Nakala




MASIKU KUMI BORA KATIKA MWEZI WA DHUL-HIJJA





Mtunzi:


Muhammad bin Ibrahim bin Suud Al-Sabri





Mfasiri:


Yasini Twaha Hassani.


Abubakari SHabani Rukonkwa.


Kimerejewa na:


Yunus Kanuni Ngenda





MASIKU KUMI BORA KATIKA MWEZI WA DHUL-HIJJA


Utangulizi:


Sifa zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu ambaye amewaneemesha waja


wake kwa kuwaletea misimu ya kheri ili iwe ni sababu ya kufutiwa madhambi yao


na awalipe kutokana na mema yao, namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na


kumsifu kwa muwafikisha anayemtaka katika waja wake kwa kuyatumia masiku


haya kwa kumtii na kumogopa, na akajaalia wengine katika waja wake ni wenye


kuzipoteza siku hizo.


Nakiri kwa moya na kutamka kwa ulimi ya kwamba hapana Mola apasae


kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu mmoja hana mshirika katika


Uungu wake, na nina kiri kwa moya na kutamka kwa ulimi ya kwamba Muhammad


ni mja wake na mjumbe wake, rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake


pamoja na familia yake na Maswahaba wake na wote watakao mfuata kwa wema


mpaka siku ya mwisho.


Amma baad.


UBORA WA MASIKU KUMI


Hakika miongoni mwa fadhila za Mwenyezi Mungu mtukufu na neema zake


juu ya waja wake amewaandalia misimu na masiku yaliyo bora ili iwe ni mavuno


kwa wenye kufanya yaliyo mema, na ni uwanja wa kushindana katika kheri kwa


wale wenye kutaka kushindana, na miongoni mwa misimu hiyo na iliyo bora zaidi


ni ile ambayo ameithibitisha Mtume Muhammad (s.a.w), ya kwamba masiku bora


kushinda yote katika masiku ya duniani ni siku kumi za mwanzo katika mwezi wa


Dhul-hijja.


Kutoka kwa Abdillahi bin Abbas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amsema:


((Hakuna masiku ambayo ni bora kufanya matendo mema ndani yake kuliko


masiku haya)).


Yaani: Masiku kumi. Wakasema Maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi


Mungu hata jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu?! Akasema: ((Hata jihadi katika


njia ya Mwenyezi Mungu!! Isipokua mtu ametoka kwa nafsi yake na mali yake na


hakurejea na chochote)).


Kaipokea Hadithi hii Imamu Bukhari na Ahmad na Abudaud na tamshi ni la


kwake, na Tirmidhi na Ibn Maaja.


 3 


Ni hakika kabisa hizi ni siku zenye baraka, Mwenyezi Mungu Mtukufu


kaziapia, na kula kiapo katika jambo ni dalili ya umuhimu wa jambo hilo na


utukufu wake ,


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Naapa kwa alfajiri. Na kwa masiku


kumi}. Suratul Fajri (1-2.)


Amesema Abdillahi bin Abbas (r.a) na wengi katika wanachuoni


waliotangulia na wa sasa: Kwa hakika ni siku kumi katika mwezi wa dhul-hijja.


Kasema Ibn Kathir na ndio sahihi.


Na Mtume (s.a.w) kwa hakika amehimiza kufanya matendo mema katika


masiku hayo kutokana na ubora wake na utukufu wake, na ubora wa zama hizo kwa


watu wa dunia nzima, na ubora wa sehemu pia-hii ni maalum kwa mahujaji wa


nyumba ya Mwenyezi Mungu Tukufu na kwasababu ndani yake kuna siku ya Arafa


na siku ya kuchinja na ibada ya hijja kwa ujumla.


Amesema Al-hafidh ibn Hajar katika fat-hulbar: Na linalo dhihirika na


kutukuzwa masiku haya kumi katika mwezi wa dhul-hijja ni kwasababu ya


kukusanyika ndani yake ibada kubwa kubwa nazo ni: Swala, funga, sadaka na hijja.


Na mambo haya hayapatikani katika masiku mengine.


Kaulizwa Sheikhul-islam ibn Taymia (r.h) kuhusu siku kumi za dhul-hijja na


mausiku kumi ya mwisho katika mwezi mtukufu wa Ramadhan ni kipi bora?


Akajibu: (Masiku kumi ya dhul-hijja ni bora kuliko masiku kumi ya mwezi wa


Ramadhan, na mausiku kumi ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ni bora mausiku


kumi ya dhul-hijja.


Kwasababu hiyo hakuna tatizo kwa wema walio tangulia kuyatumia masiku


hayo kwa kufanya matendo mema.


Kwa hakika alikua Said ibn Jubeyr (r.h) na ndiye aliyepokea Hadithi ya Ibn


Abbas (r.a) iliyo tangulia: (Pindi yanapoingia masiku kumi anajitahidi sana katika


ibada mpaka wengine wanashindwa kumuiga). Kapokea maneno haya Imamu


Da'ramy kwa upokezi mzuri.


Ndugu yangu Muislam: Kwa hakika kuyafikia masikia masiku haya ya hijja


ni neema kubwa miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya mja


wake, wanayatukuza masiku haya na kuyaheshim watu wema kwa kujipinda katika


ibada, na kwa hakika ni lazima kwa Muislam kuwa na hisia na neema hii na


kuitumia fursa hii kwa kujihimiza sana katika masiku haya na kupambana na nafsi


yake katika kufanya mema.


Amesema Abu'Othman Nahdy (r.h) kutoka kwa wema walio tangulia:


(Walikuwa wanayatukuza makumi matatu: Kumi la mwisho katika mwezi mtukufu


wa Ramadhan, na kumi la mwanzo katika mwezi wa Dhul-hijja, na kumi la


mwanzo katika mwezi wa Muharram).


Na kwa hakika miongoni mwa fadhila za Mwenyezi Mungu juu ya waja


wake ni kuwepo kwa njia nyingi za kheri na kuwekwa njia mbali mbali za kumtii


 4 


Menyezi Mungu ili Muislam azidi kuwa na uchsngamfu katika ibada na abaki katika hali ya kufanya ibada na kumtii Mola wake.


MIONGONI MWA MATENDO YA SUNNA KATIKA MASIKU KUMI YA DHUL-HIJJA


1-Funga:


Ni sunna afunge siku ya tisa katika mwezi wa dhul-hijja, kwasababu Mtume (s.a.w) amehimiza matendo mema ndani yake, na funga ni miongoni mwa matendo mema, na kwa hakika yamepokelewa yanayo julisha kufunga kwake kwa Hadithi ya Hunayda ibn Khalid kutoka kwa mke wake amesema: Nimehadithiwa na baadhi ya wakeze Mtume (s.a.w): ((Ya kwamba Mtume (s.a.w) alikua anafunga Ashura' na siku ya tisa katika mwezi wa dhul-hijja na siku tatu katika kila mwezi…)).


Kapokea Hadithi hii Imamu Ahmad na Abudaud na Nnasai na akaisahihisha Sheikh Albany (r.h.)


Na alikua Abdillahi bin Omar (r.a) akizifunga siku hizo, vilevile Mujahid na wasiokua hao miongoni mwa wana chuoni. Na wana chuoni walio wengi wanazungumzia juu ya ufungaji wake.


Kwasababu hiyo amesema Imamu Nnawawy (r.h): (Kufunga siku hizo imependekezwa mapendekezo makubwa).


Lakini yanayo fanywa na baadhi ya waumini wa kiislam kufunga kwao siku tatu katika mwezi wa dhul-hijja, wakikusudia siku ya saba ya nane na ya tisa, mpangilio kama huu hauna asili wala dalili yoyote.


2-Takbira na Tahlili:


Wanadhihirisha wanaume, na wanawake kwa sauti ya chini.


Kutoka kwa Abdallah bin Omar (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema: ((Hakuna siku zenye ubora mbele ya Mwenyezi Mungu na matendo mema kufanywa ndani yake kama masiku kumi haya, zidisheni ndani yake kwa kusema la' Ilaha illa LLah, Allahu akbar na Alhamdu liLLah)). Kapokea Hadithi hii Imamu Ahamad na Twabrany na Abuu Awana.


Amesema Imamu Bukhari (r.h): (Alikua Omar (r.a) akitoa takbira katika hema lake Mina wanamsikia waliopo msikitini na wao wanatoa takbira na watu wa sokoni wanatoa takbira hadi Mina yote inasikika takbira.


Na alikua Abdallah bin Omar (r.a) akileta takbira Mina katika masiku hayo na baada ya swala na anapokua kitandani na kwenye hema lake na katika vikao vyake na anapokua anatembea barabarani kwa masiku yote hayo).


