Nakala




MATENDO MEMA KATIKA SIKU KUMI ZA DHUL HIJJA.





Mwandishi:


Abubakari Shabani Rukonkwa.





Imerejewa na:


Yasini Twaha Hassani.





MATENDO MEMA KATIKA SIU KUMI ZA DHUL HIJJAH


(MFUNGO TATU)


Utangulizi:


Sifa zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu ambaye amewaneemesha waja


wake kwa kuwaletea misimu ya kheri ili iwe ni sababu ya kufutiwa madhambi yao


na awalipe kutokana na mema yao, namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na


kumsifu kwa muwafikisha anayemtaka katika waja wake kwa kuyatumia masiku


haya kwa kumtii na kumogopa, na akajaalia wengine katika waja wake ni wenye


kuzipoteza siku hizo.


Nakiri kwa moya na kutamka kwa ulimi ya kwamba hapana Mola apasae


kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu mmoja hana mshirika katika


Uungu wake, na nina kiri kwa moya na kutamka kwa ulimi ya kwamba Muhammad


ni mja wake na mjumbe wake, rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake


pamoja na familia yake na Maswahaba wake na wote watakao mfuata kwa wema


mpaka siku ya mwisho.


Amma baad.


Nisiku 10 bora kuliko masiku yote ya duniani Allah amebainisha ubora wake


katika kitabu kitukufu pale alipo apia masiku haya kwakuusema:





BisimiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym. ((Naapa kwa Alfajiri)) ((Na kwa masiku


kumi)) (Al-Fajr: 1-2).


Wanavyuoni wafasiri wa Qur-aan wamekubaliana kwamba zilokusudiwa hapo


ni Siku kumi za Dhul-Hijjah.


 3 


SIKU ZA MANUFAA NA KUMKUMBUKA ALLAH


Inapasa kumdhukuru mno Allaah (Subhaanah wa Ta’ala) kwa kukumbuka


Neema Zake zisizohesabika:





((Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja Jina la Allaah katika siku


zinazojulikana)) [Al-Hajj: 28[


Ibn Abbaas kasema: “Hizo ni siku kumi za Dhul-Hijjah” . Na Amesema:


“Manufaa ya dunia hii na ya Akhera” . Manufaa ya Akhera yanajumuisha


kupata Radhi za Allaah. Manufaa ya vitu vya dunia inajumuisha wanyama wa


kuchinjwa na biashara. [Tafsiyr Ibn Kathiyr.[


AMALI ZAKE NI BORA KULIKO KWENDA KTK JIHAAD FIY


SABILILLAH


Kutokana na ilivyotajwa katika usimulizi wa Hadiyth ifuatayo, kwamba amali


yoyote utendayo katika masiku kumi haya, ni bora kuliko kwenda kupigana


jihadi vitani. Ukizingatia kwenda kupigana jihadi ni jambo zito mtu kuliitikia,


kwani huko kuna mashaka mbali mbali, ikiwemo khofu ya kujeruhiwa na


kupoteza viungo vya mwili, kufariki, kupoteza mali n.k. Ila hilo si zito kwa


mwenye Imani ya hali ya juu kabisa kutaka kuyakabili mashaka hayo na


kutamani kufa shahidi. Kwa hiyo usidharau Amali yoyote hata iwe ndogo vipi


itekeleze kwani Allaah Subhaana wa Ta'ala ni Al-Jawwaad (Mwingi Wa


Ukarimu), Al-Kariym (Karimu), Al-Wahhaab (Mwingi Wa Kutunuka, Mpaji


Wa Yote), Al-Majiyd (Mwingi Mno Wa Vipawa Na Ukarimu).





Imetoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba Mjumbe wa


Allaah Amesema: ((Hakuna siku ambazo vitendo vyake vyema Anavipenda


Allaah kama siku kumi hizi)) (siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah)


Akaulizwa, je, hata Jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu (Swalla Allaahu


'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu


 4 


Aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo)) [Al-Bukhaariy.]


IBADA ZOTE ZIMEJUMUIKA KTK SIKU HIZI 10


Ibada zote zimejumuika katika siku kumi hizi nazo ni Swalah, Swawm, Swadaqah, Hajj na Umra, wala hazijumuiki hizi wakati mwingine.


KUFUNGA SIKU HIZI KHASWA SIKU YA 'ARAFA





Kutoka kwa Abu Sa'iydil-Khudhwriyy (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Mwenye kufunga siku kwa ajili ya Allaah, basi Allaah Atamuokoa uso wake kutokana na moto kwa umbali wa miaka sabini)) [Al-Bukhaariy na Muslim.[





Amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Kila Amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah Anasema isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye nitakayemlipa)) [Al-Bukhaariy na Muslim).


MATENDO MEMA YA KUTENDA KTK SIKU KUMI HIZI


Kutekeleza Hajj na 'Umrah (kwa mwenye uwezo(





Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: (('Umrah hadi 'Umrah hufuta (madhambi) baina yake, na Hajjum-Mabruur haina jazaa ila Pepo)) [Al-Bukhaariy na Muslim(.


 5 





Imetoka kwa Abu Hurayrah(Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Aliulizwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amali gani ni bora kabisa?" Kasema: ((Kumuamini Allaah na Mtume Wake)), Akaulizwa:"Kisha nini?" Kasema: ((Jihaad katika njia ya Allaah)). Akaulizwa: "Kisha nini?" Kasema: ((Hajj Mabruur)) [Al-Bukhaariy na Muslim.(


KUOMBA TAWBAH YA KWELI NA KUJIEPUSHA NA MAASI


Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala :





((Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allaah toba iliyo ya kweli!))


[At-Tahriym: 8).


Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Ametupa matumaini makubwa ya kufutiwa madhambi na makosa yetu katika usimulizi ufuatao:





Kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu 'anhu): "Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Allaah Amesema: Ee Mwana Adam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakusamehe yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee Mwana Adam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfira, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee Mwana Adam, Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na msamaha unaolingana nao)) [Imetolewa na At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan.[


 6 


KUMKUMBUKA SANA ALLAH (Subhaanahu wa Ta'ala)


Kwa Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, Takbiyr (kusema: Subhaana Allaah, AlhamduliLlaah,Laa Ilaaha Illa Allaah, Allaahu Akbar)





Imetoka kwa ibn 'Umar kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Amesema: ((Hakuna siku zilizokuwa tukufu kwa Allaah na zilizokuwa vitendo vyake vipenzi kabisa Kwake kama siku hizi, basi zidisheni Tahliyl na Takbiyr na Tahmiyd)) [Ahmad.[


INAVYOPASA KUFANYA TAKBIIR:


Katika ibada ambazo zinazo takiwa kufanywa katika masiku kumi ya Dhul Hijja nikukithirisha kutowa Takbira, kutoka kwa Muhamad bin Abubakari AL Thaqafy kwamba alimuuliza Anasi bin maliki (r.a) wakiwa wanatembea kutoka mina kwenda Arafa, mlikuwa mnafanya nini katika masiku haya kumi wakati mlipokuwa na mtume (s.a.w) akasema :alikuwa miongoni mwetu mtu anatowa Tahlil (Laiha haila Allah), na mtume hamkatazi, na miongoni mwetu kuna wanao towa takbira, na mtume hawakatazi.


Imepokelewa na imamu Bukharin a Muslim.


AINA ZA TAKBIRA KATIKA SIKU KUMI ZA DHUL HIJA.


Takbira zinazo takiwa kusemwa na muislam zimegawanyika katika sehemu mbili:


1.Takbira ambayo ni Mutlaq:


Nayo nitakbira ambayo haina muda maalumu,bali inatajwa na muislam wakati wowote na sehemu yoyote, asubuhi na jiuni, kabla ya swala na baada ya swala.


Nisuna kupiga takbira katika masiku kumi ya mwanzo katika mwezi wa dhul hijja, na baki ya masiku ya Tashriiq.


Na takbira hiyo inaanza kwa kuingia mwezi wa dhul hijja tangu kuzama kwa juwa siku ya mwisho ya mwezi wa dhul hijja (mfungo tatu), mpaka mwisho wa siu za tashriiq, yaani tarehe (11-13) katika mwezi wa dhul hija.


 7  :2.Takbira ambayo ni Muqayad Nayo nitakbari inayo semwa baada ya swala zote za faradhi, nazo zinaanza alfajiri ya siku ya Arafa mpaka kuzama juwa katiku siku za Tashriiq, ni juu ya za swala kisha akasema Adhkarikila muislam kila anapo toa salam katika kila baada ya swala basi anatakiwa atowe takbira, nah ii nikwa asiekuwa Hji, ama alhaji anaanza siku ya kumi baada ya kutupa mawe katika kiguzo kikubwa mpaka siku ta kumi na tatu katika masiku ya Tashriiq.


SIFA YA KUTOWA TAKBIRA:


Amesema Imamu Ibn Othaymin (Allah amrehemu) katika kitabu sha Sharhu Al mumty.:


Sifa za Takbira katika masiku kumi ya Dhul hijja yana Qaulii tatu katika qauli za wana wa chuoni:


1.Nimuislam kusema: Allah akbar, Allah akbar, Laa ilaha ila Allah Allah akbar Allah akbar walilahil hamdu


اللّ أكبر، اللّ أكبر، لا إله إلا اللّ، واللّ أكبر، اللّ أكبر، ولله الحمد(. )


2.Nimuislam kusema: Allah akbar, Allah akbar, Allah akbar, Laa ilaha ila Allah Allah akbar, Allah akbar, Allah akbar, walilahil hamdu.


.( اللّ أكبر، اللّ أكبر، اللّ أكبر، لا إله إلا اللّ، واللّ أكبر، اللّ أكبر، اللّ أكبر، ولله الحمد )


3. Nimuislam kusema: Allah akbar, Allah akbar, Allah akbar, Laa ilaha ila Allah waAllah akbar, Allah akbar walilahil hamdu.


"اللّ أكبر، اللّ أكبر، اللّ أكبر، لا إله إلا اللّ، واللّ أكبر، اللّ أكبر، ولله الحمد


Katika maswala haya ya sifa za takbira hakuna dalili ambazo zimekuja kusema kuwa moja katika hizi aina tatu nibora kuliko zingine, inabaki nijuu ya muislam atowe takbira kulingana na anavyo taka mwenyewe.


KUZIDISHA VITENDO VYEMA MBALI MBALI


Mbali ya kutekeleza fardhi ya Swalah kwa kuswali kwa wakati wake, kuswali Sunnah zaidi, kusoma Qur-aan, Swadaqah, Du'aa, kutii wazazi na kuwafanyia wema, kuwasiliana na jamaa (kuunga undugu), kuwafanyia wema jirani, kuamrishana mema na kukatazana maovu, kufanyiana wema na ihsani na kadhalika.


 8 


Allah tujalie na utupe tawfiiq ya kutenda mema atika masiku haya matukufu, na katika masiku mengine, wasamehe wazazi wetu na waislam wote, Allah tunakuomba mwisho mwema.



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI