao na furaha. Na Atawalipa Jannah na (nguo za) hariri
kwa kusubiri kwao.
[Al-Insaan: 8-12]
Vile vile Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) amesema:
((Muumin yeyote atakayemlisha Muumin mwenzake
mwenye njaa, Allaah Atamlisha katika matunda ya Peponi,
na atakayemnywesha Muumin mwenye kiu Allaah
Atamnywesha kutoka katika 'Rahiyqul-
Makhtuum' [Kinywaji safi kilichofunikwa kwa kizibo
madhubuti])) [At-Tirmidhiy na Isnaad yake ni nzuri]
5-Kusoma Qur-aan kwa wingi na kujifunza maana yake.
Mwezi wa Ramadhaan ni mwezi ulioteremshwa Qur-aan
kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan
ili iwe Hidaaya kwa watu na hoja bayana za Hidaaya na Al-
Furqaan (Upambanuzi). [Al-Baqarah: 185]
Jitahidi ndugu Muislam uzidishe kusoma Qur-aan na
ujitahidi kukhitimisha japo mara moja katika mwezi huu.
Jibriyl (‘alayhis-salaam) alikuwa akimfikia Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya
kumsikiliza na kumfundisha Qur-aan katika mwezi wa
7
Ramadhaan. Vile vile Maswahaba na Salafus-Swaalih
(Wema waliotangulia) walikuwa wakijihimiza sana kusoma
Qur-aan katika mwezi wa Ramadhaan; 'Uthmaan bin
'Affaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akikhitimisha Quraan
kila siku moja. Na baadhi ya Salaf wakikhitimisha Qurraan
kila siku tatu katika Qiyaamul-layl. Wengineo
walikuwa wakikhitimisha siku saba, na wengine siku kumi.
Na walikuwa wakiisoma katika Swalah na nje ya Swalah.
6-Kukaa kwa kumdhukuru Allaah baada ya Swala ya
Alfajiri hadi jua litoke
Imetoka kwa Anas kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi
wa aalihi wa sallam) amesema:((Atakayeswali Alfajiri
katika Jamaa'ah kisha akakaa anamkumbuka Allaah mpaka
likachomoza jua kisha akaswali Raka'ah mbili, atapata ujira
kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili
kamili))
8
[Imetolewa na At-Tirmidhiy na kaisahihisha Al-Albaaniy].
(Kuswali Jama'ah kumesisitizwa kwa wanaume, ama
mwanamke anaweza naye kupata ujira wa thawabu
zilizotajwa akiswali nyumbani kwake)
Thawabu hizo za kama Hajj na ‘Umrah ni katika siku za
kawaida ndugu Muislamu, seuze mwezi wa Ramadhaan?
Usiache fursa hii ikupite. Ukishindwa kuitekeleza kila siku,
basi jitahidi japo wiki mara moja, hapo utakuwa una
thawabu za Hajj na 'Umrah mara nne kwa mwezi, na
ukiendelea hivyo miezi yote kumi na mbili basi utakuwa na
thawabu za Hajj na 'Umrah mara 48 kwa mwaka.
7- Kubakia Masjid kwa ajili ya Itikaaf:
Kutoka kwa 'Aashah (Radhiya Allaahu 'anhaa) kwamba:
"Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam)alikuwa akikaa Itikaaf kila Ramadhaan katika siku
kumi za mwisho, na mwaka ambao aliondoka duniani alikaa
Itikaaf siku ishirini.
9
[Al- Bukhaariy]
Unapokuwa umo katika I'itikaaf utaweza kutekeleza amali
nyingi zitakazokufanya ubakie katika taqwa na iymaan
kuzidi moyoni. Utaweza kusoma Qur-aan kwa wingi,
kuswali Swalaah za Sunnah, kumdhukuru Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala), kuomba du’aa na maghfira.
Fadhila za I’tikaaf zinazidi inapokuwa katika kumi la
mwisho kwa sababu ya usiku mtukufu unaojulikana kama
ni: ’Laylatul-Qadr’.
8-'Umrah katika mwezi wa Ramadhaan
Ukiwa na uwezo, tekeleza ‘Umrah. Imethibiti katika Hadiyth
ya Mtume (walla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
kwamba thawabu za kutekeleza 'Umrah katika Ramadhaan
ni sawa na thawabu za kutekeleza Hijjah.
(('Umrah katika Ramadhaan ni sawa [kwa thawabu] na
Hijjah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
9-Kupata Baraka za Suhuwr (Daku)
10
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
amesema:
((Kuleni daku kwani katika huko kula daku, kuna
baraka)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
10-Kuomba Du'aa
Ramadhaan ni mwezi wa Du'aa. Allaah (Subhaanahu wa
Ta’ala) Anataja kuhusu kumuomba du’aa baada ya
kutufaridhisha Swawm:
Na watakapokuuliza (Ee Muhammad GH و E وآ EGA لله JGK (
waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Qariyb (Yu karibu
daima kwa elimu Yake); Naitikia maombi ya muombaji
anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi,
wapate kuongoka.
[Al-Baqarah:186]
11
Zinaendelea Aayah za kuhusu Swawm baada yake.
11-Kuomba maghfirah na tawbah:
Omba maghfira na tawbah kabla ya alfajiri. Kufanya hivi
utakuwa miongoni mwa waja wema Anaowasifu Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala):
Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfira
[Adh-Dhaariyaat: 18]
Vile vile Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Huteremka
nyakatii hizo kuweko katika mbingu ya kwanza:
Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu
‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’ala Huteremka
kila siku katika mbingu ya dunia inapobakia thuluthi ya
mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba
Nimtakabalie? Nani ana shida Nimtekelezee? Nani
ananiomba maghfira Nimghufurie?))
[Al-Bukhaariy Na Muslim]
12-Kuunga undugu na jamaa:
Jambo muhimu kulitekeleza siku zote. Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametahadharisha kwa
anayekata mawasiliano na ndugu au jamaa:
((Fuko la uzazi linaning'inia katika 'Arshi linasema:
“Atakayeniunga, Allaah Atamuunga, na
atakayenitenga Naye Allaah Atamtenga [Atamkatia]”))
[Al-Bukhaariy na Muslim]
13- Kukesha siku kumiza mwisho:
13
Utaweza kudiriki Laylatul-Qadr, usiku ambao ‘ibaadah yake
ni bora kuliko ‘ibaadah utakazoifanya miezi elfu. Anasema
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
Hakika Sisi Tumeiteremsha (Qur-aan) katika Laylatil-Qadr
(usiku wa cheo). Na nini kitakachokujulisha ni nini huo
(usiku wa) Laylatul-Qadr? (Usiku wa) Laylatul-Qadr ni
(usiku) mbora kuliko miezi elfu Wanateremka humo
Malaika na Ruwh (Jibriyl) kwa idhini ya Mola wao kwa kila
amri (jambo). (Usiku huo ni) Amani mpaka kuchomoza
Alfajiri. [Al-Qadr: 97]
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atujaalie
tawfiyq kutekeleza yote hayo na Atutakabalie. Aamiyn.