TAKBIRA ZIPO AINA MBILI:


 5 


1-Takbira isiyokuwa na kikomo.


2-Takbira yenye kikomo.


Takbira isiyo na kikomo: Huletwa wakati wowote kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya mwisho ya tashriq (tarehe 13).


Na takbira yenye kikomo: Huletwa baada ya swala kuanzia alfajiri ya siku ya Arafa kwa asiyekuwa Hajj mpaka siku ya mwisho ya mwisho ya tashriq (tarehe 13).


Lakini yule aliyopo katika ibada ya Hijja ataanza kuleta takbira baada ya kutupa mawe siku ya Idd.


Kwa hakika yamethibiti mambo hayo kwa makubaliano ya wana chuoni na vitendo vya Maswahaba (r.a).


MATAMSHI YA TAKBIRA


1-Allahu akbar, Allahu akbar, Allahu akbar kabira.


2-Allahu akbar, Allahu akbar, la' Ilaha illa LLahu wa LLahu akbar, Allahu akbar wa liLlahil-hamd.


3-Allahu akbar, Allahu akbar, Allahu akbar, la' Ilaha illa Llahu wa Llahu akbar, Allahu akbar, Allahu akbar wa lillahil-hamd.


Amesema katika Subuli ssalam: Na katika sheria kuna namna nyingi na mapendekezo mengi kutoka kwa Maimamu nayo hujulisha ya kwamba kuna upana katika mambo haya, na ukiiangalia Aya huonyesha hivo.


Ni juu yetu sisi Waislam kuhuisha sunna hizi zilizo achwa katika masiku haya, inakaribia kusahaulika hata kwa watu wema tofauti na walivyokuwa wema walio tangulia, takbira ziletwe misikitini, majumbani, sokoni, barabarani na kuwakumbusha watu wa nyumbani na kuwazoesha watoto hali hiyo.


KUJIKURUBISHA KWA MWENYEZI MUNGU MTUKUFU KWA KUCHINJA UDHUHIYA:


Nayo ni sunna yenye mkazo kwa kauli iliyokua sahihi ya wana chuoni, na inakua ni sunna yenye mkazo kwa yule mwenye uwezo na wasaa wa mali, lakini siyo wajibu, na hakuna tatizo mtu akikopa atakapokua na uwezo wa kulipa, inafaa kwa Mwislam mwenye uwezo asipuuzie jambo hili, kwa kauli ya Anasi (r.a): (Amechinja Mtume (s.a.w) kwenye udhuhiya kondoo wawili walioshiba wenye mapembe amewachinja kwa mkono wake na akasema Bismi LLahi Allahu akbar na akaweka miguu yake karibu na shingo lake). Amepokea Hadithi hii Imamu Bukhari na Muslim.


Anasema Abdallah bin Omar (r.a): (Ameishi Mtume (s.a.w) katika mji wa Madina kwa mda wa miaka kumi akichinja mnyama wa udhuhiya). Kapokea Hadithi hii Imamu Ahmad na Tirmidhy.


Na amesema ibnul-Qayyim (r.h): (Na hakuwa Mtume (s.a.w) akiacha kuchinja mnyama wa udhuhiya.


 6 


Apupie Muislam jambo hilo kwasababu ndani yake kuna kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu kwa kuchinja kichinjwa kwa jina lake peke yake asiyekua na mshirika, na kuhuisha sunna ya Baba yetu Ibrahim (a.s), na kumuiga Nabii Muhammad (s.a.w), na ndani yake kuna kuwawezesha watu wa nyumbani na mafakiri na masikini siku ya Idd, na ndani kuna hikma kubwa hazijifichi kwa kila mwenye muono.


TAHADHARI MUHIMU:


Yanapoingia masiku kumi ya mwanzo katika mwezi wa dhul-hijja, ni haramu kwa anaye kusudia kuchinja kunyoa nywele zake au kukata kucha zake au kunyoa chochote katika mwili wake mpaka atakapo chinja siku ya Idd, na akinuia kuchinja katikati ya masiku hayo atajizuia mara tu baada ya kuweka nia na hapatokua na tatizo juu yake ikiwa ametangulia kunyoa nywele au kukata kucha kabla ya nia.


