1
بسم الله الرحمن الرحيم
FAIDA YA KUTOA SADAKA
Imeandaliwa na Yunus Kanuni Ngenda
Imepitiwa na Yasin Twaha Hassani
Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, na rehma na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na watu wake na Maswahaba wake wote. Amma baad: Hakika Mwenyezi Mungu anawalipa malipo makubwa wale wanaotoa sadaka kwa kutafuta radhi zake. Laiti mtoa sadaka angejua kwa yakini kwamba sadaka yake inapitia kwenye (mkono) wa Mwenyezi Mungu kabla ya kuingia mkononi mwa masikini, ingekuwa ladha ya mtoaji. ni kubwa kuliko ladha ya mpokeaji.. Ibun Alqayyim.
2
Je unajua faida ya kutoa sadaka?
Sikilizeni enyi watoa sadaka, wenye kutoa na ambao
wanasaidia kufikisha sadaka.
1- Sadaka ni mlango miongoni mwa milango ya pepo
2-Sadaka ni bora ya matendo mema, na sadaka bora ni kulisha
chakula
3- Sadaka inamfunika kivuli mtoaji na inamuondosha kwenye
moto
4-Sadaka inazima ghadhabu za Mola na joto la kaburi
5- Sadaka ni jambo bora la kumzawadia maiti na inamfaa
zaidi, na Mola anaitunza
6-Sadaka ni usafisho, na utakaso wa nafsi na huongeza mema
7- Sadaka ni sababu ya furaha kwa mtoa, na ni sababu ya
kung'ara uso wake siku ya kiama
8- Sadaka inaleta amani kutokana na hofu siku ya fazaa
kubwa, na humfanya mtoa sadaka asipatwe na huzuni
9- Sadaka ni sababu ya kughufiriwa dhambi na kusamehewa
makosa
10- Sadaka ni miongoni mwa bishara za mwisho mwema na
sababu ya dua ya Malaika
11- Mtoa sadaka ni mbora wa watu, na sadaka thawabu zake
ni kwa kila aliyeshiriki
12- Mwenye kutoa sadaka ameahidiwa kheri nyingi na ujira
mkubwa
13- Kutoa ni miongoni mwa sifa za wacha Mungu, na sadaka
ni sababu ya mapenzi ya waja wa Mola kwa mtoa sadaka
14- Sadaka ni ishara miongoni mwa ishara za ukarimu na
alama miongoni mwa alama za ukarimu na wema
3
15- Sadaka ni sababu ya kukubaliwa dua na kuondoshewa
matatizo
16- Sadaka inaondoa balaa na inaziba milango sabini ya
mabaya ya dunia
17- Sadaka inazidisha umri na mali, na ni sababu ya riziki na
nusra
18- Sadaka ni ponya, dawa, na shifaa
19- Sadaka inazuia moto, gharika, wizi, na inazuia kifo kibaya
20- Sadaka ujira wake ni ule ule japo ukitoa kwa wanyama au
ndege.