بسم الله الرحمن الرحيم
Imeandaliwa na alhidaya.com
Imepitiwa na Abubakari Shabani Rukonkwa.
MIEZI MITUKUFU IMEINGIA YATAMBUE MATENDO MEMA YANAYO TAKIWA KWA MUISLAM. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((Hakika idadi ya miezi kwa Allaah ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Allaah, tangu Alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko minne mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo)) [At-Tawbah: 36]. Miezi minne hiyo imetajwa katika Hadiyth ifuatayo:
Kutoka kwa Abu Bakrah ambaye amesema: “Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema
alipokuwa katika Hijjah ya kuaga (Hijjah wa mwisho):
((Mgawanyo wa nyakati umerudikama ulivyo (wakati)
Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi
kumi na mbili, minne ambayo ni mitukufu; mitatu
inafuatana pamoja (nayo ni) Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na
Muharram, na (wa nne ni) Rajab wa (kabila la) Mudhwar
ambao upo baina ya Jumaada na Sha'abaan)). [Al-
Bukhaariy)
Hivyo tunaona kwamba ni kuanzia mwezi huu tulioingia
wa Dhul-Qa'adah na miezi miwili ijayo inayofuatia kisha
tena hadi tutakapojaaliwa kufika mwezi wa Rajab In shaa
Allaah.
Katika miezi yote kumi na mbili Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) Ameichagua hii minne na Ameifanya kuwa ni
mitukufu na kusisitiza kuitakasa, na kwamba dhambi
zitakazofanyika humo ni zaidi na hali kadhalika thawabu za
vitendo vyema zinakuwa maradufu na zaidi. [Atw-
Twabariy 14: 238]
Ni sawa kama Anavyoonya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
kufanya maasi katika sehemu tukufu Alipotaja Masjidul-
Haraam (Msikiti Mtukufu Makkah):
((Hakika wale waliokufuru na wakazuilia Njia ya Allaah
na Msikiti Mtakatifu, ambao Tumeufanya kwa ajili ya
3
watu wote sawasawa, kwa wakaao humo na wageni. Na
kila atakayetaka kufanya upotofu humo kwa dhulma,
basi Tutamwonjesha adhabu iumizayo)). [Al-Hajj: 25].
Qataadah amesema kuhusu kauli ya Allaah:
((Basi msidhulumu nafsi zenu humo))
“Dhulma itakayotendeka katika miezi mitukufu ni mbaya
na kubwa (au hatari) kuliko dhulma itakayotendeka katika
miezi mingine. Hakika dhulma daima ni makosa, lakini
Allaah Hufanya baadhi ya vitu kuwa ni vizito kuliko
vingine kama Anavyopenda.”
Akaendelea kusema: “Allaah Amechagua baadhi ya
viumbe Vyake na baadhi ya vitu kuwa bora zaidi kuliko
vingine, Amechagua Wajumbe kutoka Malaika na kutoka
binaadamu.Vile vile Amechagua baadhi ya kauli Zake
kuwa ni bora kuliko nyingine, Misikiti kuwa bora kuliko
sehemu nyingine za ardhi, Ramadhaan na miezi mitukufu
kuwa bora kuliko miezi mingine, siku ya Ijumaa kuwa ni
bora kuliko siku nyingine na usiku wa Laylatul-Qadr kuwa
ni bora kuliko nyusiku zingine. Kwa hiyo takasa vile
Alivyovitakasa Allaah, kwani kufanya hivyo ni vitendo vya
watu wenye akili na wenye kufahamu.”[Tafsiyr ya Ibn
Kathiyr].
4
Miongoni mwa yaliyokatazwa katika miezi hii mitukufu
ni kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi
mtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambi
kubwa Lakini kuzuilia watu wasiende katika Njia ya
Allaah na kumkanusha Yeye, na kuzuilia watu wasende
kwenye Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wake humo,
ni makubwa zaidi mbele ya Allaah. Na fitina ni mbaya
zaidi kuliko kuua)) [Al-Baqarah: 217].
Maasi Mengine Ambayo Tunatakiwa Tujikumbushe
Kuyaacha
Kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wata'ala)
kama kwenda kwa wachawi na waganga na
kuwaamini wanayoyatabiri kwa watu.
Kuiba;
Kuzini;
Kulewa;
Kumdhulumu mtu haki yake;
Kugombana, kutukanana, kuvunjiana heshima,
kudharauliana n.k.;
Kusengenya (Ghiybah);
Kusema uongo, na kila aina ya uovu mwengine.
5
Mambo Mema Ya Kukumbushana Kufanya Katika Miezi Hii Mitukufu Kuongeza Sunnah za Swalah; *(tazama maelezo chini) Kufunga Swawm za Sunnah kama Jumatatu na Alkhamiys, Ayyaamul-Biydhw (tarehe 13,14 na 15) na Swawm ya Nabii Daawuwd (kufunga kila baada ya siku moja); Kujielimisha mambo ya dini kwa kusoma vitabu na kusikiliza mawaidha; Kuomba Maghfirah na Tawbah; Kufanya kila aina ya dhikr (kumkumbuka na kumtaja Allaah), kwa kusoma Qur-aan kwa wingi, kumshukuru, kumtukuza, kuomba du'aa n.k.; Kuwasiliana na ndugu na jamaa; Kutenda wema kwa jirani, marafiki na watu wote kwa ujumla; Kutoa sadaka; Kulisha masikini; Kupatanisha waliogombana; Kuamrishana mema na kukatazana maovu, na mengi mengineyo katika vitendo vyema.
6
* Swalah za Sunnah Ratiba Ya Swalah Za Sunnah Zilizosisitizwa Na Zisizosisitizwa NYAKATI ZA SWALAH *MUAKKADAH (ZILOSISITIZWA) GHAYR MUAKKADAH (ZISOSISITIZWA) KABLA BAADA KABLA BAADA
ALFAJIRI
Fadhila Zake ))
((Hatoswali mja Rakaa 12 zisizo za fardhi kwa siku, ila atajengewa [na Allaah] nyumba peponi))[Muslim] Nazo ni hizo Muakkadah (Zilosisitizwa) jumla yake ni 12
** ((Rakaa mbili (za Sunnah) kabla ya Alfajirr ni kheri kuliko duniya na yaliyomo ndani yake) [Muslim]
((Mja yeyote atakayesujudu sijda moja ataandikiwa wema mmoja, na atafutiwa baya moja, na atapandishwa daraja yake, kwa hiyo zidisheni kusujudu)) [Ibn Maajah] Swalah ya Tahajjud
((Swalah iliyo bora kabisa baada ya Fardh ni Swalah ya usiku)). [Muslim]
8
Swalah Ya Dhwuhaa na Swalah Ya Witri ع
Kutoka kwa Abu Hurayrah (radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba “Ameniusia rafiki yangu Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam [mambo matatu]; kufunga siku tatu katika kila mwezi, Rakaa mbili Dhwuhaa na niswali Witr kabla ya kulala” [Al-Bukhaariy na Muslim] Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuwezeshe kujitenga na maasi na kuzidisha mema katika miezi hii mitukufu. Aamiyn.