Na hilo ni kama alivyopokea Imamu Muslim katika Swhihi yake kutoka kwa Ummu Salama (r.a) ya kwamba Mtume (s.a.w) amesema: (Mtakapouona mwezi mwandamo wa dhul-hija na akakusudia mmoja wenu kuchinja, basi ajizuie na kukata nywele zake na kucha zake). Kapokea Hadithi hii Imamu Muslim.


Na katika upokezi mwingine wa kwake: (Asikate nywele yeyote na wala asikate kucha).


Na hikma katika makatazo haya: Ili abaki na viungo vyote kamili iwe ni sababu ya kuachwa huru na moto, na pamesemwa: Ili ajifananishe na aliye kusudia Hijja. kayasema maneno haya Imamu Nnawawy katika sharhi sahihi Muslim.


FAIDA:


Katazo hili ni maalum kwa yule atakae chinja, haliwahusu watakao chinjiwa wakiwemo wake, watoto hawahusiki na katazo hili; kwa sababu Mtume (s.a.w) akuwa akichinja kwa ajili ya watu wa nyumbani kwake na haikupokelewa kutoka kwake kwamba aliwaamrisha wajizuie, vilevile atakae muwakilisha mtu kwa hakika siyo haramu juu yake kunyoa nywele au kukata kucha isipokua itakuwa ni kwa yule aliyewakilishwa, vilevile yule atakae simamia wasia kwa hakika yeye hajizuii, na atakaye kata kucha zake au kunyoa chochote katika mwili wake atakua katika udhuru; hakuna chochote juu yake atakua katika hukumu ya waliosahau, na yule atakayekua na nywele lakini zinamuudhi au kucha akizinyoa au kuzikata hakuna tatizo, ama yule atakae kusudia kunyoa nywele au kukata kucha atapata dhambi na hakuna kafara juu yake inatakiwa atubie na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu.


Na yeyote atakaekuwa katika Miiqat na anakusudia kufanya ibada ya Hijja au Umra na akiwa na nia ya kuchinja kwa hakika asinyoe chochote katika nywele zake wala kukata kucha zake, lakini wakati wa kumaliza ibada ya Hijja au Umra atapunguza nywele zake tu kwasababu ni ibada katika ibada za Umra.


 7 


KUZIDISHA MATENDO MEMA KWA UJUMLA:


Kwasababu matendo mema ni yenye kupendwa zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wakati wowote na zama zozote, na yanakua na uzito sana masiku haya yenye Baraka, kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w):


((Hakuna masiku ambayo ni bora kufanya matendo mema ndani yake kuliko masiku haya…)),


Na hili linaonyesha ubora wa matendo mema ndani yake na ukubwa wa malipo yake, ni juu ya Muislam autumie muda wake katika masiku haya kumi kwa kuzidisha kufanya yaliyo mazuri kwa kusoma Qur-ani na kumtaja sana Mwenyezi Mungu na kuzidisha dua na kutoa sadaka na kuwafanyia wema wazazi wawili na kuunga udugu na kuamrisha mema na kukataza mabaya na yasiyokua hayo katika njia za kheri.


NA MIONGONI MWA MATENDO MEMA:


Swala: Ni bora zaidi kuwahi katika swala za faradhi na kukpupia katika safu za mbele na kuzidisha swala za sunna, kwasababu hayo ni miongoni mwa yanayo mkurubisha mja kwa Mwenyezi Mungu.


Kutoka kwa Abdullahi bin Masuud (r.a) amesema: Nilisema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni matendo gani yaliyo bora? Akasema: (Swala kwa wakati wake), nikasema kisha nini? Akasema: (Kuwatendea wema wazazi wawili), nikasema kisha nini? Akasema: (Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu). Kaipokea Hadithi hii Imamu Bukharin a Muslim.


Na kutoka kwa Thaubani (r.a) amesema: Nilimsikia Mtume (s.a.w) akisema: (Zidisha sana kusujudu kwa ajili ya Allah, kwa hakika wewe huwezi kusujudu sijda yoyote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu isipokua Mwenyezi Mungu atakupandisha daraja kwa sijda hiyo, na atakufutia madhambi kwa sababu hiyo). Kaipokea Hadithi hii Imamu Muslim.


SIKU YA ARAFA:


Nayo ni katika masiku bora matukufu; kwasababu ni siku ya kusamehewa madhambi na kufutiwa makosa, nayo ni siku ya Idd kwa watu waliosimama katika viwanja vya Arafa, na ni sunna kufunga kwa watu wasiokua kuwa katika viwanja vya Arafa.


Nayo ni siku iliyo kamilishwa dini na kutimizwa neema juu ya umma huu, hawahitaji dini nyingine tofauti na hii, na kwasababu hiyo amejaalia Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa ndio hitimisho ya dini zote, haitokubaliwa kwa yeyote dini tofauti na hii.


Kutoka kwa Omar (r.a) ya kwamba bwana mmoja miongoni mwa mayahudi amesema: Ewe Amiril-muuminina Aya katika kitabu chenu mnaisoma laiti tungelijua sisi mayahudi zama iliposhuka tungelifanya siku hiyo kuwa ni sikukuu, akasema: Aya gani hiyo? Akasema: {Leo nimekukamilishieni dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislam uwe ndiyo dini}. (Suratul-Maida 3).


 8 


Akasema Omar (r.a): Tunaijua siku na sehem iliposhuka Aya hiyo kwa Mtume (s.a.w) alikua amesimama katika uwanja wa Arafa siku ya ijumaa. Kapokea Hadithi hii Imamu Bukhari na Muslim.


Na huyu bwana aliyemuuliza Omar (r.a) anaitwa Ka'bil-Ahbari, kama ilivyopokelewa katika upokezi wa Twabary, na ndani yake: Imeshuka Aya hiyo siku ya ijumaa na siku ya Arafa, na siku zote hizo mbili tunamshukuru Mwenyezi Mungu ni sikukuu kwetu.


Na kutoka kwa Aisha (r.a) hakika Mtume (s.a.w) alisema: (Hakuna siku ambayo Mwenyezi Mungu anawaacha huru na moto waja wake zaidi kama siku ya Arafa, na hakika Mwenyezi Mungu anasogea kasha anajivuna mbele ya Malaika anasema: Nini wanataka waja wangu?) Amepokea Hadithi hii Imamu Muslim.


Amesema ibn Abdul-barr: Na hii inaonyesha kwamba waja hao wamesamehewa kwasababu Mwenyezi Mungu hawezi kujivuna kwa waja wenye makosa ila baada ya kuwa wametubia na wamesamehewa.


Kutoka kwa Abuu Hurayra (r.a) alisema: alisema Mtume (s.a.w): (Hakika Mwenyezi Mungu anajivuna kwa Malaika kwasababu ya watu waliopo katika viwanja vya Arafa kasha anasema kuwaambia Malaika: Tazameni waja wangu wamekuja wakiwa ni wenye mavumbi). Hadithi hii ameipokea Imamu Ahmad na ibn Khuzeyma kwa upokezi sahihi na ameisahihisha Albany.


Hadithi hizi zinaonyesha ubora wa siku ya Arafa na siku ya Arafa ni katika masiku bora ambayo dua zinajibiwa ndani yake, na makosa yanasamehewa, ni juu ya kila Muislam afanye juhudi ya kutenda matendo mema na hasa katika siku hii kubwa afanye dhikri na aombe dua, asome Qur-ani, aswali na atoe sadaka huenda akasamehewa na Mwenyezi Mungu na akaachwa huru kutokana na moto.


Ametaja Ibn Rajab katika kitabu chake cha Allatwaifu kwamba kuachwa huru na moto ni kwa waislam wote duniani.


Nijuu ya kila Muislam afanye pupa ya kufunga siku ya Arafa, hakika Mtume (s.a.w) ameihusisha na mambo mengi ya kheri, pale alipoitaja kuwa ni katika masiku ya mfungo tatu na akabainisha ubora mkubwa wa kufunga siku hiyo.


Imepokelewa kutoka Abiy Qatada Al-answary (r.a): Hakika Mtume (s.a.w) aliulizwa kuhusu siku ya Arafa akasema: (Mwenye kufunga anasamehewa mwaka uliopita na mwaka ujao), ameipoke Hadithi hii Imamu Muslim.


Na swaumu hii ni sunna kwa wasiokua Mahujaji, lakini kwa Mahujaji sio sunna kufunga na kutokufunga ni bora kwao kwa kumfuata Mtume (s.a.w) kwasababu Mtume (s.a.w) alisimama katika viwanja vya Arafa akiwa hajafunga.


Kutoka kwa Ummul-Fadhil bintul Harith (r.a): (Hakika watu walitofautiana kwake kuhusu Mtume (s.a.w) wakasema baadhi ya watu: Mtume (s.a.w) amefunga. Wakasema wengine: Mtume (s.a.w) hajafunga. Akasema Ummul-Fadhil: Nikamtumia glasi ya maziwa akiwa amesimama juu ya mnyama wake katika viwanja vya Arafa akanywa). Ameipokea Hadithi hii Imamu Bukhari na Muslim.


 9 


Na kwasababu mtu asiyefunga anakua na nguvu ya kuomba dua kuliko mtu aliyefunga hasa wakati wa joto kali. Na dua siku ya Arafa ina ubora mkubwa kuliko dua zingine, hakika Mtume (s.a.w) alisema: (Dua bora ni dua ya siku ya Arafa, na maneno bora niliyosema mimi na Mitume waliopita kabla yangu ni la' Ilaha illa LLahu wahdahu la' sharika lahu, lahul-mulku wa lahul-hamdu wa Huwa ala' kulli shay'in qadir). Hadithi hii ameipokea Imamu Maliki na Tirmidhy .


Amesema ibn Abdil-Barr: Na katika hii kuna faida za kifqhi:


1-Dua ya siku ya Arafa ni bora kuliko dua za masiku mengine.


2-Hakika siku Arafa ni bora kuliko masiku mengine.


3-Dua ya siku ya Arafa ni yenye kujibiwa.


4-Hakika dhikri iliyo bora ni kusema:


(la' Ilaha illa LLahu wahdahu la' sharika lahu, lahul-mulku wa lahul-hamdu wa Huwa ala' kulli shay'in qadir).


Muislam afanye pupa kumuomba Mwenyezi Mungu katika siku hii tukufu ili aneemeke na fadhila za siku hiyo hali ya kuwa ni mwenye kutaraji kujibiwa na kukubaliwa, na anatakiwa aiombee nafsi yake na wazazi wake na watu wake na Uislam na Waislam, na pindi atakapo funga siku hiyo na akaomba dua wakati wa kufuturu basi ndio kukubaliwa kwa dua yake, kwani dua ya aliyefunga ni yenye kujibiwa.


Ni juu ya kila Muislam azidishe kutoa shahada na kuwa na ikhlas katika matendo mema na awe ni mwenye kusadikisha, kwasababu hayo ndiyo asili ya dini ya Uislam ambayo aliichagua Mwenyezi Mungu kwa umma huu na akaikamilisha katika siku hii tukufu ya Arafa.


KUTEKELEZA IBADA YA HIJJA NA UMRA


Hakika mambo bora yanayofanywa katika masiku haya matukufu ni kuhiji katika nyumba ya Mwenyezi Mungu takatifu, yeyote atakaye afikishwa na Mwenyezi Mungu kuhiji katika nyumba yake tukufu inavyotakiwa basi atakua na fungu katika maneno ya Mtume (s.a.w): (Umra mpaka Umra nyingine ni yenye kufuta madhambi yaliyo baina yake, na Hjja iliyo takasika haina malipo isipokua ni pepo). Ameipokea Hadithi hii Imamu Bukhar na Muslim kutoka kwa Abuu Hurayra (r.a).


Haya mambo bora na matendo bora jitahidini myapate na tahadharini na uvivu, lazima tufaham kwamba Mwenyezi Mungu ana nafahat (msukumo) katika katika siku hizi tukufu katika kufanya mambo ya kheri, basi tuitumie nafasi hii na tuzidishe kufanya matendo mema huenda Mwenyezi Mungu Mtukufu akatusamehe mapungufu yetu na makosa yetu.


Fanya haraka ndugu yangu Muislam kuyatumia vizuri masiku haya bora na yenye Baraka kwa kutenda matendo mema na kujitahidi sana katika ibada, kwa hakika hakuna chenye thamani kilichobakia katika umri wako.


 10 


Basi tubia kwa Mwenyezi Mungu kutokana na muda uliopoteza na ufahamu kwamba juhudi yako ya katika kufanya matendo mema katika masiku haya matukufu ndio kuikimbilia kheri na ndio dalili ya ucha Mungu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa moyo}.


(Suratul-Hajj 32).


Tunaomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atuandalie mambo yetu uongofu na atuafikishe kufanya matendo yalito mema na atujaalie kuwa katika waja wake wenye ikhlas. Ameen!!


Wabi LLahi Tawfiq.


 11 



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI